injinia Dkt Peter A. Mokiwa
Katibu mkuu wizara ya Maji , anasikitika kutangaza kifo cha Injinia Dkt. Peter A.Mokiwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Mjini Dodoma ( DUWASA) kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 12 Sept, 2014 katika hosipitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Habari ziwafikie Wafanyakazi wote Secta ya Maji, Ndugu Jamaa na Marafiki popote pale walipo.
Msiba uko nyumbani kwa Marehemu eneo la Kilimani mjini Dodoma na mazishi yatafanyika kijijini kwao Mgombezi Wilayani Korongwe Tanga , siku ya Jumatatu ya tarehe 15.09.2014.
“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”.
Amina
WASIFU WA MAREHEMU INJ. DKT. PETER ANDREW MOKIWA
1. KUZALIWA
Marehemu Inj. Dkt. Peter A. Mokiwa alizaliwa tarehe 27/12/1952 katika kijiji cha Mgombezi, tarafa ya Mgombezi, wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.
2. ELIMU
Marehemu Inj. Dkt. Peter A. Mokiwa alipata elimu ya sekondari ya kidato cha I-IV katika shule ya Ufundi ya Sekondari ya Tanga mwezi Januari mwaka 1969 hadi mwezi Oktoba mwaka 1972.
Kwa upande wa elimu ya kidato cha V-VI, marehemu Inj. Dkt. Peter A. Mokiwa alisoma katika shule ya Mkwawa mwezi Machi mwaka 1973 mpaka mwezi Oktoba mwaka 1974.
Mwezi Agosti mwaka 1975 hadi mwezi Juni mwaka 1979, marehemu Inj. Dkt. Mokiwa alisomea na kupata shahada ya uhandisi ya masuala ya ujenzi katika Chuo Kikuu cha Roorkee nchini India.
Mwezi Septemba mwaka 1981 hadi mwezi Oktoba 1982 alipata “Postgraduate Diploma”, ya masuala ya Hydraulics and Environmental Engineering katika Chuo cha UNESCO-IHE Institute for Water Education, Delft, The Netherlands.
Mwezi Septemba mwaka 1985 hadi mwezi Oktoba mwaka 1985, marehemu Inj. Dkt. Mokiwa alihudhuria kozi ya Water Resources Assessment and Development na kupata cheti katika Chuo cha Sophia Antipolsi kilichoko Ufaransa.
Mwezi Juni 1991 hadi mwezi Juni 1992, marehemu Inj. Dkt. Mokiwa alihudhuria kozi ya Organization Management and Human Resources
Development na kupata cheti katika Chuo Kikuu cha Texas (Hurbert Humphrey Fellowship) kilichoko Marekani.
Mwaka 2009 hadi mwaka 2013, marehemu Inj. Dkt. Mokiwa alihitimu Shahada ya juu ya Uzamivu ya Masuala ya Rasilimali Watu katika Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira yaani Doctor of Philosophy (PhD) in Human Resources Mangement in Water Supply and Sanitation Authorities katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na alitakiwa kuhudhurishwa (graduate) mwezi Oktoba mwaka 2014.
Aidha, marehemu Inj. Dkt. Mokiwa amehudhuria mafunzo mbalimbali ya masuala ya fedha, utawala na uongozi ndani na nje ya nchi. Kwa watumishi wengi nchini na hasa wale wa sekta ya maji watamkumbuka marehemu Inj. Dkt. Mokiwa kama Mwalimu, Mlezi na Kiongozi.
3. AJIRA NA UZOEFU WA KAZI
Kuanzia mwezi Juni mwaka 1979 hadi mwezi Septemba mwaka 1981,marehemu aliajiriwa na kufanya kazi Wizara ya Maji, Nishati na Madini kama Mhandisi Mkazi kwenye mradi wa maji wa Mwamashimba mkoani Mwanza.
Mwaka 1982 hadi mwaka 1984 alifanya kazi kama Mhandisi wa Ujenzi wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini.
