Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9117 articles
Browse latest View live

WAHARIBIFU WA MAZINGIRA WAKAMATWE-MAJALIWA

$
0
0

Hii ndio Goba Kibululu eneo la John Luwanda ni balaa toka 2012 mpaka leo wachimba mchanga mtoni na viongozi wanajua

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mkoa wa Lindi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaoharibu mazingira kwa kufyeka na kuchoma moto misitu kwa sababu wanaharibu mazingira na kusababisha ukame.
Amesema mkoa huo upo hatarini kugeuka jangwa na tayari vyanzo vingi vya maji vimeanza kukauka kwa sababu ya uharibifu wa mazingira unaotokana na watu kufanya shughuli za kijamii kwenye vyanzo vya maji.
 Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 18, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Nanjaru, Nachinyimba, Nambiranje, Mkaranga, Nandenje, Nachinyimba na Mandarawe.
 Amesema wakulima wa ufuta wanatakiwa kuendelea kutumia mashamba yao ya zamani na kuacha tabia ya kufyeka misitu kila mwaka na badala yake waanzishe mpango wa upandaji miti ili kuepusha taifa kugeuka kuwa jangwa.
 “Vyanzo vya maji vimekauka kwa sababu tumekata miti mingi. Mito yote iliyokuwa inatiririsha maji imekauka. Viongozi wa mkoa hakikisheni misitu inalindwa na atakayekutwa analima kwenye vyanzo vya maji akamatwe,” amesema.
 Waziri mkuu aliongeza kuwa “Ukataji miti huu unaoendelea katika maeneo yetu  hakutosababisha kukosekana kwa maji tu, bali  hata mazao yatapungua. Jambo hili  itasababisha njaa katika vijiji vyetu, hivyo tuache kukata miti.
 Waziri Mkuu amesema kwa sasa Serikari inatumia gharama kubwa kuchimba visima virefu kutafuta maji. Amesema zamani walikuwa wanachimba mita 20 au 30 wanakuta maji na gharama yake ilikuwa sh. milioni 35, ambako kwa sasa wanalazimika kuchimba mita zaidi ya 150 kwa gharama y ash milioni 75 kwa kisima kimoja.
 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi,amewataka watendaji wa kata na vijiji kuimalisha ulinzi wa maeneo ya misitu na maji, na atakayeshindwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.
 “Hatuko tayari kutengeneza jangwa hivyo tutapamba na wale wote wenye tabia za kuchoma moto misitu au kulima kwenye vyanzo vya maji,” amesema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMNNE, OKTOBA 18, 2016



UNESCO YASAINI MIKATABA NA SERIKALI YENYE THAMANI YA DOLA MILIONI SABA KWA AJILI YA KUSAIDIA ELIMU

$
0
0
UNESCO yasaini mikataba na serikali yenye thamani ya dola milioni saba kwa ajili ya kusaidia elimu

Katika kusaidia kuboresha elimu nchini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesaini mikataba miwili na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyo na lengo la kusaidia elimu nchini.

Mkataba wa kwanza unahusu mradi unaofahamika kama 'Empowering Adolescent Girls and Young Woman through Education' mradi ambao umedhaminiwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA) kwa kiasi cha pesa cha Dola Milioni tano (5,000,000), mradi ambao unataraji kufanyika katika wilaya ya Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Micheweni, Pemba.

Mkataba wa pili unahusu mradi wa 'XPRIZE - Promotion of Early Learning Through the use of Innovative Technologies' ambao umedhaminiwa na UNESCO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula (WFP) kwa kiasi cha pesa cha Dola Milioni mbili (2,000,000) ambapo utahusisha watu wa miaka 15-18 ambao hawapo shuleni kutoka Arusha na Tanga ambapo watapatiwa tablet ambazo zitakuwa na programu tumishi za kujifunza.

Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo, Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema mipango ya UNESCO ni kuona inawasaidia watoto ambao hawasomi licha ya kuwa na umri wa kuwa shuleni wakipata nafasi ya kusoma ili kupunguza idadi ya watoto ambao hawapo shuleni duniani ambapo takwimu zinaonyesha wanazidi Milioni 263.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza kuhusu mradi wa Empowering Adolescent Girls and Young Woman through Education na XPRIZE - Promotion of Early Learning Through the use of Innovative Technologies.

"Tunaandika histori leo sio kwa Tanzania bali dunia nzima, maana makubaliano yataleta ushirikiano kati ya WFP, UNESCO na Wizara ya Elimu kuwasaidia watoto zaidi ya Milioni 263 ambao hawapo shuleni duniani na kutumia nafasi ya teknolojia kutafuta suluhisho la kuwasaidia watoto hawa,

"Tunaishukuru Wizara ya Elimu kwa kutuamini, nawashukuru WFP kwa kuwa pamoja nasi na kwa washirika wengine ambao wamekubali kuungana nasi kwa ajili ya kufanikisha hili," alisema Rodrigues.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish alisema msaada huo utaweza kusaidia kuboresha elimu nchini hasa katika kipindi hiki ambacho serikali inajipanga kutoa elimu kisasa kwa kutumia njia za kidigitali na hivyo ni mwanzo mzuri kwa mfumo ambao wanajipanga kuanza kuutumia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish akitoa neno la shukrani kwa niaba ya serikali.

