Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9079 articles
Browse latest View live

Airtel yatangaza kumi bora shindano la Airtel Trace Music Stars

$
0
0



Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washiriki walioingia kumi bora wiki hii katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars .
Mashindano hayo yana lengo la kuvumbua na kusaka vipaji vya wanamuziki chipukizi nchini na Afrika kwa ujumla
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel, Anneth Muga aliwataja walioingia kumi bora wiki hii ni pamoja na Christopher kihwele akiwa na namba ya ushiriki 55100050, karen Gardner 55100107, Mwinyimkuu Hussein 55100048, John chambasi 55100005, Vanessa Galinoma 55100232, Jesca Charles 55100135, Anne Mkisi 55100004
“Tunafurahi kuona jinsi gani watanzania wanavyoitikia na kushiriki katika shindano hilo ambapo mpaka sasa limedumu kwa takribani miezi miwili na nusu. “ alisema.
Aidha  aliitaka jamii, wapenzi wa muziki kuwapigia kura ili waweze kuendelea kufanya vizuri katika mashindano haya.
Mshindi wa Airtel Trace Music Stars atapatikana kwa vigezo viwili vikubwa  kwanza ni kwa uwezo wake wa kuimba  na pili kutokana na wingi wa kura .
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema sasa wako kwenye hatua muhimu sana ya kuwawezesha washiriki kuendelea mbele kwa kupiga kura kwenye namba 0901002233 Kisha unachagua lugha  na kufuata maelekezo, ili kuupigia kura wimbo au mshiriki.
Njia ya pili ni kwa kuandika ujumbe wenye kodi namba ya ushiriki na kisha kuituma kwenye namba 15594.
“Tutaendelea kuwajulisha washiriki watakao ingia kumi bora kila wiki na ili kupata habari hizi kwa urahisi basi tembelea facebook page yetu ya Airtel Tanzania na upata kuona picha za washiriki mbalimbali, namba zao za ushiriki na kusikiliza nyimbo zao kupitia simu yako ya mkononi.” alisema Mbando.
 Akiongea wakati wa maojiano na waandishi wa habari mmoja kati ya washiriki kumi bora wa wiki hii Jesca Charles alisema:” najisikia furaha sana kuingia katika kumi bora ya wiki hii, naomba watanzania wanipigia kura kwa wingi ili nisishuke nieendelee kufanya vizuri. Napenda sana kuimba na ndoto yangu ni kuwa mwimbaji wa kimataifa na mwimbaji nae vutiwa nae ni Beyonce natumaini siku moja ntafikia na kuwa mwimbaji nyota kama Beyonce”
Mashindano ya Airtel Trace yatafikia kilele mwanzo mwa mwaka kesho ambapo mshindi wa Airtel Trace Afrika atajishindia zawadi kabambe ikiwemo, kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na  safari kwenda nchini marekani na kupata mafunzo ya kimuziki na Nguli wa Muziki wa Amerika Akon
Mwisho

mashindano ya mbio za magari ya Morogoro

$
0
0
Mkuu  wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, ( wa kwanza kushoto mezani )  akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Mt Ulunguru Rally, Pankaji Valambia ( mwenye kipaaza sauti) huku washindi wa pili wa mashindano ya mbio za magari mwaka huu, Gerard Miller  na mwongozaji wake , Peter Fox , ambaye ni rubani wa ndege ,wakishikilia vikombe vyao , Miller ambaye  ni dereva mkongwe wa  mashindano makubwa ya magari Barani Afrika ,mwaka jana alishika nafasi ya kwanza, mashindano ya mwaka huu yalishirikisha madereva wa magari 17, kutoka Arusha, Dar es Salaam na Morogoro.


Mkuu  wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, ( watano kutoka kulia  ) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindo watatu  mashindano  ya Mt Ulunguru Rally 2014, na ( wanne kutoka kulia ) ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Amanzi, mashindano yao yalifanyika juzi (DES 21) mkoani Morogoro na kushirikisha madereva wa magari 17 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Morogoro. Picha zote na Picha na John Nditi.


Watanzania waomba ofisi ya ubalozi Qatar

$
0
0




WATANZANIA wanaoishi nchini Qatar wameiomba Serikali iangalie uwezekano wa kufungua ofisi ya ubalozi  nchini humo ili iwe rahisi kwao kufikisha matatizo yao na pia wawe na uhakika wa masuala yao kushughulikiwa kikamilifu.

Wametoa ombi hilo kwa nyakati tofauti jana usiku (Jumapili, Desemba 20, 2014) wakati wakitoa hoja na amatizo yao mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye yuko nchini Qatar kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Akizungumza kwa niaba ya Watanzania waishio Qatar katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Sheraton jijini Doha, Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania wanaoishi Qatar, Bw. Said Ahmed Said alisema ubalozi wanaoutegemea kwa sasa hivi uko Saudi Arabia ambako ni mbali na kwamba inakuwa vigumu kuwasilisha shida zote zinazowakabili Watanzania.

“Kwa mfano kuna suala la fursa za watoto wetu kusomeshwa elimu ya juu na kulipiwa na Serikali ya hapa. Inakuwa vigumu kupata hiyo fursa kwa sababu hakuna mtu wa kutusemea,” alisema Bw. Said na kushangiliwa na wenzake.

“Watoto wetu waliozaliwa hapa wakimaliza sekondari hawawezi kwenda Chuo Kikuu chochote kwa sababu mfumo wa hapa hauwaruhusu. Hata wale tuliowaacha nyumbani huwezi kuwaleta wakasomea hapa kwa sababu ya huo mfumo. Lakini wenzetu kutoka nchi nyingine wanapata hizo fursa kwa sababu wana quota yao. Tunaamini tukiwa na ubalozi hapa nchini, tutaweza kupata fursa kama wenzetu,” alisema.

Watanzania wengine waliochangia hoja ya kuwa na ofisi ni Bw. Abdallah Sima Abdalla (kutoka Zanziabar), Bw. Hersi Mohammed Adam (kutoka Singida) na Bw. Iddi Ali Ameir ambaye pia anatoka Zanzibar.

Hata hivyo, Bw. Hersi Mohammed Adam ambaye amefanya kazi kwenye kamouni ya Al Mazrui Oil Industries kwa miaka tisa, alisema kuna haja ya kuwaleta Watanzania wengi  wajifunze kazi ndogondogo zinazohusu uchimbaji mafuta kwani wana fursa ya kufundishwa wakiwa kazini. “Kuna kazi ambazo hazihitaji vyeti vya juu sana kama kusafisha mabomba ya gesi lakini pia ni za muhimu na zitawasaidia wengi kupata ajira wakati kazi kama hizo zikianza nchini Tanzania,” alisema.

Akizungumzia suala la kuwa na ubalozi, Waziri Mkuu alisema wazo lao ni la msingi ikizingatiwa kwamba kuna Watanzania zaidi ya 300 wanaoishi Qatar. “Hili suala ni la Serikali na mimi naona jibu la msingi ni kuwa na ofisi ya ubalozi hapa Doha kwa sababu mko wengi na tuna mahusiano ya karibu sana na wenzetu,” alisema na kuahidi kulifuatilia kwa sababu amekwishajadiliana na  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Maalim ambaye yuko kwenye msafara wa Waziri Mkuu.

Akizungumzia suala la ajira, Waziri Mkuu aliwahakikishia Watanzania hao kwamba Serikali ya Qatar imesharidhia mkataba wa kuruhusu raia wa Tanzania waje kufanya kazi Qatar. “Sisi tulianzisha huu mkataba na wenzetu hawa wameuridhia mwezi uliopita... naamini utatusaidia sana kwenye suala la ajira za watu wetu lakini itabidi tuangalie ninyi ambao mlikuwepo zamani kabla mkataba haujasainiwa tunawafaya nini,” alisema.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Pinda alitoa nakala zipatazo 30 za Katiba Inayopendekezwa kwa Watanzania waishio Qatar na kuwataka waisome na kutoa mapendekezo yao hasa katika eneo la uraia pacha. “Hakikisheni mnaisoma na kujadili kwa kina eneo hili na kisha mtupe majibu yenu kwa sababu suala hilo liliibua mjadala mkubwa ndani ya Bunge Maalum la Katiba wakati likijadiliwa,” alisema.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali, Dk. Gideon Kaunda wa TPSF na Bw. Shigela Malocha kutoka TPDC.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, DESEMBA 22, 2014

Rais amweka Prof Muhongo kiporo

$
0
0
Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia. katika hotuba yake amezungumzia Escrow na kumtaka Tibaijuka awapishe wamteue mwingine.

Baadhi ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa  Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)



BREAKING NEWS Maiti za ajali ya meli Kongo zakutwa Kigoma,zazikwa

$
0
0

ASKARI wa jeshi la ulinzi wa Tanzania wakiongoza viongozi wa serikali ya Tanzania,DRC na viongozi na wananchi wa kijiji cha Kalilani katika mazishi ya raia 14 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) waliofariki katika ajali ya meli Desemba 12 mwaka huu katika Mkoa Kalemie DRC na miili yao
kukutwa katika hifadhi ya Taifa ya Mahale.

Miili ya watu  14  imezikwa baada ya mashauriano ya serikali za Tanzania na DRC ambapo serikali ya DRC iliwakilishwa na Balozi mdogo wa nchi kutoka Ubalozi mdogo mkoani Kigoma.
 
Akizungumza muda mfupi kabla ya mazishi ya raia hao,Balozi Mdogo wa DRC katika ubalozi mdogo wa mkoa Kigoma,Riki Moleme alisema kuwa amefarijika
kwa namna serikali ya Tanzania ilivyochukulia kwa umuhimu mkubwa maafa ya Raia hao wa DRC na namna ilivyojitoa katika kushughulikia mazishi ya miili
hiyo.
 
Awali Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Mahale,Herman Batiho alisema kuwa walianza kuona miili ya watu hao kuanzia majira ya jioni Desemba 20
mwaka huu na ndipo wakaanza kuwasiliana na mamlaka mbalimbali ambapo waliwasiliana na uongozi wa kijiji cha Kalilani ambapo uongozi na wananchi
wa kijiji hicho walianza kusaidia katika kuopoa miili hiyo.
 
