Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9183 articles
Browse latest View live

Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayesimamia Menejimenti ya Fedha za Umma (Public Finance Management).
Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Mwinyimvua alikuwa Msaidizi wa Rais wa muda mrefu wa masuala ya uchumi.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue leo, Jumatatu, Februari 2, 2015, imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwinyimvua ulianza Jumamosi, Januari 24, 2015.
Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ni mwanataaluma mwenye ujuzi na uzoefu mkubwa katika uchumi.
Anayo shahada ya kwanza ya B.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1986), Shahada ya Uzamili ya M.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1988) na Shahada ya Uzamivu ya PhDya uchumi kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Lund cha Sweden.
Dkt. Mwinyimvua amekuwa mhadhiri wa miaka mingi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako amepanda daraja kutoka Tutorial Assistant, mwaka 1986-1988, Mhadhiri Msaidizi, mwaka 1988-1996, Mhadhiri, mwaka 1996-2005, Mhadhiri Mwandamizi, mwaka 2005-2006 na Mkuu wa Idara ya Uchumi ya chuo hicho mwaka 2006.
Dkt. Mwinyimvua aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi, mwaka 2006, nafasi ambayo ameishikilia hadi mwaka huu, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

2 Februari, 2015


Taarifa kamili kilichojiri kwa bondia profesheno Cheka

$
0
0


 
Bondia wa ngumi za kulipwa duniani Francis Cheka (32) amehukumiwa kifungo
cha miaka mitatu jela na kulipa fidia ya Sh. 1 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa
kosa la kumpiga meneja wake wa baa na kwamba hukumu hiyo imemfanya mke wake aangue
kilio kizito mahakamani. 
 
Hukumu hiyo ilitolewa leo na hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya mkoa wa Morogoro Said Msuya baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuacha shaka yoyote katika kuthibitisha shtaka hilo.
 
 Akisoma hukumu hiyo hakimu huyo alisema kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa
mshtakiwa na watu wengine wanaotumia vibaya nguvu zao na kwamba mshtakiwa anatakiwa
kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh. 1 milioni.
 
Hata hivyo Cheka alipewa nafasi ya kujitetea ili mahakama impe adhabu ya huruma hata hivyo aliieleza mahakama kuwa hana maelezo yoyote ya kujitetea zaidi ya kuiachia mahakama kuamua adhabu itakayompa. 
 
Mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo mke wa Cheka ambaye alishindwa
kutaja jina lake kutokana na kilio alidai kuwa mumewe ameonewa na kwamba hakustahili
kupewa adhabu hiyo. 
 
 Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Polisi Anganile Nsiyani kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka 2014 katika baa ya Vijana Social Hall iliyopo Manispaa ya Morogoro.
 
 Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa bila halali na akijua kufanya hivyo ni kosa Cheka alimshambulia meneja wake wa baa aliyefahamika kwa jina la Bahati Kibanda kwa kumpiga ngumi usoni na tumboni na hivyo kumsababishia maumivu makali. 
 
Alipofikishwa mahamani hapo kwa mara ya kwanza Chekaalikana shtaka hilo na hivyo upande wa mashtaka uliamua kupeleka mashahidi wane kati ya saba ambao waliithibitisha mahakamani hapo bila ya shaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo na hivyo mahakama kumtia hatiani.
 Mwisho….
 
 
   

KIPA BORA WANAWAKE AZAWADIWA 500,000/-

$
0
0



Kipa bora wa michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake, Belina Julius wa
Temeke amezawadiwa sh. 500,000 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk Fenella Mukangara.
Dk Mukangara alitoa zawadi hiyo baada ya mechi ya fainali ya michuano
iliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar
es Salaam. Dk Mukangara alikuwa mgeni rasmi kwenye fainali hiyo.
Temeke ndiyo walioibuka mabingwa wa michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya
kwanza nchini baada ya kuilaza Pwani bao 1-0 katika fainali iliyoonyeshwa
moja kwa moja (live) na televisheni ya Azam.
Ilala ilifanikiwa kutwaa baada ya kuichapa Kigoma mabao 3-0. Bingwa amepata
sh. milioni tatu, makamu bingwa sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu
ameondoka na sh. milioni moja katika michuano hiyo iliyodhaminiwa na
kampuni ya Proin.

TFF YATOA RAMBIRAMBI MSIBA WA KATIBU IRFA

$
0
0


**
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko
taarifa ya msiba wa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Iringa (IRFA), John Ambwene Mwakalobo uliotokea jana (Februari 1 mwaka huu)
mkoani Iringa baada ya kuanguka akiwa nyumbani kwake.
 
Msiba huo ni pigo kwa wadau wa mpira wa mpira wa miguu kwani wakati wa uhai
wake, Mwakalobo alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi. Mwaka 2011
alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa IRFA, kabla ya 2012 kushinda nafasi
ya Katibu Msaidizi.
 
Alizaliwa Februari 4, 1954 na kupata elimu ya sekondari katika shule ya
Azania, Dar es Salaam na baadaye mafunzo ya ualimu kwenye Chuo cha Ualimu
Mpwapwa mkoani Dodoma. Alianzia kazi ya ualimu Newala mkoani Mtwara kabla
ya kuhamia mkoani Iringa mwaka 1981. Alistaafu mwaka 2013. 
 
TFF inatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu kwa msiba huo. 
 
Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho (Februari 3 mwaka huu) kwao Kyela mkoani
Mbeya. Ameacha mke, watoto wanne na mjukuu mmoja. Bwana alitoa, Bwana
ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
 
 
 
*IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)*

TFF MBIONI KUPATA MDHAMINI FDL

$
0
0



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liko mbioni kupata mdhamini wa
Ligi Daraja la Kwanza (FDL). Tunatarajia mdhamini huyo atakuwa tayari kwa
ajili ya msimu wa 2015/2016.
Ligi Daraja la Kwanza inashirikisha timu 24 zinazocheza katika makundi
mawili ya timu 12 kila moja kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Timu zinazocheza FDL msimu huu ni African Lyon (Dar es Salaam), African
Sports (Tanga), Ashanti United (Dar es Salaam), Burkina Faso (Morogoro),
Friends Rangers (Dar es Salaam), Geita Gold (Geita), Green Warriors (Dar es
Salaam), JKT Kanembwa (Kigoma), JKT Mlale (Ruvuma) na JKT Oljoro (Arusha).
Nyingine ni Kimondo (Mbeya), Kinondoni Municipal Council (Dar es Salaam),
Kurugenzi (Iringa), Lipuli (Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mwadui (Shinyanga),
Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara,
Polisi Tabora, Rhino Rangers (Tabora), Toto Africans (Mwanza), na Villa
Squad (Dar es Salaam).
 
