Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9089 articles
Browse latest View live

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AKUTANA NA RC ARUSHA

$
0
0
DSC_0175

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.

DSC_0170

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati Mkuu wa Mkoa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wkibadilishana mawazo kabla ya kuanza mazungumzo yao.

DSC_0178

Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda akizungumza na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu.

DSC_0185

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo na uongozi wa mkoa wa Arusha ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Daud Felix Ntibenda (kulia) na kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Addo Mapunda.

DSC_0189

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) katika picha ya pamoja na uongozi wa mkoa wa Arusha.

DSC_0198

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Addo Mapunda akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Daud Felix Ntibenda.


SERIKALI YAKUBALI AZIMIO ARUSHA KUHUSU HIFADHI YA JAMII

$
0
0
IMG_7245

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Arusha).

Na Mwandishi wetu, Arusha

SERIKALI ya Tanzania imeridhia azimio la arusha kuhusi hifadhi ya jamii nchini Tanzania na kusema litatumika kama dira katika kunemeesha watanzania.

Azimio hilo ambalo limetoka baada ya mkutano wa siku tatu wa wadau mbalimbali wa hifadhi ya jamii kutoka bara la Afrika na mashirika ya kimataifa limeelezwa kuwa msingi mkubwa wa ajenda ya Tanzania kuhakikisha wananchi wake wanahaki sawa katika elimu, afya na mwendelezo wa kiuchumi.

Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii inasaidia kuwa na maendeleo endelevu kwa kuangalia maendeleo ya binadamu katika ujumla wake.

Mkutano huo wa siku 3 uliohusisha wataalamu 150 kutoka sekta mbalimbali nchini na barani Afrika wakiwemo watengeneza sera, watafiti na wataalamu wa masuala ya hifadhi.

Ukiwa umewezeshwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za uchumi EPRI iliyopo Afrika Kusini (EPRI) , mkutano huo umeelezwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salumkwamba umeweka misingi imara ya kuwa na hifadhi ya jamii endelevu inayojibu mipango ya maendeleo ya taifa.

IMG_7158

Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni maadui wa taifa.

Kukiwa na wataalamu waliobobea katika mifumo ya hifadhi ya jamii kutoka Afghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe ulifanikiwa kutengeneza hoja zitakazotumika kufanya hifadhi ya jamii Tanzania kuwa endelevu.

Waziri Mkuya alishukuru kwa ushiriki wa mkutano na jinsi ulivyokuwa wazi na jinsi wataalamu walivyoweza kutengeneza azimio ambalo linaenda kuwa msingi katika utengenezaji wa sera na sheria kuhusu hifadhi za jamii nchini Tanzania na afrika kwa ujumla.

Mada kadhaa ziliwasilishwa katika mkutano huo ambazo zilizaa majadiliano yenye manufaa kuhusu mwelekeo wa hifadhi za jamii,utengenezaji wa mifumo ya kuweza kuendelea kuwepo kwa hifadhi ya jamii na umuhimu wa uratibu ndani ya serikali kuu, mitaa na mashirika yanayiotoa huduma za hifadhi ya jamii.

IMG_7135

Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) wakisikiliza azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya jamii wakati wa kufunga kongamano hilo.

Waziri huyo alisema kwamba wakati taifa linaelekea katika uchumi wa gesi utakaofanya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 masuala ya hifadhi ya jamii yatakahakikisha haki katika kugawa keki ya taifa na kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma za elimu, afya, na za kiuchumi kwa haki, kwa kuwa mifumo hiyo pia itatakiw akuchochea ajira na ujasirimali huku ilkilinda afya za wahusika.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi.

Aidha, Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.

IMG_7204

Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na kuipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake.

“Wimbo huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na Wafalme”alisema Dkt. Gulaid.

Dkt. Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa wote wapo salama na wapo kwenye mpango wa hifadhi ya jamii kwa kuwa wametambuliwa na kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania ambapo wajumbe waliimba wimbo huo na kuhitimisha kongamano hilo.

DSC_1058

Washiriki wa Kongamano hilo wakiimba wimbo wa Taifa baada ya Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid kutoa ombi kabla ya kumalizika kwa kongamano hilo.

IMG_7109

Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akisistiza jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.

DSC_1061

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitia saini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii huku viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia tukio hilo.

IMG_7267

IMG_7269

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na washiriki wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akionesha nakala ya Azimio la Arusha alilosaini kwa niaba ya Serikali.

IMG_7271

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Wazri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum baada ya kusaini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii (katikati) kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb).

IMG_7272

Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akipeana mkono na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) mara baada ya kusaini azimio hilo huku Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.

IMG_7102

Baadhi ya wajumbe wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.

IMG_7173

IMG_7003

IMG_7043

Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya kumalizika kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.

KAJALA AKUNWA NA KUMWAGA MIHELA KWA WAIMBAJI SKYLIGHT BAND

$
0
0
DSC_0028

Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village huku akipewa sapoti na Digna Mbepera.

DSC_0030

Digna Mbepera na Bela Kombo wakimpa back up Aneth Kushaba AK47 kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.

DSC_0071

Majembe ya Skylight Band yakionyesha manjonjo yao jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.

DSC_0082

Aneth Kushaba na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wao huku Digna Mbepera na Bella Kombo.

DSC_0092

Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakifanya yao jukwaani.

DSC_0147

Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka mdogo mdogo.

DSC_0149

DSC_0158

Birthday girl nae hakubaki nyuma aliunga tela na kuburudika na Skylight Band.

DSC_0279

Msanii wa bongo movie Kajala akitembeza manoti ya wekundu wa msimbazi kwa waimbaji wa Skylight Band Ijumaa iliyopita alipokunwa na uimbaji wao.

DSC_0280

Kajala akizichomoa tu kwenye pochi lake.

DSC_0281

Joniko Flower akisubiria zamu yake.

DSC_0282

Joniko Flower akipokea manoti yake kutoka kwa Msanii wa bongo movie Kajala.

DSC_0283

Na kwa wale wasanii waliokuwa back stage pia walibahatika kujizolea manoti kutoka kwa Kajala.

DSC_0298

Wapenzi wa Skylight Band wakishuhudia tukio hilo.

DSC_0306

Twende kazi... na burudani iendeleeee..!

DSC_0326

Mashabiki nao wakajibu mapigo.

