Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9292

kamandi ya anga JWTZ yaanza mazoezi

$
0
0


Kamandi ya Jeshi la Anga limeanza mazoezi ya pamoja na mataifa mengine ili kuwaongezea Maafisa na Askari wake weledi katika utendaji wao.

Hayo yalielezwa leo na Mkuu wa Kamandi ya nchi Kavu, Meja Jenerali, Salum Kijuu wakati akifungua  maadhimisho ya siku ya Kamandi ya
Jeshi la Anga yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ndege wa jiji Mwanza ambalo linafikisha miaka 32 tangu kuanzishwa kwake.

“Bila shaka huu ni mwanzo wa Kamandi yetu kuanza kuhusishwa katika majukumu makubwa zaidi ya Kimataifa, hivyo maafisa na Askari mnapaswa kujiandaa kisaikolojia katika majukumu hayo yatakapotokea,” alisema.

Alisema mafunzo ndio uti wa mgongo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambayo huwaweka Maafisa na Askari katika hali ya utayari.


Aidha aliikumbusha Kamandi ya jeshi la Anga kuwa wana wajibu wa kuzifanyia ukaguzi wa mara kwa mara silaha na vifaa vingine kwani hivi sasa wengi wao hawazingatii taratibu za kiutendaji za kila siku vikosini.

Alisema silaha na zana mpya zilizonunuliwa zimeligharimu Taifa fedha nyingi za kigeni hivyo ni jukumu la Makamanda wa ngazi ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa silaha na zana hizo
ili zidumu kwa muda mrefu katika ulinzi wa Taifa.

Naye mkuu wa kamandi ya anga Jenerali, Joseph Kapwani akizungumzia changamoto kwenye Kamandi hiyo, alisema huhitaji gharama kubwa katika kutekeleza majukumu yake.
Akitolea mfano alisema mruko mmoja wa angani huhitaji lita takribani 30,000 za mafuta na uzoefu unaonyesha mafunzo hutumia miruko miwili hadi mitatu kwa siku.
Kamandi ya anga ni mojawapo ya vijenzi vya JWTZ na jukumu lake la msingi ni kujenga AIRPOWER katika kuhakikisha hali ya anga inakuwa shwari na salama kwa ajili ya utendaji kivita wa Jeshi zima.

Majukumu mengine ya Kamandi hii ni kama ifuatavyo:

1.  Kutoa msaada wa kimapigano kwa operesheni za Majeshi ya Nchi Kavu (Army) na Majini (Navy).

2.  Kutoa ulinzi wa anga kwa maeneo muhimu ya Kitaifa, Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii.

3.  Kutoa ulinzi wa anga kwa maeneo na vituo muhimu kijeshi na mkusanyiko wa majeshi.

4.  Kutoa msaada kwa mamlaka za kiraia hasa nyakati za maafa ya kitaifa pamoja na utafutaji na uokoaji ‘search and rescue’.

5.  Kusindikiza ndege za viongozi.

6.  Kukusanya taarifa za kiusalama.

7.  Kuendeleza juhudi za mahusiano ya kijeshi na nchi nyingine (Defence diplomacy) kwa ajili ya mazoezi ya pamoja.

8.  Kushiriki katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

 Kamandi hii ambayo ipo chini ya Meja Jenerali Festo Ulomi imeendelea kutimiza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa
 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9292

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>