Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9109 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AAGIZA MAPATO YA HOSPITALI YA NACHINGWEA YAKUSANYWE KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mery Majaliwa wakimsalimia Bahati Omary kutoka kijiji cha Nangao Wilaya Liwale ambaye amejifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya wilaya ya Nachingwea  Waziri mkuu alifika katika Hospitali hapo kujionea jinsi huduma za afya zinavyo tolewa kwa wagonjwa waziri mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruwangwa  Mkoani Lindi
Picha na Chris Mfinanga

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Lindi.
Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma.
Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi milioni nne kwa siku.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na watumishi wa Hospitali ya Nachingwea pamoja na wananchi waliofika katika Hospitali ya nachingwea Waziri Mkuu alifanya ziara ya kutembelea hospitalini hapo kwa ajili yakuona na kusikiliza wagonjwa wanavyo pata huduma  

Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.
Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Mohammed kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.
“Mkurugenzi hakikisha watendaji wako wa kata na vijiji wamebaini wazee wote katika maeneo yao na kuwatengenezea vitambulisho vitakavyowawezesha kupatibiwa bure,” amesema.
Naye Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema muamko mdogo wa jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za afya.
Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.
Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia wananchi kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.
Amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi. “Serikali haitaridhika kuona wananchi wakizagaa kwenye ofisi za halmashauri hiyo bila ya kusikilizwa,” amesema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 16, 2016


TABATA KIMANGA WAOMBA DARAJA LITAKALO WAUNGANISHA NA TABATA CHANG'OMBE

$
0
0
 Mtoto Juma Ramadhan mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Tabata Kimanga, akiwa amembeba mdogo wake Sara Sadiki wakati wakipita katika daraja la miti linalounganisha wakazi wa Tabata Kimanga na Tabata Chang'ombe Dar es Salaam , ambapo wakazi wa eneo hilo wanaiomba Manispaa ya Ilala iwajengee daraja la kudumu.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Jonathan Mlay akimuonesha mwandishi wa mtandao huu, daraja la miti wanalolitumia lililojengwa kwa nguvu za wananchi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.


Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wanaoishi mpakani mwa Tabata Kimanga na Chang'ombe katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kujengewa daraja ili waweze kutumia muda mfupi wa kufika katika maeneo hayo badala ya kupitia Tataba Mawenzi.

Ombi hilo wamelitowa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com kuhusu changamoto mbalimbali zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya kujengewa daraja hilo lililopo Mtaa wa Amani.

Akizungumzia changamoto ya daraja hilo, mkazi wa eneo hilo Tusekelege Ambonisye alisema wamekuwa wakitumia muda mwingi wa kuzunguka na gari kupitia Tabata Bima na kwenda Tabata Chang'ombe lakini kama daraja hilo linalounganisha maeneo hayo lingejengwa lingewarahisishia" alisema Ambonisye.

Aliongeza kuwa adha kubwa waliyonayo ni pale ikinyesha mvua kwani maji yanajaa na barabara hiyo kushindwa kupitika ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha ya watu wanaojaribu kupita kaika eneo hilo.

Alisema kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa eneo hilo walikusanya nguvu na kujenga daraja la miti la muda ambalo linatumika lakini sio salama kwa watumiaji.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo wa Amani, Jonathan Mlay alisema changamoto ya daraja hilo ni ya muda mrefu kwani waliwahi kuiwasilisha kwa wabunge wa jimbo hilo waliopita na wa sasa Bonah Kaluwa lakini bado halijapatiwa ufumbuzi wowote.

"Kupitia vikao vyetu vya kamati ya maendeleo ya mtaa changamoto hii tuliipeleka kwa wabunge waliopita pamoja na huyu wa sasa tupo tunasubiri matokea yake" alisema Mlay.

GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA WATOA ELIMU YA AMANI KATIKA FAMILIA

$
0
0
Kila Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na wao. Katika jukwaa la mwezi huu kulikuwa na mada inayosema: "Nafasi  ya mtoto wa kike katika jamii" ambapo majadiliano yalilenga zaidi kutambua nafasi hizo, changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike pamoja, namna ya kuzitatua na jinsi gani mtoto wa kike anavyoweza kusimamia malengo yake kufanikiwa.