DSC_0340

Sam Mapenzi akitunzwa na shabiki wake.

DSC_0343

DSC_0160

Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band, Ijumaa iliyopita huku Joniko Flower na Sony Masamba wakimpa sapoti.

DSC_0164

Mashabiki wakiendelea kula raha..!

DSC_0345

DSC_0170

Birthday girl na mabeste zake wakicheza mdogo mdogo.

DSC_0189

Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma...... mashabiki wakiondoka ma-style ya Skylight Band.

DSC_0115

Hashim Donode na Bela Kombo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band huku wakipewa back up na Aneth Kushaba pamoja na Digna Mbepera.

DSC_0121

nakupenda pia pia aha...Nakupenda pia...You make me wanna say....Nakupenda pia pia ahaa.....Vijana wakiwa kwenye hisia kali jukwaani.

DSC_0196

Majembe ya Skylight Band yakisebeneka jukwaani huku yakijaribu kuwafundisha mashabiki wao.

DSC_0198

Mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Joniko Flower akiwachezesha ligwaride la sebene majembe ya Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village .

DSC_0146

Mtaalamu wa kupiga kinanda Danny akifanya yake huku akipata Ukodak.

DSC_0044

Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki huku bendi hiyo ikimpa zawadi ya kumwimbia wimbo maalum wa sherehe hizo kumpongeza.

DSC_0045

Birthday girl akiendelea na zozezi la kulisha vipande vya cake shosti zake.

DSC_0048

DSC_0053

Birthday girl akiteta jambo na mchumba wake Lota Mollel.

DSC_0054

Mahaba niuweeeeeeee! Birthday girl akipata kiss kutoka kwa mchumba wake Lota Mollel.

DSC_0056

Birthday girl akiendelea kukata cake kwa ajili ya kuwalisha ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika naye.

DSC_0058

Birthday gilr na mchumba wake wakilishana cake kimahaba zaidi....!

DSC_0207

Emma Beyz na Danny Kinanda.

DSC_0223

Wadau wakipata Ukodak.

DSC_0356

Mdau Iddi Baka na Blogger King Kif wakishow love mbele ya camera yetu.

DSC_0226

Warembo wa ukweli na wenye viwango na ubora wanapatikana Skylight Band pekee hakunaga kwingine.

DSC_0239

DSC_0358

Nyomi la mashabiki wa Skylight Band likiwa limeshona Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.

Dkt. Bilal kuzindua majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Jumatatu

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania) itakayofanyika Jumatatu, tarehe 22 Disemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo itafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi – saa 6:00 mchana katika eneo lililopo nyuma ya Jengo la Mawasiliano (Mawasiliano Towers), barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam yalipojengwa majengo hayo. Aidha, majengo haya yapo karibu kabisa na kituo kipya cha daladala cha Ubungo. 
Majengo yatakayozinduliwa ni Mahakama ya Mafunzo (Teaching Court); Vyumba vya Madarasa (Lecture Theatres); Maktaba (Library); Jengo la Utawala (Administration Block); Mgahawa (Cafeteria); na Nyumba za Watumishi (Staff Quarters). 
Pamoja na Makamu wa Rais, viongozi wengine watakaohudhuria ni Mawaziri, Majaji, Makatibu Wakuu, Mawakili, Wabunge, Wahadhiri na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria.  
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilianzishwa na Sheria ya Bunge (Sura 425) mwaka 2007 kufuatia jitihada na mapendekezo ya muda ya muda mrefu ya Tume na Kamati mbalimbali zilizofanya utafiti katika sekta ya sheria nchini na kuona umuhimu wa kuwa na chuo cha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ili kuongeza ujuzi na stadi baada ya kupata mafunzo ya nadharia katika vyuo vikuu.  
Ujenzi huo wa majengo ya kudumu ya Taasisi umeigharibu Serikali zaidi ya Tshs 16.1 bilioni na ulianza mwezi Oktoba, 2010 na kukamilika mwezi Juni, 2013. Ujenzi ulifanywa na Kampuni ya BECG (Beijing Engineering Construction Group) kutoka China na ulisimamiwa na kampuni ya Co-Architecture yenye makao makuu yake hapa nchini. Kampuni hizi ndizo zilizoshinda zabuni za kazi zao. 
Wanahabari kutoka vyombo vyote mnakaribishwa katika hafla hiyo.


Imetolewa na:
Wizara ya Katiba na Sheria
Dar es Salaam
Ijumaa, Disemba 19, 2014

Punguzo Kabambe la tiketi za Sauti za Busara kwa Watanzania

$
0
0





Tamasha kubwa la muziki linalofanyika kila mwaka la Sauti za Busara, maarufu pia kama tamasha  kirafiki duniani mara zote limekua likitoa kipaumbele katika upatikanaji wake kwa wenyeji. Tamasha lijalo litavikutanisha vikundi 19 kutoka Tanzania kutumbuiza kuanzia tarehe 12 hadi 15 Februari 2015. Kiingilio ni burekwa waenyeji kabla ya saa 11 jioni na baada ya hapo ni shilingi 3,000/= tu kwa watanzania wote ili waweze kuhudhuria Tamasha! Zaidi ya hapo, watoto wanaruhusiwa kuingia bila kutozwa chochote hivyo basi wenyeji  wanachotakiwa ni kujitokeza nakusherekea muziki wa Afrika huku wakipeperusha bendera ya Bongo, pamoja na wageni.

Kwa kupitia mchango wa Sauti za Busara, Tanzania inaendelea kujidhatiti katika ramani ya dunia katika suala zima la utalii wa kiutamaduni. Mkurugenzi wa tamasha, Yusuf Mamoud anasema “Sauti za Busara inawaleta watu pamoja, hutoa ajira, inasaidia kuimarisha tamaduni za asili, inaendeleza wasanii pamoja na kukutana na kujifunza kutoka kwa wenzao, lakini pia inatangaza utalii wa kiutamaduni wa Tanzania. Mbali na hapo, Sauti za Busara inafanya kazi kubwa katika nchi: kukuza amani na umoja kwa kuheshimu utofauti na mchanganyiko wa tamaduni mbali mbali”.