MECHI ZA MWISHO FDL SASA FEB 8 NA 10
 
Mechi za raundi mbili za mwisho za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa makundi
yote mawili zimerudishwa nyuma kutokana na maombi ya klabu hizo kupungaza
gharama za kuendelea kuziweka kambini timu zao.
Hivyo, Februari 8 mwaka huu kundi A litacheza mechi zake za raundi ya 21
wakati zile za raundi 22 ambayo ndiyo ya mwisho zitafanyika Februari 13
mwaka huu. Mechi za Februari 8 ni KMC vs African Lyon, Kurugenzi vs African
Sports, Majimaji vs JKT Mlale, Kimondo vs Friends Rangers, Ashanti United
vs Villa Squad, Polisi Dar vs Lipuli.
Februari 13 mwaka huu ni African Lyon vs Polisi Dar, Kurugenzi vs Lipuli,
Kimondo vs Majimaji, JKT Mlale vs Ashanti United, Friends Rangers vs
African Sports, na Villa Squad vs KMC.
Kwa upande wa kundi B wataanza mechi za raundi 22 Februari 10 mwaka huu ili
kupisha mechi za viporo za Polisi Mara zinazomalizika Februari 5 mwaka huu.
Hivyo, Februari 10 mwaka huu itakuwa ni Burkina Faso vs JKT Kanembwa,
Mwadui vs Polisi Tabora, Polisi Dodoma vs Green Warriors, Rhino Rangers vs
JKT Oljoro, Panone vs Polisi Mara, Geita Gold vs Toto Africans.
Raundi ya 22 itachezwa Februari 15 mwaka huu kwa mechi kati ya JKT Kanembwa
vs Green Warriors, Mwadui vs Burkina Faso, Polisi Tabora vs JKT Oljoro,
Polisi Dodoma vs Panone, Toto Africans vs Rhino Rangers, na Geita Gold vs
Polisi Mara.
 
 
 

Waainjilisti wa Kikristo wapinga mahakama ya kadhi ndani ya mfumo rasmi wa utawala

$
0
0


UMOJA wa Wainjilisti wa Kikristo Tanzania (Uwakita) umesema utafanya
kampeni kushawishi wananchi wapinge katiba mpya iwapo muswada wa
mahakama ya kadhi utapitishwa na bunge kuwa sheria.
Wamesema iwapo mahakama hiyo itapitishwa kuwa sheria ni kufanya dini
ya kiislam kuwa dini rasmi inayotambuliwa kisheria na kuna hatari kwa
maeneo mengi kuongozwa kwa kufuata sheria ya dini hiyo kama ilivyo
Zanzibar na kuitaka serikali na bunge kutoingilia masuala ya dini
kwani itaipeleka nchi kubaya.
“Hatukatai waislam kuwa na mahakama ya kadhi tunachotakaa wasiingize
kwenye katiba tunaweza kuwa Islamic state na tunapinga hatua na
mikakati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wa kutaka kufanya uislam kuwa
dini rasmi kikatiba jambo hili halikubaliki”
Walitoa kauli hiyo wakati wakitoa tamko kuhusu marekebisho ya sheria
mbalimbali wa mwaka 2014 ikiwemo wa mahakama ya kadhi.
Akisoma tamko hilo, mwenyekiti wa umoja huo Samson Bullegi aliitaka
serikali na bunge kutojihusisha na mikakati yoyote ile ya uanzishaji
na uendeshaji wa mahakama hiyo na iachiwe waislam wenyewe.
Pia tamko hilo lilitaka Serikali na Bunge vimetakiwa kutojihusisha na
mikakati yoyote ile ya uanzishaji na uendeshaji wa mahakama ya kadhi
bali suala hilo iachiwe waislam wenyewe kwani kinachoonekana sasa ni
kutaka kuifanya dini ya kiislam kuwa dini rasmi inayotambulika
kikatiba hali ambayo inatishia uhuru wa dini nyingine.
Alisema sasa Wakristo wa Zanzibar wamekuwa wakipata adha kutokana na
kuwepo kwa mahakama ya kadhi kwa kutolewa kwa amri kwa watu wwote
wanaoishi Zanzibar na wanaoingia Zanzibar kuendana na Mgungo wa
Ramadhanio, kuimarisha hoteli zote na restaurant zote zisiuze vyakula
wakati wa asubuhi na mchana na yeyote atakayepatikana anakula chaku;la
wakati wa machana mamlaka zinazohusika zinatakiwa kuchukua hatua.
“Kiuweli inaondoa kabisa ile maana halisi ya ya uhuru wa kuabudu
uliobainishwa kwenye katiba” alisema
Alisema suala la uhuru wa kuabudu kwa kila mtu hauzingatiwi katika
kipindi cha mwezi Ramadhani kwa upande wa Zanzibar hasa kwa kuwa kuna
sheria zinazotambua mahakama ya kadhi.
Alisema hata Waziri Mkuu  Mizengo Pinda amekuwa akitoa kauli za
kupotosha kuhusu kuanzisahwa kwa mahakama ya kadhi na kutetea uwepo wa
mahakama hiyo.
Alisema kama umoja wa wainjilisti wanaunga mkono mapendekezo yote ya
tume ya kurekebisha sheria iliyokuwa chini ya Jaji Prpfesa Ibrahim
Juma kuhusu msimamo na utaratibu wa uanzishaji wa mahakama ya kadhi,
uwe ni wa waislam wenyewe ndani ya uislam wao na wataiendesha wenyewe
na haitaigharimu seruikali” alisema
Mwenyekiti huyo alisema pia wanaunga mkono tamko la halmashauri Kuu ya
Chama cha Mapinduzi Taifa walilolitoa katika kikao chao cha Agosti 16
na 17 mwaka 2009 lililoelekeza mahakama ya kadhi ianzishwe na waislamu
wenyewe.
Aidha alisema wanaunga mkono tamko lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete
 wakati akihutubia baraza la Idd Mjini Dodoma Septemba 2011 , ambapo
alinukuliwa akisema mahakama ya kadhi itaundwa na waislam wenyewe
ndani ya uislam na wataiendesha wenyewe na haitagharamiwa na
serikali.
“Kwa maelezo hayo ya rais Kikwete hatukutegemea Waziri Mkuu
kuliendeleza tena jambo hilo maana mapendekezo hayo yametoka kwenye
Tume ya Kurekebisha Sheria ya Serikali ambayo tunaamini ina wataalam
wa kutosha wa masuala ya kisherioa katika nchi” alisema
Alisema hata tamko la waziri Mkuu ndani ya bunge la katiba linaonesha
wazi kuwa kwa makusudi seruikali ilidhamiria kuwapa bakshishi waislam
ili walegeze msimamo wao kuhusu katiba pendekezwa na kuipigia kura ya
ndio na ndivyo walivyofanya.
Pia walimataka Waziri Mkuu kuzingatia maoni ya tume ya kurekebisha
sheria iliyokuwa chini ya Profesa Ibrahim Juma, Tamkoa la Halmashauri
kuu ya CCM na tamko la Rais Kikwete alilotoa kwenye baraza la Idd
DSeptemba 30, 2011
Mjumbe wa umoja huo, Elioteru Kobelo alisema mahakama ya kadhi
ikikubalika kikatiba na kisheria italeta madhara kwa mtu ambaye si
muislam huku Katibu wa umoja huo, Cecil Simbaulanga alisema makadhi
wako katika mikoa mingi nchini na kuna kadhi mkuu pia na kazi
wanazozifanya zipo wakubaliane utendaji wao wa kazi na suala hilo
lisiingizwe kwenye katiba litaleta mgogoro mkubwa wa kidini.
mwisho