Aidha katika jukwaa hilo la vijana Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation  kupitia Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini, Martha Nghambi alitoa pia elimu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha  amani ndani ya familia, ambapo alisema kuwa ili amani iweze kudumishwa na watu waishi bila kuwepo na mifarakano ni lazima kujenga mahusiano mazuri kuanzia chini yaani wanafamilia kuweza kuelewena kwa kuwahusisha wazazi na watoto ambapo hawa wakiishi vema basi hakutakuwa tena na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa kila mtu analojukumu la kulinda amani.
Mwendeshaji wa Jukwaa la Vijana lililofanyika Tandale leo Jamal Magabilo akitoa neno la utangulizi na kuwakaribisha wageni waalikwa wote katika jukwaa
Mkurugenzi wa Gida Rahma Bendera akiitambulisha rasmi mada katika Jukwaa la vijana inayosema nafasi ya mtoto wa kike katika jamii
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi akitoa Elimu kwa kina juu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha amani kwenye familia ambapo aligusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na visababishi vya uvunjishi wa amani pamoja na namna ya kuzuia uvunjifu huo wa amani katika familia.
Mwandaaji wa Matukio wa TYDC Imani akitoa neno la shukurani kwa wote waliohudhulia jukwaa hilo
Afisa Mahusiano wa TYDC Anna Emmanuel akielezea historia fupi ya umoja wao
Mdahalo ukiwa umeanza
Loveness Msuya akizungumzia mada inayohusu jinsi gani mtoto wa kike anaweza kusimama kwenye ndoto na malengo yake na mwisho wasiku kufanikiwa, alieleza njia na mbinu mbalimbali zinazoweza kumfikisha mtoto wa kike kule anapo pataka.
Anna Mwalongo kutoka DUCE akisisitiza kwa nguvu na kupaza sauti ya kuwasihi Mabinti kujitambua ili waweze kuepukana na vishawishi mbalimbali vinavyo sababishwa na vijana.
 Ni Binti Mdogo mwenye umri wa miaka 12 na mwenye upeo mkubwa Zurpha Issa yeye alitaka kujua ni namna gani anaweza vipi kujizuia na mabadiriko yake? ambapo pia alieleza kuwa yeye anandoto ya kuwa msanii hapo baadae.
Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi  akifuatilia kwa makini mdahalo huo
Steven Mfuko Maarufu kwa Jina la Babu Zero akichangia mada katika mdahalo huo ambapo alizungumzia changamoto za mabinti kuvunja ungo wakiwa katika umri mdogo na kuelezea namna vijana wanavyo warubuni na kuwadanganya mabinti wadogo.
Muongozaji Mdahalo huo wa Nafasi ya Mtoto wa Kike kwenye Jamii Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo(wa pili kulia) akiendelea kutoa mwongozo
Bi. Mwafine Kimwaga mkazi wa Tandale akielezea namna alivyo mpokonya simu mwanae kwa kuhofia kuwa inaweza kuwa ni chanzo cha kumharibu kisha kumpa adhabu kali
Bi Stella Francis Mganga akielezea jinsi mabadiliko makubwa ya Teknolojia yalivyo na yanavyo endelea kuporomosha maadili ya vijana wengi na kutumia muda wao mwingi huko kulipo kufanya maswala mengine.
Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania  akichangia mada katika jukwaa hilo
Asha Furaha mkazi wa Tandale akieleza mambo mbalimbali yanayowakabili mabinti na kuwasihi kuendelea kupata elimu zaidi juu ya usichana wao
Madam Sophie Mbeyela akitoa mchango wake wakati wa kujadili mada ya Nafasi ya Mtoto wa kike kwenye jamii
Vijana, Wazazi na wadau mbalimbali wakiwa katika jukwaa hilo
 Picha ya Pamoja
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

Mkurugenzi Msaidizi,Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma,Bi.Hellen Semu afa kwenye ajali

$
0
0
TANZIA
Katibu Mkuu ,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto anasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi wake ambaye alikuwa Mkurugenzi Msaidizi,Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma,Bi.Hellen Semu,kilichotokea leo mchana tarehe 16/10/2016 kwa ajali ya gari eneo la Mkwazu kwa Msakamali,Wilayani Chalinze akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma kikazi.
Taarifa zingine za msiba zitatolewa baada ya kuwasiliana na familia ya Marehemu.
Katibu Mkuu anawapa pole Familia ya Marehemu pamoja na wafanyakazi wote wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
BWANA ALITOA,BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMEN
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Afya)
16/10/2016


RATIBA YA MAZISHI YA MWANASHERIA YUSTA MSOKA HAPA DAR ES SALAAM

$
0
0
Jumuiya ya wanafunzi kutoka Shule ya msingi Changa na Shule ya sekondari Usagara zilizopo mkoani Tanga pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam tunasikitika kutangaza kifo cha aliyewahi kuwa mwanafunzi mwenzetu Marehemu Advocate Yusta Msoka kilichotokea Majuzi hapa Dar es salaam.

Sisi kama wanajumuiya wenzake kupitia shule mbalimbali tulizopitia tunatoa pole zetu kwa pacha mwenzake Mwanasheria Felista Msoka na wana familia kwa ujumla, tunaungana nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.  

