↧
MKE WA RAIS ATEMBELEA WAZEE WENYE MAHITAJI MOROGORO
↧
TAARIFA YA NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA KUHUSU VIGEZO VYA UTOAJI MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA 2016-2017
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
TAARIFA KWA UMMA
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, imekuwa ikiwakopesha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kugharimia masomo yao. Katika utekelezaji wa jukumu hili, Serikali huandaa Sifa na Vigezo vya Utoaji Mikopo kila mwaka ili kuendana na malengo na matarajio yaliyopo katika mipango na mikakati ya kitaifa kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17 -2020/21), Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) na Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Kwa kuzingatia mipango mikakati na sera hizo, pia Mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/2017 katika mwaka wa masomo 2016/17, Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo kama ifuatavyo:
(i) Vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na mpango wa maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele kama vile:
· Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
· Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
· Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia
· Sayansi Asilia na Mabadiliko ya Tabianchi
· Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu
(ii) Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile Ulemavu na Uyatima
(iii) Ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri
Kwa hivi sasa Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2016. Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo.
Imetolewa na:
Mhandisi Stella M. Manyanya (Mb)
NAIBU WAZIRI
ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Oktoba 14, 2016
↧
↧
MIGOGORO YA ARDHI JIJINI MWANZA MBIONI KUMALIZIKA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa jijini humo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela kabla ya kuyafanyia urasimishaji na kutoa hati ya makazi kwa wamiliki wake.
Kiomoni alifanya ziara ya kutembelea Kata za Buhongwa na Luchelele na kuzungumza na wakazi wa kata hizo juu ya maeneo yenye migogoro na ambayo bado wananchi wanadai fidia ili kutatua changamoto hizo.
Na BMG
Diwani wa Kata ya Buhongwa, Joseph Kabadi (mwenye suti) akizungumza kwenye ziara hiyo na kuelezea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Kata yake kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi kabla ya urasmishaji wa makazi yaliyojengwa kiholela kufanyika katika kata hiyo.
Wengine ni viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo watendaji wa idara ya ardhi.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa ambaye kiwanja chake kina mgogoro akitoa malalamiko yake mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Hatimaye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza aliahidi kumpatia kijana huyu kiwanja kingine ili kuondokana na kiwanja hicho chenye mgogoro.
Wakazi wa Kata ya Buhongwa Magharibi Kata ya Buhongwa wakiwa kwenye kikao baina yao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kilicholenga kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.
Wakazi wa Kata ya Luchelele Jijini Mwanza
Diwani wa Kata ya Luchelele, Vicent Lusana, akizungumza katika mkutano huo ambapo alihimiza halmashauri ya Jiji la Mwanza kulipa fidia kwa wakazi wa kata hiyo kwani ni muda mrefu tangu zoezi la uthamini wa ardhi ulipofanyika katika Kata hiyo.
Alfredy Ngendelo ambaye ni Mthamini wa Jiji la Mwana, akifafanua jambo kwa wakazi wa Kata Luchelele kuhusiana na taratibu za ulipaji fidia baada ya uthamini kufanyika.
Afisa ardhi mteule Jijini Mwanza, Halima Nassor, akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Luchelele wakiuliza maswali ikiwemo kulipwa fidia baada ya zoezi la uthamini wa ardhi yao kukamilika muda mrefu bila kulipwa fidia, ambapo waliombwa kulipwa fidia zao mapema ili waondoke katika maeneo yao ambayo yamepimwa kwa ajili ya miradi ya kijamii.
Baadhi ya maeneo hatarishi yenye miinuko ambayo Mkurugenzi wa Jiji Mwanza amezuia ujenzi wake kuendelea.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa akitoa malalamiko yake kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa akitoa malalamiko yake kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.
Na George Binagi-GB Pazzo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanza zoezi la kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela ili kuyafanyia urasimishaji.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema zoezi hilo limelenga kuondoa migogoro yote ya ardhi na kutoa hati ya makazi kwa wananchi ambao makazi yao yaliyojengwa kiholela yatarasimishwa.
Amesema wale waliojenga katika maeneo hatarishi ikiwemo milimani, hawatahusika katika zoezi hilo hivyo wasiendelee na ujenzi wa makazi hayo.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Buhongwa na Luchelele, wameomba migogoro yote ya ardhi inayowakabili ikiwemo kulipwa fidia katika maeneo yao, itatuliwe kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanya tathmini upya na katika maeneo yenye migogoro na kutoa hati za umiliki.
Zoezi hili limejili ikiwa siku chache baada ya Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi, kufanya ziara Jijini Mwanza na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kutembelea maeneo yote yenye migogoro na makazi holela kabla ya zoezi za usaminishaji kufanyika.
↧
WANAUME WA KATOLIKI JIMBO LA DAR ES SALAAM WATEMBELEA MASISTA WA DADA WADOGO WA MTAKATIFU FRANSISKO MBAGALA
Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia), akishiriki sakramenti takatifu wakati wa ibada hiyo. |
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakinunua mvinyo wa Arovela.
Waumini wakisali mbele ya msalaba nje ya kibanda maalumu cha msalaba wa Yesu.
waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
waumini wakitafakari katika ibada hiyo.
Makofi yakipigwa wakati maandamano yakiingia kabla ya kuanza kwa ibada hiyo.
Picha zikipigwa katika ibada hiyo.
Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Kanisa Katoliki Mbagala Kizuiani wakiimba katika ibada hiyo.
Ma padri mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo.
