Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9300

HOSPITALI YA IMTU YAFUNGIWA KWA KUKOSA VIWANGO

$
0
0


Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) inayomilikiwa Chuo cha Udaktari kinachohusishwa na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya takataka, imefungiwa kwa muda usiojulikana baada ya kugundulika kutokidhi viwango na maadili ya utoaji huduma za hospitali nchini.
Taarifa iliyosikika TBC 1 inasema kwamba kufungwa huko kumefanywa na Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza na kubaini uwepo wa mapungufu kadhaa.
Mapungufu yaliyobainika kuwepo katika hospitali hiyo ni pamoja na kutokuwa na wauguzi wa kutosha, kutokuwa na vifaa vya kutosha ikiwemo kifaa cha kuchomea taka ngumu, kuchanganya dawa zilizokwisha muda na ambazo hazijaisha muda wake na pia wauguzi kufanya kazi ambazo si za kwao.
Akizungumza wakati wa kufunga hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk Gunini Kamba alisema, hospitali hiyo inastahili kufungiwa kutokana na kutokidhi viwango hivyo.
"Baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza tumebaini kuwepo kwa mapungufu haya, kwa hiyo tunaifungia hospitali hii mpaka pale watakaporekebisha," alisema Dk Kamba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Profesa Yassin Mgonda alikiri kuwepo kwa mapungufu hayo ambayo aliahidi kuyafanyia kazi.
Hata hivyo Profesa Mgonda aliiomba Manispaa na Wizara ya Afya kuangalia adhabu hiyo waliyoitoa .


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9300

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>