Taarifa kutoka kwa familia ya marehemu zinasema mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 17/10/2016 hapa jijini Dar es salaam katika makaburi ya Chamanzi - Mbagala ambako ni jirani na wazazi wake wanapoishi huko Mbagala kuanzia saa 5 asubuhi kwa kutanguliwa na Chakula/ Ibada kisha kuishiwa na Mazishi katika nyumba yake ya Milele.

Kwa wale wote ambao watapata taarifa hii tunaomba umjulishe na mwingine ili tuweze kuungana pamoja kumsindikiza mwenzetu. 

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

AMIN. 


MBONI MASIMBA NDANI YA 102.5 LAKE FM MWANZA AKIZUNGUMZIA KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Na BMG
Konagamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kujikomboa kiuchumi ambapo wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu watakuwepo kuzungumza na wanawake Jijini Mwanza ambapo kiingilio itakuwa elfu 40 tu na utapata elimu, burudani pamoja na chakula.

"Atakuwepo Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambaye amefanikiwa kwenye biashara, atakuwepo Mkandarasi Maida Waziri ambaye amekuwa mkandarasi na amefanikiwa pamoja na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni inaitwa Namaingo Agri_Busness Agency ambayo inawawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo na wengine wengi". Amefafanua Masimba.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba akiwa ndani ya 102.5 Lake Fm Mwanza akizungumzia Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu ndani ya Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

MKURUGENZI UBUNGO AZURU GHAFLA NEW HABARI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo (Kushoto) akiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Mariam Malliwadh mara baada ya kuwasili katika kampuni ya New Habari Corparation
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo akisikiliza kelele hizo ambazo zimekuwa zikiwasumbua wafanyakazi wa kampuni hiyo
Kelele ziosizo za kawaida huenda zikawasababishia wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari Corparation matatizo ya kutesikia kutokana na kutokuwa na vifaa madhubuti vya kuzuia kelele hizo.

Hayo yamebainika wakati wa Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo ambapo miongoni mwa mambo yaliyobainika ni pamoja na kelele hizo zisizo za kawaida ambazo zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni hiyo ambazo zinahatarisha uwezo wa wafanyakazi wa kusikia .

Ziara ya Mkurugenzi Kayombo ya kutembelea katika kampuni hiyo imekukuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hicho.

Baadhi ya wananchi wanaofanya biashara jirani na eneo hilo wamesema kuwa kwa muda mrefu wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi, hivyo kuamua kufikisha kwa kiongozi shupavu mwenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi Mh. John Kayombo.


Baada ya malalamiko ya wananchi kumfikia ,bila kupepesa macho Mkurugenzi Kayombo akaenda New Habari House bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kuona hali halisi.

Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanayozunguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye mashine inayochapisha magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo.

Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia au kupunguza sauti hizo.

'' Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti,huu ni ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu"alisema Kayombo.
KAWAIDA...!

WAZIRI MKUU ACHOSHWA NA MADUDU BODI YA KOROSHO

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahutubia wananchi wa wilaya ya Nachingwea katika kiwanja cha Sokoine waziri mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na biashara ya korosho  Ikamlazimu waziri mkuu kumuagiaza Waziri wa kilimo afanye mapitio makini kweznye bodi nzima ya korosho
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