Masista wa shirika hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Waumini wa kanisa katoliki wakiwa katika ibada hiyo.
Kiongozi wa kwaya hiyo, Fednandi Constantino akifanya vitu vyake.
Ibada ikiendelea.
Waumini wakipokea sakramenti ya Ekaristi Takatifu.
Kinanda kikipigwa.
waumini wakipiga picha za matukio mbalimbali.
Mapadri na watumishi wa kanisa wakitoka kwenye ibada hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.
Hayo yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista wa Shirika la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini, Dares Salaam.
Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi iwe ya halali.
“Tusidharau tufanye kazi na asiye fanya kazi hastahili kula. Hata familia yaYesu ililala njaa…hata ukilala njaa usidharau kazi,”alisema.
Akimzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, PadriMbiku alisemaalikuwa mtu wa kwanza kuwaomba masista kuombea nchi ilipovamiwa na majeshi yaIdd Amin wa Uganda.
“Nyerere aliwashukuru sana watawa masista kwa kushinda vita ile dhidi ya Idd Amin. Tanzania haikuzoea vita.
“Hivyo aliomba masista wasali sana. Tanzania ikashinda.
Nyerere alisema waziwazi na washukuru masista kwa kushinda vita,” alisemaMbiku.
Vita kati ya Tanzania na Uganda iliibukamwaka 1978 nakufikia tamati mwaka 1979 baadayamajeshi ya Amin kuchakazwa vibaya na Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).
Kutokana na umuhimu wa sala za masista hao, Padri Mbiku aliwaomba Uwaka kuhakikisha wanawasaidia masista kwani wanamchango mkubwa kwa taifa na kanisa.
“Masista wanajitoleakuombea kanisa na watu wote wapate wokovu pasipo kubagua dini zao. Sala yao nimuhimu, ina nguvu na Mungu anaisikiliza kwa kujitoa kwao,” alisema.
Kwa msingi huoaliwaomba Uwaka ambao kaulimbiu yao “Nguzo Imara Hekalu la Bwana”
↧
NAIBU WAZIRI WA ELIMU MHANDISI STELLA MANYANYA NA KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE
div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">![]()
Mwanasiasa Wilson Mkama akitoa mada kwenye kongamano hilo.
![]()
![]()
Mgeni rasmi Mhandisi Stella Manyanya (katikati walio kaa), akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Na Dotto Mwaibale
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akihutubia wakati alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alipokuwa amewasili kwenye kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika chuoni hapo Dar es Salaam jana. Kushoto ni mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila. Manyanya alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo.
Mgeni rasmi wa kongamano hilo Mhandisi Stella Manyanya (wa tatu kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto niMwanasiasa Wilson Mkama akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Joseph Butiku akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Mwenyekiti wa kongamano hilo, Spika wa Bunge mstaafu, Anna Makinda akizungumza kwenye kongamano hilo.
wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.![]()
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Mangula akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Mangula akitoa mada kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila, akizungumza kwenye kongamano hilo. Kongamano hilo liliandaliwa na chuo hicho.
Waalikwa wakisikiliza wakati mada zikiendelea kutolewa.
Na Dotto Mwaibale
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philipo Mangula,amesema ameanza kupokea mafaili ya wana CCM ambao wameanza kujipitisha kutoa rushwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho unaotajariwa kufanyika mapema mwakani.
Mangula amesema ana taarifa kwamba wanaCCM wengi wameanza kutumia mbinu chafu za fedha kutaka nafasi mbalimbali na kwamba imekulakwao kwakuwa hawataweza kupenya atawashughulikia.
Mangula alitoa kauli hiyo alipokuwa akitoa mada ya maadili ya viongozi kwenye kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Chu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam jana na kueleza kukerwa na tabiya ya wafanyabishara wenye fedha ya kutaka kuteka kila mahali.
Alisema ndani ya CCM nimaarufu kwa jina la mzee wamafaili, hivyo ataendelea kupitia mafaili hayo ilikuhakikisha maadili yanazingatiwa na kuenzi misingi yaAzimio la Arusha kwani hakuna atakayepenya kwa njia za rushwa.
“Zipo taarifa kuwa wapo baadhi wameanza kujipitisha na kutoa rushwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwakani, nawahakikishia kwangu watu hao hawawezi kupitani tamfuatilia kila mmoja atakaye jihusisha na rushwa hapati nafasi hiyo,” alisema.
Alisema ili kudhibiti mianya hiyo atahakikisha sheria inatungwa ya kutenganisha kati ya wafanyabiashara na uongozi kwa vile wafanyabishara wanatafuta nafasi ya uongozi ilikuendeleza biashara zao.
Mangula alisema ni aibu kwa mpiga kura kuhongwa kiasi kidogo cha pesa na kupoteza haki ya msingi ya kumchangua kiongozi mwenye sifa kwa ajili ya maendeleo.
Alisema iwapo tabia ya kununua uongozi itaendelea baadaye vijana wanaohitimu masomo watakosa nafasi ya kugombea uongozi kutokanana kukosa pesa za kuhonga.
Watanzania wanapaswa kufahamu hatua zinazochukuliwa naRais John Magufuli kuwatumbua watumishi wazembe, imetokana na kauli ya vikao halali vya CCM ili atekeleze hayo.
“Huo ni mpango mkakati wa chama kwa lengo la kuondokana na rushwa, vinginevyo misingi na maadili ya uongozi itapotea,” alisema.
Spika mstaafu na Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Anna Makinda amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuwapeleka vijana wao katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere (MNMA) kujifunzasomo la maadili ya kiongozi ili kuepuka rushwa.