"Kwa niaba ya serikali ya Tanzania tunashukuru kwa msaada wenu kwa kuwa tayari kusaidia elimu ya Tanzania kwa kutumia teknolojia, tunataka kutoa elimu kwa njia ya kidigitali na nyie mmekuwa tayari kutusaidia tunawashukuru,

"Madhumuni makubwa ni kutaka kuboresha elimu na tukaona ni vyema kushirikiana na mashirika mengine ili kuwasiadia watoto kupata elimu bora kwa kufuata zile njia tatu, Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, shuleni atafundishwa na akirudi nyumbani anaweza jifunza kusoma kwa kutumia tablet," alisema

Kwa upande wa Mwakilishi wa WFP nchini, Michael Dunford alisema WFP imekuwa ikishirikiana na serikali ya Tanzania katika maeneo mbalimbali hivyo kuwa sehemu ya kusaidia elimu nchini ni jambo kubwa na lengo lao ni kuona teknolojia inakuwa na faida kusaidia elimu kukua.

Mwakilishi wa WFP nchini, Michael Dunford akielezea jinsi WFP imeguswa hata kufikia hatua ya kuwa tayari kushirikiana na UNESCO kufanya mradi wa XPRIZE.

"WFP na Wizara ya Elimu wamekuwa wakishirikina kwa muda mrefu na hata UNESCO tunataka kutumia teknoloji kusaidia elimu, kuona jinsi gani teknoloji itatumika madarasani na WFP tayari ina watu ambao watasimamia kuhakikisha jambo hili linafanikiwa," alisema Dunford.

Nae Mkurugenzi wa KOICA nchini, Joonsung Park alisema mradi huo ni sehemu ya miradi ambayo KOICA imepanga kuifanya kwa ajili ya kusaidia kukuza elimu katika nchi ambazo zinaendelea.

Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akieleza jinsi miradi hiyo itakavyofanya kazi.
Mkurugenzi wa KOICA nchini, Joonsung Park akizungumza kuhusu mradi ambao wamedhamini ambao pamoja na una lengo la kusaidia elimu na zaidi kwa wasichana.

"Huu ni moja ya miradi mitatu ambayo KOICA imekubaliana na UN kwa ajili ya kuifanya na kusaidia elimu, tumekuwa tukishirikiana na UNFPA, UNWOMAN, UNV katika kufanikisha hilo na matarajio yetu ni kuwa ushirikiano wetu uzidi kudumu na kuleta matokeo mazuri," alisema Park.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish wakisaini mkataba wa mradi wa XPRIZE.


Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish wakisaini mkataba wa mradi wa Empowering Adolescent Girls and Young Woman through Education.

VIJANA WATAKIWA KUJIKITA ZAIDI KUFANYA KAZI

$
0
0


Kufuatia changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam kuelekea sherehe za maadhimisho ya wiki ya Umoja Mataifa, amesema vijana inabidi wawajibike katika kuleta maendeleo ya uchumi kwenye jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.

Pia amesema vijana waache kuhoji serikali kuwa inawafanyia nini badala yake wawe wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Taifa lao.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

"Tuna kazi kubwa ya kujenga fikra za vijana kwamba ili kufanikiwa katika maisha siyo lazima kuajiriwa, vijana wengi ukiwahoji wanakwambia changamoto kubwa wanayoikabili ni ukosefu wa ajira. Lakini wanasahau kuwa changamoto zipo nyingi zinazowakabili," amesema.

Prof. Ole Gabriel amezitaja changamoto nne zinazokabili vijana ambazo zinasababisha washindwe kujiajiri au kushindwa kujiendeleza pindi wanapojiajiri kuwa ni, ukosefu wa fikra kutokana kwamba wengi hawaziruhusu fikra zao kubuni mbinu za kujiajiri. Changamoto nyingine aliyoitaja ni vijana kukosa uelewa, mbinu na ubunifu wa kuongeza thamani ya shughuli wanazofanya.

Changamoto nyingine aliyoitaja ni mfumo mbovu na usio rafiki kwa vijana hasa mifumo duni ya upatikanaji mitaji na masoko, hususani katika kipindi hiki ambacho kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.

Ameshauri kuwa "Hivi sasa kuna elimu ya ujasiriamali lakini niseme tu haitomsaidia kijana kujikwamua sababu hutoa elimu ya uzalishaji pekee. Ili kijana afanikiwe na ujasiriamali, kwanza inabidi apewe elimu ya kufanya utafiti wa bidhaa inayohitajika kwa kipindi husika, akishajua bidhaa hitajika ndipo afanye uzalishaji kisha hatua ya mwisho kutafuta masoko ambayo tayari ameshayafanyia uchunguzi."

Pia ameshauri vijana kuwekeza katika biashara kilimo kwa kuwa ndiyo sekta pekee yenye fursa ya kutoa ajira kwa wingi kwa kuwa imeajiri asilimia 84 ya vijana.

"Tanzania ina vijana zaidi ya milioni 16.2 ni sawa na asilimia 70 ya watanzania, waliofanikiwa kuajiriwa katika sekta binafsi ni milioni 1, waliojiajiri milioni 1.1 waliopo katika sekta ya umma ni 18,8000 na katika sekta ya kilimo wapo vijana milioni 13.2 na bado nafasi zipo katika sekta hiyo," amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza machache kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

Hata hivyo, Prof. Gabriel amewaasa vijana kutotumia utandawazi vibaya hasa mitandao ya kijamii kutokana kwamba imekuwa sababu ya vijana wengi kutokuwa na maadili.

"Utandawazi unabomoa uwezo wenu wa kufikiri, zamani vijana walikuwa wanakimbilia kuwekeza katika sekta ya kilimo ila sasa kutokana na utandawazi wanakimbilia kutafuta ajira hata kama fursa hakuna," amesema na kuongeza.

