Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9041

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

$
0
0
Rais  John Magufuli akitangaza mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2017. Wakimsikiliza ni Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na maafisa waandamizi wa Ofisi ya Rais. Picha na Ikulu


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Oktoba, 2017 amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo Mhe. Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.
Iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini, na iliyokuwa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametangaza mabadiliko hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam na lifuatalo ni Baraza la Mawaziri baada ya kufanyiwa mabadiliko.
1.     Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
                     I.        Waziri –                       George Huruma Mkuchika

2.     Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
                     I.        Waziri -                       Selemani SaidJafo
                   II.        Naibu Waziri -Joseph Sinkamba Kandege
                III.        Naibu Waziri -             George Joseph Kakunda

3.     Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
                     I.        Waziri -                       January Yusuf Makamba
                   II.        Naibu Waziri -             Kangi Alphaxard Lugola

4.     Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
                     I.        Waziri -                       Jenista Joackim Mhagama
                   II.        Naibu Waziri -             Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)
                III.        Naibu Waziri -Stella Alex Ikupa (Walemavu)
                       
5.     Wizara ya Kilimo.
                     I.        Waziri -                       Dkt. Charles John Tizeba
                   II.        Naibu Waziri -             Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa

6.     Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
                     I.        Waziri -                       Luhaga Joelson Mpina
                   II.        Naibu Waziri -             Abdallah Hamis Ulega

7.     Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
                     I.        Waziri -                       Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
                   II.        Naibu Waziri -             Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
                III.        Naibu Waziri -Elias John Kwandikwa

8.     Wizara ya Fedha na Mipango.
                     I.        Waziri -                       Dkt. Philip Isdor Mpango
                   II.        Naibu Waziri -Dkt. Ashatu Kijaji

9.     Wizara ya Nishati.
                     I.        Waziri -                       Dkt. Medard Matogoro Kalemani
                   II.        Naibu Waziri -             Subira Hamis Mgalu

10.   Wizara ya Madini.
                     I.        Waziri -                       Angellah Kairuki
                   II.        Naibu Waziri -             Stanslaus Haroon Nyongo

11.   Wizara ya Katiba na Sheria.
                     I.        Waziri -                       Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko 
                               Kabudi.


12.   Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
                     I.        Waziri -                       Dkt. Augustine Philip Mahiga
                   II.        Naibu Waziri -             Dkt. Susan Alphonce Kolimba

13.   Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
                     I.        Waziri -                       Dkt. Hussein Ali Mwinyi

14.   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
                     I.        Waziri -                       Mwigulu Lameck Nchemba
                   II.        Naibu Waziri -Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

15.   Wizara ya Maliasili na Utalii.
                     I.        Waziri -                       Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
                   II.        Naibu Waziri -Josephat Ngailonga Hasunga

16.   Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
                     I.        Waziri -                       William Vangimembe Lukuvi
                   II.        Naibu Waziri -             Angelina Sylivester Mabula

17.   Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
                     I.        Waziri -                       Charles Paul Mwijage
                   II.        Naibu Waziri -             Mhandisi Stella Martin Manyanya

18.   Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
                     I.        Waziri -                       Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
                   II.        Naibu Waziri -             William Tate Ole Nasha

19.   Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
                     I.        Waziri -                       Ummy Ally Mwalimu
                   II.        Naibu Waziri -             Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile

20.  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
                     I.        Waziri -                       Dkt. Harrison George Mwakyembe
                   II.        Naibu Waziri -             Juliana Daniel Shonza

21.   Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
                     I.        Waziri -                       Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
                   II.        Naibu Waziri -             Jumaa Hamidu Aweso

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw. Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wateule wotewataapisha Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Oktoba, 2017


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9041

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>