Alisema kongamano hilo limezingatia mada kuu tatu ambaoni Azimio la Arusha, miiko ya uongozi na maadili ya viongozi ambayo kiongozi anapaswa kujitathimini.
Mmoja wawatoa mada, Wilson Mkama alisema viongozi wengi wasiasawapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi kupata utajiri, ikiwamo nyumba, gari nafedha.
Hali hiyo inawafanya watumiegharama yoyote kupata nafasi ya uongozi huku akijua fedha hizo alizotoa zitarudi na kutengeneza maisha mapya.
“Wapo viongozi kwa ajili ya maslahi yao na siyo kwa maslahi ya jamii, huko nikutoka nje ya maadili,” alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
↧
↧
MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA MELI MPYA NA YA KISASA YA MV NYEHUNGE II
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa (Kivuko) ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
"Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe". Alisema Mongella na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
Mmoja wa watoto akisalimiana na viongozi waliohudhuria uzinduzi wa meli hiyo
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo
Mama Gertrude Mongella (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha, wakati wa uzinduzi huo.
Mama Gertrude Mongella (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha (kulia), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonard Masale (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo.
"Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe". Alisema John Mongella (katikati) na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyehunge, Said Mohamed (kushoto), alisema Meli hiyo itakuwa mkombozi kwa wasafiri wa Ukerewe ambapo kutakuwa na Meli tatu kwa siku zitakazokuwa zikifanya safari zake za Jiji la Mwanza na Ukerewe huku nauli ikiwa ni nafuu kabisa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, George Nyamala, akielezea umuhimu wa meli hiyo kwa wakazi wa wilaya yake.
Mmoja wa wakazi wa Ukerewe akielezea furaha yake baada ya uzinduzi wa Meli ya Mv Nyehunge II
Mwonekano wa ndani wa Meli ya Mv Nyehunge II
Abiria wakiingia kwenye Meli ya Mv Nyehunge baada ya uzinduzi kwa ajili ya kusafiri kutoka Jijini Mwanza kuelekea Ukerewe.
↧
KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAZINDULIWA RASMI ENEO LA PAKACHA KATA YA TANDALE JIJINI DAR
Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa Ambassador Angelo akizindua rasmi kampeni ya Binti wa Kitaa
Binti Zawadi Mansende akizungumzia anayesoma Shule ya Sekondari ya Manzese Kidato cha Tatu akizungumzia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kama wasichana wa mtaani ikiwa ni pamoja na kurubuniwa na Vijana jambo linalowapelekea kukumbia majumbani mwao na wengine kupata Mimba za utotoni, wakati wa uzinduzi Rasmi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa.
Baadhi ya Mabinti waliokati ya umri wa miaka 14 na kuendelea wakiwa wanafuatilia kwa makini uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa iliyofanyikia Tandale
Baadhi ya waliofanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa wanaonesha #tag Binti ya Kitaa.
Baadhi ya wadau na Mabinti wa Kitaa wakiwa katika uzinduzi huo
Bwana Godfrey Nteminyanda ambaye ni Mkurugenzi wa Applemackbooks_tz akielezea namna alivyo ipokea kampeni hiyo na wao kuahidi kuisapoti kwa hali na mali
Baadhi ya akina mama wa Tandale pamoja na waendeshaji wa Kampeni ya Binti wa kitaa wakiwa katika uzinduzi
Mama Consalva Genes Samba ambaye ni Mkazi wa mda mrefu wa Tandale akielezea namna mabinti wamekuwa wakirubuniwa na kudanganywa .
Baadhi ya wawezeshaji, na wakazi wa Tandale wakionesha Mabango ya Binti wa Kitaa
Madam Sophia Mbeyela akizungumza jambo wakati wa Uzinduzi huo
Ulifika Muda wa kupata mambo ya Kitaa yaani Bagia, Vitumbua Chachandu na Ujii ilikuwa ni safi sana
Hawa ni Baadhi ya Timu ya waandaaji wa Kampeni ya Binti wa Kitaa
Hii ni timu nzima ya kitengo cha habari cha Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi kuisha
Pamoja na kuwa ni Kampeni ya Binti wa kitaa wanaume nao wamehamasika kuisapoti mwanzo mwisho hapa wakiwa pamoja na Mabinti wengine wanaosapoti.
Picha ya pamoja
Picha zote na Fredy Njeje/Story na Mwana Libeneke wa Funguka Live Dickson Mulashani
Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF) imezindua kampeni kwa jina BINTI WA KITAA eneo la Pakacha kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni itakayodumu kwa mwaka mmoja yenye lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.
"Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo" alisema George.
BINTI WA KITAA imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.
"Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo" alisema George.
BINTI WA KITAA imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.
Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazowapelekea mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,hii ndio iliyosababisha kampeni hii kuzinduliwa mtaa wa Pakacha Tandale kwani.
Kadhalika mmoja kati ya mabinti waliohudhuria katika uzinduzi huo Zawadi Isihaka ameomba wazazi kufuatilia maendeleo na kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kuyagundua mapema mabadiliko ya tabia pamoja na kuwapa elimu ya makuzi sambamba na kutokuwa wakali kupitiliza kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo waratibu wa eneo ambao ni Tandale Youths, Applemacbooks Company,wakazi wa eneo la Pakacha ,Tandale, waandishi wa habari pamoja.