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani,Songoro Saidi alisema kuwa waliona mwili wa moja ya maiti hizo asubuhi ya Desemba 21 ambapo pia walipata
taarifa ya kuwepo kwa miili mingine ndani ya hifadhi ya Mahale na ndipo waliposhirikiana na kuiopoa miili hiyo hadi kufanikisha mchakato wa mazisho.
 
Desemba 12 mwaka huu jumla ya 128 walifariki dunia na wengine zaidi ya 250 waliokolewa kufuatia meli waliyokuwa wakisafiria iliyokuwa ikitoka Moba
kuelekea Kalemie ilizama katika mwambao wa ziwa Tanganyika katika mkoa Kalemia nchini DRC.

Kairuki: Tuache kufanya kazi kwa mazoea

$
0
0

Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde akijaribu baiskeli ya mazoezi aliyokabiodhiwa kama zawadi katika hafla ya kuwapongeza watumishi wa Wizara waliostaafu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi.
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakumbushwa kuwa chachu ya mabadiliko katika utumishi wa umma na kuondokana na utendaji kazi wa mazoea kwa kila mtumishi kufanya kazi kwa malengo yenye kutoa matokeo yanayopimika.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga watumishi waliostaafu katika Wizara hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki amesema utendaji kzi wenye kujali matokeo unawezekana na kuwataka watumishi wote kubadilika kimtazamo na kifikra ili kufikia lengo hilo.

Watumishi waliostaafu na kuaagwa katika hafla hiyo ni Bw. Fanuel Mbonde aliyekuwa Katibu Mkuu. Bi. Christinat Sonyi (Mkurugenzi wa Sera na Mipango), Bi. Anna Mayawalla (Mkurugenzi Msaidizi – Sera), Bi. Mariam Mwaisabila (Mtunza Kumbukumbu Mkuu Msaidizi), Bi. Giditha Peter (Mwendeshaji Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta) na Bi. Clara Mlamyingu aliyekuwa Mtunza Kumbukumbu Mkuu Msaidizi.
Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde akijaribu baiskeli ya mazoezi aliyokabiodhiwa kama zawadi katika hafla ya kuwapongeza watumishi wa Wizara waliostaafu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi.

Watumishi Wastaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa na vyeti vyao katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri Mhe. Angellah Kairuki na Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi. Hafla ya kuwapongeza ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde akikabidhiwa cheti na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria katika hafla ya kuwapongeza watumishi waliostaafu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Katibu Mkuu Mstaafu ni Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi

Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakisakata rhumba katika hafla ya kuwapongeza Watumishi waliostaafu iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
(Picha zote Wizara ya Katiba na Sheria)


Akifafanua, Naibu Waziri Kairuki amesema ni muhimu kwa watumishi wote kujenga uelewa wa pamoja wa majukumu ya Wizara ya kupanga mkakati wa kuyatekeleza kwa ushirikiano.

“Hatuna budi kujenga uelewa wa pamoja wa majukumu tuliyonayo katika Wizara yetu na kujenga ushirikiano wa hali ya juu. Tunapaswa kuondokana na utendaji kazi wa mazoea, lazima ukome sasa. Kila mmoja wetu kwa nafasi yake anapaswa kufanya kazi kwa malengo yenye kutoa matokeo,” amesema Kairuki katika hafla iliyohudhuriwa na Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi, wastaafu na watumishi wengine wa Wizara hiyo na wawakilishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara.

Kuhusu watumishi waliostaafu, Naibu Waziri Kairuki amesema watumishi wote waliostaafu wanapaswa kupongezwa na kutimiza wajibu wao kwa uadilifu, umoja na ushirikiano hadi kufikia hatua ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

“Katibu Mkuu alitufanya sote kujisikia kama timu moja iliyolenga kutekeleza majukumu ya Wizara kwa ufanisi huku ikizingatia maslahi ya watumishi. Kipekee, ninamshukuru sana kwa uongozi wake katika Wizara hii ambao umeweka misingi ambayo sisi viongozi tuliopo tunaisimamia, tunaiendeleza na kuiboresha,” alisema Naibu Waziri Kairuki na kuongeza:

Katibu Mkuu huwa hafanyi kazi peke yake. Ana Timu. Nyie wote kwa umoja wenu ndiyo timu yake. Na kama mnavyofahamu, mchezaji mmoja akiwa mzembe basi timu yote inaathirika. Kwa msingi huo, Ndugu Mbonde alikuwa na timu ambayo baadhi ya wachezaji wake ni wastaafu tunaowaaga leo na sisi tunaoendelea na utumishi,” aliongeza Mhe. Kairuki.

Aidha, Naibu Waziri Kairuki alitumia hafla hiyo kuwakumbusha watumishi kuhusu masula mbalimbali ya kitaifa likiwemo la kushiriki katika Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa na mapambano dhidi ya UKIMWI.

Sisi kama watumishi wa Wizara yenye dhamana ya mambo ya Katiba na Sheria, tunapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuisoma, kuielewa na hatimaye kushiriki katika kupigia Kura ya Maoni Katiba Inayopendekezwa ifikapo tarehe 30 Aprili mwakani (2015)” alisema na kuongeza watumishi wa Wizara wanapaswa kuwa waangalifu na kujikinga na maambuikizi ya virusi vya UKIMWI.

“Sote tunajua jinsi janga hili linavyoathiri nguvu-kazi ya taifa na hata familia zetu. Sidhani kama kuna mtu kati yetu ambaye hajaguswa na tatizo hili. Wito wangu ni kuwa waangalifu na kujikinga na maambukizi. Kwa wale wanaoishi na virusi, Serikali itaendelea kuwahudumia kwa mujibu wa miongozo iliyopo,” alifafanua.

Akizungumza kwa niaba ya Wastaafu, Katibu Mkuu Mstaafu Mbonde aliwashukuru watumishi Wizara kwa kutambua mchango wake na watumishi wastaafu wengine na kuahidi kutoa ushirikiano pale utakapohitaji.

“Sisi tupo na ujuzi wetu, wakati wowote mtakapoona mnatuhitaji tuwasiliane na tupo tayari kutoa mchango wetu ili kufanikisha majukumu ya Wizara,” alisema Bw. Mbonde.

Kuhusu maadili, Katibu Mkuu huyo Mstaafu aliwakumbusha watumishi kuzingatia maadili na kuepuka vitendo vya rushwa ili kulinda heshima ya Wizara na utumishi wa umma.



MSHINDI WA PILI WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 NDIYE ATAIWAKILISHA NCHI MASHINDANO YA KIMATAIFA

$
0
0


Miss Universe Tanzania 2014,  Carolyne Bernard
Kamati ya Miss Universe Tanzania imemteua mshindi wa pili wa Miss Universe 2014, Nale Boniface kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa  ya Miss Universe yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwa kwanza 2015 Miami, Marekani.
Hatua hii imechukuliwa baada ya mshindi husika Miss Universe Tanzania 2014,  Carolyne Bernard kupata ajali na kuvunjika kidole chake cha mguu. Ripoti ya daktari imeonyesha kuwa kupona kwake kutachukua mwezi mmoja wakati mrembo anatakiwa awe mashindanoni baada ya siku kumi kuanzia sasa. Isitoshe awapo mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa viatu virefu (High heels) wakati wote ambapo haishauriwi kiafya kutokana na tatizo lake.
Hivyo kutokana na hali hii, Nale Boniface ambaye alishika nafasi ya pili na aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth ndiye atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala yake kama mkataba unavyoainisha na hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania 2014.
Kamati inasikitishwa na kuumia kwa Carolyne na inaahidi kuendelea kuwa nae bega kwa bega katika matibabu yake kwani bado yupo chini ya mkataba wa Miss Universe Tanzania kwa mwaka mzima.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe 31 mwezi wa Kumi na yalidhaminiwa na  Insignia, Golden Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Seif Kabelele Blog , Missie Popular blog, Urban Rose Hotel, na New York Film Academy.

HOTUBA KAMILI YA RAIS SAKATA LA ESCROW

$
0
0

Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kulihutubia taifa kwa kupitia wazee wa
Dar es Salaam jana.



HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DAR ES SALAAM,
TAREHE 22 DESEMBA, 2014