"Msipoangalia miaka michache ijayo tutakuwa watu wa teknolojia na mitandao. Maadili mema tuliyojengewa yatapotea kwa sababu ya kufikiri kwamba mitindo ya kimaisha kutoka nje ndiyo inafaa kuliko ya kwetu, inabidi turudishe yale maadili ya zamani sababu nchi yoyote isiyokuwa na maadili, tamaduni imeparanganyika na haina maendeleo," amesema.

Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza kwa niaba ya UN amesema kuwa shirika hilo litahakikisha linawezesha vijana kushiriki katika maendeleo ya uchumi kwa kuwainua kiuchumi pamoja na kutoa elimu ya namna ya kujiajiri.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza jambo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mbunifu wa mavazi Johari Sadiq akizungumzia jitihada, changamoto, fursa na mafanikio aliyoyapata katika yake ajira binafsi kama mtoto wa kike, kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
MC maarufu nchini ambaye pia ni Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda akizungumzia ajira yake binafsi na mafanikio aliyonayo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji ambaye ni Mjasiriamali kijana Stella Imma, akizungumza kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mshauri na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) akitoa hamasa kwa vijana kutoka shule mbalimbali na vyuo waliohudhuria kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwanafunzi Matilda Moses wa kidato cha pili kutoka shule ya sekondari ya Gerezani akimuuliza swali Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) juu ya kusimamia maadili ya Kitanzania na kuwaelimisha wazazi namna bora ya kusimamia malezi ya watoto wao jijini Dar es salaam wakati wa kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililoandaliwa na Shirika Umoja wa Mataifa linalishughulikia Maendeleo (UNDP).
Pichani juu na chini vijana pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakiuliza maswali kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa tatu kulia) akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji MC Anthony Luvanda akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwatambulisha baadhi maafisa wa wizara hiyo waliochini ya idara yake ambao ni vijana na wamepata nafasi ya ajira serikalini na kuwasifia kwamba ni wachapakazi na hodari katika vitengo vyao wakati wa kongamano la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Vijana wakiwa wamejipanga huku wakishikilia mabango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwapiga msasa vijana kuhusiana na Malengo ya Dunia kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Picha ya pamoja.
Pichani juu na chini ni Sehemu ya wanafunzi wa shule mbalimbali na vyuo vikuu walioshiriki kongamano la vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).





Baadhi ya maafisa wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa katika picha ya pamoja wakati wa kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

DOLA 20,000 KUCHUKULIWA NA WABUNIFU WA KIDIGITALI KATIKA TUZO YA TANO YA MWAKA YA TIGO KIDIGITALI YA CHANGE MAKERS

$
0
0

Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael akizngumza na wanahabari wakati wa Uzindizi wa shindano hilo leo Jijini Dar es salaam 
 Kampuni ya simu ya Tigo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Reach For change wamezindua shindano la Tuzo ya mwaka ya kidigitali ya Tigo Change Makers,shindano linalolenga kuwatambua na kuwasaidia wajasiriamali jamii kwa kutumia zana za kidigitali na Technologia katika kuboresha Jamii pamoja na matokeo yake kwa Vizazi vya Baadae,ambapo kwa mwaka huu Tigo inaangalia ubunifu uliojikita katika mtazamo wa elimu kupanua kujumuisha kidigitali na ambao unalenga kusaidia shiughuli za Ujasiriamali.
 Faraja Nyarandu Pichani  alishinda dola 20,000/- Mwaka 2014 katika shindano la @TigoTanzania #DigitalChangemakers.leo akizungumza mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi na kuwezeshwa na Tigo Tanzania
Jumla ya fedha taslim dola za marekani 20,000 zitatolewa kwa kila wazo litakaloshinda kati ya mawazo mawili yatakayoshinda na hivyo kutoa  nafasi ya kuingia katika malezi ya Reach For change,mafunzo ya kibiashara na mtandao wa dunia wa wajasiriamali wengine wa kijamii.ambapo kipindi cha kutuma maombi kwa ajili ya kushiriki katika shindano hilo kimefunguliwa Rasmi leo hadi November 21,2016.

Akiangumza katika mkutano wa wanahabari wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael amesema kuwa Tigo inayo furaha kuendesha Tuzo ya kidigitali ya Tigo change makers mwaka huu ikiwa na mtazamo Mpya,huku akisema kuwa Timu ya tigo ina hamu sana ya kusaidia Ubunifu wa Kidigitali na shughuli za ujasiriamali nchini Tanzania.

Shisael ameongeza kuwa Tuzo ya kidigitali ya Tigo Changemakers ni niia kubwa ya kuwasaidia wabunifu kijamii wazuri walio na weledi ambao wanahitajika nchini katika kuwawezesha kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya Kidigitali.
Ikiwa ni mwaka wa Tano ambapo Tigo Reach For change wanaendesha shindano hilo la kutafuta mjasiriamali jamii,Bi Woinde amepongeza kazi za washindi waliotangulia na kuhimiza wengine kushirikiana nao katika mawazo yao.
“Hivi sasa tutawasaidia wajasiriamali 9 kupitia mkakati wa kidigitali wa Tigo Changemakers.wametumia vizuri fedha walizopewa,mafunzo ushauri,na Zaidi ya yote kuleta mabadiliko nchini Tanzania”amesema Meneja huyo wa Huduma za kijamii Tigo.
Carolyne Ekyarisiima Mshindi wa mwaka 2015 akieleza machache mbele ya wanahabari
Akitaja mifano ya washindi ambao wamenufaika na shindano hilo tangu lianzishwe  amesema kuwa Carolyne Ekyarisiima ni mmoja washndi wa tuzo ya Tigo Change makers ambaye amekua akifanya kazi ya kuziba pengo la kijinsia katika Technologia ya Habari na mawasiliano kupitia ujasiriamali kijamii wa Vifaa na watoto wa kike(Apps &girls)
“Mwaka 2015 Carolyne alileta mabadiliko kwa wasichana 1000,kupitia mfumo wa klabu mashuleni, warsha,maonesho,mawasiliano ya simu,kambi za mijadala na mashindano”amesema Shisael na kuongeza kuwa “sio tu kwamba mkakati huu unasaidia kuhakikisha watoto wengi wa kike kuzifikia Teknolojia za kidigitali,hali kadhalika inawezesha kuwa Viongozi wa baadae wa Teknolijia Ya habari na mawasiliano.