Wakiwemo pamoja na wasanii wakubwa wa kimataifa kama Blitz the Ambassador kutoka Ghana, Tcheka(Cape Verde), Isabel Novella(Mozambique), Aline Frazao(Angola), Octopizzona Sarabikutoka Kenya na Ihhashi Elimhlophe wa Afrika kusini, wasanii watakaowakilisha Tanzania katika Sauti za Busara 2015 ni: Alikiba, Msafiri Zawose, Leo Mkanyia, Culture Musical Club, Mgodro Group, Mabantu AfricaIfa Band, Cocodo African Music,Rico Single, Mwahiyerani,Zee Town Sojaz, Kiki KIdumbaki na wengine wengi.


Rais aongeza miezi sita kukamilisha maabara

$
0
0




·        . Awapongeza wananchi na viongozi kwa kazi kubwa ya ujenzi
·        . Atunukiwa Digrii ya Heshima ya Uzamivu
·        . Achangia Sh.milioni 200 Taasisi ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaongezea muda wa miezi sita viongozi na wasimamizi wa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari nchini, ili kuwawezesha kukamilisha kazi hiyo ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete ametoa pongezi kwa wananchi wa Tanzania na viongozi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika ujenzi wa maabara nchini.
Rais kikwete pia ametangaza kuwa anachangia Sh.Milioni 200 katika Mfuko Maalum wa Dhamana (Endowment Fund For Excellence) wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (The Nelson Mandela African Institution of Science and Techonolgy).
Rais Kikwete ametangaza mambo hayo makubwa jana, Alhamisi, Desemba 18, 2014, wakati alipozungumza na uongozi, wahitimu na wana-Jumuiya ya Taasisi hiyo, baada ya kuwa ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (PhD honoris causa) ya taasisi hiyo katika Mahafali ya Pili ya Taasisi hiyo yaliyofanyika kwenye Taasisi hiyo Tengeru, Arusha.
Rais Kikwete alitunukiwa digrii hiyo ya heshima ya Uzamivu na Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Mheshimiwa Mohamed Gharib Bilal ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taasisi hiyo ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ni chombo cha aina ya pekee cha elimu ambacho hutoa wahitimu wa Shahada za Uzamili (Masters Degree) na Uzamivu (PhD)tu katika sayansi na teknolojia na ni moja ya taasisi mbili tu za aina hiyo katika Bara la Afrika.
Katika hotuba yake iliyofafanua kwa undani kabisa maana ya maendeleo ya sayansi na teknolojia katika maendeleo ya Tanzania na nchi yoyote dunia, Rais Kikwete pia alizungumzia maendeleo ya ujenzi wa maabara ya masomo ya sayansi nchini ambao lengo lake ni kutekeleza agizo lake la kuhakikisha shule zote za sekondari nchini zinajenga maabara ya kufundishia masomo ya sayansi.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo miaka miwili iliyopita, Novemba 2012 na akatoa miaka miwili kukamilisha kazi hiyo ifikapo Novemba 30, mwaka huu, 2014. Rais Kikwete alitoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa ukosefu wa maabara kwa ajili ya masomo ya fikizia, kemia na biolojia ilikuwa moja ya sababu ya kuwakatisha tamaa wanafunzi nchini kupenda masomo ya sayansi.
Aidha, Rais Kikwete alisema kuwa umuhimu wa kujenga maabara uliongezwa kasi na ongezeko kubwa la shule za sekondari ambazo ziliongezeka kutoka shule 828 mwaka 2004 hadi kufikia 3, 551 kwa sasa. Kati ya shule hizo 3,551 ni shule 88 zilizokuwa na vyumba vitatu kwa ajili ya masomo hayo matatu ya sayansi.
Rais Kikwete amesema kuwa tathmini ya sasa inaonyesha kuwa zinatakiwa zijengwe maabara kwenye shule 3,463 ambazo ni sawa na vyumba 10,389 na kuwa tathmini hiyo inaonyesha kuwa hadi Desemba 7, 2014, vilikuwa vimejengwa vyumba 3,867 vya maabara ambavyo ni sawa na asilimia 37.2 ya mahitaji ambavyo vimekamilika, vyumba 5,891, sawa na asilimia 56.7 ambavyo viko katika hatua mbali mbali za kukamilishwa na vyumba 631 ama sawa na asilimia 6.1 ambavyo ujenzi wake haujaanza.
Aliongeza Rais: “Natoa pongezi za dhati kwa viongozi na wananchi wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya.  Kwa ajili ya kumaliza palipoishia nawaongezea miezi sita.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2014

AISHA MADINDA AZIKWA LEO KIBADA,KIGAMBONI

$
0
0





WAKURUGENZI wa bendi hasimu za dansi Tanzania, African Stars, Asha Baraka na Extra Bongo, Ali Choki, leo wameongoza mamia ya waombolezaji kumzika aliyekuwa mnenguaji wa zamani wa bendi hizo, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.

Mazishi ya Aisha Madinda yamefanyika leo kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe, Kigamboni jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kufanyika jana kutokana na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha ghafla cha mnenguaji huyo.

Baada ya uchunguzi huo kufanyika na ripoti kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi na familia, mazishi hayo yakafanyika leo jioni yakihudhuriwa na Asha Baraka na Choki, pamoja na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Salim Omari Mwinyi.

Akizungumza katika mazishi hayo, Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment inayoimiliki Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, alimuelezea Aisha kuwa ni sawa na mwanaye kutokana na muda mwingi aliotumia akiwa Twanga.

Baraka aliongeza kuwa licha ya kutokuwa na Aisha katika siku za karibuni, bado Twanga Pepeta inatambua na kuthamini mchango wa mkali huyo wa jukwaa na kwamba pengo lake halitasahaulika kirahisi ndani ya bendi hiyo kongwe.




Kwa upande wake Choki alisema daima atakumbuka uwajibikaji, usikivu na upendo wa Aisha akiwa na Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ na kwamba kwake yeye marehemu ni sawa na dada yake, huku akimtaja kama mtumishi mwema.

“Alikuwa na Extra Bongo kwa muda mfupi, lakini aina yake ya utumishi utabaki katika kumbukumbu zetu daima. Huu ni mwaka wa taabu kwangu, kwani siku ya arobaini ya marehemu mke wangu, alifariki pia mzee wangu Shem Karenga,” alisikitika Choki.

