Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9109

FILAMU YA JAMILA NA PETE YA AJABU

$
0
0

Filamu inayotazamwa
kwa raha za familia


KAMA kuna ukatili wanadamu huufanya kwa wenzao basi unaweza kuusoma katika sinema hii. Kama kuna dhiki katika maisha  basi unaweza kuyasoma katika filamu hii na kama una kiu ya mambo mema unaweza pia kuyasoma katika filamu hii ambayo huenda ikabadili jina la Haji Adam kutoka baba Haji hadi Baba Jamila.

Naam Jamila na Pete ya Ajabu ni kazi moja ya kazi za Big One Entertainment ambazo zimemshirikisha Haji Adam al maarufu kama Baba Haj na kufanya jumla ya filamu alizocheza mwaka huu kufikia nne. Filamu nyingine ni Kwanini Mama, Who is My Child na Kitendawili.

Katika filamu hii mtoto, Sophia Michael, ambaye ameigiza nafasi ya Jamila ameweza kufanya vyema na kwa karibu mtu wa grafiki alijitahidi ingawa katika kufutafuta vitu fulani alizidisha sana na sisi wengine tunaona kama anafutafuta  vile.

Kazi kubwa iliyofanywa na Adam ni ule ubaba ambao ameushiriki kwa njia moja hadi nyingine mpaka alipogundua uhusiano wake na Chokoraa aliyempeleka pale nyumbani kwake,Jamila.

Simulizi la filamu hii pamoja na kushindwa kuwaonya watu kuhusu uchukuaji wa watoto bila kuangalia sheria na kukaa nao bila kutazama DNA ni filamu linalofurahisha kwa msingi wa kwamba Sophgia amefanya vyema katika filamu na hasa alivyokuwa anajiamini na anavyofikisha hisia zake mwanzo akiwa amekata tamaa na wakati alipopata pete yake.

Ushiriki wa Benny Branco  umefanya  sinema hii kuwa na watu wanaojua kazi zao na kubaki kazi ya Dairekta kuifanikisha sinema hiyo ambayo mimi kimsingi ukiachia vitu flani naona kama amefanikisha.

Baba Jamila, bwana Jabir ana historia katika kumpata mtoto huyu. Mtoto Jamila alizaliwa kutoka kwa mama mfanyakazi wa ndani kwa akina Jabir. Alipachikwa mimba bila ridhaa yake na kisha kuondoka kwa namna isiyofaa. Mama huyu alihangaika sana lakini baadae aligongwa na kufa na mtoto Jamila kuwa chokoraa.

Pamoja na kukimbia nyumbani akiwa na mimba ya Jabir alijifungua salama akazaliwa Jamila, mtoto akakosa malezi ya baba na mama akawa chokoraa na kisha mama naye akaaga dunia.

Katika uchokoraa siku moja Jamila alipata mkate na wenzake wakata kumnyang'anya akakimbilia gari moja lililokuwa wazi na bahati nzuri lilikuwa gari la Jabir lililokuwa limewekwa kwa haraka wakati Jabir mwenyewe akiingia duka la dawa.

Jabir aliingia ndani ya gari na akitaka kuondoka akamuona binti yule na kumuuliza maswali mfululizo kuhusu yeye na akaona kwamba mtoto yule ni chokoraa na hata bila kulipeleka shauri hilo kwa polisi au maafisa ustawi wa jamii alimfikisha mtoto nyumbani na kumwambia mkewe kwamba atakuwepo hapo na kuishi na wenzake.

Jabir alikuwa ameoa lakini ingawa walikuwa hawajapata mtoto, mama yule aliyekuja kuishi naye alifika na watoto wake. Mama yule alikuwa amemuua mume wake.

Pamoja na nia njema ya Bw. Jabir wa kumsaidia mtoto ambaye hakika ilikuwa damu yake bila mwenyewe kujua akidhani kwamba anamsaidia mtu wa kawaida, mama mwenye nyumba alimchukia mtoto yule akimrundikia kazi zote pamoja na kumnyanyasa.

Mama yule alihakikisha kwamba anamtesa na kumdhalilisha mtoto yule pamoja na kumzuia kwenda shule.

Baada ya kuulizwa mara kwamara mama yule alienda kwa mganga kuimarisha uwezo wake na kumwondolea mbali mtoto yule ndipo alipoambiwa na mpiga falaki kwamba yule mtoto ni mtoto wa Jabir ila mwenyewe hajajua. Ndipo mama alipozidisha chuki kwa mtoto yule.

Kwa sababu Mungu hutunza watu wake alileta uwezo kwa Jamila katika mfumo wa pete, akarahisisha kila kitu. Mama akimtuma mtoto yule kazi za hovyo ili asiende shule, pete inamsaidia kufanya kila kitu na kumfikisha shule. Pamoja na  kumchukia zaidi baada ya taarifa ya mpiga falaki bado hakuweza kumdhuru mtoto yule.

Mtoto mwishoni  mwa siku alitaka pete imwadhibu mama yule na kumlazimisha kusema kweli ndipo Jabir alipojua ukweli na akamtimua mjama yule ambaye alikuw andio chanzo cha matatizo.

Nimekata maneno ili uone ladha yake kidogo. Lakini kwa mwaka huu ni moja ya filamu nzuri alizocheza Adam katika safari yake ya kuigiza sinema na ikiwa miezi michache tu baada ya kutwaa diploma chuo cha sanaa Bagamoyo.

Laini ambayo niliipenda ni ile ya Sophia aliyozungumzia kuhusu ... kumbe hamnipendi... na kipande kinachoudhi ni pale alipokuwa anafokewa na mama yake huyo kwa Jabir. Filamu hii  bado inasomeka kwa watoto, inaweza kuangaliwa kwa familia.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9109

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>