Carolyne ni mmoja wa mfano wa wabunifu weledi wa kidigitali ambao Tigo inawatafuta ili iwasaidie kupitia tuzo ya mwaka huu,Shisael amesema anatarajia kupitia Upya ubunifu wa kidigitali wa kuvutia ambao utawasilishwa katika shindano la mwaka huu.

WAJASIRIAMALI 3000 KUNUFAIKA NA MRADI WA KUKU CHOTARA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Namaingo Business Agency (T) LTD, Ubwa Ibrahim akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wajasiriamali kuhusu jinsi ya kuzichangamkia fursa mbalimbali za ujasiriamali katika Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga, Dar es Salaam leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Namaingo Business Agency (T) LTD, Ubwa Ibrahim akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wajasiriamali kuhusu jinsi ya kuzichangamkia fursa mbalimbali za ujasiriamali katika Makao Makuu ya Taasisi  hiyo, Ukonga, Dar es Salaam jana.
Kushoto ni Mratibu wa Wanahabari wa kampuni hiyo, Jamila Abdalah.
 Ubwa akifafanua jambo wakati wa mkutano huo, ambapo aliwaomba wanahabari kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi kuhusu fursa hizo za kijasiriamali ili waondokane na umasikini.

 Baadhi ya wanahabari na wajasiriamali wakiwa katika mkutano huo

KAMPUNI ya Namaingo Business Agency (T) LTD, mwezi ujao inazindua mradi mkubwa wa ufugaji kuku chotara wenye thamani ya sh. bilioni 30 utakaowawezesha wananchi 3,000 wa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Makao Makuu ya kampuni hiyo, Ukonga, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ubwa Ibrahim  amesema mradi huo mkubwa na wa aina yake umeanza kujengwa Lindi Vijijini.

Amesema kuwa watakaonufaika ni wananchi wa mikoa hiyo watakao timiza taratibu zote, ambapo kila mmoja atakopeshwa na benki sh. mil. 10 ambazo zitakwenda moja kwa moja kwenye mradi wa kuku utakaokuwa unaendeshwa na watalaamu kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Anasema kuwa mradi mzima utasimamiwa na JKT kwa ushirikiano na Kampuni ya Namaingo ambapo mfugaji atafaidika kwa kupata faida baada ya mauzo yatakayokatwa gharama zote za mradi huo.

Katika mradi huo kila mwanachama atajengewa banda la kufugia kuku chotara 1,000 watakaofugwa kisasa na kwa utalaamu unaotakiwa ili kupata kuku wenye ubora na kilo nyingi hivyo kuuzwa kwa bei nzuri.

Alitaja baadhi ya vigezo na taratibu anazotakiwa mwanachama kukamilisha kabla ya kupatiwa mkopo huo kuwa ni; Kwanza kuwa mwanachama wa Namaingo, kufungua akaunti katika benki za NMB, CRDB,  pia kujiunga na NSSF, NHIF, PSPF, Bima ya Maisha, kusajili jina la biashara Brela.

Pia mwanachama anatakiwa kuwa na Tin number,  ajiunge Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja (UTT-AMIS),  awe na leseni ya biashara, cheti cha TDFA, cheti cha GSI, cheti cha TBS bila kusahau kopi ya kitambulisho cha mpigakura, leseni ya udereva au kitambulisho cha utaifa.

Pia Kampuni hiyo inatarajia kufungua miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji mikoani itakayowanufaisha wananchi wengi.

Nape awasilisha hati ya sheria ya huduma za habari kwa makati ya bunge

$
0
0
Waziri Nape akiwasilisha 



WADAU wa habari leo wanaanza kuujadili muswada wa sheria ya huduma za

habari huku wabunge wakisema jambo hilo linahitaji mjadala mrefu ili
kulinda maslahi mapana ya tasnia ya habari na wanahabari nchini.