Choki alienda mbali zaidi kwa kulalama kuwa, siku moja baada ya kumzika Shem Karenga, ndio siku aliyofariki Aisha Madinda, hivyo kuendeleza mfululizo wa majonzi kwake na wadau wa tasnia nzima ya muziki wa dansi nchini.

Kwa upande wake, mtoto wa dada wa marehemu, Sheikh Mohamed Mussa, ambaye aliongoza mazishi upande wa familia, aliwashukuru Watanzania kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha mazishi hayo, huku akiwataka kuuendelea kumuombea.

Source:Michuzi

Jokate asaini mkataba wa thamani ya Sh8.5 bilioni na kampuni ya Kichina

$
0
0

Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini

Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006,  mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate
Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano hayo yalisainiwa leo kwenye hotel ya  Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.


Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.

Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa
nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.


 Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo


 “Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa,
lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.


Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha
aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals)
ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania.



“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika
Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.


Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya
Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao naTanzania.

 

  “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.
Source:Michuzi


Msichana auawa kikatili Ilalangulu, kata ya kibaoni

$
0
0


Elizabeth Richard (16) Mkazi  wa Kijiji cha Ilalangulu  Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele  Mkoani Katavi  ameuwawa  kikatili  kwa  kuchinjwa  shingo  na kunyofolewa baadhi ya viungo vya mwili.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo  alisema  yalitokea  juzi  saa nane mchana katika mashamba ya kijijini hapo.
 Alisema siku ya tukio  marehemu  na  mumewe,  Hevinie  Kagembe  waliondoka  nyumbani asubuhi  kwenda shambani kulima katika eneo linaloitwa Kazaroho ambapo wanandoa hao walikuwa wakilima  mashamba tofauti.
 Alisema mume wa marehemu  alirudi nyumbani na  kukuta  mkewe  hajarudi toka shamba alikoenda tofauti na mazoea yao kwani mke huwa anawahi kurudi shamba kabla ya mumewe ili aweze kuandaa chakula cha familia kungali mapema.
Kamanda Kidavashari alisema  alipofikia majira ya saa mbili usiku mume wa marehemu aliingiwa na shaka  na kuamua  kumpigia simu  Mama  mzazi wa marehemu anayeishi kijiji cha jirani  kutaka kujua kama  mkewe yuko  huko na kujibiwa na mama mkwe wake kuwa mkewe hajafika kijijini hapo.
Baada ya  kuona muda unaenda juhudi za  kumtafuta  marehemu  ziliendelea  kwa kutoa taarifa  kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji na kuendesha msako wa kumtafuta kwa kushirikiana na wanakijiji wengine  na kufanikiwa kuuona mwili wa marehemu jana majira ya  saa mbili  asubuhi  kwenye shamba alilokuwa analima marehemu.
 Kamanda Kidavashari alisema  raia mwema hao  baada ya kuuona  mwili  wa marehemu  walikwenda kutoa taarifa kituo cha  Polisi  Kibaoni ambapo polisi walikwenda kwenye eneo hilo huku wakiwa na viongozi wa kijiji hicho.
Alifafanua kuwa marehemu  alikutwa  amechinjwa shingo  ambapo kichwani alikuwa  amekatwa na mapanga  ubongo wake ukiwa umetoka nje  pia  akiwa amenyofolewa sehemu zake za siri,  ziwa lake moja la kushoto limenyofolewa na  mikono yake yote miwili imekatwa na kuondolewa haipo.
 “Uchunguzi kwenye eneo hilo  ulibaini  kuwa jirani na eneo walilokuta mwili wa marehemu  kulikuwa na dalili za  kuchimbwa   na kufukiwa kitu kwenye eneo hilo baada ya kufukua eneo hilo  walikuta viungo vya mwili wa marehemu   mikono  yake miwili,  ziwa lake moja  na nguo za marehemu zikiwa ndani ya shimo  lakini sehemu zake za siri hazikuweza kupatikana kabisa katika eneo hilo.” Alisema Kamanda Kidavashari.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema  jeshi la polisi  kwa kushirikiana  na uongozi wa  Kijiji hicho  wanaendelea  na upelelezi  katika maeneo  mbalimbali  ili  kubaini  na kuwakamata   wale wote walihusika  katika mauwaji hayo kwani hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Source:  WILLY SUMIA, MPANDA

RAIS JACOB ZUMA KUWASILI KESHO KWA ZIARA RASMI

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21 Desemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Mhe. Zuma atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Zuma atakutana kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 22 Desemba, 2014 kabla ya kuondoka nchini siku hiyohiyo kurejea nchini kwake.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

20 DESEMBA, 2014

UJENZI WA MABWENI SHULE ZA PEMBEZONI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WANAFUNZI MIJINI

$
0
0



Jamii imetakiwa kuendelea  kuunga mkono juhudi za Serikali za ujenzi wa mabweni katika shule  za Sekondari  zilizoko pembezoni mwa miji hasa maeneo ya vijijini ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa wanafunzi mijini.

Imeelezwa kuwa msongamano huo unasababishwa na baadhi ya wanafunzi kushindwa kujaza nafasi wanazopangiwa   maeneo ya pembezoni mwa miji kutokana na umbali.

Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es salaam na Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando wakati akizungumza na viongozi wa Elimu wa mkoa na walimu wakuu wa Shule za Sekondari za mkoa wa Dar es salaam wakati wa kikao cha Kamati ya Uchaguzi wa wanafunzi wa watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.

Alisema  mwaka huu  mkoa wa Dar es salaam umekuwa na kiwango cha juu cha ufaulu  kitaifa kwa kuwa na wanafunzi wanaokidhi vigezo vya kuendelea na masomo ya sekondari kwa kiwango cha asilimia 78 ukifuatiwa na mkoa wa Kilimanjaro ambao umepata asilimia 69.

Alifafanua kuwa kati ya wanafunzi 60,709 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu , wanafunzi 59,577 ambao ni sawa na asilimia 98.14  waliofanya mtihani huo, wavulana wakiwa 28,419 na wasichana 31,158.

Bi. Mmbando alibainisha kuwa  kati ya hao watahiniwa 1,132  sawa na asilimia 1.86 katika mkoa wa Dar es salaam hawawakuweza kufanya mtihani huo kutokana sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo, ugonjwa na sababu nyinginezo.