*Aagiza ifanyiwe marekebisho makubwa
*Aishangaa kung’ang’ania minada

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba kuifanyia marekebisho makubwa Bodi ya Korosho na menejimenti yake  baada ya kushindwa kusimamia zao hilo ipasavyo.
Amesema Serikali itafanya mapitio ya bodi zote za mazao ya biashara na imeanza na zao la korosho kisha zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai. Katika tathmini na mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa kutekeleza majukumu yake itavunjwa.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Alisema anaishangaa bodi hiyo kuacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia minada ya korosho na kuzuia baadhi ya wafanyabiashara wasiweze kununua zao hilo hali inayoashiria kuwepo kwa watu waliopangwa kununua bila ya kufuata utaratibu.
“Bodi leo wamejipa jukumu la kusimamia minada ! sio kazi yao ni kazi ya chama kikuu, zao la korosho linalimwa kutoka mkoani Ruvuma hadi Tanga, mtasimamia minada mingapi viachieni vyama vikuu. Vyama vikuu vikiharibu walalamikaji waje kwenu kama sehemu ya rufaa. Sasa nyinyi mnasimamia minada mnaharibu walalamikaji watakwenda kwa nani  ?  kwa nini mng’ang’anie kwenda kwenye minada,” alihoji Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alisema Ijumaa (Oktoba 14,2016) bodi hiyo  ilisitisha mnada wa korosho Lindi kwa sababu wanunuzi hawakuweka bondi (dhamana ya mauzo) na alishatoa maagizo ya kuwataka wanunuzi wasiruhusiwe kununua hadi waweke asilimia 25 ya malipo.
Alisema maagizo hayo aliyatoa tangu mwezi Aprili ila  watendaji wa bodi hiyo hawakuyafanyia kazi kwa wakati na badala yake waliwazuia wafanyabiashara waliotaka kununua korosho Lindi kwa madai ya kutokuwa na bondi huku wakiwaruhusu wa Mtwara.
“Kama kule walinunua bila bondi kwa nini wasiwaruhusu na Lindi wakanunua bila  bondi ili nijue kwamba mliamua kugoma kuteleza maelekezo ya Serikali? Au hamkumtaka aliyeshinda  nyie  mlikuwa mnamtaka nani nitashughulika na nyie,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa “Nimesema tukitoa maelekezo lazima yatekelezwe na atakayeshindwa hatufai, Mheshimiwa mbunge umelalamika juu ya bodi hawa ndio wabeba maelekezo hatujawahi kuona bodi ya korosho ikienda vijijini kuzungumza na vyama vikuu hata mara moja,”.
Akizungumzia kuhusu suala la wakulima kulazimishwa kufungua akaunti  za kupitishia malipo yao alisema wasiwalazimishe.“Waelimisheni wakulima umuhimu wa kufungua akaunti lakini si kwa kuwalazimisha wote wawe na akaunti hadi yule mwenye kilo tano…na akaunti yenyewe inafunguliwa kwa sh. 100,000,” alisema.
Alisema “’wanashindwa kutekeleza niliyowaagiza, halafu wanasingizia utendaji wao mbovu kuwa ndio maagizo yangu,’ niliwaagiza wapi,” alihoji na kuongeza kuwa  “yapo makundi yanafanya mambo yanavyotaka alafu yakiwazidi mambo wanasingizia viongozi wajuu na ndio wale wanaosema kila kitu nimeagizwa kutoka juu, juu wapi?
“Lazima tuendelee kudhibiti nidhamu ya vyombo vya tunavyoviunda kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Tutaendelea kusimamia nidhamu kwa taasisi zinazowahudumia wakulima nchi nzima,” alisisitiza.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alimkabidhi Waziri Mkuu msaada wa sh. milioni 16.3 pamoja na nguo kwa ajili ya kusaidia  wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 17, 2016



Mchezaji apigwa risasi na kufa

$
0
0

MCHEZAJI nafasi ya ulinzi wa timu ya Shooting Stars nchini Nigeria, Izu Joseph  amepigw arisasi na kufa akijiandaa kuingia uwanjani mjini Bayelsa.
Mchezaji huyo alikuwa mmoja wa timu ya  Oluyole Warriors ambayo ilimaliza nafasi ya 14 katika msimu uliopita (2015/2016) wa kinyang’anyiro cha Nigerian Professional Football League ambapo Enugu Rangers ndio mabingwa.
Twita kutoka katika klabu hiyo yenye makao makuu yake mjiniIbadan  iliandika; “A Shooting STAR is gone! Izu Joseph is gone! Flamboyant defender is gone! RIP, brother. What a life! May God strengthen his family #Tragedy.”
inasadikiwa kwamba mchezaji huyo alipigwa na risasi iliyotoka katika uwanja wa mapambano kati ya vikosi vya nchi hiyo Joint Task Force (JTF) vinavyokabiliana na wanamgambo katika delta za Niger Delta Oktoba 16 mwaka huu.
 Izu Joseph alijiunga na Shooting Stars mwaka  2014 kutoka timu ya  Bayelsa United wakati timu hiyo ya Ibadan ikiwa nafasi ya Nigeria National League.

WASHINGTON POST YAMKUBALI RASMI HILLARY CLINTON

$
0
0
The Washington Post  Moja ya magazeti yaliyoshiba umri nchini Marekani na linalojipambanua kwa namna linavyoripoti masuala ya siasa nchini humo limesema kwamba Hillary Clinton ndiye anayefaa kuwa Rais wa taifa hilo na watampigania.

Gazeti hilo ambalo linaingia katika miongoni mwa magazeti yaliyomkubali  mdada huyo kuwa Rais wa Marekani wamesema kwamba chaguo lao linatokana mdada huyo kuonesha umahiri mkubwa.

Gazeti hilo katika maoni yake ya mhariri limesema kwamba Hillary Clinton  ana uwezo mkubwa wa kuwa rais wa Marekani na wanampitisha bila hofu wala kusita. Maoni hayo yalisema mapungufu yake yamepitwa na uzuri anaouweza kuuleta kw amarekani kwa kuangalia uwezo wake.

Wamesema hawafanyi hivyo kwa sababu ya kumuona mpinzani wake ni dhaifu au mkorofi lakini kutokana na jinsi mdada huyo alivyoonesha umahiri wake.

Gazeti hilo limeandika, adding, "no, we are not making this endorsement simply because Ms Clinton's chief opponent is dreadful."