Shukrani
Mheshimiwa Makamu wa Rais;
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;
Viongozi wa CCM Mkoa;
Viongozi Wenzangu;
Viongozi wa Dini;
Wazee Wangu;
Wananchi Wenzangu;
Nawashukuru sana wazee wangu wa Dar es Salaam, kwa kukubali mwaliko wangu na kuja kuzungumza nami siku ya leo.  Natambua kuwa taarifa ilikuwa ya muda mfupi lakini mmeweza kuja kwa wingi kiasi hiki.  Naomba radhi kwamba ilikuwa tukutane Ijumaa lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu tukaahirisha mpaka leo. Asanteni sana kwa uvumilivu wenu.  
Kama mjuavyo, kila ninapoomba kukutana nanyi ninalo jambo au mambo muhimu kitaifa ambayo napenda kuzungumza nanyi, na, kwa kupitia kwenu taifa zima linapata habari.  Leo nina mambo mawili.
Wazee Wangu;
Kwanza kabisa, nataka kurudia kuwashukuru Watanzania wenzangu kwa moyo wenu wa upendo mliouonyesha kwangu katika kipindi chote cha matibabu yangu nikiwa nje na hata baada ya kurejea nchini. Kwa kweli nina deni kubwa kwenu.    Lazima nikiri kuwa, salamu zenu na taarifa kwamba watu wamekuwa wananiombea uponaji wa haraka na uzima zinanipa faraja kubwa na kunitia moyo.  Nadhani zimechangia sana kuifanya afya yangu kuendelea kuimarika kila kukicha.  Bado sijawa “fit” kabisa lakini naendelea vizuri. Hali yangu ilivyo sasa sivyo ilivyokuwa wiki iliyopita au siku niliporejea nchini.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Ndugu Wananchi;
Jambo la kwanza ninalotaka kulizungumzia leo ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita tarehe 14 Desemba, 2014 na jana tarehe 21 Desemba, 2014 katika maeneo ambayo uchaguzi huo uliahirishwa.  Bila ya shaka sote tumesikia taarifa ya awali ya zoezi la upigaji kura iliyotolewa na Mheshimiwa Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tarehe 17 Desemba, 2014.  Katika taarifa yake hiyo, Mheshimiwa Waziri alieleza kwamba kwa jumla zoezi limeenda vizuri kwenye maeneo mengi nchini.  Uchaguzi ulifanyika kwa ukamilifu katika Halmashauri 141kati ya 162.  Katika Halmashauri 21 uchaguzi wake uliahirishwa na umefanyika jana tarehe 21 Desemba, 2014.
Kwa jumla, katika maeneo mengi uchaguzi ulifanyika kwa salama na amani na hivyo kuwapa wananchi fursa ya kuchagua viongozi wanaowapenda kuongoza vijiji vyao, vitongoji vyao na mitaa yao.  Kufanyika kwa uchaguzi huu ni uthibitisho mwingine wa kuendelea kukomaa kwa demokrasia nchini.  Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wale wote walioshiriki katika uchaguzi huu kwa maana ya vyama vya siasa na wagombea.  Natoa pongezi maalum kwa walioshinda.  Nawaomba sasa wakae chini kutengeneza mikakati na mipango ya kuwaongoza wananchi wa maeneo yao katika kupata ufumbuzi wa changamoto za maendeleo na za maisha, zinazowakabili.
Ndugu wananchi;
Katika taarifa yake hiyo pia, Waziri Hawa Ghasia alielezea masikitiko yake kuhusu kasoro za uendeshaji wa zoezi zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali.  Aidha, aliahidi kuchukua hatua stahiki za kinidhamu dhidi ya watendaji na viongozi wa Serikali waliosababisha kasoro hizo.  Alifafanua kuwa miongoni mwa hatua zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, kusimamishwa kazi, kushushwa cheo, kukatwa mshahara au kupewa onyo.
Napenda kuelezea kufurahishwa kwangu na msimamo huo wa Waziri wa TAMISEMI na nampongeza kwa hatua alizochukua.  Namuunga mkono na namtaka aendelee na msimamo huo katika kukabili vitendo vya utovu wa nidhamu wa watumishi wa umma.  Lazima kila mtumishi wa umma ajue kuwa asipotimiza ipasavyo majukumu yake kuna adhabu inayolingana na kosa alilofanya.  Isitoshe, watu hao ndio watakaoendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwakani wakiwa mawakala na wasaidizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  Hivyo basi, kuwajibishwa wale waliozembea katika uchaguzi, itakuwa fundisho kwao na kwa wengine katika uchaguzi wa mwaka 2015 na chaguzi nyingine zijazo.
Ndugu wananchi;
Kwa upande wa ghasia, fujo na ugomvi uliotokea wakati wa zoezi la uchaguzi, nimezungumza na viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi na kuwataka kuhakikisha kuwa wale wote waliofanya vitendo vya kuvunja sheria wanatiwa nguvuni na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.  Nimewataka wasifanye ajizi na watu wa aina hiyo.  Hawa ni watu hatari ambao hawana budi kuchukuliwa hatua thabiti za kuwadhibiti na kuwaadabisha. Tusipofanya hivyo tunawakatisha tamaa raia wema na watiifu wa sheria.  Aidha, watu wakikamatwa na kuachiliwa muda mfupi baadae, wakati mwingine hata bila dhamana ya namna yo yote inawachanganya sana watu wema.  Isitoshe tutakuwa tunalea maradhi ya watu wabaya na kuwafanya waendelee kusumbua jamii.  Nimewakumbusha kuwa wasipokuwa wakali sasa  tunaweka mazingira ya hatari ya kuja kutokea mambo mabaya zaidi  mwaka ujao kwenye uchaguzi mkuu.