Akizungumzia  kuhusu ufaulu wa wanafunzi hao kimkoa alisema wanafunzi 46,434 sawa na asilimia 78 walifaulu mtihani huo na kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuongoza kwa kuwa na ufaulu wa juu kitaifa wavulana 22,389 na wasichana 24,086.

Alibainisha kuwa wanafunzi 36,610 walichaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule mbalimbali za Sekondari za ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam na kufafanua kuwa wanafunzi 9824 waliobaki sawa na asilimia 21 ambao nao wamefaulu watachaguliwa katika chaguo la pili kufuatia baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule zisizokuwa za serikali na nafasi zao kubaki wazi.

Katika kufanikisha zoezi hilo Bi. Mmbando alieleza kuwa mkoa tayari umeunda timu tatu zitakazofuatilia idadi ya wanafunzi watakaoshindwa kufika katika shule walizopangiwa  kuanzia Januari 14, 2015 katika halimashauri za Temeke, Ilala na Kinondoni ili nafasi zao zijazwe na wanafunzi wengine.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda akitoa tathmini ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika nchi nzima mwezi Septemba mwaka huu alisema mkoa wake ulifanya vizuri kutokana na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi kuuelewa vizuri mfumo wa ufanyaji mitihani uliotumika wa Optical Mark Reader (OMR).

Alisema kuwa wanafunzi wa shule 506 za jiji la Dar es salaam walifanya mtihani walitumia mfumo huo kwa ufanisi mwanafunzi 1 alifutiwa matokeo yake kwa sababu za udanganyifu, 2 walipata alama 0  huku  wavulana 10 na wasichana 10 kutoka wilaya ya Ilala na Kinondoni waliibuka washindi wa nafasi 10 bora kitaifa.

Source: Aron Msigwa – MAELEZO.

Waziri Mkuu awasili Qatar kwa ziara ya kikazi

$
0
0
                                                             
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili jijini Doha, Qatar jana usiku (Jumamosi, Desemba 20, 2014) kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo inayotarajiwa kuanza leo.

Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia fursa za kiuchumi na miradi mikubwa inayoweza kuzinufaisha nchi hizo na nje ya mipaka yake kwenye Ghuba ya Arabuni (Arabian Gulf) na bara la Afrika.

Vile vile Waziri Mkuu anatarajiwa kutangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania, fursa za biashara, za utalii na kutafuta mitaji kwa ajili ya sekta za uchimbaji gesi na mafuta, usindikaji mazao, uvuvi na mifugo, ajira na uendelezaji miundombinu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu atakuwa na mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani. Vilevile atakutana na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa nchi hii. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.

Vilevile Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Atatembelea pia Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali na wakuu wa taasisi za TPSF na TPDC.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, DESEMBA 21, 2014
https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif

Muhammad Ali akimbizwa hospitali

$
0
0


Bingwa wa ngumi wa uzito wa juu duniani  mara tatu Muhammad Ali amekimbizwa hospitalini baada ya kubanwa na nyumonia.
Msemaji wake amesema kwamba hali yake inaendelea vyema.
Ali, ambaye ambaye anaumwa ugonjwa wa Parkinson kwa miaka 30 anaendelea vyema.
Msemaji wake, Bob Gunnell amesema kwamba familia ya bingwa huyo mwenye miaka 72 inahitaji faragha.

JK: ubishi wa siasa hauwezi kutoa majawabu ya changamoto za maendeleo

$
0
0


*Aonya hatuwezi kuendelea kwa kutegemea mazingaombwe na ramli

*Asisitiza umuhimu wa internet akielezea kuwa elimu ya sayansi
haipatikani kwenye magazeti*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa kamwe Tanzania, kama ilivyo nchi nyingine yoyote duniani,
haiwezi kuendelea kwa kutegemea mazingaombwe ama ramli bila katika kuwekeza
kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, Rais Kikwete ametaka Watanzania kuacha mwenendo wa kutumia ubishi wa
kisiasa kutafuta majawabu ya changamoto za maendeleo akisisitiza kuwa
majawabu ya maendeleo yatapatikana katika maendeleo ya sayansi na
teknolojia.

Aidha, Rais Kikwete amewataka Watanzania kuongeza kasi yao ya matumizi ya
*internet* akisema kuwa mfumo huo wa habari na mawasiliano ni chimbuko
kubwa la elimu ikiwemo elimu ya sayansi kuliko kutegemea kupata elimu hiyo
katika magazeti.

Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza katika
Mahafali ya Pili ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela
iliyoko Tengeru, Arusha, taasisi ambayo hutoa shahada za juu za uzamili na
uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi.

Akizungumza baada ya yeye mwenyewe kuwa ametunukiwa Digrii ya Heshima ya
Uzamivu (PhD Honoris Causa) katika mahafali hayo ya pili, Rais Kikwete
alielekeza sehemu kubwa ya hotuba yake kuelezea umuhimu wa maendeleo ya
sayansi na teknolojia katika uhai na maendeleo ya Tanzania na taifa lolote
duniani.

“Somo tunalolipata ni kwamba hakuna mazingaombwe wala njia ya mkato ya
kujipatia maendeleo ya juu. Hatuna budi kuwekeza katika kuendeleza sayansi
na teknolojia nchini, kama kweli tunataka kutoka hapa tulipo. Hakuna ramli
wala pumba za uchawi zinazoweza kuendelea nchi yetu hata ukiimwaga pumba
hiyo katika kila njia panda ya barabara na sehemu zote za Tanzania. Bado
Tanzania haitabadilika hata inchi moja,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Hatuna budi kuwekeza zaidi katika kufundisha wanasayansi, na katika tafiti
na ujenzi wa miundombinu ya kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti zao. Kwa
muda mrefu sana hili ni eneo ambalo hatukulipa uzito unaostahili.”

Alisistiza: “Tumefundisha na kuwekza sana katika kuwaandaa vijana wetu
katika fani za sayansi ya jamii, uongozi, siasa, sheria na biashara. Pamoja
kada hizo kuwa muhimu, lakini wanasayansi muhimu zaidi.”