WAZIRI MKUU AVUTIWA NA SHAMBA LA KAHAWA SONGEA

$
0
0



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema amevutiwa sana na kazi iliyofanywa katika muda mfupi kwenye shamba la kahawa la Aviv lililoko kwenye kijiji cha Lipokela, wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma. 
Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, eneo kubwa la shamba limepandwa miche ya kahawa na mingine imezaa na imeshavunwa ikilinganishwa na wakati alipofika shambani hapo Julai 2013 na kutembelea tu kitalu cha miche ya zao hilo. 
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Februari 2, 2015) wakati akizungumza na wafanyakazi na menejimenti ya shamba la Aviv baada ya kulitembelea na kukagua miundombuinu ya umwagiliaji wa matone ya maji kwenye shamba hilo. 
“Mkuu wa shamba hili, Bw. Medu amenieleza kwamba mpaka sasa, wameshavuna kahawa mara moja na wanatarajia kuvuna tena hivi karibuni; lakini ili waweze kuanza kupata faida ni lazima wavune mara nne.” 
“Kilimo kinataka uvumilivu na kinataka uwekezaji mkubwa... ni lazima kiwepo; hata kwa wakulima wadogo ni lazima kiwepo licha ya ugumu wake. Sasa ukisema kilimo ni kigumu na ukaacha kulima wakati una mke na watoto, je hao watakula wapi?”, alihoji. 
Aliwasifu wamiliki wa shamba hilo kwa kuchagua kulima zao la kahawa kwani lina walaji kila mahali ulimwenguni kote. “Wameamua kulima kahawa aina ya Arabicaambayo inakubalika duniani. Uhitaji wa kahawa hii upo kila mahali kwa sababu wanywaji wapo,” alisema. 
Waziri Mkuu alisema pamoja na mafanikio hayo, shamba la Aviv linakabiliwa na changamoto ya nishati kwani linahitaji megawati 2.5 ili liweze kuendesha mitambo yake ambayo kwa sasa inatumia mafuta yanayoligharimu fedha nyingi.

Aliwataka wamiliki wa shamba hilo waendelee kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa suala hilo. 
Mapema, akisoma risala ya kampuni ya Aviv, Mkuu wa shamba hilo ambaye pia anasimamia uzalishaji wa zao la kahawa Afrika Mashariki, Bw. Medu Medappa alisema hadi sasa wamekwishalima hekta 1,060 na zote zimekwishawekewa miundombinu ya umwagiliaji wa matone na kati ya hizo, hekta 810 zimekwishapandwa miche ya kahawa.
“Shamba letu lina ukubwa wa hekta 2,000 na hadi sasa tumeshalima hekta 1,060 na zilizobakia ni kwa ajili ya kutunza mazingira na uoto wa asili kwenye vilima vinavyotuzunguka,” alisema.
Alisema hadi sasa wamekwishaajiri wafanyakazi 1,500 kwenye shamba hilo na kutoa mafunzo kwa wakulima wanaoishi vijiji vya jirani. “Pia tumewapatia miche ya bure kaya 673 na kutokana na mafunzo tunayowapa, wanavijiji wameweza kulima kahawa inayoendana na viwango vya kimataifa vya uzalishaji kahawa ambavyo ni miezi 22,” alisema.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu akijibu moja ya hoja kwenye risala ya Bw. Medappa iliyohusu eneo la hekta tisa kuchukuliwa na Wakala wa Ujenzi wa Barabara (TANROADS), alisema eneo hilo ni muhimu kwa ujenzi wa barabara za mkoa huo kama ambavyo shamba hilo ni muhimu kwa mkoa huo. 
“Lile eneo limetengwa na TANROADS kwa ajili ya kutengeneza kokoto za ujenzi wa barabara. Barabara za lami tunazitaka. Tunahitaji kazi hii iendelee la sivyo barabara zetu zitakufa,” alisema. 
Alisema watu wa TANROADS wakimaliza kazi yao, lile eneo litabaki tupu na mwekezaji huyo anaweza kulitumia kadri atakavyoona inafaa kwa sababu liko ndani ya eneo lake.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 3, 2015.

DKT. NCHIMBI ASEMA CCM HAINA TATIZO LA KIMUUNDO WALA MFUMO

$
0
0
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-3.jpg">http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-3.jpg
" alt="nchimbi 3" width="640" height="280" />
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe za maika 38 ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kuwa chama chake kina kila sababu ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa kina mfumo na muundo imara.
Akizungumza muda mfupi baada ya maadhimisho hayo mjini Songea, Dkt Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho alisema kuwa chama chake hakina tatizo la kimfumo wa muundo na kuongeza kuwa ushindi ni lazima.
“Chama hakina tatizo la muundo wala mfumo na tutakachofanya ni kubadilisha mikakati tu ili kujihakikishia ushindi katika uchaguzi ujao,” alisema
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-4.jpg">http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-4.jpg
" alt="nchimbi 4" width="640" height="427" />
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho.
Aliongeza, “Kwa kwa kaida hakuna mkakati unadumu. Mar a zote mikakati hubadilika kulingana na mazingira na hiki ndicho tutakachokifanya,”
Akizungumzia kuhusu kauli ya mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa chama kuwatembelea wanachama na kushawishi wanachama wapya, alisema  CCM ni chama kikubwa na ndani yake wapo viongozi waliolala ambao mwenyekiti wa taifa aliwakumbusha kuamka na kufanya kazi.
“Chama hakiwezi kuwa na maisha marefu kama viongozi katika ngazi zote ha hawajitumi. Katika jeshi kubwa kama hili la CCM wapo watu ambao lazima wasukumwe na ndiyo ahwa mwenyekiti wetu wataifa aliwasukuma kupitia hotuba yake.
Hawa wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kukiwezesha chama kushinda kwa kishindo kama ambavyo kimekuwa kikishinda tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi,” alieleza
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-2.jpg">http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-2.jpg
" alt="nchimbi 2" width="640" height="427" />
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dkt Nchimbi aliishukuru halmashauri kuu ya chama kwa kuweza kuuchagua mkoa wa Ruvuma  kwa ajili ya maazimisho ya miaka 38 ya chama hicho na kueleza kuwa kwa miaka mingi Ruvuma imekuwa ngome imara ya CCM.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa alisema kuwa chama chake kimeshaanza  kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu .
“Nimeshawaagiza viongozi wa chama katika ngazi ya mkoa na wilaya kuanza vikao kwa ajili ya na kuweka mikakati thabiti ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao,”
Alieeleza kuwa, chama katika mkoa wake tayari kilishaanza mikakati ya kujitegemeza ikiwa ni kufuata agizo la mwenyekiti wa taifa ambapo tayari kimejipanga vyema kuendeleza vyanzo vyake vya mapato pamoja na kuanzisha vyanzo vipya kwa ajili ya kukifanya kujitegemea.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-1.jpg">http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/02/nchimbi-1.jpg
" alt="nchimbi 1" width="640" height="427" />
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.