Wakizungumza jana mara baada ya Waziri wa   Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye kuwasilisha hati ya muswada huo mbele ya
kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii baadhi ya
wabunge walitaka waandishi wa habari kama wadau muhimu washiriki kutoa
maoni yao kwenye kamati hiyo ya bunge.
Mbunge wa Buyungu ,Kasuku Billago (Chadema), alisema muswada huo
umekuja kwa wakati muafaka na  kuwataka waandishi wa habari kukomaa
katika suala linalohusu.
“Haki nyingi za waandishi wa habari hazijaelezwa kwenye muswada huo,
suala lingine la kuhoji ni nani mwenye mamlaka ya kufuta chombo cha
habari kwani kosa moja linafanya chombo kizima kifungiwe” alisema
 Alisema chombo ni taasisi kinatoa ajira na adhabu iwe inalenga kwa
aliyetenda kosa.
“ Chombo ni taasisi inayotoa ajira aadhibiwe mtu sio taasisi ili
kuwezesha taasisi husika kuendelea kuwepo kuna watu maisha yao
yanakuwa mle mnapofungua hata familia zinaathirika” alisema
inahitaji linatakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa kwani serikali
imekuja na lengo jema lakini kuna vitu ambavyo vinatakiwa kujadiliwa
kwa kina ili kuwe na tija kwa kila upande wenye maslahi.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia alisema unahitajika mjadala mrefu sio
jambo la kukurupuka.
“Serikali imekuja na lengo jema ila kuna vitu ambavyo vinatakiwa
kujadiliwa kwa kina “ alisema
Alisema kwa mtazamo wake kama muda hautoshi haiwezi kuzuia wadua kutoa maoni.
“Sio lazima kitu kiletwe leo na kupita, unaweza kufutwa pia ukatetwa
tena kwa majadiliano ya kina” alisema
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe aliwataka waandishi wa habari
kama wadau muhimu kushiriki kutoa maoni yao.
“Kama mwandishi wa habari ukikatazwa kuingia kwenye kamati kusikiliza
majadiliano ingia kama mdau ili uweze kutoa maoni yako, maoni yenu ni
muhimu sana katika muswada huu” alisema
Hoja hizo za wabunge zimekuja baada ya Waziri Nape kuwasilisha hati ya
muswada huyo kwa kamati ya bunge  ya huduma na maendeleo ya jamii,
alisema lengo la muswada huo ni kuweka masharti ya kukuza na
kuimarisha taaluma na weledi katika tasnia ya habari nchini pamoja na
kuundwa kwa bodi ya ithibati ya wanahabari,Baraza huru la habari
pamoja na kuweka mfumo wa usimamizi wa huduma za habari.
Nape alisema Muswada wa sheria ya huduma za habari umeandaliwa ili
kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika tasnia ya habari
nchini ambazo ni pamoja na upungufu wa sheria zinazosimamia tasnia ya
habari na mabadiliko ya teknolojia ya habari.
Pia alisema changamoto ya kutokuwepo kwa udhibiti wa mzuri na
usimamizi madhubuti ya viwango kwenye taaluma ya habari na utangazaji
kumechangia madhila kwa jamii ikiwemo kuandikwa habari za
upotoshaji,zinazokiuka maadili na zinazoweza kusababisha
chuki,machafuko na uvunjifu wa amani.
‘’Hivyo kuifanya serikali na wadau wengi wengine kuona umuhimu wa kuwa
na sheria kama hii itakayoainisha bayana sifa na viwango vya kitaaluma
katika tasnia ya habari.kukamilika kwa sheria hii kutapanua wigo kwa
wananchi kupata haki yao ya kikatiba yak upata habari’’alisema
Nape alisema kutokana za muingiliano wa teknolojia mwaka 2003 serikali
iliona kuna umuhimu wa kuunganisha vyombo hivi viwili Tume ya
Mawasiliano na tume ya Utangazaji ili kuleta ufanisi  wa usimamizi wa
sekta na utoaji wa huduma bora kwa walaji.
‘’Kwa ujumla sekta hii changamoto kubwa ni taaluma ya habari
kutotambulika kama taaluma kamili inayopaswa kuheshimiwa,kukosekana
vyombo madhubuti na huru vya usimamizi  na badala yake mambo mengi
kuwa chini ya serikali moja kwa moja’’alisema
Pia alisema changamoto nyingine ni wadau wa habari kutoshirikishwa
kikamilifu katika utungwaji wa sheria zilizopo hivyo kutokidhi matakwa
ya wadau katika sekta ya habari.
‘’Sheria hii inaleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa sekta ya
habari hapa nchini ni sheria mabyo inakwenda kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi yetu,kuifanya rasmi sekta ya habari kuwa sekta
rasmi’’
Aidha alisema ushahidi uliowazi kwamba waliowengi wamekuwa waathirika
wa kadhia ya uandishi usiozingatia maadili na weledi wa taaluma ya
habari na utangazaji kwa kukashifiwa au kuzushiwa taarifa zisizokuwa
na ukweli wowote.
Alisema mapendekezo yaliyomo katika sheria ya habari kwa kiasi kikubwa
yamelenga kutatua changamoto ya kuwa na wanahabari waliosomea kazi yao
na ambao waewekeana wao wenyewe maadili ya kufuata.
Pia alisema changamoto ya kukuwa kwa teknolojia ya habari na
utangazaji kumefanya sheria zilizokuwa zikisimamia  tasnia ya habari
na utangazaji kupitwa na wakati na kutoendana na
‘’Ni sheria itakayoleta mifumo ya kisasa ya usimamizi na ni mifumo
ambayo inaweza kugusa au kubadili namna tutakavyotenda na
tunavyofikiria sasa,niwaombe wanatasnia wenzangu tuwe tayari kwa
mabadiliko ili taaluma yetu iheshimiwe na sisi  wenyewe tuheshimike
zaidi’’alisema
Nape alisema serikali imeona kwa sasa ni muhimu kuwa na sheria ambayo
itakidhi pia matakwa ya Matumizi ya Teknolojia katika sekta ya habari.
‘’Hivi sasa magazeti ambayo yalikuwa yakitolewa kwa njia ya nakala
ngumu kwa sasa yanaweza kutolewa njia ya mtandao wa internet na
wananchi wanawe kuyasoma katika mfumo huo’’alisema
Nape alisema mambo muhimu na matokeo ya sheria inayopendekezwa
kutungwa ni kama kuwepo kwa sheria inayoendana na sera ya habari na
utangazaji, kuwepo kwa mfumo madhubuti ya kisheria wenye kukidhi
mahitaji katika eneo la usimamizi na uendeshaji wa taaluma ya uandishi
wa habari na utangazaji.
Alisema sheria hiyo inaleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa sekta
ya habari hapa nchini.
Ni sheria ambayo inakwenda kwa mara ya nkwanza katika historia ya nchi
yetu, kuifanya sekta ya habari kuwa taaluma kamili
Source: Sifa Lubasi