Rais Kikwete amesema kuwa Watanzania hawana budi kusaka elimu yenye manufaa
zaidi ya maendeleo siyo kushinda katika mambo ambayo hayana manufaa kama
vile kushinda kwenye ubishi wa kisiasa. “Watanzania kwenye ubishi wa siasa
usiseme – kila mtu fundi. Wanatumia siasa kujadili maendeleo na kazi ni
kulaumu watu wengine tu.”

Kuhusu umuhimu wa kusaka elimu, Rais amesema kuwa Watanzania wanapaswa
kusaka elimu kila inapopatikana. Kwenye *internet,* kwa mfano, ni mahali
ambako unapata kila kitu duniani. Elimu yetu hii ya kutafutwa kwenye
magazeti haitupeleki mbali – magazeti yenyewe yamejaa siasa tupu, nani
kashinda kura zaidi kuliko mwingine nani kashinda kidogo…”

Ends

Kasi ya kuwapatia wanajeshi makazi bora yaongezeka

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Adolf Mwamunyange wakati wa
hafla ya uwekaji jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa nyumba za maafisa wa
jeshi huko Monduli mkoani Arusha jana(picha na Freddy Maro)

Kasi ya Serikali kuwapatia askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) makazi bora na kuwarudisha kambini, ilishika moto jana,
Jumamosi, Desemba 20, 2014, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Amiri Jeshi Mkuu. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alipoweka jiwe la
msingi la ujenzi wa nyumba 6,064 za makazi ya askari katika sherehe
hiliyofanyika Monduli, Arusha.
 
Nyumba hizo 6,064 za kubeba familia nane kila moja ni sehemu ya
nyumba10,000  za makazi ya wanajeshi zinazojengwa katika vikosi mbali mbali
vya JWTZ katika mikoa tisa ya Tanzania kwa gharama ya dola za Marekani
milioni 300.
 
Mradi wa kuwapatia wanajeshi makazi bora na kuwarudisha makambini ulianza
mwaka 2011, wakati Serikali ya Tanzania ilipopata mkopo wa ujenzi wa nyumba
hizo za wanajeshi ambako kati ya dola za Marekani milioni 300, Jamhuri ya
Watu wa China kupitia Benki ya China-Exim inatoa mkopo wa dola milioni 285
na Serikali ya Tanzania inatoa dola milioni 15.
 
Ujenzi wa nyumba hizo unaofanywa na Kampuni ya Shanghai Consturuction Group
General Company umepangwa kukamilika katika muda wa miezi 50, ifikapo
Septemba mwaka 2017.
 
Mikoa tisa ambako nyumba hizo zinajengwa ni Arusha, Dar Es Salaam, Dodoma,
Kagera, Kigoma, Morogoro, Pemba, Pwani na Tanga na ni sehemu ya mpango
kabambe wa maboresho na uimarishaji wa JWTZ ambayo ni pamoja na kulipatia
Jeshi hilo zana za kisasa, vifaa bora zaidi, makazi mazuri, mafunzo na
huduma nyingine bora zaidi mbali mbali.
 
Akizungumza kabla ya kuweka rasmi jiwe la msingi kwenye ujenzi wa nyumba
hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo ni sehemu ya mpango
wa miaka 15 ya maboresho na uimarishaji wa JWTZ ambao hata hivyo, Serikali
yake imeamua kuutekeleza na kuukamilisha katika miaka saba tu.

THE 13thZANZIBAR BUDOKAN JUDO CUP2014

$
0
0

BudokanJudoCup-1st-winners

THE PRESS RELEASE


Zanzibar Judo Association organizedthe 13th ZANZIBAR BUDOKAN JUDO CUP2014on 21/Dec/2014(Sun) at Zanzibar Budokan,situated in Amani National Stadium in Zanzibar.
th
ZANZIBAR BUDOKAN JUDO CUP2014>
*ZANZIBAR BUDOKAN JUDO CUP2014 is weight category National Judo Championship in Zanzibar and one of Qualifying competition for selecting the National team 2015.
*Zanzibar Budokan Judo Cup has been held by ZJA since 2001, this is the 13th.
*Participators wereabout 70 people 60 players from Unguja and Pemba from 9clubs
*Pemba Team 11people participated, this is the first competition for them.
itwas so  exiting Judo Championship.!
*Pemba team continue to train inUngujaat Zaznibar Budokan amanitill 25/Dec/2014(Fri)
BudokanJudoCup-allwinners

BudokanJudoCup-participators-afterclosingceremoney

certificate-from minister of Japan


*Competitions started at 9:00 in the morning Final started PM2:00, before Final ,Ambassador of Japan awarded Certificate of Appreciation as on behalf of The Minister of Foreign Affairs in Japanto Mr. Tsuyoshi Shimaoka who is Honorary President of Zanzibar Judo Association for his efforts of long time.

*This is the last competition for Ambassador of Japan in Tanzania Mr.Okada(his team neary to finish) so that ZJA prepare the gift for remembering (Zanzibar Chest)

The 1STwinners  (They got150,000/: , Gold Medal and Certificate)
60KG  MEN 1st winner---     Ali Juma Khamis
66KG  MEN 1st winner----  AbudulShakuru
73KG  MEN 1st winner ---- Abdulsamad Alawi
90KG  MEN 1st winner ----  Mbarouk Selemani
100KG MEN  1st winner --- Masoud Amour




The 2NDWinners  (They got Silver Medal and Certificate and 100,000/:)
60KG          MEN  2nd winner----Jakob Lukas
66KG           MEN  2nd winner ---- Hakim Haji
73KG           MEN  2nd winner---- Mansab Alawi
90KG           MEN  2nd winner ----Rajab Khassum
100           MEN 2nd winner ---- Othman Issa

The 3RDWinners (They got Silver Medal and Certificate and 50,000/:)
60KG   MEN  3rdwinner---- Mussa Haji
60KG   MEN  3rdwinner---- Abdulrabbir Alawi
66KG   MEN 3rd winner ---- Nassir Juma
66KG   MEN 3rd winner ---- AbdallaSalum
73KG   MEN 3rdwinner  ----Mwinyi Ali
73KG   MEN 3rdwinner  ----HafidhMakame
90KG   MEN 3rd winner ----  Mrid Haji
100KG   MEN 3rd winner ---- Mohamed Abdulrahaman
Zanzibar Judo Association try to prepare big prize every year, for motivation and level up of Judo Players in this country.
In this time ZJA prepared prize for winners of each categories (1st winner 150,000/:
2nd winners 100,000/: 3rd winners 50,000/:) and gifts for all participators—Furana.