Sambamba na uzinduzi huo katika kata ya Tandale,Ndg. George David ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono kampeni hii ili kuweza kuwasaidia mabinti kwani ni wazi kuwa hili limekuwa sehemu kubwa ya kuzalisha wimbi kubwa la watoto wa mitaani, vifo wakati wa kujifungua, athari za kisaikolojia na kiuwanyima mabinti nafasi ya kupata haki yao ya msingi ya elimu.
↧
MBUNGE WA SINGIDA MJINI AMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya kipimo cha ugonjwa wa Malaria
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mtamaa
Na Mathias Canal, Singida
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima
Shukrani na Pongezi
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kijijini Mtamaa kwa ajili ya mkutano na kukabidhi kifaa maalumu kwa ajili ya kupimia Malaria Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mtamaa
Baadhi ya wananchi wakifurahia kifaa cha kupimia Malaria
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima akisisitiza jambo wakati wa MkutanoNa Mathias Canal, Singida
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.
Tatizo hilo sugu limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili nchini Kenya.
Mhe Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.
Sima alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.
Sima Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.
Alisema kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.
Sima ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.
Kuhusu kadhia ya uduni wa upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Mtamaa A Mbunge huyo amesema kuwa hadi kufikia mwezi aprili mwakani maji yatakuwa yameanza kutoka ili kumaliza kadhia hiyo kwani mradi mkubwa wa maji utakuwa umemalizika.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo kwa kufanya mkutano wa tatu katika eneo hilo tangu aingie madarakani huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha shughuli za maendeleo.
Chima amesema kuwa Mbunge huyo ni muwakilishi mzuri wa shughuli za wananchi wake na ameonyesha uwezo mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutetea hoja na kusimamia misingi ya uwajibikaji.
Naye mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai amesema kuwa kifaa hicho maalumu kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni madhubuti na imara hivyo kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali wa karibu kilomita 20 kwenda kupima ugonjwa huo.
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, April 1922 katika Kijiji cha Butiama Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Maadhimisho ya Mwalimu Nyerere hufanyika kila mwaka ambapo watanzania popote ulimwenguni huadhimisha kwa sala na matembezi mbalimbali kama ishara ya heshima kwa muasisi wa Taifa lao.
Mhe Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.
Sima alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.
Sima Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.
Alisema kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.
Sima ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.
Kuhusu kadhia ya uduni wa upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Mtamaa A Mbunge huyo amesema kuwa hadi kufikia mwezi aprili mwakani maji yatakuwa yameanza kutoka ili kumaliza kadhia hiyo kwani mradi mkubwa wa maji utakuwa umemalizika.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo kwa kufanya mkutano wa tatu katika eneo hilo tangu aingie madarakani huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha shughuli za maendeleo.
Chima amesema kuwa Mbunge huyo ni muwakilishi mzuri wa shughuli za wananchi wake na ameonyesha uwezo mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutetea hoja na kusimamia misingi ya uwajibikaji.
Naye mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai amesema kuwa kifaa hicho maalumu kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni madhubuti na imara hivyo kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali wa karibu kilomita 20 kwenda kupima ugonjwa huo.
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, April 1922 katika Kijiji cha Butiama Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Maadhimisho ya Mwalimu Nyerere hufanyika kila mwaka ambapo watanzania popote ulimwenguni huadhimisha kwa sala na matembezi mbalimbali kama ishara ya heshima kwa muasisi wa Taifa lao.
↧
SAFARI ZA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER JIJINI ARUSHA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHINI





Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
↧
↧
WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI AZINDUA RASMI KAMISHENI YA TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI

Dr. Stephen Nindi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania akitoa utambulisho wakati wa uzinduzi wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
Mwenyekiti wa Kamisheni Mstaafu Bw. Abubakar Rajabu akizungumzia hatua walizofikia wakati akiwa mwenyekiti mpaka walipofikia kabla ya kumaliza muda wake na kumpongeza hatua zinazoendelea kwa sasa katika Tume hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akitoa neno la Shukurani kwa Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya uzinduzi rasmi wa tume na kuleleza kuwa wanaanza kuyafanyia kutekeleza mara moja maelekezo waliyopewa na Mh. Lukuvi
Makamishna wateule, Pamoja na Menijimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wakiwa katika uzinduzi huo.
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi,Mwenyekiti,Katibu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo
Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
↧
KILIMANJARO WAADHIMISHA MIAKA 17 YA KUMBUKUMBU CHA KIFO CHA BABA WA TAIFA KWA KUOTESHA MITI









Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
↧
Mwaname adai kubakwa na wanawake wawili na kuibiwa gari la kifahari, pete ya harusi
GAZETI moja la Dailysun SA limeandika habari ambayo inaonekana kama kituko kuhusu na mwanaume mmoja kubakwa na wanawake wawili kisha kuibiwa kila kitu chake ikiwamo gari lake la kifahari Mercedes Benz.
Mtu huyo amedai kwamba alipumbazwa kwa mihadarati kabla ya kubakwa na kuibiwa kila kitu.
Imeelezwa kuwa mtu huyo aliwasili nyumbani kwake East Park, maeneo ya Kagiso, Mogale City nchini Afrika Kusini kutoka katika pilikapilika za wikiend na akiwa anaegesha gari lake wanawake wawili walimfuata na kusema kwamba wameponea tundu la sindano kubakwa na genge kubwa la wahuni.
Wanawake hao walisema kwamba wanahitaji ulinzi; na kwa kuona kwamba shida yao aliwaalika ndani wapumzike kidogo kabla ya kuendelea na safari yao.