Mwezi Machi 1984 hadi mwezi Machi 1988, alifanya kazi kama Mhandisi wa Ujenzi wa Kanda wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini kwa mikoa ya
Mwanza, Tabora, Shinyanga, Mara na Kagera.
Mwezi Machi 1988 hadi mwezi oktoba 1992 alifanya kazi kama Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Lindi.
Mwezi Oktoba 1992 hadi mwezi Juni 1998 alifanya kazi kama Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Pwani.
Mwezi Juni 1998 mpaka sasa amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA). Marehemu
atakumbukwa sana kwa mafanikio aliyoyaleta DUWASA kwa kushirikiana na WanaDUWASA kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
Kuiwezesha DUWASA kuondokana na tatizo la huduma ya maji nakuwa na huduma ya maji nzuri yenye wastani wa saa 24 kwa siku.
Kuiwezesha DUWASA kupanda daraja kutoka C hadi A bila kupitia B mwezi Julai mwaka 2003.
Kuwezesha Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya uhakika ya maji kuanzia hatua ya ujenzi hadi uendeshaji na kuwa na huduma ya
uhakika ya uondoshaji wa majitaka kwenye maeneo yote ya chuo.
Kusimamia mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya majisafi uliokamilika mwaka 2003 ambao ulifadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China.
Kusimamia mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya majisafi unaogharamiwa na Serikali ya Tanzania kupitia mkopo wenye masharti
nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Januari 2015.
Kuunganisha WanaDUWASA wote na Wadau kwa manufaa ya huduma kwa wananchi.
Marehemu Inj. Dkt. Mokiwa amesimamia na kufanya kazi mbalimbali za uhandisi na ujenzi kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo: jengo la
ghorofa moja la Mwenge Engineering Unit, mradi wa maji wa Mwamashimba
– Mwanza, mradi wa maji wa Liwayawaya Lindi, mradi wa maji wa Wami-Ruvu ambao unahudumia maeneo ya Mbwewe, Miono, Msata, Lugoba na Chalinze mjini.
4. VYAMA VYA KITAALUMA NA VYA KIJAMII
Marehemu Inj. Dkt. Mokiwa alikuwa mwanachama wa vyama vya kitaaluma na vya kijamii kama ifuatavyo:
• American Society of Civil Engineers (MASCE).
• Mhandisi namba 448 aliyesajiriwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB).
• Mhandisi namba 1206 wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (MIET).
• Mwanachama na Kiongozi wa Mwalimu Nyerere Rotary Club Dodoma.
• Amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi wa shule ya Jamhuri Sekondari.
• Amewahi kuwa Mjumbe wa Bodi wa ofisi ya Bonde la Wami-Ruvu.
• Alikuwa Mjumbe wa Bodi wa Umoja wa Watoa Huduma za Maji (ATAWAS).
• Marehemu amekuwa mzee wa Kanisa tangu mwaka 2000 hadi alipofariki. Pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Kanisa na Mjumbe wa Kamati ya Fedha
ya Kanisa la Anglikana Dodoma hadi alipofariki.
5. KUUGUA NA KUFARIKI
Marehemu Inj. Dkt. Mokiwa aligundulika kuwa na matatizo ya figo mwaka 1998 na alipata matibabu mara kadhaa na kuwa katika afya njema. Marehemu
aliendelea kufanya kazi kama vile hana tatizo la figo na alifanya kazi kwa weledi mkubwa kuliko hata wafanyakazi wazima.
Mnamo tarehe 10 Septemba 2014, marehemu aliugua ghafla na kupata tatizo la kushindwa kupumua na ndipo alipelekwa hospitali ya UDOM kwa matibabu na baadaye kuhamishiwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Marehemu Inj. Dkt. Mokiwa alifariki Ijumaa tarehe 12 Septemba 2014 majira ya saa 6.00 za usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital).
6. HITIMISHO
Marehemu Inj. Dkt. Mokiwa ameacha Mjane, watoto 3 na wajukuu 3.
“BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA
LIHIMIDIWE”
Maziko
Mwili wa marehemu unatarajiwa kupumzishwa katika nyumba ya milele kijijini kwao Mgombezi, Korogwe Tanga kesho.