Clinton, the Democratic presidential nominee "is dogged, resilient, purposeful and smart," the newspaper wrote while acknowledging her many political and personal missteps of the past -- failings it said are outweighed by her strengths.

"She has executive experience. She does not let her feelings get in the way of the job at hand. She is well positioned to get something done," the daily wrote.

The newspaper took note of the former first lady's litany of shortcomings, writing: "We recognize that many Americans distrust and dislike Ms Clinton. The negative feelings reflect in part the bitter partisanship of the nation's politics today; in part the dishonest attacks she has been subjected to for decades; and in part her genuine flaws, missteps and weaknesses.

"We are not blind to those," wrote The Post, which nevertheless gave Clinton its full-throated support.

Kwa maoni hayo toka  moja ya magazeti yenye umri mrefu likiwa limeanzishwa  Desemba 6,1877  na likiwa limejishindia tuzo 47 za Pulitzer, waandishi wak wakishinda tuzo 18 za Nieman na wakiwa na tuzo 368 za Ikulu ya Marekani ni dalili wazi kwamba marekani imtarajie Rais wa Kwanza mwanamke kama walivyomtarajia rais wa kwanza Mweusi.
Gazeti hilo ndilo lililoibua kashifa ya Watergate iliyomfanya rais Richard Nixon ajiondoe .
Gazeti la The Washington Post  linatambulika kuwa moja ya magazeti yanayoongoza Marekani sanjari na The New York Times na The Wall Street Journal.  Linatambulika zaidi katika taarifa za kisiasa, Ikulu ya Marekani, Bunge na masuala ya serikali.

DED KIZIMBANI KW AKUTISHIA KUUA NA KUENDESHA GARI BILA LESENI WALA BIMA

$
0
0

MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mkinga, mkoa wa Tanga , Emmanuel Mkumbo (41) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa  Morogoro kwa tuhuma za kutishia kumuua kwa  bastola askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa na kuvunja sheria za usalama barabarani.

Mkumbo ambaye ni  mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam , leo alipandishwa kizimbani na kusomewa  mashtaka hayo mbele ya hakimu Agripinas Kimanze , kutoka kwa  Mwendesha mashtaka wa Serikali ,Sunday Hyera, akisaidiana na Ediga Bantulaki.

Kwa mujibu wa waendesha mashitaka hao wa Serikali kuwa,  mtumiwa huyo anakabiliwa na kesi mbili ya kwanza ikiwa ni kesi ya jinai kifungu cha 226 ya mwaka 2016 na ya pili ni kesi ya usalama barabarani kifungu cha 222.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 15, mwaka huu eneo la Mkambarani, wilaya ya Morogoro katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaamm wakati akiendesha gari aina ya Totota Pajero yenye namba za usajili T 845 CTJ .


Kosa la kwanza linalomkabiri Mkurugenzi mtendaji huyo ni  kujaribu kumtishia kumuua kwa bastola askari aliyejulikana kwa jina la Koplo Titunda, akiwa katika majukumu yake ya kikazi  na makosa mengine ni  kuendesha gari lenye namba T845 CTJ aina ya Totota Pajero bila ya kuwa na leseni na kuendesha gari bila  bima.

Leonardo DiCaprio abambwa akila denda kwa modo Nina Agdal

$
0
0
Leonardo DiCaprio (41) kwa mara nyingine tena amedhihirisha kwamba yeye na mdenishi modo, Nina Agdal (24) ni kitu kimoja baada ya kuonwa wakibusiana katika fukwe ya malibu mwishoni mwa wiki.
Hii ni baada ya kuonwa wakitembea kwapamoja katika mitaa ya New York City Septemba 29 wakiwa na mazingira ya kutulia zaidi.





Hiyo Alhamisi ya September 29 mjini New York City walibambwa wakipata chakula cha mchana pamoja eneo la Bar Pitti kabla ya kuingia mitaani.
Tangu wakati huo kumekuwepo na maneno kwamba wawili hao wanataka kufunga ndoa ya kisiri, lakini mameneja wao wamekanusha taarifa hizo.
Leo ambaye unaweza kumuita kama msela mwandamizi katika mitaa ya Hollywood na ambaye amewapa shida sana warembo toka alipocheza filamu ya Titanic kwa sasa anaonekana kuzama katika penzi la Nina Agdal.
Nina,  anasema Leo ni boifrendi mwema kabisa akimpa kampani katika mambo yake mengi na akionesha kumjali.
Na wakiwa Malibu Leonardo DiCaprio alionwa na mapaparazi akimbusu kimahaba mdenishi wake.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Akutana na wamiliki wa Daladala

$
0
0





Na Mathias Canal

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekutana na umoja wa wamiliki wa Daladala Wilayani Iringa katika ukumbi wa Siasa na kilimo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Baadhi ya madereva na Makondakta wameomba kurudishwa katika Stendi ya miyomboni kama ilivyo kuwa hapo awali wakidai kuwa eneo la walilohamishiwa kwa sasa la Mashine tatu ni finyu na lina msongamano mkubwa wa watu jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wananchi.