< Participators >
70 peoples from 9clubs (60 players, 10 officials)
ZanzibarBudokan /Chuo cha Mafunzo  / Zanzibar Police/
Mwanakwerekwe / Dole   /Mlandege/*Nungwi /*Pemba Budokan/*Kengeja
・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・・
< Honor Guests >
Ambassador, Embassy of Japan in Tanzania, -------Mr.Masaki Okada
Director, Departmant of Informantion-------Mr.YussufChunda
Executive Secretary, National Sports Council----Mr.HassanHilallaTawakar

ZANZIBAR JUDO ASSOCIATION   toutenkou@hotmail.com
Chief Organizer&H/President,ZJA  Tsuyoshi SHIMAOKA 0777-422819
V/President ZJA    Mohamed Khamis    0776-758520

UNESCO YAFADHILI MAENDELEO YA SAYANSI AFRIKA

$
0
0
IMG_7359

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu, Arusha

SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha.

Alisema shirika lake limejikita zaidi kuhakikisha kwamba inatoa elimu itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na hivyo kuwezesha wanaume kwa wake kufanyakazi kama wajasirimali.

“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema Naibu Mkurugenzi huyo.

IMG_7369

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Taasisi hiyo kushiriki mahafali hayo.

Akizungumza mbele ya wahitimu wa Taasisi hiyo na Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba sayansi na teknolojia vina nafasi ya pekee katika jamii na hivyo shirika kama UNESCO inachofanya ni kusaidia kuwapo kwa elimu hiyo.

Alisema sayansi na teknolojia ni msingi wa maendeleo kwani kupitia kuboreka kwa vitu hivyo viwili serikali nyingi zitaweza kukabiliana na umaskini uliokithiri na kupeleka watu wake katika maendeleo na ustawi.

Kiongozi huyo wa Unesco pia alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha kuwepo kwa Taasisi hiyo ambayo ilibuniwa katika mkutano wa aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia, James Wolfensohn, na Rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini mwaka 2001.

Ubunifu huo ulifanyiwa kazi na viongozi wa nchi za Afrika Januari 2005 katika mkutano wao wa Abuja ambapo walikubaliana kuanzisha vyuo vinne vya sayansi na teknolojia kwa jina la Nelson Mandela.

IMG_7570

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida wakipitia ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, mjini Arusha.

Alisema sayansi inashikilia majibu ya maswali ya maendeleo ya Bara la Afrika katika kukabili umaskini na kuwa na maendeleo endelevu katika sekta zote na jamii.

Naye Rais Kikwete akihutubia mkusanyiko huo aliwapongeza viongozi wa Taasisi hiyo kwa kuendeleza umaalumu wake.

“Taasisi hii ni sehemu ya mtandao wa vyuo vya Nelson Mandela vya Sayansi na Teknolojia katika Bara la Afrika. Chuo hiki cha Arusha ni mahsusi kwa ajili ya kanda ya Afrika Mashariki. Ndiyo maana Hati Idhini (University Charter) niliyokipa Chuo hiki inaeleza bayana kuwa Chuo hiki kinapaswa kuwa chenye hadhi maalum (special status). Hadhi hii yapaswa pia ionekane katika ubora wa elimu inayotolewa hapa. “ alisema Rais Kikwete.

Alisema ubora wake ni matokeo ya ubora wa wahadhiri wake, programu zake na miundombinu yake.

IMG_7509

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida akitoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wa juu wa chuo hicho.

IMG_7496

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakifurahi jambo wakati Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.

IMG_7542

Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Madela, Sayansi na Teknolojia wakitoa burudani kwenye mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.

IMG_7527

IMG_7483

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

IMG_7487

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.

IMG_7492

Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.

IMG_7619

Pichani juu na chini ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiwatunuku wahitimu mbalimbali wa shahada za juu za uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi wakati wa mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma, Tengeru jijini Arusha.

IMG_7626

IMG_7353

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria mahafali hayo.

DSC_0641

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya maprofesa wa taasisi hiyo.

DSC_0653

Pichani juu na chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.

DSC_0668

DSC_0703

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandali ya mahafali hayo.

WATANZANIA WASHAURIWA KUITUMIA NEEMA YA GESI KUPELEKA HIFADHI YA JAMII KWA KILA MTU

$
0
0
DSC_0013

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Arusha

MTAALAMU mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi wake.

Dhliwayo alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025 ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.

Dk. Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini Zimbabwe na Msumbiji.

Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.

DSC_0005

Ofisa anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza miundombinu ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake wa gesi kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.

Alisema kama taifa linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta ya gesi kuingia katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha uwapo wa huduma sawa kwa wote.

Alisema uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua kwa kasi ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi wamejikuta wakiwa katika umaskini wa kukithiri.

Alisema kutokana na tatizo hilo la umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa hali hiyo kunasababisha na sekta husika kutotoa ajira za kutosha ambazo zingewezesha watu kuneemeka na uchumi unaokua kwa kasi.

DSC_0079

Mtaalamu wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa mada chokonozi wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ambao umemalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi umaskini unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema unaowakuta wasichana.

Alisema pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza umaskini wa kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha mipango ya kupunguza umaskini inafanikiwa.

Alisema iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji kuwapo kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na madaktari na dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote yaliyolengwa” alisema Dhliwayo.

Alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Rwanda na Eritrea ambayo yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya kufikia zaidi ya asilimia 90 huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya jamii kwa kaya.

DSC_0093

Kuki Tarimo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mada chonokonozi wakati wa mkutano huo.

Aidha amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya millennia na kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi.

Katika mkutano huo ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya utengenezaji wa sera na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na haki katika kei ya taifa kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa kukithiri ulihudhuriwa na watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Pia ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.

DSC_0101

Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa mkutano huo uliomalizika hivi karibuni.

DSC_0109

Meneja Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel Mboya akiuliza swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayopelekea ugonjwa kansa ya ngozi.

DSC_0135

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe, akijibu swali kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi katika kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

DSC_0159

Mwakilishi wa wazee waliostaafu akiuliza swali kwa Wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhusiana na uboreshwaji wa huduma za afya kwa wazee ambapo imekuwa changamoto kubwa kwao.