Kigoma yakumbwa na kipindipindu, watano wafariki

$
0
0


WATU watano wamekufa na wengine zaidi ya 170 wamelazwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulioukumba mkoa Kigoma.  
Akizungumza mjini Kigoma leo Mganga Mkuu wa mkoa kigoma,Leonald Subi amesema kuwa Manispaa ya Kigoma Ujiji imeathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo na kwamba tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa kukabiliana na hali hiyo.    
Subi alisema kuwa tangu mwezi Januari mwaka huu ugonjwa huo ulioanza kuripotiwa kwenye wilaya ya Kasulu na manispaa ya Kigoma Ujiji watu 175 walikuwa wamekumbwa na ugonjwa huo katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku wilaya ya Kasulu ikiwa na wagonjwa wanane. 
Alisema kuwa kwa manispaa ya kigoma Ujiji eneo lililoathiriwa ni kata ya kibirizi ambako sehemu kubwa ya wagonjwa waliougua na kufariki walitoka huko na kwamba tayari kambi ya wagonjwa wa kipindu pindu imefunguliwa kwenye kituo cha afya cha Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji. 

Washauriwa kuacha kuosha uke kwa mvuke

$
0
0

Ukiangalia  video hiyo unaweza kabisa kusema ni vyema na wewe (mke) ukapigwe na stimu mambo yaende safi, lakini hapa pana maneno yasome.

WATAALAMU wameingiza maneneo katika kampeni kubwa inayoendeshwa na Gwyneth Paltrow ya kusafisha uke kwa mvuke.
Wataalamu wamesema tabia hiyo inayopigiwa debe na muigizaji huyo si nzuri na kuna hatari ya kuharibu utaratibu wa kawaida wa uke.
Hayo yameandikwa na jarida moja la Marekani.
Katika makala yake imesema kwamba pamoja na  Gwyneth Paltrow kupigia debe shughuli hiyo na kushawishi watu wanaofika Mji wa Los Angeles kuhakikisha wanafika katika kliniki yake na kufanyiwa au kupewa maelekezo ya namna ya kusafisha uke na mvuke.
Muigizaji huyo anasema kwamba tiba yenyewe ni  nyepesi tu kwani unachofanya unakaa kwenye kiti na unaachia mchanganyiko uliomo kwenye mvuke kufanyakazi ya kutakasa sehemu zako za kizazi.
Huduma hiyo ina gharimu dola 50 lakini madaktari waliozungumza na NewsBeat wanasema hawana uhakika na usalama wala faida ya tiba hiyo.
Tikkun Spa wanasema kwamba  huduma hiyo husaidia kutibu hali mbalimbali ikiwamo ya kuhami tumbo la uzazi dhidi ya kansa na majipu.
Pamoja na maelezo hayo, wanaohusika natiba hiyo wanakiri kwamba haijatathminiwa wala kukubaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.
Pamoja na ukweli huo, madaktari wanasema kwamba uke umetengenezwa kwa namna ya kwamba unajitunza wenyewe kutokana na majimaji yeye dawa yanayotoka mwilini.
Wataalamu hao wamesema kwamba usafishaji wa uke kwa namna hiyo si lazima utafanya uwe msafi na salama.
"Utoko katika uke si lazima uwe ni dalili mbaya," anasema Dk Suzy Elneil, Mtaalamu wa ushauri wa masuala ya uke wa Hospitali ya Chuo Kikuu  cha London.
"Kuna kauli zinazoamini kwamba utoko huo unaambatana na magonjwa ya zinaa, hii si kweli." alisema na kuongeza kuwa mabadiliko katika utoko uwingi au uchache wake unaweza kuwa ni shida ya homoni  ambayo inaunganishwa kwenye mzunguko wa hedhi wa mwanamke.
Aidha matumizi ya mvuke, sabuni zinazonukia, jeli, dawa za kuua wadudu zinaweza kabisa kubadilisha  afya ya uke na mizania ya  pH.
Madaktari wanasema ni vyema wanawake wakatumia sabuni zisizo na pafyumu kusafishia sehemu ya nje  ya  na ndani ni kazi ya asili kusafisha, uke wenyewe unajisafisha kwa kutumia kemikali mbalimbali zilizopo.
"Siwezi kufikiria kwamba usafishaji wa uke kwa kutumia mvuke (kuflashi kwa maneno mengine) kunasaidia. Kwa kufanya hivyo utaondoa na bakteria muhimu wanahitajika kwa ajili ya kusafisha  na kuuliza uke," anasema Professora Ronnie Lamont wa Royal College of Obstetricians and Gynaecologists.
Wataalamu wamesema matumizi ya mvuke kama ilivyo katika matumizi mengine inaweza kuleta madhara katika uke.

Filamu kwenda 'Buku Jero' ni kizunguzungu cha ukweli

$
0
0


DESEMBA mwaka jana, mwezi ukiwa katikati kuna watu walipata bahati ya kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari ambapo moja ya wasambazaji wakubwa wa filamu nchin i Steps Entertainment walitangaza kushusha mauzo ya filamu zake kufikia buku jero yaani elfu moja na mia tano.
Katika mkutano huo walieleza sababu za kuamua kuuza filamu kwa bei hiyo.
Mwezi mmoja baadae serikali nayo ikasema zoezi lisimamishwe kwa kuwa linaonekana linaingilia kati mwenendo wa tasnia nchini.Lakini kingine kigumu sijui utakisemaje, mmoja wa wasanii machachari kabisa Steve Mengele “nyerere” amesema  sinema kwenda buku jero ni laana.
Yeye alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Kanumba The Great Fallen huko landmark Hotel.
 “Nasema tena filamu zetu kuuzwa buku Jero ni laana ya Kanumba, unafiki kutopendana ni Laana ya Adam Kuambiana, tumewaacha wenzetu waliotutangulia bila chochote,”
Msanii huyo alizidi kulalamika kuwa kuna watu waliwahi kusema kuwa yeye alikuwa chanzo cha ugomvi wa marehemu na kundi la Bongo movie lakini yeye ndio kafika katika uzinduzi lakini wale waliojifanya wema hakuna hata mmoja aliyefika katika uzinduzi wa kitabu cha Tree uliofanyika katika ukumbi wa Landmark Hotel.
Naam, hayo ndio maneno ambayo yanaweza kusababisha mazungumzo marefu na majadiliano ya kina miongoni mwa wadau wa sinema.
Wasambazaji wadogo wanaona kwamba kuuza kwa bei hii ni kuua tasnia.Lakini msambazjai huyu mkubwa anasema kwamba itasaidia sana kuondoa uharamia ambao umeshamiri sana nchini.
Pamoja na kauli hiyo kuna kauli za waziwazi kwamba moja ya wasambazaji wakubwa anafanya wizi na watu wanaukubali.

Filamu zinatengenezwaje?