Baadhi ya wananchi waliojumuika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini
Dar es Salaam kusikiliza hotuba ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
Sakata la Akaunti ya Tegeta ESCROW
Ndugu Wananchi;
            Jambo la pili ninalotaka kulizungumzia si geni masikioni kwenu, nalo ni sakata la Akaunti ya Escrow ya Tegeta. Bila ya shaka mtakumbuka kuwa wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti mwezi Juni, 2014, kulitolewa madai kuwa fedha zilizokuwemo katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta iliyoko Benki Kuu zimechotwa kinyemela na mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power Solution (PAP) akishirikiana na Maafisa wa Serikali.
  Serikali iliahidi kufanya mambo mawili.  Kwanza, kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi wa Akaunti hiyo na kwamba taarifa yake itawasilishwa Bungeni.  Na, pili, kumuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa mwenendo mzima wa miamala katika Akaunti hiyo na kama kuna uhalifu wo wote uliopo kwenye mamlaka yake achukue hatua  zipasazo kwa mujibu wa mamlaka na madaraka aliyonayo.
Ndugu Wananchi;
            Yote mawili tuliyoahidi tumefanya.  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefanya ukaguzi wa miamala katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta iliyoko Benki Kuu na taarifa yake ilishawasilishwa Bungeni.  Pia niliagiza taarifa hiyo ichapishwe kwenye magazeti na tovuti ya Serikali ili watu waweze kuisoma. Agizo hilo nalo limetekelezwa. TAKUKURU  wameendelea na uchunguzi wao na watakapomaliza na kuridhika kuhusu makosa yaliyofanywa watawafikisha wahusika Mahakamani.  Mkurugenzi Mkuu wa PCCB alifika kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali na kutoa baadhi ya mambo kuhusu suala hili aliyoyaona ni muhimu Kamati iyajue.
Mambo Manne Makuu
Ndugu Wananchi;
            Tarehe 8 Desemba, 2014 nilipoanza kazi baada ya mapumziko ya ugonjwa nilikabidhiwa taarifa mbalimbali kuhusu sakata hili.  Tangu wakati huo nimekuwa nazisoma pamoja na kuzungumza na watu mbalimbali na kuagiza nipatiwe ufafanuzi wa mambo mbalimbali kutoka kwa wahusika.  Shabaha yangu ni kuyaelewa vizuri mambo hayo ili niweze kufanya uamuzi ulio sahihi na wa uhakika.  Nimebaini kuwa yapo mambo makuu manne:-
(a)    Akaunti ya ESCROW
(b)  Miliki ya PAP kwa IPTL
(c)   Kodi za Serikali,  na
(d)  Tuhuma za Rushwa
Akaunti ya ESCROW
Ndugu Wananchi;
            Katika Mikataba ya Kununua Umeme (Power Purchase Agreements) ambayo TANESCO imetiliana sahihi na kampuni binafsi za kuzalisha umeme za IPTL, SONGAS, SYMBION POWER na AGGRECO, kuna malipo ya namna mbili yanayofanywa na TANESCO.  Kwanza, hulipia umeme ilionunua kutoka kwa kampuni hizo yaani tozo ya umeme (energy charges). Na, pili hulipia gharama za uwekezaji uliofanywa na kampuni hizo, yaani tozo ya uwekezaji (capacity charges). Katika mikataba yote hiyo imekubaliwa kuwa iwapo kutatokea kutofautiana, au mzozo unaohusu uwekezaji, upo utaratibu wa usuluhishi. Utaratibu huo unataka kwanza kufanyike mazungumzo, wakishindwa kuelewana watafute mtu wa kuwashauri na kuwasuluhisha; wakishindwa kukubaliana wapeleke shauri lao kwenye Kituo (Mahakama) cha Kimataifa cha Usuluhisi wa Migogoro ya Uwekezaji, (International Centre for Settlement of Investment Disputes – ICSID) kilichopo London, Uingereza
Ndugu Wananchi;    
Mwaka 1998 TANESCO walifikisha kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji, London, malalamiko kwamba gharama za uwekezaji za IPTL ni kubwa mno kuliko kiasi halisi walichowekeza.  Mwaka 2001 Kituo cha Usuluhisi kilifanya uamuzi wa shauri hilo.  Madai ya TANESCO yalikubaliwa kuwa uwekezaji halisi uliofanyika ni Dola za Marekani 127 na siyo Dola milioni 163.17 walizodai IPTL.  Kutokana na kupungua huko kwa gharama za uwekezaji, tozo ya uwekezaji (capacity charges) nayo ilipunguzwa kutoka Dola za Marekani milioni 3.6 kwa mwezi mpaka Dola za Marekani milioni 2.6 kwa mwezi.  Kituo pia, kilitoa mwongozo kuhusu ukokotoaji wa tozo hiyo.
Ndugu Wananchi;
Miaka minne baadaye TANESCO ilianza vuguvugu la kutaka kupata nafuu zaidi.  Waliamua kugomea kulipa tozo ya uwekezaji kwa mkokotoo wa mwaka 2001.  Nimeambiwa kuwa wanasheria wa TANESCO walishauri Shirika hilo lidai ukokotoaji kiwango cha tozo ya uwekezaji wa IPTL ufanyike kwa kuzingatia thamani ya hisa walizolipia wawekezaji ambayo ni shilingi 50,000 badala ya kutumia msingi wa mtaji uliotokana na mkopo wa Dola za Marekani milioni 38.16 wa wanahisa uliotumiwa na usuluhisho wa kwanza ICSID-1.
Wakati wakisubiri mchakato wa usuluhishi wa mzozo huu mpya kuanza, pande zote mbili zilikubaliana kuanzisha Akaunti ya Escrow ya Tegeta. Tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ikaanzishwa kwa mkataba uliyotiwa sahihi na IPTL upande mmoja na Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya TANESCO upande mwingine.  Aidha, Benki Kuu iliteuliwa kuwa wakala wa kutunza akaunti hiyo nayo ilitia sahihi. 
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa mkataba huo, Kampuni ya IPTL iliendelea kupeleka madai ya tozo ya uwekezaji kwa TANESCO ambayo nayo iliwajibika kulipa madai hayo.  Malipo hayo yalitakiwa kupelekwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta tofauti na ilivyokuwa kabla ambapo yalipelekwa IPTL moja kwa moja.  Utaratibu huu mpya ulikubaliwa kutumika hadi pande mbili zitakapofikia mwafaka kuhusu kiwango cha ukokotoaji.    Kwa upande wa malipo ya gharama ya umeme (energy charges) TANESCO imeendelea kulipa moja kwa moja kwa IPTL bila kupitia Akaunti ya Tegeta ESCROW maana hizo hazikuwa na mgogoro. 
Ndugu Wananchi;
Kwa miaka saba tangu tarehe 5 Julai, 2006, akaunti hiyo ilipoanzishwa mpaka tarehe 5 Septemba, 2013, wakati Mahakama Kuu ilipokabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP, hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa tozo ya uwekezaji baina ya ITPL na TANESCO.  Pande mbili husika hazikuwahi kukaa kuzungumza na wala hakuna shauri lililofikishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Mogogoro ya Uwekezaji kama ilivyofanyika mwaka 1998.    
            Wakati wote huo, TANESCO iliendelea kulipa madai ya tozo ya uwekezaji ya IPTL na kupeleka malipo hayo kwenye Akaunti ya Escrow.  Ulipaji ulisimama katika kipindi kifupi wakati kampuni ya IPTL ilipowekwa kwenye ufilisi.  Kwa mujibu wa taarifa ya CAG, wakati akaunti hiyo inafungwa tarehe 20 Novemba, 2013, kulikuwa na fedha taslimu shilingi 8,020,522,330.37; Hatifungani zenye thamani ya shilingi 159,231,370,000 na Dola za Marekani 22,198,544. Fedha zote hizo ni sawa na shilingi bilioni 202.9.
Ndugu Wananchi;
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kama TANESCO ingelipa tozo ya uwekezaji ipasavyo, wakati huo Akaunti hii ingekuwa na shilingi bilioni 306.7.  Kwa sababu ya kutolipa fedha zote ipasavyo, wakati Akaunti inafungwa TANESCO walikuwa wanadaiwa na IPTL shilingi bilioni 103.8.    Kwa mujibu wa Mkataba wa Mauzo ya Umeme (PPA) malipo yaliyocheleweshwa, yanatozwa riba ya asilimia mbili ya fedha zote ambazo hazikulipwa kwa wakati.  Hivyo basi, riba iliyotokana na TANESCO kuchelewesha malipo ilikuwa Dola za Marekanimilioni 33.6.    
Ni matumaini yangu kuwa ufafanuzi uliotolewa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali unasaidia kuweka kumbukumbu sawa na sahihi kuhusu kiasi gani kilichokuwepo kwenye Akaunti ya ESCROW siku uamuzi wa Mahakama ulipofanya akaunti hiyo ifungwe.  Kwa kifupi Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaeleza kuwa Akaunti hiyo ilikuwa na shilingi bilioni 202.9 na siyo shilingi bilioni 306.7 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.  
Fedha za Nani
Ndugu Wananchi;
            Ni matumaini yangu pia kwamba maelezo haya kwa kiasi fulani yamesaidia kutoa jibu kwa swali maarufu la fedha za kwenye akaunti hii ni za nani?  Je ni za umma au za IPTL?  Pengine nianze kwa kuelezea Akaunti ya ESCROW ni nini?  Akaunti ya ESCROW ni tofauti na akaunti nyingine tunazozijua katika Benki zetu ambazo mtu anaweka fedha zake.  Kama tujuavyo, katika Benki zipo Akaunti za aina tatu ambazo wengi tunazifahamu na kuzitumia yaani Akaunti ya Akiba (Savings Account), Akaunti ya Hundi (Current Account) na Akaunti ya Muda Maalum (Fixed Deposit Account).  Akaunti ya Escrow ni akaunti maalum inayoanzishwa kwa ajili ya kufanya kazi maalum, kwa masharti maalum na kazi hiyo ikiisha akaunti yenyewe hufungwa.  Akaunti hiyo husimamiwa na wakala aliyeteuliwa kwa makubaliano ya wale wanaofungua akaunti hiyo.  Wakala ndiye mwenye jukumu la kusimamia akaunti na kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.  Kwa akaunti ya Escrow ya Tegeta pande mbili husika zilikubaliana kuwa Benki Kuu ndiyo iwe Wakala.  Ni muhimu kujua kuwa akaunti hiyo ingeweza kufunguliwa kwenye Benki yoyote siyo lazima BoT. 
Akaunti ya Tegeta ESCROW ilifunguliwa BoT mwaka 2006 kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya uwekezaji (capacity charges) zilizokuwa zinalipwa na TANESCO kabla hazijakabidhiwa kwa anayelipwa ambaye ni IPTL.  Kabla ya hapo TANESCO ilikuwa inalipa moja kwa moja kwa IPTL.  Kama  nilivyokwishasema, awali ilifanyika hivyo ili kutoa nafasi kwa pande hizo mbili husika kumaliza tofauti zao kuhusu kiwango cha tozo ya uwekezaji ya IPTL. 
Kimsingi basi, fedha hizi ni za IPTL kwani ndiye mlipwaji na ni malipo yanatokana na madai ya IPTL kwa TANESCO kuhusu tozo ya uwekezaji.  Hata hivyo, kwa mujibu wa CAG, inawezekana katika fedha hizo kuna fedha za umma.  Hi ni kwa namna mbili. 
Kwanza, kama mgogoro baina ya TANESCO na IPTL ungetatuliwa na kiwango cha tozo ya uwekezaji kupungua kama ilivyofanyika mwaka 2001 katika ICSID-1 na kama pande mbili husika zingekubaliana au kuagizwa kuwa punguzo hilo lianze kuhesabiwa tangu tarehe ilipofunguliwa Akaunti hiyo (tarehe 5 Julai, 2006), basi kungekuwepo pesa za kurejeshwa TANESCO.   Maadamu hili halikufanyika mpaka Mahakama ilipofanya uamuzi uliosababisha akaunti hiyo kufungwa.  Katika mazingira hayo fedha zote zinakuwa ni za IPTL maana hakuna madai ya TANESCO.
Ndugu Wananchi;
Namna ya pili ni ile ambapo katika fedha hizi kunaweza kuwepo fedha za umma na iwapo kuna kodi za Serikali ambazo hazijalipwa.  Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuthibitishwa na TRA ni kwamba kulikuwa na kodi ya VAT ambayo haikulipwa.  Nimeambiwa kuwa TANESCO ndiyo ilikuwa na wajibu wa kukata kodi hizo kabla ya kulipa madai ya IPTL lakini kwa baadhi ya malipo haikufanyika hivyo. Hivi IPTL inastahili kudaiwa kodi ya Serikali?  Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa, kodi inayotakiwa kulipwa na IPTL ni shilingi bilioni 21.7. IPTL wameshapelekewa madai na TRA, na IPTL wamekubali kulipa.
Katika ukaguzi wa Hesabu za TANESCO za mwaka 2012, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu fedha zilizopo kwenye Akaunti ya ESCROW kama ni fedha zao.  CAG aliwaambia TANESCO kwamba fedha hizo si zao.  

Maagizo hayo ya CAG yanasomeka kama ifuatavyo:
“As a result, the deposit balance in Escrow account does not meet the definition of an asset of the Company and therefore an adjustment has been made to de-recognize the asset and related liability to the tune of the amounts available in the Escrow account” 

Kwa tafsiri yake ni kuwa: “Hivyo basi, fedha zilizowekwa kwenye akaunti ya Escrow hazina sifa ya kutafsiriwa kama ni mali ya kampuni (TANESCO) hivyo, marekebisho yamefanywa ili kutotambua mali na madeni yanayohusu fedha hizo kwa kiasi cha fedha zilizopo kwenye akaunti ya Escrow.” 