DSC_0025

Ujumbe wa Makatibu wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukishiriki wa mkutano huo.

DSC_0115

Mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la UNICEF Tanzania, Jacqueline Namfua akifurahi jambo wakati wa mkutano huo.

DSC_0029

Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.

DSC_0107DSC_0128DSC_0067

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano.

Watanzania kunufaika na ajira Qatar - Pinda

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania watanufaika na kipato na maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira ambazo watapata katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Desemba 20, 2014) jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani.

Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla, Waziri Mkuu Pinda amesema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi hii inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni wachache.

 “Hivi sasa wapo Watanzania wanaofanya kazi hapa lakini ni wachache mno. Mazungumzo yalishaanza siku za nyuma. Tukisaini mkataba katika muda mfupi ujao, tutajua ni idadi gani wanahitajika na wanaweza kuja kila baada ya muda gani,” alifafanua Waziri Mkuu.

“Hapa Qatar kuna uwekezaji mkubwa umefanyika, kwa hiyo wanahitaji watu wa kufanya kazi... kwenye mahoteli, viwandani, na kikubwa hapa ninachokiona watu wetu watapata kipato lakini pia watapata ujuzi kwa maana ya maarifa yanayoendana teknolojia ya kisasa,” aliongeza.

Akeleza mambo mengine ambayo wamekubalina kushirkiana kama nchi rafiki, Waziri Mkuu alisema kuna mambo makuu manne likiwemo hilo la ajira. “La kwanza ni Kilimo.  Hapa Qatar ni jangwa kila mahali. Wamekubali kuja kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwa sababu sisi tuko karibu nao zaidi kuliko Marekani au Brazil.”

“Wanaweza kupata mchele, matunda, nyama kwa maana ya machinjio na viwanda vya kusindika nyama lakini pia katika uvuvi wa samaki. Tunayo bahari ila mitaji yetu ni midogo. Kwa hiyo wamekubali kuangalia eneo hilo pia,” alisema.

Alisema eneo la pili ni la gesi na mafuta. “Wamekubali kutusaidia utaalmu ili tushirikiane nao katika namna kutumia gesi kwenye ngazi ya chini hasa viwanda kwa sababu wenzetu wana uzoefu wa muda mrefu. Hata kwenye mafuta wameonyesha kuwa wako tayari,” alisema.
Eneoa la tatu alilitaja kuwa ni kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania na la nne ni TEHAMA. “Hawa wenzetu wamechanganya TEHAMA na sayansi na sasa wana Jiji la Sayansi na Teknolojia. Chini ya makubaliano tutakayofikia, watu wetu watakuja kujifunza masuala ya gesi na mafuta.”

Alisema wamekubaliana na Sheikh Abdulla al Thani kuunda timu ya pamoja baina ya nchi zao ili ifanye kazi ya kuainisha ni maeneo gani wanataka waanze nayo kwanza kulingana na mahitaji. “Nimemuahidi nikifika nyumbani nitaandika barua ili mchakato wa kuunda timu uanze rasmi,” alisema.

Mchana huu, Waziri Mkuu Pinda atakuwa na mazungumzo ya Kiserikali na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa Qatar. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.

Jioni Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Kesho (jumatatu, Desemba 22, 2014) atatembelea Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali, Dk. Gideon Kaunda wa TPSF na Bw. Shigela Malocha kutoka TPDC.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, DESEMBA 21, 2014

WAPIGA KURA KIMARA KING'ONGO WAKUSANYA SAINI KUMPINGA MWENYEKITI MPYA

$
0
0


CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeanza kukusanya saini za wananchi wa King’ongo kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo tayari wameandika kuyapinga kwa msimamizi wa uchaguzi  wilaya ya Kinondoni.
Tayari hadi kufikia jana saini zaidi ya 200 zimekusanywa .
Ukusanyaji wa saini hizo ambazo zinakusanywa ndani ya mtaa huo ambao upo kata ya Saranga unafanyika kutokana na msimamizi wa uchaguzi wa mtaa huo, Rebecca Rioga kudaiwa kutangaza mshindi kinyume na utaratibu.
CUF ambao walishiriki katika kivuli cha ukawa wamesema pamoja na CCM kutangazwa mshindi, hawakuwa wameshinda kwani kilichotokea ni msimamizi kukiuka  utaratibu  katika uthibitishaji wa kura.
Ushindi wa CCM ulitangazwa saa tano usiku chini ya usimamizi wa Polisi kutoka kituo cha  Mbezi.
Awali mawakala wa CUf wakati wa kuhesabu kura pamoja na ushindi waliokuwa nao waliona kuna idadi kubwa ya kura zinazozidi ambazo pia zina mfumo  mmoja wa mkunjo na kupigiwa mgombea wenyekiti  wa CCM . Kura hizo zilipata 32.
Mzozo wa matokeo ulianzia hapo kwani msimamizi alishindwa kueleza zilipotokea kura 32.
Jumla ya kura zote zilizopigwa zilikuwa 930 kati ya watu 1,364 waliojiandikisha kupiga kura, lakini idadi ya kura zote za wagombea uenyekiti ni 956 zikiwa ni kura 32 zaidi hasa baada ya kura 6 .
Katika barua ya kupinga matokeo kwa msimamizi wa uchaguzi halmashauri pamoja na kueleza bayana nini kilitokea katika uchaguzi huo pia wamesema kwamba mgombea Demetreus Mapesi wa CCM alitumia nafasi ya yeye kuwajua wasimamisi kutengeneza hila ya ushindi mwishoni.
Mapesi ni mwenyekiti wa Shule ya Msingi King’ongo ambacho kilikuwa kituo cha kupigia kura na wasimamizi pia wanatoka shule hiyo hiyo.
Katika kura kituo A waliopiga kura walikuwa 485 na kituo B waliopiga kura walikuwa  445 na kufanya jumla kuwa 930.Wagombea uenyekiti CUF Abubakari  Nyamguma kituo A alipata kura 253 na kituo B 224 ambapo mgombea wa CCM Demetreus Mapesi kituo A alipata kura 232 na kituo B 247  .
Ukijumlisha kura walizopata wagombea zinakuwa 956 na kuwa na ongezeko la kura 32.
mwisho

Viewing all 9089 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>