Ilipoanza  Bongo Movie kama masikhara, lakini waliochochea uwapo wa hiki kitu  ni televisheni ambapo makundi ya kuigiza baadae yalijiingiza katika kutengeneza sinema ingawa hazikupendeza na kiwango lakini angalau  mbuyu wa sasa ulianza kama mchicha tu na ilikuwa kazi sana kuuza VHS kwa watu watu walikaa katika luninga kuona michezo ya kuigiza iliyokuwa inaandaliwa na kundi la Kaole.
Nakumbuka sinema za Mwanzo na nakumbuka pia majadiliano yangu  George Otieno  al maarufu kama Tyson katika filamu yake ya Girl Friend iliyozinduliwa kwa mbwembwe, nakumbuka sinema ya Kibuyu ya Hammie Rajab, sinema zilizotoa sura fulani ya ugumu wa utengenezaji wa sinema hapa nchini.
Sikuwa na shaka na sinema ya Hammie rajab kwani yeye kitaaluma alikuwa mtengeneza sinema na alishafanyakazi nyingi ambazo wakati huo niliziandikia makala mbalimbali.
Mzee Hammie sehemu kubwa ya filamu zake alitengeneza kwa kuomba fedha  na zile sinema za elimu alifanikiwa kupata fedha kwa mashirika husika na elimu anayoitoa na hivyo sinema hizo kimsingi zikabaki yeye kuwa dairekta na projuza wakati Projuza Mtendaji (mwenye hela) anabaki kama mwenye mamlaka. Kibuyu ilidhaminiwa na NSSF.
Katika miaka hiyo waliibuka wasambazaji wenye nguvu ambao pia walisambaza muziki Wananchi. Taratibu ikaja kampuni ya Steps baada ya hapo yamekuja makampuni mengine madogo yakifanya usambazaji. Na sasa zipo Sas O entertainment, Kapico Tanzania, Papazi entertainment na Pilipili Entertainment
Lakini kiukweli wakali wote unaowajua leo katika tasnia hii wanafanyakazi na Steps Entertainment. Hii ni moja ya kampuni ambayo imesaidia sana kusukuma tasnia ya filamu nchini hapa.
Kampuni hii pamoja na  kusambaza sinema , bali pia ilianza kuwa executive producer ikitoa fedha kwa skripti mbalimbali na hivyo kimantiki kumiliki sinema hizo.
Uharamia
Moja ya vitu vinavyoleta shida kubwa katika tasnia ya burudani nchini, ni uharamia wa sinema.Uharamia ni ile hali  ya  bidhaa za filamu kuwa katika soko bila ridhaa ya wahusika.
Kwangu  mimi anayelamba  hasara hii  mmiliki  wa sinema ambaye ni projuza mtendaji ambaye ndiye anayetoa hela za kufanyia kazi skripti.
Uhalifu huu unaofanyika Tanzania unatokana na sababu nyingi lakini kibaya zaidi ni kwamba sheria inayobana haki miliki bado kueleweka vyema hata kwa watengenezaji wenyewe ambao hata saundi traki zake si zao.
Juhudi zinafanyika  kuondoa hilo tatizo pamoja na uwekaji wa alama lakini mambo yanaonekana kuwa bado mabaya.

Kwangu mimi  naona hilo linatokana na uchumi wan chi na mfumo wa kuingia katika DVD moja kwa moja badala ya  DVD kuwa hatua ya mwisho baada ya thieta na kufungua duka la vitu vilivyotumika kutengeneza sinema.

Kutokana na  uchumi kuw amdogo na kwenda moja kwa moja katika DVD ni dhahrii uharamia utakuwepo kwani uwezo wa kuuza na kununua upo ndani ya raha ya watazama sinema ambao hawana nguvu kubwa kiuchumi.

Maamuzi ya Steps

Steps Entertainment Ltd ambayo ilianzishwa mwaka 2007 imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja.
Ameweza kufanya hivi kwa kuwa anatoa fedha zake kuwapa maprojuza, kununua bidhaa zao na kuzisambaza mpaka nchi za nje.
Kutokana na kukithiri kwa uharamia wa filamu za Kitanzania na kuuzwa kwa bei ya chini mno, ambapo wananchi tumeweza kuzinunua kwa wingi kutokana na kuwa ni za bei rahisi sana. Maamuzi ya Steps ya kujaribu kupunguza bei za filamu zake ili kuona kama inaweza kusaidia kupunguza uharamia wa filamu hizi kuna mantiki.
Kuna ukweli wa wazo hilo kwani kama bidhaa ya uharamia ni buku buku na ninaenda kununua kuuziwa original buku jero siwezi kuenda kwa uharamia.
Mimi ninaamini Kampuni ya Steps Entertainment ltd ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka mbali nje ya nchi zinawafikia walaji kwa bei ya chini sana .
Ikiwa tayari ina mtambo mkubwa wa kisasa wa kutengeneza cd/dvd na kuzirekodi hapa hapa nchini tofauti na siku za nyuma kupunguza bei za filamu zake ni muonekano wa kibiashara zaidi hasa ikizingatiwa kwamba  yenyewe ndiyo inayotoa fedha za kutengeneza sinema.
Manufaa yapo
Uharamia umesababisha watu kama Steps ambao wao sit u wanazingatia filamu lakini marejesho ya fedha inazowekeza kubuni njia hii.
Suala hili linaweza kuwa na manufaa kwa wanaotaka kuona sinema, na hii itataka anayeingia katika fani pia kuwa bora ili aweze kumpata anayefaa kumsambazia sinema.
Akiwa mlipaji kodi mkubwa hainipi shida kuona mantiki ya Steps na kuacha kuangalia wasambazaji wadogo wanaofikiria elfu tatu ndio malipo halali wakati tunajua sote kwamba kinyume na kiwanda cha Steps huwezi kuuza bei hiyo kluna gharama zake.
Hodhi kubwa aliyonayo Steps huwezi ukaidharau, kwani maprojuza wakubwa wapo chini yake kwa kumkubali yeye kuwa Executive Producer na kumuondoa katika biashara ni kusababisha kuyumba ikizingatiwa kwamba serikali haifanyi biashara kazi yake ni kukusanya kodi.
Shida yetu nini
Mimi nafikiri shida ya tasnia hii ni mikataba ambayo haina maslahi makubwa na waigizaji na maprojuza wao.
Hili linawezekana kwa mfumo wa mikopo kubadilika katika mabenki na kuanza kutoa fedha kwa ajili ya watengeneza sinema. Nataka kusema hali ya kumtegemea mtu mmoja nayo inaleta uwiano mbovu wa maslahi lakini wigo wa kupata fedha za kazi ukitanuka itakuwa bora zaidi.
 Kuongeza uwezo utasaidia kuwa na sinema bora yaani miradi inayotoa filamu zenye kusisimua ili makampuni yanayotengeneza sinema kuwa na uwezo zaidi wa malipo na kujiendesha.
Tatizo jingine ni watanzania kujipambanua zaidi na  DVD badala ya kwenda thieta . Theita husaidia mauzo na kama wakianza kwenda thieta kama zamani  fedha kwa wasanii wetu zitaongezeka.
Lakini ukiwa na maduka 79 pale Kariakoo na 9 tu ndio wanaouza sinema za kitanzania unahitaji mfumo unaofikiriwa na steps ili usifilisike.
mwisho

OLOLOSOKWAN WAPIGWA MSASA KUKITUMIA VYEMA KIJIJI CHA DIJITALI

$
0
0
DSC_0022

Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (aliyeipa mgongo kamera) wakati wa ukaguzi wa mwisho wa eneo la mradi wa kijiji cha digitali wa Samsung unaoendeshwa na UNESCO lilitolewa na serikali ya kijiji. Katikati ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan wilaya ya Ngorongoro, Kerry Dukunyi .(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

SHIRIKA la Elimu ,sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, limeanza maandalizi ya kuumilikisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa wananchi wa kijiji hicho kwa kuendesha warsha ya siku mbili ya kutambua vipaumbele vya wananchi vitakavyoingizwa katika mradi huo.

