Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9275

Hasira za Trim Saleem kwa Africa Magic,DStv: Aataka wajitambue na kujiongeza

$
0
0


Dear Africa Magic(DStv), tumechoshwa na kinachoitwa Africa Magic Viewers Choice Awards which is more Nigerian and more western, Please call it Nigerian Magic Viewers Choice Awards. Filamu za Nigeria kwa zaidi ya miaka 8 sasa hazina nafasi katika soko la Africa Mashariki na Kati kutokana na soko kutekwa na filamu za Tanzania. hata leo ukimuweka star wa filamu Nigeria na star wa filamu Tanzania katika nchi hizi star atakayepata attention kubwa ni star wa Tanzania sasa basi tunaomba muanzishe tuzo za Africa Magic Swahili zitakazohusu filamu za lugha ya Kiswahili toka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi etc kisha muweke vipengele 2 vya Kiingereza kwa ajili ya filamu za Nigeria kama mnavyotufanyia sisi sasa hivi huko Nigeria.
Kutuweka katika vipengele viwili pekee katika kinachoitwa Africa Magic Viewers Choice Awards sio fair ni kukuza na kutangaza filamu za Nigeria kibiashara na kudidimiza filamu za Tanzania na Kiswahili kwa ujumla. mlianzisha @Africa Magic East na Maisha Magic Bongo kwasababu mliona filamu za Tanzania kuchanua. Ikiwa stations zenu zote 2 zinategemea contents kutoka Tanzania, Kenya na Africa mashariki kwa ujumla na sio Nigeria, kwanini msitoe heshima kuanzisha tuzo kuzidi kuchochea maendeleo ya film industry Tanzania na Africa Mashariki kwa ujumla tofauti na sasa Tanzania kuonekana wadogo mbele ya Nigeria wakati si kweli.
We have big movie stars here instagram inawatosha kudhibitisha Tanzania kuwa na mastaa wenye fan base kubwa kuliko wengi wa Nigeria, These big stars can grace the event and be talk of the town. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ni kuwa mnaifanyia Africa Magic Viewers Choice Awards kutokana na viewership kubwa Nigeria ambapo ndio filamu zao mnaziweka katika kila categories hata kama hazikidhi vigezo sababu tu zimetumia kiingereza au pijini english.
Lakini mnasahau kuwa best film, best actor, best actress, best editor, best director, best make up artist, best costume hazijali lugha iliyotumika kwasababu ni sanaa na sisi Tanzania, Kenya tuna filamu kila mwaka zenye vigezo vya kupambana katika categories zote hizo.
Africa Magic Viewers Choice Awards haina viewership ya kueleweka Tanzania wala Africa mashariki na kati so kwanini msitupe heshima ya kuanzisha Africa Magic Viewers Choice Awards Swahili kila mwaka ambayo itakuwa na viewership kubwa zaidi Africa Mashariki !!. Tutafurahi sana na kuona kweli mnajali maendelo ya filamu za Kiswahili kwasababu biashara mtafanya huku tena wakati huu ikiwa hatuna tuzo kubwa za filamu you can be the giant one. Na tuzo kurushwa kwenye vituo vya Africa Magic Bongo na East
Tumesema haya kwasababu tumechoka tunaona sanaa haifanyiwi balanced, Siri Ya Mtungi, Aisha, Kati Kati, Zilizila, Naomba Niseme zilistahili categories zaidi ya moja katika tuzo zenu kuchuana na Nigeria na hata kushindwa baadhi ya vipengele kuwabwaga Nigeria. Tunaomba mufikirie haya maoni yetu, Nimeandika kuwafikishia ujumbe kwasababu ni wasanii wengi sana wanalalamikia kuitukuza Nigeria na kuicha Africa Mashariki ambapo tumepigana kufika tulipo.
Tunajua mnafanya biashara but tunaombeni mbadilike, event mkiandaa itajaza watu wengi tu. Ni matumaini yetu mtakuwa sehemu ya kuchochea maendeleo ya filamu za Kiswahili kwasababu nyie ni network kubwa na sio kuchochea maendeleo ya filamu za Nigeria pekee. Filamu za Tanzania kufanikiwa kuziondoa sokoni filamu za Nigeria Africa Mashariki na Kati ni ushindi pekee unaohitaji wasanii wetu kupongezwa kwa tuzo kubwa zinazojitegemea.
Nawatakia kazi njema


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9275

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>