Dc Kasesela amesema kuwa kurudi katika standi ya miyomboni ni jambo lisilo wezekana kutokana na eneo hilo kuwa dogo na limezungukwa na makazi ya watu pamoja na majengo makubwa ya biashara jambo ambalo linafanya eneo hilo kuwa hatarishi zaidi kama iwapo kunaweza kutokea janga la moto.

"Unajua Miyomboni ni padogo sana pia pamejibana sasa kama ikitokea moto umewaka pale ni ngumu sana kupafikia kwa wepesi lakini pia Watu wa zima moto ndio waliopendekeza kuwa kituo kile kihamishwe sasa nadhani mnafahamu kuwa sheria ya zimamoto huwa ni ngumu kuipinga" Alisema Kasesera

Lakini pia amewataka madereva kuacha kutumika kisiasa kwani wanaofanya hivo wanafanya kwa maslahi yao binafsi.

DHIBITINI BIASHARA ZA MAGENDO-MAJALIWA

$
0
0
17 Oktoba, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi kuhakikisha anadhibiti wafanyabiashara wanaonunua korosho kwa njia ya magendo na atakayekamatwa achukuliwe hatua.
Pia amewataka wananchi wa mkoa huo kutouza korosho zao kwa walanguzi maarufu kangomba na badala yake wazipeleke kwenye masoko rasmi ili waweze kupata tija.
“biashara ya kangomba ni mwiko atakayekamatwa amebeba korosho za kangomba atachukuliwa hatua za kisheria na chombo chake cha usafiri kitataifishwa” amesema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Oktoba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Mibure, Namakuku, Ng’imbwa, Chienjele, Mkata, Mitope na Kitandi
“Marufuku kuuza korosho kwa kangomba kwani mnapata hasara kipimo kinachotumika si rasmi. Mkoa kamateni na taifisheni korosho na chombo cha usafiri kitakachotumika kubeba korosho za magendo,” amesema.
Amesema ni vema wakulima wakaachana na biashara ya kangomba kwa sababu haina tija na badala yake wasubiri na kwenda kuuza korosho zao katika minada kwa bei nzuri.
“Mwaka huu korosho itauzika kwa bei ya juu zaidi isiyopungua sh.3500, msikubali kuuza korosho mlizizitolea jasho kwa walanguzi wanaotumia kangomba kwa sh. 1000 huu ni wizi, kwani kile kipimo cha wanachotumia ni sawa na kilo mbili, hivyo unapoteza zaidi ya sh. 6000”. amesema
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao kuongeza idadi ya mazao ya  biashara na kuanza kulima alizeti ambapo wataweza kupata faida ya zaidi ya sh. milioni moja kwenye  shamba la ukubwa wa ekari moja.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa miezi miwili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue kuhakikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mibure unakamilika.
“Ndani ya miezi miwili Zahanati iwe imekamilika, tuache kuzungumza sasa ni vitendo tu”amesema.
Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya ufuta na karanga cha Ilulu kilichoko wilayani Nachingwea na kukuta kimetelekezwa. Ameagiza uongozi wa kiwanda kumpelekea nyaraka zote za umiliki. Kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa marehemu Abbas Gulamali na sasa kinasimamiwa na familia yake.
“Nawahitaji Dodoma Oktoba 22 waje na nyaraka zao ili nijue walipokabidhiwa kiwanda hiki walitaka kufanya nini,” alimuagiza Msimamizi wa Kiwanda hicho Dinna Mavumbi kuwajulisha wahusika.
Waziri Mkuu alisema haiwezekani kiwanda hicho kilichojengwa kwa fedha za umma kikatelekezwa bila ya kuendelezwa. Alisema baada ya kupitia nyaraka zao ataangalia namna ya kurudisha majengo hayo ya kiwanda kwa  Serikali. “Hatuwezi kuacha raslimali hii ikiwa imetelekezwa msituni inaharibika.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 17, 2016


WAZIRI MKUU ASIKITISHWA NA MWEKEZAJI KUBADILI MATUMIZI YA KIWANDA NA KUKITELEKEZA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyo haribika ambayo yalikuwa yanamilikiwa nakiwanda cha kukamua ufuta  ILULU kiwanda hicho kipo wilani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliye kichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala lakuhifadhia bidhaa kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi    picha zote  na Chris Mfinanga

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda  cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji amekifanya kuwa Ghala nakukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa Kiwanda hicho kipo wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi


Msimu wa Tigo Fiesta wahitimishwa mikoani kwa kumalizia Jijini Mbeya

$
0
0
BarakaDaPrince akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa Mbeya waliojitokeza katika tamasha la  Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumapili

Benpol katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia ijumaa

JohMakini akitumbuiza katika tamasha la Tamasha la tigo fiesta


Jux 


Wasanii Man Fongo na  Shilole   wakitoa   burudani ya singeli kwenye  tamasha la Tigo fiesta lililofanyika uwanja wa  Sokoine  jijini Mbeya usiku  wa  jumapili




Mr blue akitumbuiza umati wawakazi wa Mbeya waliojitokeza katika viwanja vya Forest Mbeya

Msanii Msami akiwa  amemnyanyua   mcheza shoo wake stejini  kuonyesha   uwezo wake wa kumiliki  jukwaa  kwenye  tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika  uwanja wa  Sokoine  jijini Mbeya usiku    wa jumapili.



Wasanii Roma Mkatoliki   na Stamina wakionesha  umahiri  wao  wa  kufokafokakwakupokezana   kwenye   tamasha la Tigo fiesta lililofanyika  uwanja wa   Sokoine  jijini Mbeya usikuwa  jumapili.



Mashabiki wakimshangilia Roma Mkatolili
Maelfu ya wakazi wa Mbeya wakifurahia burudani toka kwa wasanii waliotumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta

Weusi wakilishambulia jukwaa la Fiesta


WATAKIWA KUITUMIA MV NYEHUNGE II KUJIINUA KIUCHUMI

$
0
0

Mwonekano wa Mv Nyehunge kwa ndani, sehemu ya abiria kukaa.

Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, mwishoni mwa wiki amefanya uzinduzi wa Meli Mpya ya Mv Nyehunge ya pili (II) inayofanya safari zake kati ya Mwanza na Ukerewe na kuwataka wakazi wa Ukerewe kuitumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi.

Mongella alisema Meli hiyo itasaidia kuondokana na adha ya usafiri kwa wakazi wa Visiwa vya Ukerewe kwa kuwa imeongeza idadi ya Meli zinazofanya safari kati ya Jiji la Mwanza na visiwa hivyo.

Aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kusafirisha bidhaa zao kati ya Ukerewe na Jiji la Mwanza ili kujiinua kiuchumi huku akisisitiza Kampuni ya Nyehunge inayomiliki Meli hiyo kuzingatia vigezo vya usalama katika uendeshaji wa safari zake.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyehunge, Said Mohame, alisema Meli hiyo inaongeza safari kati ya Visiwa vya Ukerewe na Jiji la Mwanza na kufikia safari tatu kwa siku huku suala la nauli nafuu likizingatiwa ili kuondoa changamoto ya usafiri waliyokuwa nayo wakazi wa Ukerewe. Nauli za Ukerewe katika Meli hiyo ni Shilingi 6,000 kwa 7,000.

Baadhi ya wasafiri wa Ukerewe walipongeza ujio wa Meli ya Mv Nyehunge ambapo wamebainisha kwamba itawasaidia kusafirisha kwa wakati bidhaa na mazao ya chakula kati ya Ukerewe na Jiji la Mwanza.

Meli hiyo ya Mv Nyehunge II ina uwezo wa kubeba abiria 500, magari madogo 40 na tani 284 za mizigo ambapo imejengwa na kampuni ya wazawa ya Songoro Marine Transport ya Jijini Mwanza kwa zaidi ya shilingi Milioni 800.

Tazama HAPA Uzinduzi Ulivyokuwa

MKE WA WAZIRI MKUU MARY MAJALIWA AMEIOMBA JAMII MASHIRIKA NA MAKAMPUNI KUWASAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI HAPA NCHINI

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa kwaniaba ya familia yake ametoa mchango wa fedha zaidi ya shilingi laki sita kwa Mama Hakika Swalehe kwa ajili ya kuwasidia watoto wake wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) Rashidi  Juma (5)na Iklamu Juma (miezi 9) Mama Majaliwa amehidi kuwasidia watoto hao vifaavingine vya kutunza ngozi  Watoto hao wanaishi katika kijiji cha Mtope wilaya ya Ruwangwa Mkoani Lindi  
Picha na Chris Mfinanga

Njombe wapewa mafunzo ya ulishaji watoto wachanga na wadogo

$
0
0

Ofisa Lishe Mkoa wa Njombe Bertha Nyigu (aliyesimama) akitoa mafunzo ya  namna ya kunyonyesha watoto mapacha kwenye mafunzo kwa watoa huduma za afya Njombe Mjini