Alisema wakiwa hapo waliamua kupta kinywaji lakini anachokumbuka ni kuamka saa tatu asubuhi akiwa kama alivyozaliwa na alipojitazama akagundua kwamba amebakwa.
Aidha alipoangalia gari lake halikuwepo.
Vitu vingine ambavyo vilitoweka pete yake ya ndoa, kadi za benki, simu, leseni ya udereva, mfuko wake wa safari na Samsung Galaxy Grand Prime
Msemaji wa polisi wa Kagiso kapteni Solomon Sibiya amesema kwamba polisiw anafanyia uchunguzi wizi huo ingawa hawajafungua shauri la kubakwa.
↧
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI ,MHANDISI GERSON LWENGE AZINDUA BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)














Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael aliyekuwa mjumbe wa bodi ya MUWSA , zawadi ya Tablet.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi ambaye pia ni mjumbe wa bodi hiyo,Hajira Mmambe zawadi ya Tablet.









Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
WAJUMBE WA BODI MPYA YA MUWSA
- BIBI ELIZABETH MINDE
- ENG: ABDALLA MKUFUNZI
- BW: BONIFACE MARIKI
- BW: FILBERT KAHETA
- BIBI HAJIRA MMAMBE
- Mh. RAYMOND MBOYA
- Eng. AISHA AMOUR
- BW. MICHAEL MWANDEZI
WAJUMBE WA BODI ILIYOMALIZA MUDA WAKE
- Mh. SHALLY RAYMOND (MB)
- Mh. JAPHARY MICHAEL (MB)
- Eng. ALFRED SHAYO
- BW. JESHI LUPEMBE
↧
↧
UVCCM MUFINDI WATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO


katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo na
mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo wakielekea kufanya usafi katika hospitali ya mafinga
hawa ni baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakiwa wamemaliza kufanya usafi katika hospital ya mji wa Mafinga wakiongozwa na katibu msaidizi wa mufindi.
na fredy mgunda,iringa
VIJANA wa chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wamewataka wafanyakazi na viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kujituma ili kumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo.
Haya yalisemwa na katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo wakati akisoma lisala kwa mgeni rasmi wakati wa maazimisho ya siku ya vijana wa chama cha mapinduzi yaliyofanyika wilayani Mufindi.
viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.
“nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yake” Alisema Ngailo
Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.
“Kupitia kumbukumbu hizi sisi vijana tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Alisema Ngailo
Akiongea kwenye sherehe hizo mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo Alieleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.
“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Lwimbo
Lwimbo amebainisha kuwa serikali itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.
“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali, matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao” Ameainisha Lwimbo
Lwimbo amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.
Kwa upande wake katibu wa CCM mkoani Iringa Hassani Mtenga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika sherhe hizo alisema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.
Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.
“kwa wale mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho na jua mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania” alisema Mtenga
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohannes Kaguo aliwataka vijana kuacha kulalamika kwa kukosa ajira kutoka na mfumo wa serikali na kuwaomba wajitume na kuwa wabunifu ili waweze kujiajiri wenyewe.
“Saizi unakuta vijana wengi wanashinda mitaani na kupiga siasa tu na sio kupanga mipango ya kutatua changamoto zao za kimaendeleo ,saa moja asubuhi unawakuta vijana kwenye mabao,pooltable na draft sasa unafikiri hapo utapata maendeleo”alisema Kaguo
↧
WANANCHI WAJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAUA PANYA ROAD MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM
' Samahani kwa kutumia picha hii nia ya kuitumia ni kujaribu kuonesha changamoto ilivyo kwa vijana hawa wanaopoteza maisha kwa kujihusisha na kundi hilo la panya road'
Wananchi wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem Dar es Salaam leo jioni. Katika tukio hilo vijana wengine wawili walipoteza fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.
Wananchi wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem Dar es Salaam leo jioni. Katika tukio hilo vijana wengine wawili walipoteza fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.
Wananchi wakiangalia mwili wa kijana huyo (haupo pichani)
Wananchi wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem Dar es Salaam leo. Katika tukio hilo vijana wengine wawili walipoteza fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wa Mbagala sabasaba wamemuua kwa kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma moto kijana mmoja anayedaiwa kuwa ni mharifu wa kundi la panya road ambaye alikuwa na wenzake zaidi ya 15 ambapo wawili kati yao walipoteza fahamu kutokana na shambulio hilo.
Tukio hilo la kushambuliwa kwa panya road hao lilitokea majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mbagala Sabasaba baada ya vijana hao kukurupushwa walipokuwa wakikimbia walipokuwa wakifanya uhalifu maeneo ya sabasaba Magengeni na Mbagala Zakhem.
Polisi waliofika eneo la tukio walilazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya wananchi ili waweze kuuchukua mwili wa kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake.
Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Khalfan alisema usalama wa wananchi upo mashakani kufuatia kundi hilo la panya road.
"Hawa panya road walikuwa zaidi ya 15 wakitokea Mbagala Zakhem ambako walikuwa wakikimbizwa na wananchi baada ya kufanya uhalifu na walipofika hapa Sabasaba walizingirwa na wananchi ambapo watatu kati yao walianza kushambuliwa na mmoja kupoteza maisha baada ya kuchomwa moto " alisema.