Kutokana na maelezo haya ni dhahiri kwamba, fedha zilizokuwa kwenye Escrow siyo za TANESCO na hazikupaswa kuingizwa kwenye vitabu vya TANESCO kama mali yake. 
Chimbuko la Sakata
Wazee Wangu;
Chimbuko la kadhia yote hii Bungeni na kwenye jamii ni uamuzi wa tarehe 5 Septemba, 2013, wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuitambua PAP kuwa mmiliki halali wa IPTL na kuagiza Mfilisi akabidhi shughuli zote za IPTL kwa PAP.  Katika utekelezaji wa uamuzi huo wa Mahakama Kuu ukazuka  mjadala mkali kuhusu fedha zilizomo kwenye akaunti ya ESCROW kukabidhiwa kwa PAP.  Kwanza kabisa mjadala ulikuwa ndani ya Serikali miongoni mwa viongozi na watendaji wa Wizara na Taasisi zinazohusika moja kwa moja na akaunti hiyo.  Hizi ni Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO na Benki Kuu.  Viongozi na Watendaji husika walikuwa wanajiuliza na kuuliza kama walipe au wasilipe.  Walipotaka ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakaelekezwa watekeleze uamuzi wa Mahakama Kuu.  Alisema uko sawa na hauna matatizo.  Halikadhalika, Benki Kuu walipoulizia kuhusu kodi za Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza kuwa hakuna kodi ya kulipwa.
Kwa kuzingatia ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, malipo yakafanyika kwa IPTL tena bila ya kodi kulipwa.  Baada ya malipo kufanywa ndipo mjadala huo ukahamia katika jamii na Bunge na kugeuka kuwa kadhia kubwa iliyochukua sura ya kashfa yenye dalili za rushwa na wizi. 
Uamuzi Unaotiliwa Shaka
Wazee Wangu na Ndugu Wananchi;
Kwa jumla uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu akaunti ya Escrow, ushauri wa Mwanasheria Mkuu kwa Serikali wa kuelekeza uamuzi huo utekelezwe na viongozi wa Serikali kutekeleza ushauri huo vimetiliwa shaka.  Umeonekana kuwa haukuwa uamuzi sahihi na kwamba umeitia hasara nchi.  Isitoshe uamuzi huo umeibua hisia za kuwepo harufu na vitendo vya rushwa. Wapo waliosema si bure iko namna!  Wapo waliotaja majina na watu wanaodai wamepata mgao wa Escrow tena wengine wamechukua fedha kwa viroba, sandarusi na rumbesa.  Bahati mbaya sana katika mjadala ilijengeka dhana isiyokuwa sahihi kwamba jambo hili lilianzishwa na Maafisa hao wa Serikali kwa nia ya kujinufaisha wao binafsi.  Ukweli ni kwamba uamuzi ulifanywa na Mahakama Kuu na kwenye Serikali ilikuwa utekelezaji wa amri hiyo.
Wazee Wangu;
Nilipokutana na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata maoni yake kuhusu kadhia hii ameendelea kusema alichosema Bungeni kuwa hakukosea katika ushauri wake na wala Mahakama haikufanya makosa.  Hivyo basi, hakuona sababu ya kwenda Mahakamani kuomba marekebisho ya uamuzi wa Mahakama kuhusu fedha zilizokuwepo kwenye akaunti ya Escrow ya Tegeta kukabidhiwa kampuni ya PAP mmiliki wa IPTL.  Vilevile haoni kama kuna hasara yo yote ambayo nchi imepata kwa sababu fedha zile ni za IPTL na imelipwa IPTL. 
Akifafanua, alisema kuwa akaunti ya Escrow ilianzishwa kwa ajili ya kutunza fedha za malipo ya tozo ya uwekezaji kwa IPTL yaliyokuwa yanafanywa na TANESCO.  Kabla ya mzozo kuhusu ukokotoaji wa tozo hiyo na kuanzishwa kwa akaunti ya Escrow ya Tegeta, TANESCO ilikuwa inalipa tozo ya uwekezaji moja kwa moja kwa IPTL.  Baada ya kutokea mzozo na akaunti kuanzishwa mambo mawili hayakubadilika.  Kwanza kwamba IPTL haikuacha kupeleka madai ya tozo ya uwekezaji kwa TANESCO.  Na, pili, kwamba TANESCO haikuacha kulipa madai hayo.  Mdai na mdaiwa hawakubadilika.  Kuwepo kwa akaunti ya Escrow hakubadili mwenye fedha zake.  Akaunti hiyo iliundwa kuhifadhi fedha za IPTL wakati suluhu inatafutwa kuhusu kiwango cha tozo.  Matumaini ni kwamba kama kiwango kitapunguzwa, TANESCO inaweza kupata nafuu ya malipo. 
Kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu kuruhusu IPTL ilipwe fedha za akaunti ya Escrow, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema ni uamuzi sahihi na wala taifa halikupata hasara kwa sababu pesa zimelipwa IPTL na siyo mtu mwingine.  Isitoshe anaona uamuzi wa Mahakama umeisaidia TANESCO kutua mzigo mkubwa iliyokuwa nao kwa miaka saba.
            Kama mjuavyo, akaunti ya Escrow ilianzishwa kuhifadhi pesa za malipo ya tozo ya uwekezaji ya IPTL.  Ilianzishwa kwa matumaini kuwa TANESCO watapata nafuu ya tozo ya uwekezaji.  Lakini, hapakuwahi kufanyika mazungumzo baina ya TANESCO na IPTL kuhusu jambo hilo na wala suala hilo halijafikishwa ICSID.  Haikuweza kufanyika hivyo kwa sababu washauri wa kisheria wa TANESCO hawajafanya hivyo.  Wapo wanaodai kuwa hawafanyi hivyo kwa sababu hakuna sababu mpya zinazoweza kupatikana kuifanya ICSID ibadili uamuzi wake wa 2001 kuhusu kiasi cha tozo na namna ya ukokotoaji wake.
            Matokeo yake ni TANESCO kuwa na akaunti ya Escrow ambayo mwisho wake haujulikani.  TANESCO inaendelea kudaiwa na IPTL tozo ya uwekezaji na kulazimika kulipa kwenye akaunti hiyo.  Kwa masharti ya akaunti ya Escrow wanaposhindwa kulipa wanatozwa riba.  Kwa mujibu wa taarifa ya CAG mpaka tarehe 20 Novemba, 2013, TANESCO ilikuwa inadaiwa shilingi bilioni 103.8ambazo hawajalipa kwenye akaunti ya Escrow na riba ya Dola za Marekani milioni 33.  Kwa sababu hiyo basi uamuzi wa kufunga Akaunti ya Tegeta Escrow unalipatia unafuu TANESCO dhidi ya kulimbikiza madeni na riba.
            Kwa upande wa kodi za Serikali ambazo hazikulipwa, Mheshimiwa Jaji Werema alisema yeye alitoa ushauri tu.  Hata hivyo, kama mamlaka husika inaona zipo kodi zinazostahili kulipwa izidai.  Hakuna kilichopotea kwa sababu anayedai, yaani TRA yupo, na mdaiwa yupo, IPTL.
Uamuzi wa ICSID II Kuhusu Tozo ya Uwekezaji
Wazee Wangu;
Yalitolewa mawazo kuwa kama fedha za akaunti ya Tegeta Escrow zingelipwa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji (ICSID II) kutoa uamuzi wake, TANESCO ingepata nafuu ya kupungua kwa tozo ya uwekezaji.  Kuhusu jambo hilo nimeambiwa kwamba kuna mambo mawili ya msingi.  Kwanza kwamba Mahakama hiyo haikutoa viwango vipya vya tozo kama ilivyofanya mwaka 2001 kwenye ICSID–I.   Haikubadili mwongozo wa ukokotoaji wa tozo.  Imesema madai yanaweza kuzungumzwa na kusisitiza kuwa katika mazungumzo hayo TANESCO watambue kwamba wanahisa waliwekeza mtaji wao binafsi wakati wa kununua mtambo na pia walikopa madeni, na kwamba kiasi cha fedha walichowekeza kilitakiwa kiwe na kiwango cha juu zaidi cha faida.
Jambo la pili ni kwamba, shauri hili la pili la ICSIDI II halikuihusisha kampuni ya IPTL mwenye Mkataba wa Kuuza Umeme na TANESCO na siyo Benki ya Standard Charterd.  IPTL wameweka pingamizi la utekelezaji wa uamuzi wa shauri hilo hapa nchini, hivyo inakuwa vigumu kwa TANESCO kufanya mazungumzo kwa msingi wa shauri hilo.
Kinga Dhidi ya Madai
Wakati wa kufunga akaunti ya Escrow, upande wa Serikali ulielezea hofu yake ya uwezekano wa siku za usoni mtu kudai tena kulipwa fedha hizi hizi ilizolipwa PAP.  Nimeambiwa kuwa suala hilo haliwezi kutokea kwani limetengenezewa wigo imara wa kimkataba kuzuia.   PAP imetiliana sahihi na Serikali kwamba iwapo kutatokea mdai yo yote PAP itawajibika kulipa.
Mashaka ya Miliki ya PAP kwa IPTL
Ndugu Wananchi;
            Hofu nyingine kuhusu uwezekano wa Serikali kupata hasara ni yale madai kuwa huenda miliki ya PAP kwa asilimia 70 za hisa za IPTL zilizokuwa za kampuni ya Mechmar Berhard ya Malaysia siyo halali.  Pale mwanzoni ilidaiwa kuwa kampuni ya Mechmar ilipouza hisa zake kwa kampuni ya Piper Link ya British Virgin Islands ilikuwa chini ya mchakato wa ufilisi kule Malaysia.  Kama ingekuwa hivyo, kisheria mtu hawezi kuuza hisa zake akiwa kwenye mazingira hayo.  Katika uchunguzi wa CAG alieleza kuwa amethibitisha kwamba madai hayo si kweli,  Mechmar walipouza hisa zao tarehe 9 Septemba, 2010 kampuni haikuwa kwenye ufilisi.  Iliingia kwenye mchakato wa ufilisi mwaka 2012.
            Lakini kwa upande wa kampuni ya Piper Link ya Uingereza inasemekana iliuza hisa hizo baada ya kuwa wamepokea amri ya Mahakama ya Malkia ya BVI kuizuia isiuze hisa hizo.  Je ni kweli?  Imefanyika hivyo?  Kama ni kweli je PAP waliponunua hisa hizo walijua kama kuna zuio au hapana?  Kama walijua basi na wao ni sehemu ya njama za kufanya udanganyifu.   Kama hawakuwa wamejua basi wametapeliwa.  Nimeagiza uchunguzi wa kina ufanyike kupata ukweli.  Natambua hivi sasa Mahakamani zipo kesi zinazohoji uhalali wa PAP kumiliki asilimia 70 za hisa za Mechmar Berhad.  Uchunguzi wetu hautaingilia mchakato huo lakini unaipa Serikali fursa nzuri ya kuchukua hatua zipasazo kuhusu suala hili lenye mjadala mkubwa.             Jambo lingine muhimu ambalo limeleta matatizo kwa Mahakama zetu nchini na BRELA ni uuzaji wa hisa za IPTL au kuwekwa rehani hisa hizo bila ya uamuzi huo kusajiliwa BRELA na kwenye Mahakama zetu.   Sheria zetu ambazo ndizo za nchi ya Jumuiya ya Madola kama ilivyo kwa Hong Kong, Malaysia, na BVI, inaitaka kampuni ya Piper Link ya BVI iliponunua hisa za Mechmar katika IPTL kusajili BRELA ununuzi huo.  Hali kadhalika, inaitaka SCB ya Hong Kong na kupata amri ya Mahakama kuzuia deni la Mechmar na kuwekwa dhamana ya hisa za Mechmar katika IPTL.  Piper Link isiuze hisa 70 za Mechmar katika IPTL.  Walitakiwa wasajili na BRELA na Mahakama yetu.  Kutokufanya hivyo ndiko kunazua maneno mengi na mzozo kuhusu uuzaji wa hisa hizo kwa PAP.  Kwa SCB wanapata usumbufu wa kudai madeni yao IPTL kwa sababu hiyo hiyo.  Uchunguzi utakaofanyika utapata ukweli wa yote kwa uhakika.   
Ndugu Wananchi;
            Taarifa niliyopewa wakati najiandaa kuzungumza nanyi ni kuwa katika  Mahakama zetu nchini kuna mashauri yahusuyo miliki ya PAP ya hisa 70 zilizokuwa za Mechmar katika IPTL na yapo mashauri yahusuyo PAP kupewa fedha za akaunti ya Escrow.  Zipo pia nyingine za masuala mbalimbali yakiwemo mashauri yaliyofunguliwa na PAP dhidi ya watu, na makampuni binafsi na vyombo vya Serikali.  Naamini uamuzi wa Mahakama zetu utatoa majibu kwa masuala yote hayo.
            Pamoja na hayo yatakayokuwa yanaendelea Mahakamani, Serikali itaendelea kufanya uchunguzi wake na kuamua namna ya kushughulikia taarifa zitakazopatikana ili nayo iweze kwenda Mahakamani itakapolazimu kufanya hivyo. 
            Jambo lingine muhimu nataka uchunguzi wa kina ufanyike ni kujua nani ni nani katika uuzaji na ununuzi wa hisa za Mechmar.  Hususan nataka tujue kwa ukweli na uhakika hisa hizo zimeuzwa kwa bei gani.  Je, ni kweli gharama zinazosemwa  ndizo zenyewe?  Nataka kuthibitisha ukweli huo ili tujue kodi yetu ya ongezeko la mtaji (Capital Gains Tax) inayostahili kulipwa Tanzania ni kiasi gani? Je kiasi gani kimelipwa na kipi hakijalipwa ili kidaiwe? 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mbunge wa Kionondoni Iddi
Azzan muda mfupi baada ya kulihutubia taifa kwa kupitia wazee wa
Dar es Salaam.