Vipaumbele hivyo ni katika elimu, afya na uchumi.

Warsha hiyo ilishikirikisha wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi.

Katika majadiliano yao wananchi walitambua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na mazingira na mfumo wa utamaduni walionao wakazi wa eneo hilo.

DSC_0042

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikagua eneo la mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongro. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mratibu wa miradi wa Taasisi ya Irkiramat, Salanga Mako.

Wakazi hao ambao ni wafugaji wenye kuheshimu mila na utamaduni wa kimasai na mfumo wa maisha wamesema kwamba lugha inayotumika katika kufundishia ni tatizo na ingawa wana shule mbili za msingi na sekondari lugha ya Kiswahili ni tatizo na wakifika sekondari lugha ya kiingereza nayo inakuwa tatizo.

Aidha walisema kutokana na wazazi kutokuwa na elimu hawaoni sababu ya kuwafanya watoto wao wenye maarifa makubwa kwenda shule na badala yake hao wanaoelewa vitu hupelekwa kuchunga au wale wenye umri mdogo wa kike huolewa.

Warsha hiyo pia ilibainisha tatizo la afya ya wanawake na watoto, ndoa za utotoni na magonjwa ya zinaa ya kuambukiza.

DSC_0047

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiteta jambo na ujumbe wake aliombatana nao kwenye kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya kuwapiga msasa wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni maadalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali hivi karibuni.

Kijiji hicho cha digitali ambacho ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa umma kitakuwa na huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa mifugo pekee na kutambua thamani yao katika rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Warsha hiyo ambayo imesimiwa na wataalamu kutoka UNESCO imelenga kuwafungua macho na kuwashirikisha wananchi kuhusu mradi huo mkubwa wa aina yake nchini na duniani.

Kijiji cha dijitali nchini Tanzania ni cha nne cha kwanza kikiwa nchini Afrika Kusini, kingine Gabon na Ethiopia.

DSC_0060

Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi wakimsikiliza Mkurugenzi mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani).

Kijiji hicho ili kiwe endelevu wananchi wanaohusika wanatakiwa kuelewa mradi huo kuweka vipaumbele vyao na kuangalia jinsi ya kutumia mradi huo katika kukabili changamoto zinazowakabili kwa sasa.

Katika majadiliano kwenye ngazi za elimu wananchi walielezea haja ya kushawishi wamasai kuanza kujifunza Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kufuatilia kwa karibu masomo na pia kuwepo kwa sheria ndogo ili kuzuia utoro wa wanafunzi kwa ajili ya kwenda kuchunga mifugo na pia kuolewa mapema kwa mabinti.

Mathias Herman, mratibu wa program za Afya , UNESCO, alisema kwamba pamoja na kwamba kijiji hicho kitakuwa na zahanati na huduma za mawasiliano ya tiba (telemedicine) hamasa kubwa inatakiwa kutolewa ili wananchi waweze kutumia huduma hizo kwani kwa sasa wamejikita zaidi huduma za waganga wa jadi.

DSC_0066

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendesha mjadala kwa wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi ikiwa ni maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Alisema katika warsha kulielezwa kuwa kukosekana kwa madaktari katika zahanati zilizopo kijijini hapo kumefanya watu wengi kuendelea kuamini waganga wa jadi na kujifungulia huko hali ambayo imezaa kuwapo kwa idadi kubwa ya wanawake wanaokufa wakati wa uzazi na pia watoto wasiopata chanjo.

“Wakifika hakuna madaktari hawawezi kuamini huduma hii wakati kuna waganga wa kienyeji na wakunga wa kienyeji” alisema Mathias na kuongeza kuwa katika warsha ilihimizwa kwamba watu watambue tatizo lililopo la kiafya linalosababishwa na mfumo wa mazingira na maisha ya wafugaji na kuhakikisha kwamba huduma zinazoletwa zinatumiwa vyema.

Aidha alisema kuwapo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ndoa za utotoni na mimba katika umri mdogo ni sehemu ya matatizo ambayo yanaaminika kwamba yanaweza kutanzuliwa kwa kutolewa elimu na kushawishi wakubwa wa mila kutambua nafasi zao na elimu ya kisasa katika kushughulikia changamoto za kiafya.

DSC_0095

Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) akiwa kwenye majadiliano na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla katika kijiji hicho na kuishirikisha halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.

“mila na heshima kwa wakubwa wa mila kumefanya wamasai kutegemea tiba za asili na mfumo wa asili wa kuendesha maisha bila kujua athari kwao ziwe hasi au chanya” alisema Mathias kauli iliyoungwa mkono na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues ambaye alisema kunahitajika sana ushirikiano wa jamii, viongozi, wazazi kuhakikisha kwamba kijiji kinafanikiwa na kuwa cha kupigiwa mfano.

Kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kikiwa na watu 9000 kupitia mradi huo kitapewa pia mbinu za kuimarisha soko la utalii, kulitambua na kulitumia kwa manufaa yao na pia elimu ya ubunifu ambayo itawafanya wanawake wanaotengeneza urembo mbalimbali kuweza kumudu soko la utalii na la kawaida.

DSC_0103

Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mjadala na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana mradi wa kijiji cha kidigitali na kuuboresha ili kutatua matatizo ya wananchi pamoja na kuwapata taarifa za maendeleo kupitia redio jamii ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni katika maandalizi ya kuupokea mradi huo wa kijiji hicho unaotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.

Aidha mradi huo utafikisha umeme na elimu kwa njia ya Tehama huku, elimu hiyo ya Tehama ikikusudiwa kutumika kutoa elimu ya darasani kwa wanafunzi ambao wapo machungani.

Mfumo wa wamasai ambao umejengwa katika utamaduni na kuthamini mifugo unatakiwa kubadilishwa kwa wazazi kupewa elimu ya kuwawezesha kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao.

DSC_0163

DSC_0145

Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akiongoza mjadala wa nini kifanyike katika kuboresha sekta ya afya na changamoto zinazowakabili wanakijiji wa Ololosokwan kwa ajili ya maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha Kidigitali unaoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijijini hapo. Wa pili kushoto ni Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia.

DSC_0226

Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akiwasilisha kazi ya kikundi chake baada ya kujadiliana na wanakijiji wa Ololosokwan katika kuboresha sekta ya elimu ikiwa ni maandali ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali kinachotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.

DSC_0124

Mmoja wa washiriki wa kikundi kilichokuwa kikijadili masuala ya utamaduni na utalii akiandika changamato mbalimbali zinazowakabili wakinamama wakimasai wanaofanya biashara za urembo wa kimasai kwa watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro.

DSC_0089

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akishiriki kwenye mjadala na wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijiji hapo.

DSC_0231

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini mkataba wa kukabidhiwa ardhi iliyotolewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya mradi wa kijiji cha kidigitali huku tukio hilo likishishudiwa na uongozi wa juu wa serikali ya kijiji, wataalam kutoka UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wanakijiji.

WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA SENSA YA VIWANDA.

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya NBS na wadadisi wa Sensa ya Viwanda



SERIKALI imewataka wamiliki wa viwanda kuwapa ushirikiano wadadisi wa Sensa ya Viwanda watakaopita katika maeneo yao kwa lengo la kukusanya takwimu sahihi za viwanda  vilivyopo nchini na mchango vinaotoa katika maendeleo ya taifa.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14 ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda yanayoendelea katika chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa mafanikio ya Sensa hiyo yatatokana na wamiliki wa viwanda kuthamini na kutambua umuhimu za Sensa hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaopita katika maeneo yao kupata taarifa zinazohusu masuala mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa bidhaa na masuala ya ajira;

Amesema upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Sekta ya Viwanda nchini Tanzania utaiwezesha Serikali kuweka Sera na mipango endelevu ya maendeleo itakayoisaidia sekta hiyo kupiga hatua kimaendeleo.

“Sensa hii ya viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, na mafanikio yake yatatokana na wenye viwanda kutupa ushirikiano maana bila  wao kutoa takwimu sahihi mipango ya maendeleo kuhusu viwanda haitatekelezeka kwa sababu ya kukosa takwimu sahihi” Amesema Bilia.

Kuhusu sampuli ya viwanda  vitakayoguswa na Sensa hiyo amesema  ni pamoja na maeneo ya viwanda yaliyoajiri watu wengi  na yanayohusisha uzalishaji mkubwa wa bidhaa za viwandani ,maeneo ya uzalishaji wa bidhaa za kokoto, bidhaa za vyakula na maeneo yaliyoajiri mtu zaidi ya mmoja.

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda itayofanyika nchi nzima  mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.

Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na wadadisi watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema kuwa Sensa hiyo ya viwanda itakayohusisha viwanda vyote nchini inafanywa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Amesema kukamilika kwa Sensa hiyo kutaliwezesha taifa kuwa na takwimu sahihi za viwanda na kutambua mchango wa Sekta ya viwanda katika uchumi wa taifa na mchango wa ajira kwa wananchi.

Kuhusu mafunzo hayo ya siku 14 kwa wadadisi 200 watakaoendesha zoezi hilo amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika inaendesha mafunzo hayo kwa vitendo na nadharia ili kuwawezesha na kuwajengea uwezo wadadisi hao kukusanya takwimu bora.

“Lengo la kuendesha Sensa hii  ni kuhakikisha kuwa nchi yetu inapiga hatua na kuwa nchi yenye maendeleo ya kati kwa kuwa na matumizi sahihi ya takwimu ztu”

Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein Kamote akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya wamiliki wa Viwanda nchini amesema kuwa Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini mwezi huu italiwezesha taifa  kuwa na takwimu sahihi zinazohusu sekta ya viwanda.

“Sensa hii ya viwanda ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa nawaomba wenye viwanda watoe ushirikiano wa kutosha maana bila wao zoezi hili litakuwa gumu”

Ameongeza kuwa Sensa ya viwanda ni muhimu kutokana na mchango wake katika nchi nyingi za Asia ambazo zimefanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo kwa sababu ya kuwa Sensa endelevu na takwimu sahihi za sekta ya viwanda na mchango wake katika pato la taifa.

Source: Aron Msigwa – MAELEZO

ELEPHANT LIVE COMES WITH THAIS DIARRA IN CONCERTS

$
0
0
RainMaker Ltd and Culture Connect cordially invite you to Thais Diarra’s inaugural performance in Kenya. Although distinctively afro-soul, her music is a melange of styles, ranging from reggae, mbalax and mandingue music.
The live concert will take place on the 6th of February, featuring Thais on guitar and vocals. Her melodic voice reminscinent of other nu-soul greats, will definitely soothe the week’s sorrows away.

BREAKING NEWS! ASKARI AUAWA AKIKAMATA MSHTAKIWA

$
0
0


Askari polisi ameuawa leo asubuhi katika maeneo ya Chang’ombe manispaa ya Dodoma wakati akikamata mtuhumiwa. Habari zaidi baadae
 

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA SHERIA NCHINI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za Siku ya Sheria
nchini katika viwanja wa Mahakama barabara ya Chimala jijini Dar es
salaam leo February 4, 2015





MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD

$
0
0
DSC_0100 

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Andrew Chale

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.

Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.

“Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.

DSC_0239

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.

Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.

DSC_0140

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

“Ofa hii ni kwa ajili ya kipindi hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo michuano hii itakapofikia tamati ambapo bei itabadilika kutoka hizi za sasa, hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara ya kwanza, kupata kitu cha ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.” Alisema Furaha Samalu.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alieleza kuwa, siku zote MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma zilizo bora na za kisasa katika ulimwengu huu wa digitali ambapo bidhaa hizo za DStv zimeendelea kuwa bora kila siku.

“Huduma za DStv siku zote zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta usumbufu. Ving’amuzi vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na hutoweza kusumbuliwa na ukatikaji wa picha ama mikwaruzo... Hivyo ni wakati sasa wa kuchangamkia ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.

DSC_0194

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za king'amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya Tsh. 99,000/ kuanzia leo hadi siku Jumapili kilele cha fainali za michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa gharama ya Tshs. 39,000/ ambayo pia ni ofa. Ving'amuzi hivyo vipya vya DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.

Katika hatua nyingine, DStv wamezindua huduma mpya kwa wateja wao waliounganishwa na ving’amuzi hivyo vya DStv kuweza kuendelea kufurahia huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’, Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet, na vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea usajili wa ‘App’.

Akielezea, juu ya huduma hiyo, Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama Tablet na kisha kujisajili kupitia ‘App’ kwa kujisajili kwa kuandika ‘DStv Now’.

Aidha, Ronald Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya DStv Now ni kwa wateja waliouganishwa na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.

Pia kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti ya DStv.com

DSC_0209

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma mpya ya DStv Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia simu yake ya kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet. Huduma hii ni kwa wateja ambao wameunganishwa na ving'amuzi vya DStv kupitia akaunti zao.

DSC_0225

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia promo ya namna ya kujiunga na huduma ya DStv Now "application" inayopatikana katika simu zote za Android pamoja na kompyuta mpakato (Laptop) unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com

DSC_0228

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.

DSC_0247

Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na king'amuzi kipya cha DStv HD.

Kamanda Misime aeleza kilichomuua askari wake

$
0
0


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, David Misime  ameeleza kisa cha askari wake kuuawa leo asubuhi katika eneo la Chang’ombe Juu manispaa ya Dodoma.
Mchana blogu hii iliwaletea breaking news ya askari kuuawa na kuahidi kukamilisha breking news hiyo baadae leo kwa kuzungumza na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma. Hata hivyo kamanda huyo aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo.
Kamanda Misime alisema kwamba askari huyo huyo mwenye namba  G.7168 Joseph Swai aliuawa kwa mapanga na Tisi Sirili Malya wakati akijaribu kumuokoa mtoto wa miaka minane.
Akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari Kamanda Misime alisema askari huyo alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa Chang'ombe Juu akimjulisha kuwa amepokea taarifa Ofisini kwake kutoka kwa Oliver Baltazar (52) mkazi wa Chang'ombe juu kuwa mtoto wake aitwaye Tisi Sirili anaonekana anataka kumuua au ameshamuua mtoto wake wake wa miezi minane Valerian Tisi .
Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo askari huyo alienda Ofisini kwa Mtendaji huyo ambapo waliongozana hadi nyumbani kwa mtuhumiwa.
 