Alisema vijana wawili kati yao walijeruhiwa vibaya na kupoteza fahamu lakini wenzao wengine walifanikiwa kukimbia kuelekea maeneo ya Yombo Dovya huku wakiahidi kurudi kulipiza kisasa kufuatiwa kuuawa kwa mwenzao.
Mkazi mwingine wa Mbagala kwa Mangaya aliyejitambulisha kwa jina la Seif Mwarami alisema vijana hao wataendelea kuuawa na wananchi kwa kuwa kila wanapokwenda kutoa taarifa polisi hawachukuliwi hatua yoyote badala yake uachiwa na kurudi mitaani kuendeleza uhalifu wao" alisema Mwarami.
Aliongeza kuwa kutokana na kuwa na umri mdogo wanashindwa kupelekwa kwenye mahakamani kutokana na kulindwa na sheria ya utoto jambo linalowatia hasira wananchi na kuamua kujichulia hatua mkononi na kuanza kuwaua.
Alisema vijana hao wamekuwa wakitokea maeneo ya Kitunda, Moshi Baa na Yombo kwenda kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Gilles Muroto alipopigiwa simu jana jioni ili kuzungumzia tukio hilo alisema alikuwa kwenye mkutano hivyo apigiwe baadae.
Hata hivyo jeshi la polisi mara kadhaa limekuwa likataa kuwepo kwa kundi hilo la panya road likieleza kuwa wao wanawahesabu kama walivyo wahalifu wengine wa matukio ya ujambazi na mengine.
↧
TAZAMA FILAMU FUPI YA KUSISIMUA "KIFO" KUTOKA BONGO MOVIE SHINYANGA & AGAPE- NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
![]() |
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi |

Tazama video hii fupi ya kusisimua hapa chini
Kwa mambo mbalimbali ya sanaa ya uigizaji ,wasiliana na mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Ibrahim Songoro kwa /whatsapp/simu namba0767831036
↧
KONGAMANO LA KUMUENZI MWALIMU J.K NYERERE LAFANYIKA WILAYANI IKUNGI

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi mahitaji kwa wanafunzi walemavu mara baada ya kuwasili shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
Baadhiya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini mada zikiwasilishwa kwenye mdahalo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi ya Wilaya wakati kongamano likiendelea
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsalimu Bi Fumbo Shishiwa aliyejifungua salama mtoto wa kiume na kumuita Magufuli
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi akichangia mada iiliyokuwa inajadiliwa kwenye Kongamano la Kumuenzi Mwalimu J.K Nyerere kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Bi Faidha Athumani mara baada ya kumkuta akisubiri matibabu katika Kituo cha afya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
Baadhi ya washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Mashine ya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo ini katika kituo cha afya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimuelekeza Mganga Mkuu wa kituo cha Afya Ikungi kuhakikisha anasimamia ujenzi wa upanuzi wa chumba cha kuhifadhia maiti
Na Mathias Canal, Singida
Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeungana na Watanzania kote ulimwenguni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Mwasisi wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Octoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.
Katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi limejumuisha Viongozi wa kada tofauti wakiwemo viongozi wa serikali, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vitongoji na vijiji, Viongozi wa siasa, Wazee wa mji wa Ikungi, Maafisa Tarafa na Watendaji, Madiwani, Walimu na wanafunzi ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuchangia mada na kupitisha maadhimio zaidi ya kumi na tano yatakayotoa taswira ya namna ya kumuenzi Mwalimu Nyerere mwakani.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewasihi wananchi kwa umoja wao kumuenzi Mwalimu Nyerere katika matendo makubwa na muhimu aliyokuwa anayafanya hususani misingi ya Haki, Ukweli na uwajibikaji.
Amewataka watanzania kuishi katika matakwa ya Mwalimu Nyerere ikiwa ni pamoja na kutokubali kutoa na kupokea Rushwa kwani hayo ni miongoni mwa mambo mengi aliyoyahubiri wakati akiwa waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo na hatimaye kuyahubiri na kuyaishi kipindi akiwa Rais wa kwanza wa Tanzania.
Dc Mtaturu alisema kuwa Tanganyika wakati wa uhuru ilikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi yatokanayo na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, Pia kulikuwa na ujinga uliosababishwa na ukosefu wa elimu bora kwa kiasi kikubwa kwani watanganyika wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu walikuwa ni zaidi ya asilimia 90.
Alisema kuwa sambamba na hayo pia kulikuwa na umasikini mkubwa na uliokithiri kwani asilimia kubwa ya watanzania walikosa mahitaji ya msingi kama vile malazi, Chakula, na Mavazi ambapo Mwalimu Nyerere alifanikiwa kupingana na maadui hao watatu kwa kuongeza udahili kwa kiasi kikubwa katika shule muhimu za Sekondari Kilakala, Kibaha na Mzumbe.
Mtaturu alisema kuwa pia Mwalimu Nyerere alitaifisha taasisi zote za watu binafsi ili kuleta usawa katika jamii pamoja na kuimarisha upatikanaji mzuri wa huduma za afya katika zahanati, vituo vya afya, na Hospitali ili kuboresha afya za watanzania na kuwafanya kuweza kufanya kazi vizuri na kwa ufasaha.
Dc Mtaturu Amewataka washiri wote wa Kongamano hilo na watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa viungo muhimu katika kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Kudumisha Lugha ya Kiswahili, Kukuza Utu na uadilifu katika kazi na jamii inayotuzunguka.