Tuhuma za Kuwepo kwa Harufu ya Rushwa
Wazee Wangu;
            Kumekuwepo na tuhuma za vitendo vya rushwa katika mchakato mzima wa kufunga akaunti ya Escrow na kukabidhi fedha hizo kwa kampuni ya PAP.  Halikadhalika, kumekuwepo na hisia hizo hizo kwa upande wa jinsi kampuni ya VIP Engineering and Marketing ilivyotumia pesa zake zilizoko kwenye Benki ya Mkombozi.  Yamesemwa mengi sana na mmeyasikia na kuyasoma. 
            Rushwa ni kosa la kijinai ambalo kwa Serikali yetu ni kosa ambalo ni vigumu kulivumilia wala kulifumbia macho.    Mara baada ya kupata fununu za uwezekano wa vitendo hivyo kufuatia taarifa ya awali ya CAG ya kwenda kukagua miamala, niliagiza taarifa husika zifikishwe kwenye Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa (PCCB) kwa uchunguzi zaidi.  Naambiwa taarifa hizo zimefika na kazi ya uchunguzi inaendelea.  Tayari watu kadhaa wamehojiwa na wengine wanaendelea kuhojiwa.  Wakati nawasihi wananchi kuvuta subira ili tuwape nafasi PCCB wakamilishe kwa ufanisi wa hali ya juu kazi yao waliyokwishaianza, nawaomba PCCB waongeze kasi ya uchunguzi.  Napenda kufafanua kwamba kwa upande wa miamala iliyotoka katika akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Marketing ya Ndugu James Rugemalila, Serikali inashughulika na watumishi wa umma kwa kuzingatia Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma, maana suala lao ni la kimaadili.  Hatuwahoji wasiokuwa watumishi wa umma. 
Maazimio ya Bunge
Ndugu Viongozi;
Wazee Wangu;
Ndugu Wananchi;
            Niliona nianze kwa kutoa maelezo hayo ya utangulizi kabla ya kuyazungumzia maazimio ya Bunge.  Serikali imepokea maazimio hayo ya Bunge na kuyafanyia kazi kwa ajili ya utekelezaji wake.  Nawapongeza Wabunge wetu kwa moyo waliouonesha wa kuchukia maovu na kutaka yashughulikiwe ipasavyo.  Napenda kuwahakikishia kuwa niko pamoja nao.  Nampongeza Mheshimiwa Anna Makinda, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, Naibu Spika na Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Mussa Zungu kwa uongozi wao mahiri.  Hakika haikuwa kazi rahisi, lakini chini ya uongozi wao mambo yameisha salama na tumepata maazimio nane yanayozungumzika na kutekelezeka.  Nawashukuru na kuwapongeza sana Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), chini ya uongozi wa Mheshimiwa Zitto Kabwe na Mheshimiwa  Deo Filikunjombe na pia Wajumbe waliounda Kamati ya Mapendekezo kwa kufikia mwafaka wa mapendekezo haya 8 ambayo yaliazimiwa na Bunge. 
Mwisho lakini si ya mwisho kwa umuhimu, nawapongeza Wabunge wote kwa michango yao mizuri.  Jambo lililonifurahisha sana ni ushirikiano wa Wabunge wa kambi zote katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili muhimu,.  Hivi ndivyo inavyotakiwa Bunge liwe.  Kwa kweli lazima nieleze mshangao wangu niliposikia kambi ya upinzani ikijaribu kufanya maamuzi yale ni yao wao na wenzao hawamo.  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ina Wajumbe 19wa CCM na wa Upinzani 5. Bunge lina Wabunge wa CCM asilimia 74 na wa upinzani asilimia 26. Hivi kama ni yao wao pekee na wa upande wa CCM wangepinga yangekuwa?  Yasingefika po pote, yangefia kwenye Kamati.  Huku ni kutafuta umaarufu kwa mgongo wa wengine.  Na, Wabunge wengi wa CCM na nyie semeni msikike kwa uamuzi mliyofanya wote.
              Napenda kuwahakikishia kuwa mimi na wenzangu Serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kutekeleza yale maazimio yanayoangukia katika dhamana yetu.  Napenda kuainisha mtazamo na mwelekeo wa Serikali katika utekelezaji wa maazimio hayo manane kama ifuatavyo:-

Azimio la kwanza:  Serikali iangalie uwezekano wa kuchukua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa mujibu wa Sheria za nchi.
Pendekezo tumelipokea, ni jambo linalowezekana kufanya.  Hata hivyo, tunapopima ujumbe tunaoupeleka kwa jumuiya ya wawekezaji tunachelea kuwa inaweza kuleta hofu na kuwatisha wawekezaji waliopo  na wajao.  Nalisema hivyo kwa sababu sisi tuna historia ya kutaifisha mali za kamapuni binafsi.  Hofu hiyo bado ipo.  Tukichukua mitambo hii tunaweza kurudisha hofu za kurudi tulikokuwa na kukimbiza mitaji tunayohitaji kwa uchumi kukua na nchi kupata maendeleo.  Nashauri tuendelee kuyapatia ufumbuzi matatizo ya IPTL kila tunapoyabaini.   Aidha, Mahakama imetusaidia sana kwa kuamuru mitambo ya IPTL ibadilishwe ili itumie gesi asilia na kutoza bei ya umeme isiyozidi senti nane za Marekani. Tuyafuatiliye haya kwanza.

Azimio la Pili:  Azimio hilo linazungumzia kuhusu uwazi wa Mikataba linasomeka ifuatavyo:  “Bunge limeazimia kwamba Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti.  Serikali iwasilishe taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba ya umeme”.
Azimio hili tumelipokea na tunaangalia namna bora ya kulitekeleza ili kuweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja.  Kwanza, kuitikia kilio cha muda mrefu kuhusu uwazi katika mikataba ambayo Serikali inaingia na wawekezaji; na pili kuhakikisha usiri wa mikataba hiyo ambayo ni haki ya wawekezaji hao dhidi ya washindani wao inazingatiwa.  Serikali na Bunge tutakaa chini hivi punde kutafuta namna bora ya kisheria na tutafanya hivyo kwa kujifunza pia kutokana na uzoefu wa nchi ambazo zina utaratibu wa aina hii.

Azimio la Tatu:  Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama vichukue hatua stahili kwa mujibu wa sheria za nchi yetu dhidi ya watu waliotajwa kwenye taarifa maalum ya Kamati husika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya ESCROW, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusu kuhusika kwao katika vitendo hivyo vya jinai”
             Vyombo husika vimekwishaagizwa kufanya hivyo na kazi imeanza na inaendelea.  Ikiwa wapo watu wenye makosa hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Azimio la nne:  Linasomeka, “Kamati za Bunge kuwavua nyadhifa zao wenyeviti wa Kamati za Bunge waliotajwa kupewa fedha na kampuni ya VIP Engineering kabla ya kikao kijacho cha Bunge”
            Azimio hilo liko chini ya mamlaka ya Bunge lenyewe.  Nawaachia wao waamue.

Azimio la Tano:  Linasomeka; “Bunge linaazimia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania”
            Azimio hili nimelipokea, tumelijadili hata hivyo, itabidi tufuate utaratibu wa kikatiba na kisheria wa kushughulikia masuala ya namna hiyo.  Inatakiwa suala kama hili lianzie kwenye Mhimili wa Mahakama yenyewe na siyo kwa Rais au Bunge.  Tume ya Mahakama ndiyo yenye mamlaka ya kumtaka Rais aunde Tume ya Kijaji ya kumchukulia hatua Jaji yeyote pale inaporidhika kuwa amepoteza sifa za kuendelea kufanya kazi hiyo.  Nashauri suala hili tumuachie Jaji Mkuu wa Tanzania alishughulikie atakavyoona inafaa. 

Azimio la Sita:  “Bunge linaazimia kwamba mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Ltd. na benki yeyote itakayogundulika kufuatia uchunguzi wa mamlaka ya uchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika akaunti ya ESCROW kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (Institutions of money laundering concerns).
            Pendekezo la Bunge ni zuri kwamba mamlaka husika na udhibiti wa vitendo vya utakatishaji fedha vifanye uchunguzi kwa mujibu wa Sheria.  Serikali imelipokea na mamlaka husika yaani Financial Intelligence Units kulishughulikia.  Naamini wameshaaza, tuwape muda watimize wajibu wao kwa mujibu wa sheria. 

Azimio la Saba:  “Bunge liliazimia kwamba Serikali iandae, na kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria iliyounda TAKUKURU kwa lengo la kuanzishwa Taasisi mahsusi itakayoshughulikia kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
            Kazi ya kufanya mageuzi katika TAKUKURU inaendelea.  Tayari Sheria mbalimbali zimetungwa ikiwa ni pamoja na Sheria Mpya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2008, Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Fedha Haramu ya mwaka 1991 ambazo zote zinaweka utaratibu wa kushughulikia vitendo vya rushwa.  Tutaendelea kuziboresha sheria hizo kwa kadri itakavyohitajika.  Kazi iliyopo mbele yetu ni kuimarisha usimamizi wa sheria hizo.  Jambo hilo nalo litazingatiwa katika maboresho hayo.  Ni dhamira yangu na ya Serikali ninayoiongoza kupambana na kushinda  vita dhidi ya rushwa.  Kwa hiyo tuko tayari kulifanyia kazi pendekezo lolote linaloimarisha dhamira yetu hii njema.

