Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9109

TUZO ya Golden Lion Tamasha la venice yaenda kwa Mswidi

$
0
0


TUZO ya Golden Lion katika tamasha la venice mwaka huu ambalo ni tamasha la 71, imeenda kwa Mtengeneza sinema (dairekta) wa Kiswidishi, Roy Andersson kupitia sinema yake ya A Pigeon Sat on a Branch Reflecting on Existence.
Majaji wamesema katika maamuzi yaio kwamba ilikuwa ni sinema bora kabisa.
Sinema hiyo inaelezwa kuvuti kutokana na kuangalia kw aundani nini maana ya kuwa binadamu.
Andersson alisema akipokea tuzo hiyo kwamba alikuwa amefurahishwa sana na dairekta wa kitaliano Vittorio De Sica na sinema yake ya mwaka 1948 ya Bicycle Thieves.
Sinema ambayo ilifikiriwa sana kwamba ndioyo itakayotwaa tuzo ya Golden lion ya Joshua Oppenheimer, The Look of Silence  ilipata tuzo ya majaji.
Muigizaji wa Marekani, Adam Driver alipata tuzo ya muigizaji bora kwa kazi aliyoifanya katika sinema ya Saverio Costanzo inayogusa simulizi za New-York ya Hungry Hearts akicheza kama baba anayejaribu kumuokoa motto wake.
Muigizaji wa kike wa Kiitalia, Alba Rohrwacher  alipata tuzo ya muigizaji bora wa kike kutokana na kazi aliyoifanya katika sinema hiyo hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9109

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>