KUMBE LUSINDE ALIHOJIWA KWA DAKIKA 45 MAUAJI YA WATAFITI

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma limekiri kumhoji Mbunge wa
Mtera,Livingstone Lusinde kwa dakika 45 kuhusiana na tukio la mauaji
ya kikatili ya watafiti watatu wa kituo cha Utafiti cha Selian Arusha
(SARI) baada ya kubainika alikuwa na mawasiliano kwa njia ya simu na
baadhi ya wananchi wa eneo hilo siku ya tukio.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa alisema hayo jana
mjini hapa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo mmoja ya
waandishi hao alitaka ufafanuzi kama ni kweli Mbunge huyo alihojiwa na
jeshi a Polisi kuhusiana na mauaji hayo.
Alisema walimhoji Lusinde kwa dakika 45 baada ya kutajwa na baadhi ya
wakazi hao kuwa alikuwa na mawasiliano ya simu na baadhi ya watu wa
eneo hilo.
“Ni Kweli Mbunge Lusinde alihojiwa kuhusiana na mauaji ya Iringa
Mvumi, tuna taaluma ya upelelezi wa kesi za jinai katika hili tulipata
taarifa kama kulikuwa na  mawasiliano kati ya Mbunge na wananchi”
alisema
Kamanda Mambosasa alisema licha ya kumhoji Mbunge huyo lakini
hawakupata viunganishi vya kumuunganishana na tuhuma hizo.
“Kama angehusika moja kwa moja angepelekwa mahakamani,” alisema
kamanda Mambosasa.
Hivi karibuni baada ya kuchapishwa taarifa za kuhojiwa na Jeshi la
Polisi, mbunge huyo alikuja juu na kudai kuwa taarifa hizo zilikuwa za
kizushi huku akitishia kulishtaki gazeti hili.
Wakati akitoa ufafanuzi wa taarifa  awali ambayo gazeti hili iliripoti
juu ya kuhojiwa kwake na jeshi la polisi, Lusinde alisema akiwa kama
kiongozi wa
Jimbo hilo analaani tukio baya la kumwaga damu za watu wasio na hatia
Pia aliwataka wananchi waliokimbia  kurudi kwenye makazi yao na kutoa
ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili wote waliohusika katika tukio hilo
waweze kukamatwa.
“Sijawahi kuhojiwa kuhusu uchochezi na taarifa hizo si za kweli
zimeniletea usumbufu mkubwa” alisema. Nimesikitishwa na taarifa kuwa
nilihojiwa na polisijuu ya tukio la kuuawa kwa watafiti, jambo ambalo
si kweli tangu niwe kiongozi sijawahi kuchochea wananchi kwa jambo
lolote” alisema.
Alisema amekuwa Mbunge katika jimbo la Mtera kwa kipindi cha pili sasa
 hakuwahi kushuhudia watu wakifanya matukio ya kinyama kama
lililotokea Iringa Mvumi.
“Siku ya tukio sikuwa kijijini Iringa Mvumi nilikuwa kwenye ziara ya
Waziri Mkuu na tangu uchaguzi umepita sijawahi kufanya mkutano wowote
kwenye kile kijiji” alisema.
Alisema amekuwa akifanya kazi kama timu na madiwani na wenyeviti wa vijiji.
“Kichwa cha habari kuwa Lusinde ahojiwa kuhusiana na mauaji ya
watafiti hakikuwa na ukweli wowote, habari ile imenipa usumbufu mkubwa
na kupewa pole nyingi na hata kupigiwa simu” alisema
Alisema alikwenda kituo cha Polisi kwa ajili ya kuwasalimia viongozi
na wananchi ambao wako mahabusu kuhusiana na tukio lile akiwemo Diwani
Robert Chipole, Mwenyekiti wa Kijiji Albert Chimanga na alipata fursa
ya kuwaona na kuwasalimia viongozi hao na mwananchi mmoja aitwaye Noco
Kwanga.
Akizungumza jana Kamanda Mambosasa alisema katika tukio hilo tayari
watu 13 wamefikishwa mahakamani.
Alisema kabla ya mauaji hayo watuhumiwa walieneza taarifa za uongo
kuwatuhumu watafiti hao kuwa ni wanyonya damu (mumiani) au au kwa
lugha yao waliwaita ‘Wanyobanyoba’ na kuwaua pasipo kuwahoji japo
walikuwa na vitambulisho, barua ya utambulisho kutoka halmashauri ya
Chamwino na gari la serikali. Alisema tukio hilo lilihusisha watu
wengi ambapo wengine walitoroka kwenda mafichoni, msako mkali
unaendelea na kuwakamata wote waliohusika ili kufikishwa mahakamani
kuungana na wenzao.
Kamanda Mambosasa alisema kati ya watu 30 waliokuwa wakishukiliwa
tayari 13 wamepelekwa mahakamani na 17 wameachiwa.
“Bado tunaendelea kuwatafuta kila aliyeshiriki siku ya tukio
atakamatwa ili nao wajutie kitendo walichofanya” alisema
Alisema wengi waliokimbia ni wahusika wa tukio hilo na jeshi la polisi
litawasaka na kuwakamata.
Waliouawa katika tukio hilo ni Nicas Magazine (53), dereva, Faraja
Mafuru (27) na Theresia Nguma (42) ambao ni watafiti.

WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA MABATI 100

$
0
0
waziri mkuu akipokea m saada wa mabati kutoka kwa mbunge wa viti maalumu



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa mabati 100 yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni mbili kutoka kwa Mbunge wa Viti maalum mkoa  wa Lindi Mhe. Hamida Abdallah.
 Msaada huo umetolewa leo (Jumatano, Oktoba 19, 2016) katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara  ya Waziri Mkuu hospitalini hapo.
 Mbunge huyo amesema amekabidhi msaada huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu wakati Waziri Mkuu alipofanya ziara katika Hospitali hiyo.
 “Ulipofanya ziara ya mwezi wanne hospitalini hapa nilikuahidi kukupa mabati  100 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake. Nilitoa ahadi hii baada ya kuona jitihada kubwa unazozifanya katika kuimarisha hospitali hii,” amesema. 
 Akipokea msaada huo Waziri Mkuu amemshukuru Mhe. Hamida kwa kutekeleza ahadi yake na kumuomba aendelee kuisaidia hospitali hiyo pindi anapopata nafasi.” Nashukuru sana kwa msaada wako tunajua kutoa ni moyo na si utajiri,”.
 Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema mkakati wake kwa sasa ni kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na zahanati ili kuwawezesha wananchi kupata matibabu karibu na makazi yao.
“Nataka sekta ya afya inapata mafanikio makubwa. Nitashirikiana na wananchi  kuhakikisha kunakuwa na zahanati katika kila kijiji na vituo vya afya kwenye kata zote,” amesema.
 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue alimshukuru Waziri Mkuu kwa jitihada zake za kuboresha huduma hospitalini hapo.
 Amesema hivi karibuni walipokea sh. milioni 100 kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi kwa ajili ya ukarabati wa wodi mbili ambazo tayari ukarabati huo umekamilika na zitaanza kutumika kuanzia Novemba 15 mwaka huu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, OKTOBA 19, 2016


MKOA WA SONGWE WAPIGWA JEKI MIFUKO 125 YA CEMENT KUTOKA TPB

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe (katikati)  Luteni Mstaafu Chiku Galawa akipokea msaada wa Cement mifuko 125 yenye thamani ya shilingi mil 2 kutoka kwa benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya.kulia aliyevalia T.shart Meneja Benki ya Posta Mbeya Humphrey Julias ,kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo na Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduma Teddy Msanzi aliyshikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa mifuko ya cement 125 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB)Tawi la Mbeya ,hafla ambayo imenyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Songwe Octobar 18 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo akishukuru mara baada ya kupata msaada wa Cement1 kutoka benki ya Posta Tanzania (TPB)

Mkuu wa Mkoa Songwe Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Songwe na wadau mbalimbali .




BENKI ya Posta Tanzania(TPB) kupitia tawi lake Mkoani Mbeya, imetoa msaada wa mifuko ya saruji  125  thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa serikali ya Mkoa mpya wa Songwe.

Akikabidhi mifuko hiyo , kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Songwe, Meneja wa benki ya Posta mkoa wa Mbeya, Humphrey Julius amesema benki hiyo iliguswa na suala la ujenzi wa majengo mapya ya ofisi za Mkoa wa Songwe hivyo kuona umuhimu wa kuchangia ikiwa kama faida wanayoipata kutoka kwa wateja wanaowahudumia.

Amesema, mbali na kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji, pia benki hiyo imeshakabidhi madwati 130  kwa baadhi ya shule za msingi za Wilaya ya Tunduma, Ileje zilizopo Mkoani Songwe na dawati 30 kwa shule ya Mbeya Day Mkoani Mbeya.

Amesema, serikali pekee haiwezi kufanya mambo yote ni lazima wadau zikiwemo Taasisi, Mashirika, Asasi na mtu mmoja mmoja kuingiza mikono yao ili kuipungizia serikali mzigo.

Hata hivyo, akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu  Chiku Galawa, aliishukuru benki ya Posta kwa msaada huo, muhimu kwani serikali ya Mkoinahitaji zaidi ya mifuko 50 elfu ya saruji na mabati  laki moja kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya ofisi pamoja na shule na Zahanati.
Mwisho.



SBL yatoa elimu kuhusu unywaji pombe kistaarabu

$
0
0
Meneja wa SBL wa  Uwajibikaji Katika  Jamii, Hawa Ladha  akitoa maelezo katizo kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu katika mkutano na wadau mbali mbali wakiwepo toka vyombo vya usalama na wafanyabiashara wanaofanya kazi na SBL na wafanyakazi wa kiwanda cha SBL moshi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro

Meneja wa mauzo wa Sbl Mkoani Kilimanjaro Godwin Seleliii akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu iliyofanyika katika mji wa Moshi mkoani kilimanjaro mapema jana.

Mkaguzi wa polisi Mkoa wa kilimanjaro Peter Mizambwa akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa keampeni ya unywaji kistarabu iliyozinduliwa mapema jana na Sbl katika mji wa Moshi

Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini elimu juu ya unywaji wa kistaarabu katika uzinduzi wa kampeni hiyo mapema jana
Waendesha bodaboda wakipata elimu ya unywaji kistaarabu kutoka kwa mfanyakazi wa SBL aliyekuwa anapita mitaani 

Mdau akiwa na zawadi ya kava la gari mara baada ya kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa kuhusu unywaji wa pombe kistaarabu

Moshi, Oktoba 18, 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.  
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkaguzi wa polisi Mkoa wa Kilimanjario, Peter Mizambwa , amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia  bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mizambwa .  
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Zauda.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia Mizambwa anasema “ma kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.  
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.