Zaidi amesisitiza wakulima kwa kushirikiana na maafisa kilimo kulima kilimo chenye tija ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuhakikisha wanakuwa na mavuno mengi yenye faida kubwa na kuwaongeza uchumi wao kwani wastani wa pato la Mtanzania aishie Wilaya ya Ikungi ni shilingi elfu mbili kwa siku ambapo kwa mwezi ni shilingi elfu sitini.
Hata hivyo Dc Mtaturu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo hususani kusimamia vyema mapato ya serikali, Kupambana katika misingi ya utu, haki na usawa kwa kila Raia wa nchi hii, Kupinga Rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Umma.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor ameyataja baadhi ya maadhimio yaliyojadiliwa katika kongamano hilo kuwa ni pamoja na Kupata viongozi wa Haki na halali katika chaguzi zetu, Jamii kuwa na moyo wa uzalendo na kujitolea katika kufanya kazi.
Mengine ni kuepuka kejeli na dharau katika maisha ya kila siku, Kuboresha mazingira ya kufundishia, Jamii na viongozi kuweka miiko ya uongozi, Kudumisha umoja na mshikamano wa Taifa letu.
Naye katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Aluu Segamba amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuamua kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya kongamano kwani imekuwa taswira njema kwa wakazi wa Wilaya hiyo ambao hawajawahi kushiriki katika kongamano kama hilo tangu kuanzishwa kwa Wilaya hiyo.
Baadhi ya wachangiaji katika kongamano hilo la kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wamependekeza kuwa na siku moja ambayo Mkuu wa Wilaya atakutana na wananchi wote kwa ajili ya kujadili kwa pamoja namna ya kuiboresha Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na shughuli za kijamii hususani kuboresha kilimo, Uchumi na Miundombinu.
Wengine wamependekeza bendera kupeperushwa nusu mlingoti ni kuenzi na kutoa heshima kubwa kwa Baba wa Taifa kwani kufanya hivyo itakuwa njia sahihi ya kuongeza uwajibikaji na nidhamu ya Taifa.
Kabla ya Kongamano hilo mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi akishirikiana na viongozi wote wa Wilaya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama alitembelea Shule ya Msingi mchanganyiko Ikungi ili kutoa baadhi ya mahitaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo Wenye ulemavu wa ngozi, Walemavu mchanganyiko na wasioona.
Sambamba na hayo pia amewatembelea wagonjwa katika Kituo cha afya Ikungi kwa kuzuru katika wodi za wanawake waliojifungua, sambamba na Wodi ya wanaume na Wanawake.
Dc Mtaturu amemuagiza mganga Mkuu wa Zahanati hiyo kuhakikisha anafanya utaratibu wa kujenga Sehemu ya kuhifadhia maiti kutoka na sehemu iliyopo kuzidiwa kwani ina sehemu mbili tu za kuhifadhia maiti.
Aidha Dc Mtaturu alipotembelea kituo cha Afya cha Ikungi alipitia maagizo yake aliyowahi kuyatoa hivi karibuni ya kupanua chumba cha maabara na kuagiza kutengenezwa kwa mashine ya kupimia magonjwa mbalimbali ndani ya muda mfupi ili kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wanaotumia kituo hicho kwa ajili matibabu.
Aidha Dc Mtaturu alipotembelea kituo cha Afya cha Ikungi alipitia maagizo yake aliyowahi kuyatoa hivi karibuni ya kupanua chumba cha maabara na kuagiza kutengenezwa kwa mashine ya kupimia magonjwa mbalimbali ndani ya muda mfupi ili kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wanaotumia kituo hicho kwa ajili matibabu.
Akifunga Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesisitiza kuwa katika kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni lazima kuhakikisha huduma za Afya, Elimu, Uchumi, Kilimo na Miundombinu zinaboreshwa.
↧
↧
WAHITIMU ST. EMMANUEL CHAMAZI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM WAASWA KUZINGATIA ELIMU
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya ST. Emmanuel High School, Ernest Masaka, akizungumza katika mahafali ya saba ya Kidato cha Nne yaliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahali hayo, Katibu wa Diwani huyo na Lucy Peter, mke wa Mkurugenzi wa shule hiyo.
Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, akizungumza katika
mahafali hayo. Kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Ally Mkamba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata na Katibu wa Diwani.
Taswira ya meza kuu kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa kidato cha nne wakionesha vyeti vyao.
Mahafali yakiendelea.
Ndugu na Jamaa yake mhitimu Winfrida Komba wakiwa kwenye mahafali hayo.
Walimu wa shule hiyo wakishiriki kwenye mahafali hayo.
Wazazi na walezi wa wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu hao wakionesha jinsi ya kujifunza somo la Sayansi.
Wanafunzi wa shule hiyo wakipata burudani kupitia madirishani.
Burudani zikiendelea kutolewa na wahitimu hao.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Katibu wa Diwani (kulia), akitoa vyeti kwa niaba ya diwani huyo.
Mwanafunzi akikabidhiwa cheti na Katibu wa Diwani wa Kata ya Chamazi.
Katibu wa Diwani wa Kata ya Chamazi, akimkabidhi cheti mhitimu, Winfrida Komba katika mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba.Na Dotto Mwaibale
WAHITIMU wa Kidato cha Nne mwaka 2016 katika Shule ya St. Emmanuel iliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam wametakiwa kuzingatia elimu ili kutimiza ndoto za maisha yao badala ya kujihusisha na vitendo viovu na utoro.
Mwito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata wakati akiwahutubia wanafunzi hao kwenye mahafali ya saba ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika Dar es Salaam jana.