Azimio la nane:  “Bunge linaazimia kwamba Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi na Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.
            Azimio hili ndilo Azimio ambalo limevuta hisia za watu wengi, na pengine ndilo ambalo utekelezaji wake unasubiriwa kwa hamu.  Utekeelzaji wake umeanza.  Kwanza, ni kuhusu Bodi ya TANESCO,   tumeanza mchakato wa kuunda Bodi mpya kwani iliyopo imemaliza muda wake.  Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,  kwa vile ni mtumishi wa umma anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshajiuzulu.  Tumelitafakari suala la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi la kupokea fedha kutoka VIP Engineering and Marketing ambazo kwa maelezo yake ni kwa ajili ya shule anayoimiliki na kuiendesha.  Mwenyewe ameeleza wazi kupitia vyombo vya habari. Pamoja na hayo yapo mambo ya msingi kimaadili ambayo hayakuzingatiwa, hivyo tumemwomba atupishe tuteue mwingine.  Kuhusu Prof. Muhongo nimemuweka kiporo, kuna uchunguzi niliagiza ufanywe na vyombo vyetu bado nasubiri taarifa hiyo ili nifanye uamuzi ndani ya siku chache zijazo. 

Hitimisho
Wazee Wangu;       
            Nawashukuruni kwa kunisikiliza.


OLOLOSOKWAN WAJIWEKA TAYARI KUTIMIZA NDOTO YA KIJIJI CHA DIJITALI

$
0
0
DSC_0010

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliposimama kwenye Kijiji cha Ngeresero kwa ajili ya kuwaungisha wanawake wa kimasai wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali za shanga kwa watalii wanaosimama kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali, wakati akielekea kijiji cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake la UNESCO.

Na Mwandishi wetu, Arusha

NDOTO ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili kutoka kampuni ya Samsung Electronics.

Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano mwakani.

Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.

Akizungumza na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan , Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya dijitali.

DSC_0007

Alisema mambo ambayo wanastahili kuyaweka sawa ili kufanikisha ndoto zao kuhakikisha eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi ipo ni lazima lisajiliwe kisheria ili kusiwepo na tatizo katika siku za usoni.

Aidha kutokana na ukubwa wa mashine zinazohusika, hasa makontena ni vyema wanakijiji wakaangalia maeneo korofi katika barabara za kuelekea huko na kuzirekebisha, ili magari hayo makubwa yenye vifaa yapite kwa usalama.

Alisema mradi huo wa miaka mitatu unatarajia kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kuwa na ujasirimali, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika mawasiliano na utafutaji wa masoko, elimu na afya.

Kwa mujibu wa Bi. Rodrigues kijiji hicho pia kitakuwa na shule iliyoungwa na mtandao wa kompyuta duniani (intaneti), kliniki ya kisasa, tiba kwa kutumia teknolojia ya kompyuta na jenereta kubwa linalotumia nishati ya jua.

DSC_0019

Bw. Abdulaziz Ali wa kitengo cha Transportation and Logistic kutoka UNESCO akitafsiri bei za bidhaa hizo za kimasai kwa wakimama hao wanaofanya biashara za urembo wa shanga kwa watalii na wazawa wanaopita katika kituo kijiji hicho ambapo wengine wao husimama kupata huduma ya chakula na vinywaji.

Aidha kuwapo na mtandao wa kompyuta kutawezesha UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha mtaala utakaowawezesha vijana wa kimasai ambao ni wafugaji kupata elimu wanayoihitaji.

Mwakilishi huyo wa UNESCO amesema kwamba amefurahishwa na namna watu walivyoitikia mradi huo ambao umelenga kubadili maisha ya wafugaji hao kwa kuwawezesha pia kuitumia vilivyo sekta ya utalii.

“Kupitia mradi huu wananchi wanaweza kujifunza kusoma, kupata maarifa na katika harakati hizo kujua lugha ya kiingereza ili kuwasaidia kuwa na mawasiliano na watalii na watu wengine”, alisema Rodrigues.

DSC_0038

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwasili kwenye kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan na kupokelewa na diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.

Alisema ni nia ya Unesco kuhakikisha kwamba inasaidia kufuta ujinga miongoni mwa wafugaji hao bila kuathiri utamaduni wao wanapoingia katika maisha ya kisasa.

Kijiji cha digitali cha Ololosokwan kitakuwa cha nne barani Afrika na yapo makubaliano ya msingi kwamba kijiji kingine kitajengwa Zanzibar mwakani.

DSC_0039

Diwani wa kata ya Ololosokwan, Bw. Yannick Ndoinyo akiongozana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyefika kijijini hapo kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNESCO pamoja na kukagua eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kijiji cha digitali cha Samsung.

DSC_0048

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisalimiana na baadhi ya kinamama wa mradi wa utalii unaofadhiliwa na shirika la UNESCO kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

DSC_0063

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza na wakina mama wa kimasai waliojumuika na waume zao mara baada ya kuwasili kijijini hapo ambapo aliwaasa kushiriki elimu ya afya ya uzazi wa mpango ili waweze kuzaa watoto wachache watakaoweza kuwahudumia na aliwaahidi kuwaanzisha program ya kusoma na kuandika kwa ajili ya kuboresha mawasiliano yao na watalii wanaotembelea kijiji chao na kununua biashara zao.

DSC_0111

Pichani juu na chini ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwaonyesha jambo wakina mama wa kimasai jinsi gani teknolojia inayvowaleta watu kwa ukaribu zaidi kupitia "Tablet" ambapo katika kijiji hicho cha digitali cha Samsung wakazi wa eneo hilo watakua wakipewa mafunzo kutumia kifaa hicho cha "Tablet".

DSC_0129

DSC_0192

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo nje ya maktaba inayofadhiliwa na UNESCO na kuwanufaisha wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo kupanua uelewa zaidi kwa kusoma vitabu mbalimbali wakati akikagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake. Kushoto ni Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo.

DSC_0356

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa juu wa halmashauri ya kijiji wakati wa ziara yake kijijini hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

DSC_0422

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na uongozi wa halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan mara baada ya mazungumzo.

DSC_0427

Bi. Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

DSC_0432

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues katika picha ya pamoja na wakina mama wa kimasai wa kata ya Ololosokwan kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha mara baada ya kikao na halmashauri ya kijiji hicho.

DSC_0440

Bi. Zulmira Rodrigues akiagana na baadhi ya wakinamama wa kimasai mara baada ya kikao cha halmashauri ya kijiji hicho.

DSC_0228

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) akifafanua jambo wakati wa kukagua eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi itawekwa kwenye sehemu iliyotengwa na halmashauri ya kijiji kwa ajili ya kijiji cha dijitali cha Samsung. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya RAMAT, Pokare Koitumet, Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ndoinyo pamoja na Chifu wa kijiji cha Ololosokwan kata ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.

DSC_0204

Muonekano wa eneo hilo huku Bi. Zulmira Rodrigues akiendelea kulikagua.

HII NDIO RATIBA YA SKYLIGHT KUANZIA MKESHA WA KRISMAS

$
0
0
10675565_408778115946839_5013196848087740184_n

24.12.14 Mkesha wa XMASS tutakua ESCAPE1, show itaanzaa saa mbili usiku, kiingilio buku 7000/= tu: tukutane ESCAPE1 tuikaribishe XMASS

Vile vile tunapenda kutoa taarifa na kuwaomba radhi wadau wetu kutokana na safari yetu ya kanda ya ziwa XMASS hii, show zetu za ijumaa tarehe 26.12.14 thai village na jumapili 28.12.14ESCAPE1 hazitofanyika.

Ila tukutane tena kwenye mkesha wa mwaka mpya 31.12.14 ndani ya ESCAPE1. .. Burudika na bendi yako katika msimu huu wa siku kuu...Skylight Band...just follow the light ♫

 

katibu mkuu nishati na madini asimamishwa kazi

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


maswi
PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi,  Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014

LEO ni Birthday party ya Asia Idarous Khamsin ..Ndani ya M.O.G Bar

$
0
0

WABUNIFU wa Mavazi wachanga na chipukizi wamemwandalia Sherehe za kuzaliwa ya Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin, zitakazofanyika usiku wa Desemba 24, ndani ya ukumbi wa M.O.G Bar (Nyumbani Lounge) huku ikisindikizwa na Spice Modern Taarab pamoja na Mini fashion show.
Katika usiku huo maalum, kiingilio ni sh 5,000, huku vazi maalum likiwa Black & White, ambapo pia wadau watakaojumuika na Mama wa Mitindo, watapata burudani kali ya muziki kutoka kundi hilo la Spice Modern taarab, Dj Mapuu pamoja na  shoo ya ubunifu wa mavazi (Min fashion show) itakayopambwa na wabunifu wanaochipukia.
Usiku huo wa Black &White Bash 55th Asia Idarous Khamsin, pia itakuwa na Red Carpet na wadau watapiga picha na mastaa mbalimbali sambamba na pongezi za kunyakua tuzo ya ‘Life Time Achievement Swahili Fashion Week 2014’.
Source:  Andrew Chale


