Taarifa kwa vyombo vya habari
Yah:- kusogezwa kwa tarehe ya mashindano ya ngumi ya taifa 2014
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limesogeza tarehe ya kufanyika kwa mashindano ya ngumi ya Taifa na sasa yatafanyika kuanzia tarehe
03-08/11/2014.Dar es salaam.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe
08-14/10/2014 Dar es salaam.
Sababu za kusogeza mashindano hayo ni kuyapisha mashindano ya ngumi ya kimataifa yaliyoandaliwa na chama cha ngumi wilaya ya Temeke yanayotarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, lakini pia ni kutoa nafasi zaidi kwa mikoa ili kujiandaa vizuri na kufanya mashindano ya kuwapata wawakilishi wa mikoa yao katika mashindano ya taifa.
BFT tunawataki maandalizi mema na tunatoa wito kwa maafisa michezo wa mikoa yote ya Tanzania bara kuhakikisha wanaleta wachezaji kutoka katika mikoa yao ili kuleta upinzani utakaopelekea kupata timu ya taifa iliyo bora kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara.
Aidha BFT inawapongeza kampuni ya simu za mkononi ya Z antel kwa udhamini wa mashindano hayo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 10,000,000/=ambazo zitasaidia baadhi ya mahitaji ya msingi ya kufanikisha mashindano hayo.
Natanguliza shukrani.