"Zingatieni masomo yenu ili mtimize ndoto za maisha yenu ya baadae, wazazi wenu wanawalipia ada ni vizuri mkawaonesha mafanikio yenu katika elimu na sio tabia mbaya," alisema Karata ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Alisema kwa maisha ya leo bila ya kuwa na elimu kuna changamoto kubwa ya maisha hivyo aliwaasa wahitimu hao kufanya bidii ya kusoma hata watapokuwa kidato cha tano na sita na elimu ya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Ernest Masaka aliwaomba wazazi kushirikiana na uongozi wa shule katika kuwalea wanafunzi hao wawapo nyumbani na shuleni.
"Ushirikiano baina ya wazazi, wanafunzi na walimu ni muhimu sana katika kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kupata elimu bora hivyo nawaombeni tuendelee kushirikiana," alisema Masaka.
Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba alisema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe.
Alisema licha ya shule hiyo kuwa na mafanikio, changamoto ndogo ndogo zinakuwepo lakini wanajitahidi kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja na wazazi.
↧
MTANDAO WA WIZI WA BAJAJI NA BODABODA WANASWA MBEYA
Mkutano wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Waandishi wa habari. |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akionesha baadhi ya Bjajai na Pikipiki ziizokmatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo la POLISI Mbeya. |
Askari Polisi wakiwa wamebeba moja ya bajaji iliyokamatwa mara baada ya Jeshi la Polisi Kufanya masako . |
Bajaji zilizokamatwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kufanya msako. |
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kuunasa mtandao uliokuwa ukihusika na matukio mbalimbali ya wizi wa bajaji na Pikipiki (bodaboda) katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.
Mtuhumiwa anayehusika na matukio hayo imefahamika kwa jina la Getruda Mwakyusa Mkazi wa Mtaa wa Manga Veta jijini hapa.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema jeshi la polisi limeendelea kufanya misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kudhibiti uhalifu .
Amesema Octobar 13 katika misako hiyo jeshi hilo la polisi lilifanikiwa kuunasa mtandao wa wizi wa bajajai na pikipiki ambapo mtuhumiwa wa matukio hayo alifanikiwa kutoroka ambapo nyumba yake mara baada ya kufanyiwa upekuzi zilikutwa pikipiki 3,bajaji 3,bodi 7 za bajaji .
Amesema kati ya mali hizo pikipiki mbili tayari zimekwisha tambuliwa na wamiliki wake kuwa ziliibiwa wilayani Chunya septemba25 mwaka huu katika kijiji cha Isenyela kata ya Mbugani.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani humo ametoa wito kwa jamii husasani vijana kuacha tabia ya kutaka mali kwa njia ya mkato badala yake wafanye kazi kihalali ili kijipatia kipato sanjali na kutumia fursa zilizopo ili kujitafutia ajira.
Mwisho.
↧
MAKAMBA ABARIKI KUONDOLEWA KWA WALIOJENGA CHANZO CHA MAJI MAMBONGO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kushirikiana na Mamlaka ya Bonde la Wami -Ruvu na Manispaa ya Morogoro kuwaondoa watu waliojenga makazi katika chanzo ya maji cha Mambogo safu ya Milima ya Uluguru ifikapo Novemba mwaka huu.
Hatua hivyo inatokana na uharibifu wa mazingira na uchepushwaji wa maji katika chanzo cha mto huo kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji na kusababisha kukosekana kwa maji kwenye chanzo chake kutoa ya uzajo mita milioni saba kwa siku na kupungua hadi milioni tatu kwa siku.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba, ( kati kati aliyeweka mikono kufuani ) akijadiliana jambo na watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Bonde la Wami -Ruvu pamoja na Manispaa ya Morogoro eneo la chanzo ya maji cha Mambogo katika safu ya Milima ya Uluguru jana , ( Okt 16) alioanza ziara ya siku mbili mkoani Morogoro, iwango cha uzajo wa maji kimepungua katika chanzo hicho.
Waziri Makamba baada ya kutembelea chanzo hicho cha Mambogo na kujionea upungufu mkubwa wa maji kutokana na maeneo ya milima ya chanzo cha mtu hiyo kuvamiwa na watu kwa kujenga makazi na uchepushaji maji kwa ajili ya shughuli zao za kilimo cha umwagiliaji alisema , bila kuchukua hatua hiyo , Serikali itakuwa imepata hasara kubwa baada ya kujenga miundombinu ya kisasa ya matangi makubwa na mitambo ya kuchunja maji ambapo kwa pamoja imegharimu zaidi ya Sh bilioni 15 hadi 16 , fedha za ndani na misaada ya wahisani.
“ Watu ambao hawajaondoka , waondoke mapema na haraka sana , waambiwe hilo na tupeane muda ni lini waondoke , Novemba mwishoni mwa mwaka huu wamewaomeondolewa waliojenga kwenye eneo la chanzo hiki” alisema Makamba mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro.
Waziri Makamba , pia Ofisa wa Bonde la Wami – Ruvu, Praxeda Kalungendo ,na watu wake kushirikiana na maofisa wa NEMC Kanda ya Mashariki ambao wana nguvu za kisheria na halmashauri ya Manispaa hiyo kuendesha ukaguzi ili kubaini watu waliochepusha maji.
Waziri aliwataka kuanza kazi hiyo mara moja na wale watakaokutwa wamechepusha maji kwa shughuli zao wakamatwe na wafikishwe mahakamani kulingana na sheria ya hifadhi ya mazingira .
Source: John Nditi, Morogoro
↧