JK awapa big high Nassib Andul al maarufu Diamond, mshindi wa BBA

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amewapongeza mwanamuziki Nassib Abdul maarufu kwa jina la Diamond na Mshindi wa Shindano la Big Brother Africa, Idris Sultan kwa kuiletea sifa Tanzania kupitia sanaa.
Rais Kikwete ametoa Pongezi hizo alipokutana na Msanii Diamond Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014 , ambapo Msanii huyo amemwonyesha tuzo tano alizoshinda baada ya kupambanishwa na wasanii wengine wa Afrika.
Pamoja na pongezi hizo kwa  Diamond na Idris kwa kile alichosema wameitoa nchi kimasomaso, Rais Kikwete amewasihi wasanii hao kujihadhari na athari za umaarufu na utajiri katika umri mdogo,zikiwemo kujitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya na ulevi.
Kikwete amewaasa kuwa ni muhimu kwa wasanii hao kutumia mapato wanayoyapata katika kazi zao za usanii kwa kujijenga kifamilia ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba zao za kuishi na wanafamilia wanaowategemea pamoja  kuwasaidia wasanii wenzao.
“Umaarufu katika sanaa yoyote ile ni wa kupita hivyo tumieni umaarufu mlio nao sasa kama fursa ya kujijenga kimaisha na sio kutumbukia katika kadhia za kidunia kama vile ulevi, ukorofi mbele ya jamii na mambo mengine yasiyofaa", aliwaasa Mhe. Rais.
Rais Kikwete pia alimpongeza Sultan  kwa kuiletea Tanzania sifa na kumtakia mafanikio zaidi katika shughuli zake za baadaye. Rais Kikwete alisema kuwa Sultan hakuifedhehesha Tanzania kwa kutofanya mambo yaliyo kinyume na maadili ya Mwafrika alipokuwa katika jumba la Big Brother Africa.
Kwa upande wake,Diamond amemshukuru na kumpongeza Rais Kikwete kwa ushirikiano anaoutoa kwa wasanii hapa nchini, hali ambayo amesema ndiyo  iliyowawezesha kupata mafanikio kitaifa na kimataifa.
Diamond pia amemuahidi Rais Kikwete kutekeleza yote aliyomuasa kuhusu kujiheshimu na kutolewa umaarufu alionao, na kwamba ataendelea kufanya kazi zake za usanii wa Muziki kwa juhudi zake zote  kuitangaza nchi.
Msanii huyo pia amemweleza Rais Kikwete kuwa hivi karibuni atapokea tuzo nyingine ya sita kutoka huko Nigeria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014


Uchaguzi wa serikali za mitaa CCM yashinda kwa kishindo

$
0
0

katibu mkuu tamiseni Sagin akizungumza leo

SERIKALI imetangaza matokeo ya jumla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi mkubwa.

Kulingana na matokeo hayo kwa upande wa wenyeviti wa vijiji CCM imeshinda kwa asilimia 79.8, Wenyeviti wa vitongoji CCM imeshinda kwa asilimia 79.3, Wenyeviti wa mitaa asilimia 66.6, wajumbe wa serikali
za vijiji na mitaa asilimia 80.2 na wajumbe wa viti maalum asilimia 82.3.

Katika uchaguzi huo Watanzania 18,716,281 walitarajwa kujiandikisha kupiga kura ambapo waliojandikisha ni 11,598,776 sawa na asilima 62.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Serikali za mitaa Khalist Luanda alisema  uchaguzi wa mwaka huu umekuwa nahamasa kubwa ya watu kujandikisha na kupiga kura tofaut na uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2009 ambapo walioandikishwa ni asilimia 48
ya matarajio.

Pia alisema uchaguzi wa mwaka huu umehusisha vyama vingi zaidi tofauti na wa mwaka 2009 hali inayoonesha kupanuka kwa demokrasia.

Tume 'Operesheni Tokomeza' yahamia Kati na Kaskazini kukusanya maoni

$
0
0


ume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza itakusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini mikoa ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe  24 Desemba, 2014 na Katibu wa Tume hiyo, Bw.Frederick Manyanda, Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni na taarifa kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe 21 Januari,2015 katika maeneo mbalimbali ya kanda ya Kaskazini na Kati Nchini. 
Katika kutekeleza jukumu hilo, Bw. Manyanda ameeleza kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4 Januari 2015 mpaka tarehe 8 Januari 2015 na  itakuwa Mkoa wa Singida tarehe 9 Januari,2015mpaka tarehe 10 Januari,2015. 
Aidha Tume itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11 Januari, 2015 mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile, Wakili Manyanda ameeleza kuwa Tume itakusanya maoni Mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 13 Januari, 2015 mpakatarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha tarehe 16 Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015. 
Mpaka sasa Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza imefanikiwa kukusanya taarifa na kupokea malamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza katika mikoa kumi na tano (15) ya Tanzania Bara ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, MbeyaKagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro. 
Pamoja na mikutano hiyo, Bw. Manyanda ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi na watanzania wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa njia ya barua, simu na barua pepe ambapo ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa maeneo husikawanaweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa namba za simu za Tigo:0714 826826; Vodacom:0767 826826; Airtel:0787 826826; na Zantel:     0773 826826.

Mwisho.


HELP THEM TO MAKE THIS CHRISTMAS SPECIAL FOR THE LESS FORTUNATE. YOU CHOOSE, THEY DONATE!

$
0
0
Untitled

In light of the holiday season Hellofood and Rotary Club of Bahari (Dar es Salaam) is running a Corporate Social Responsibility campaign called Light Up A Soul. This campaign allows the public to go to the following page http://lightupasoul.hellofood.co.tz/csr/ and choose what they would like to donate and Hellofood will donate it for them.

 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MSANII NASSIB ABDUL ‘DIAMOND’ IKULU, AWAPONGEZA YEYE NA IDRIS SULTAN KWA KUILETEA SIFA TANZANIA

$
0
0
unnamed-1
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond”  na  kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Desemba 23, 2014 . Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, Mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan hakuweza kufika Ikulu kuonana na Rais Kikwete siku hii. 

unnamed-4
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Nassib Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya  tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.
unnamed-3
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Nassib Abdul “Diamond”  juu ya ushindi wake wa  tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014.

Gangnam staili yafumuakaunta ya google

$
0
0


Video ya muziki  ya mwanamuziki wa Korea Kusini inayoondoka kwa staili ya Psy's Gangnam imefumua uwezo wa YouTube.

YouTube imesema video - ambayo ndiyo iliyotazamwa sana - imetazamwa kwa zaidi ya mara 2,147,483,647.

Kutokana na hali hiyo You tube wamelazimika kubadili kaunta za uangalizi wa video kufikia 9,223,372,036,854,775,808, au zaidi ya  quintillion 9 .

Gangnam Style ilipasua anga kwa fujo ilifyatuliwa mwaka 2012.

Why was Psy nearly too much for YouTube?
Gangnam Style has been watched more than 2.15 billion times as of 4 December

YouTube's counter previously used a 32-bit integer, which is a unit used to represent data in computer architecture. This means the maximum possible views it could count was 2,147,483,647.

On 1 December, it posted a statement saying: "We never thought a video would be watched in numbers greater than a 32-bit integer... but that was before we met Psy."

Google, which owns YouTube, later told website The Verge that engineers "saw this coming a couple months ago and updated our systems to prepare for it".

YouTube now uses a 64-bit integer for its video counter, which means videos have a maximum viewer count of 9.22 quintillion.

Psy has yet to comment although news of YouTube's change was posted on his Facebook and Twitter pages.

The second most-watched video on YouTube - Baby by Justin Bieber - lags behind Gangnam Style by more than a billion views.
How do you say 9,223,372,036,854,775,808?

Nine quintillion, two hundred and twenty-three quadrillion, three hundred and seventy-two trillion, thirty-six billion, eight hundred and fifty-four million, seven hundred and seventy-five thousand, eight hundred and eight.

TAIFA CUP WANAWAKE KUANZA JANUARI MOSI

$
0
0

Mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake)
yanazinduliwa rasmi Januari Mosi mwakani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza kwa mechi kati ya wenyeji Mwanza na Mara.

Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam itachezwa
kuanzia saa 10 jioni. Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin
yatachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya kwanza.

Januari 10 mwakani ndipo zitachezwa mechi kwa mikoa yote ambapo Geita
itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora vs Kigoma (Ali Hassan
Mwinyi), Simiyu vs Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha vs Manyara (Sheikh
Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika).

Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma
vs Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya vs Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi
vs Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma vs Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani
itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.

Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwakani, ambapo baada ya matokeo ya
nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata
ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.

Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwakani wakati zile
za marudiano zitafanyika Januari 21 mwakani.

Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali
ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya
kwanza nchini.

Mdhamini atatoa jezi kwa timu zote zinazoshiriki kabla ya kuanza mashindano
hayo.



*SDL KUTIMUA VUMBI KRISMASI*

Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) inayochezwa katika makundi manne
tofauti inaingia raundi ya nne kesho (Desemba 25 mwaka huu) kwa mechi ya
kundi C kati ya Kiluvya United na Abajalo itakayochezwa Uwanja wa Mabatini
uliopo Mlandizi mkoani Pwani.

Mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Mshikamano FC na Transit Camp yenyewe
itachezwa keshokutwa (Desemba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam.

Kundi A litakuwa na mechi Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu) ambayo
itazikutanisha timu za Ujenzi Rukwa na Mji Mkuu (CDA) kwenye Uwanja wa
Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Desemba 28 mwaka huu ni kati ya Mvuvumwa
FC na Milambo SC kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Jumamosi (Desemba 27 mwaka huu) kundi B litakuwa na mechi kati ya Arusha FC
na Pamba (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha), na Mbao FC vs
JKT Rwamkoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).

Kundi D siku ya Jumamosi hekaheka itakuwa kati ya Mkamba Rangers na Volcano
(Uwanja CCM Mkamba), Njombe Mji vs Wenda FC (Uwanja wa Amani, Njombe) na
Town Small Boys vs Magereza FC (Uwanja wa Majimaji, Songea).

Ratiba ya michuano ya Taifa Cup Wanawake pamoja na msimamo wa SDL
vimeambatanishwa (attached).



*IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)*

LUKWANGULE INAWATAKIA KRISMASI NJEMA

$
0
0

Sisi kutoka katika ofisi zetu zilizopo Kimara jijini Dar es salaam tunawatakia Krismasi njema wasomaji wetu wote, wachangiaji na wale ambao wamekuwa wakitutia Moyo. 

Tuna deni kubwa kwenu na malipo yetu ni kuwatakia Noeli yenye utulivu mkubwa kama Malaika walivyowaambia wachungaji Utukufu mbinguni na amani kwa watu wake duniani.

Viewing all 9079 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>