Pc swai enzi za uhai wake
Alisema alipofika askari huyo aligonga mlango huku akijitambulisha kuwa yeye ni askari ili mtuhumiwa atoke nje,lakini alichofanya mtuhumiwa ni kumnyanyua mtoto wake mdogo wa miezi minane kwa mkono mmoja kichwa chini miguu juu na kutaka kumkata kwa panga.
Kamanda Misime alisema kwamba askari aliamua kumuokoa mtoto huyo kwa kumrukia mtuhumiwa lakini kwa bahati mbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani .
Aidha alisema  muuaji huyo aliendelea kumkatakata kwa panga huku Mtendaji na kijana waliyekwenda naye katika eneo la tukio,wakimbia huku wakipiga kelele za kuomba msaada .
Alisema,mtuhumiwa Baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama,alikimbia akiwa na panga lake huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu .
Aidha alisema kwamba katika hekaheka hizo mama wa mtoto baada ya kuona mtoto amebwagwa na askari alimeanguka  chini ,naye alimkwapua mtoto na kukimbia naye mahali pasipojulikana.
Amesema polisi wanamsaka  baba huyo na mama huyo  kwa ajili ya usalama wake.
Askari huyu muda mfupi kabla ya tukio hili alikuwa ametokea katika kituo cha Redio cha Dodoma FM kwa ajili ya kuandaa kipindi cha kuielimisha jamii juu ya ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) tunapoelekea kipindi cha uchaguzi, kwani mbali na kazi anazofanya mojawapo ni kushiriki katika vipindi vya kutoa elimu ya Polisi Jamii hapa mkoani Dodoma.
          Msako bado unaendelea ili kuweza kumtia nguvuni mtuhumiwa huyu aliyesababisha kifo cha askari wetu wakati alipojitolea maisha ya ili kumwokoa huyo mtoto mdogo.
          Kamanda Misime amesema Malya mwenye umri wa miaka 29 ni na kwa kabila mchaga ni maji ya kunde, mwembamba, siyo mrefu sana saizi ya kati  na alikuwa amevaa suruali rangi ya blue iliyopauka na T-Shirt rangi ya dark blue na kofia nyeupe yenye alama nyekundu .

Filamu mpya ya Vanilla yaingia sokoni

$
0
0


 
Moja ya aksheni ndani ya Vanilla

WADAU wa sanaa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya wameombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa filamu mkoani hapa kwa kununua kazi zinazofanywa na kuacha kasumba kuwa filamu bora zinaweza kutengenezwa na wasanii walioko Dar es salaam pekee. 
Mwongozaji wa filamu wa kampuni ya Pritauj Filim Prince Hekela alitoa rai hiyo jana alipokuwa akitambulisha Filamu mpya ya Vanilla iliyochezwa na wasanii kutoka mkoani Mbeya. 
Prince Hekela alisema kumekuwa na kasumba ya baadhi ya wadau kuamini filamu nzuri ni zile zinazochezwa na wasanii wa Dar es salaam jambo alilosema limekuwa likididimiza sana wasanii wa mikoani. 
Alisema ni wakati kwa wadau hao kutambua kuwa ubora wa filamu hautokanani na mahali anakofanyia kazi zake msanii,bali umakini na maandalizo bora ndiyo msingi wa kutengenezwa kwa filamu bora. 
Akizungumzia filamu ya Vanila aliyosema tayari imeingizwa sokoni,alisema imeandaliwa katika mazingira yenye kuzingatia staha hivyo haina vipande vyenye kuonesha aibu kiasi cha familia kushindwa kuitazama kwa pamoja. 
“Vanilla ni filamu ambayo hata ukienda kuonesha uwanjani hakuna kinachozuia.Kwa nyumbani hata awepo baba mama na watoto wanaweza kuiangalia kwa pamoja.Na ina mafundisho ya kila mtu kulinagana na umri wake” 
“Muhimu pia wadau watambue kuwa tumejipanga kuhakikisha tunaleta burudani nzuri kutokana na filamu zetu.Ndiyo sababu hata katika Vanila utaona tumechanganya wasanii wapya na wa zamani.Wasanii wapya ambao wamefanya vizuri sana katika filamu hii ni pamoja na Issa Ngoda,Regina Mwinyi, Kelvin Kaziyandege na Joachim Nyambo.Lakini pia tumemshirikisha mwanadada Riyama Ally ambaye ni mkongwe katika sanaa” alisisitiza Hekela. 
Kwa upande wake mmoja wa wasanii waliocheza filamu ya Vanila Joachim Nyambo alisisitiza kuwa filamu hiyo imekuja kuwadhihirishia wadau kuwa kazi nzuri ya sanaa inaweza pia kufanyika mikoani. 
Nyambo aliwasihi wadau kuendelea kushirikiana na wasanii mikoani wanaoonekana kukuza sanaa kwa kuwa michango ya hali na mali ili kuwezesha kukua kwa sanaa. 

Mke (50) amuua mume (72) kwa mchi

$
0
0



Clemencia Nowa (50) mkazi wa kijiji cha Nampako kata ya Miangalua wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe  Stephen Shauri (72) kwa kutumia mtwangio kutokana na wivu wa mapenzi.
Akithibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa mwanamke huyo alitenda kosa hilo alfajiri Februari 4, 2015 nyumbani kwa wanandoa hao mara baada ya kutokea kutokuelewana baina ya wanandoa hao kulikosababishwa na tabia ya mumewe kuchelewa kurudi nyumbani kwake.
Alisema  Clemencia alipokuwa akijibizana na mumewe Stephen Shauri (72) alichukua mtwangio wa mahindi uliokuwepo jirani yake na kumtwanga mumewe kichwani na kwa bahati mbaya mume alifariki dunia papo hapo.
Kamanda Mwaruanda alisema tayari mama huyo amekamatwa na anaendelea kuhojiwa ambapo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilisha taratibu za kiupelelezi.
Kamanda Mwaruanda ametoa wito kwa wananchi kuwa na tabia ya kuepuka hasira pindi inapotokea kutokuelewana kwa baina ya wanajamii na badala yake wawe na utaratibu wa mazungumzo ya kifamilia, kiukoo na hata kwenye mabaraza ya usuluhishi ili kuepuka mauaji yasiyo ya lazima.
“Kimsingi hawa ni watu wazima, mama ana miaka 50 na baba ana miaka 72 hatuwezi kusema ni akili za ujana au jazba za ujana, hapana kutakuwa na tatizo ambalo lingeisha kwa mazungumzo, nawaomba wengine wanapokuwa na utofauti wazungumze kwanza” alisema Mwaruanda.
Source:  Willy Sumia


Viewing all 9183 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>