Watoa huduma za afya Halmashauri ya mji Njombe wamepatiwa mafunzo ya ulishaji watoto wachanga na wadogo.
Akieleza madhumuni ya mafunzo hayo afisa mafunzo ya lishe kutoka taasisi ya chakula na lishe doris katana amesema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuinua kiwango cha uelewa kuhusu ulishaji watoto wadogo na wachanga.
“kama tunavyojua ulishaji wa watoto wachanga na wadogo ni muhimu sana na unasaidia sana   kupunguza vifo vya watoto na kupunguza uwezekano wa kupata  magonjwa ya kuharisha na magonjwa mengine  ambayo yanaondoa sana uhai wa watoto wetu hapa tanzania. Kwa kupata hii elimu ya unasihi wa ulishaji watoto wachanga na wadogo tunategemea kiwango chao cha elimu kitakua na wataweza kutoa elimu ipasavyo kwa ufasaha zaidi kwa wamama ambao wana watoto kuanzia pale mama anapojifungua mpaka pale mtoto anapokua na umri chini ya miaka mitano.”Alisema doris.
Aidha doris amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga vituo vya huduma ya afya kwani katika vituo hivyo ndio sehemu pekee ambapo mama anahudhuria kwanza akiwa mjamzito hivyo kwa kipindi mama anapokua mjamzito akiweza kupewa taarifa sahihi ya ulishaji mtoto wake tunategemea pale anapojifungua ataweza kumuhudumia mtoto  kwa ufanisi zaidi, na hata pale anapojifungua kuna vitu ambavyo mama anatakiwa asaidiwe na apewe taarifa sahihi zitakazomwezesha kunyonyesha mtoto wake chini ya miezi sita na hata pale baada ya miezi sita anapomwanzishia chakula cha nyongeza aweze kumwanzishia kwa usahihi zaidi na kuweza kuhakikisha mwanae anakua na afya njema.
Akitoa takwimu za viwango vyunyonyeshaji kitaifa afisa mafunzo huyo amesema kuwa kadiri miezi ya mtoto inavyozidi kuongezeka ndivyo hivyo asilimia na kasi ya unyonyeshaji inazidi kupungua jambo ambalo linakosesha virutubishi muhimu kwa mtoto kwa kukosa kupata maziwa ya mama kwa wakati muafaka.
Takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa watoto wanaopata maziwa ya mama pekee chini ya miezi miwili ni 70.0%, 42% ikiwa hupata maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi 2-3 na 13% ya watoto hupata maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi 4-5. Ameendelea kusema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 33 ya watoto wenye umri chini ya miezi 6 huanzishiwa vyakula vya nyongeza hali inayopelekea tatizo la udumavu kwa watoto.
Awali, akifungua mafunzo hayo kaimu mganga mkuu halmashauri ya mji njombe dkt allen kitalu amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watoa huduma wa halmashauri ya mji njombe kwani licha ya kuwa mkoa wa njombe umebarikiwa kuwa na vyakula vya kutosha na uchumi mzuri lakini bado mkoa huo unaongoza kwa tatizo la utapiamlo.
Kwa wakati huo huo dkt kitalu amewataka washiriki wa mafunzo kuwa watulivu na wasikivu wakati wote wa mafunzo ili elimu watakayoipata ikatumike vizuri na kwa wakati sahihi ili kuhakikisha kuwa wanawasaidia wale wanaohitaji msaada walengwa wote wanafikiwa na mabadiliko yanakuwepo.
Mafunzo  hayo  yatakayofanyika kwa muda wa siku tano yanahusisha wahudumu wa afya 20 kutoka katika zahanati 18 zilizopo katika halmashauri ya mji njombe.
mwisho


UKIPOTEZA SMARTPHONE UKIWA NA AKILI INAREJEA, JIUNGE HIVI...

$
0
0

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kusiana na huduma mpya ya linda simu ya Airtel Simu Bima itakayowasaidia wateja wote wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya Airtel Money, kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce na kushoto ni Muwakilishi wa shirika la Bima la UAP bw, Charles Matondane

WATEJA wa simu wanaotumia simu za kisasa za smartphone wamezinduliwa huduma ya  kuziwekea bima simu zao pindi zinapopotea au kuibiwa.
Huduma hiyo imewezeshwa na Kampuni ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP .
Huduma hiyo imezunduliwa jana na kwamba bima hizo zitalipwa kupitia huduma ya Airtel Money.
Huduma hiyo mpya  ya “Airtel SimuBima” itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kampuni yake imeongeza sababu nyingine kwa wateja wao kuendelea kufurahia huduma zao.
“Mteja ambaye ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena” alisema Mmbando.
Akifafanua zaidi alisema:“Mteja wa Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima”mara baada ya kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore na kusajili taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na gharama ya simu yake  na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama ya Bima ya simu hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa anailipa kwa kila mwezi.”
Alisema kwa mpango huo wa ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na shirika la bima la UAP kupitia ‘Airtel SimuBima’  unahamasisha watumiaji wa simu za mkononi kununua simu orijino ili waweze kufurahia huduma hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UAP Bw, Raymond Komanga alisema “tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa Bima ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na kutujulisha sisi.”

Viewing all 9109 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>