MBUNGE VENNANCE MWAMOTO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA KILOLO

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya wanawake wa  kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo

na fredy mgunda,iringa.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu  za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.

Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni  kutokana na ahadi yake  yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku  baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto.
Mwamoto ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
“Mimi nimecheza mpira kwa mafanikio ndio maana hadi saizi,kwa hilo mimi najua kuwa michezo ni ajira rasmi hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”.Mwamoto
Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi  na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
“Leo nimetoa mipira na jezi hizi kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya jirani kwa timu zote za wanaume na wanawake kwa lengo la kuendeleza vipaji vyenu”alisema Mwamoto
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA MAJI LINDI

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Lindi (LUWASA), Mhandisi Adam Alexander(PICHANI) kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kushindwa kusimamia ujenzi wa kituo cha kuzalisha maji katika Manispaa ya Lindi.
 Waziri Mkuu amemkabidhi Mhandisi huyo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi, Bw. Stephen Chami na kumuelekeza afanye uchunguzi zaidi juu ya suala hilo.
 Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 19, 2016) wakati alipotembelea mradi wa maji wa Ng'apa ambapo ameagiza nafasi hiyo ikaimiwe na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Idrisa Sengulo.
 "Kamanda wa TAKUKURU fanya mapitio ya kina ya mshahara wake. Yeye anasema analipwa Wizarani, mimi najua analipwa na LUWASA. Angalia kazi aliyokwenda kuifanya Dar es Salaam kama inalingana na siku alizokaa,” amesisitiza Waziri Mkuu.
 Mhandisi hiyo anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za ofisi pamoja na kupokea mshahara bila la kulipa kodi ya mapato ya mshahara (PAYE), kujilipa kiwango kikubwa cha posho pamoja na kusafiri kwa muda mrefu.
 Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona wananchi wanapata shida huku watendaji waliopewa dhamana ya kuwatumikia hawaonekani kwenye vituo vyao vya kazi. "Huyu nimemuita mimi aje huku, hadi jana alikuwa Dar es Salaam."
 Alipoulizwa sababu za kutokuwepo ofisini kwake kwa muda mrefu, Mkurugenzi huyo alisema kwamba alikuwa Dar es Salaam akiandika maombi ya fedha kwa ajili ya kutatulia changamoto mbalimbali zinazoikabili mamlaka hiyo.
 "Unatumia siku ngapi kuandika proposal, msomi unatumia mwezi mzima kuandika proposal na unakaa Dar es Salaam hata Katibu Mkuu wako hajui na huko unajilipa posho tu! Tena baada ya kulipwa sh.120,000 kwa siku wewe unajilipa sh.150,000. Hatuwezi kuvumilia hali hii,” amesema.
 Waziri Mkuu amemaliza ziara yake siku tatu mkoani Lindi na amerejea jijini Dar es Salaam.
 (mwisho)    
                            
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM
JUMATANO, OKTOBA 19, 2016.

NHIF yalipa bilioni 200/- gharama z ahuduma kwa wateja wake

$
0
0


MENEJIMENTI ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imekanusha ya madai ya kupungua kwa uwezo wake wa kuhudumia wanachama na kusema kama wangelikuwa na hali mbaya wasingeweza kulipa zaidi ya bilioni 200 kwa mwaka uliopita wa fedha 2015/2016.
Aidha imesema kitendo walichofanya cha marekebisho ya malipo katika huduma zake imelenga kuboresha na si kweli kwamba imetokana na kukosekana kwa wake  imetoa ufafanuzi wa ongezeko la bei za matibabu na kusema kwamba halitaathiri michango ya wanachama wake na kwamba imelenga kuboresha zaidi huduma wanazopatiwa wanachama wanapotafuta msaada wa tiba katika vituo vilivyosajiliwa na mfuko huo.
Aidha, menejimenti hiyo imesema kwamba bei mpya ambazo zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 13 zimeridhiwa baada ya majadiliano ya muda mrefu.
Imesema mabadiliko yaliyotokea ya kuboreshwa kwa bei yamelenga kutanua wigo huduma na uwezeshaji, ikiwamo za upasuaji na ada ya kumwona daktari huku pia wakiongeza fao la vipimo na matibabu ikiwemo upasuaji wa magonjwa ya moyo nchini.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bernard Konga alisema majadiliano ya kufanya mabadiliko ya bei hizo yaliyofanyika kwa miaka miwili na kushirikisha wadau mbalimbali, yapo maeneo ambayo gharama zimeongezeka, mengine kupungua lakini pia kukiwa na maeneo ambayo hayajaguswa kabisa kutokana na mifumo na sera za afya za nchi.
Mkurugenzi huyo akifafanua zaidi alisema si kweli kuwa mabadiliko hayo yametokana na Mfuko huo kushindwa kulipa watoa huduma kama inavyodaiwa bali ni kutokana na tafiti zilizoonesha kuwepo kwa haja ya kufanyika mabadiliko kukidhi mahitaji ya matibabu bora kwa wanachama wake na kuondoa utofauti katika malipo.
Alisema kama mfuko huo ungekuwa na tatizo usingeweza kulipa zaidi ya shilingi bilioni 200 kwa mwaka wa fedha 2015/16 kwa kuhudumia wahitaji 6,505,492.
Aidha alisema kwamba wana uwezo wa kuhudumia wanachama wake  kwa miaka minne ijayo bila michango zaidi.
Akizungumzia mabadiliko yaliyofanywa kwenye maboresho, alisema nia ilikuwa kubadilisha mfumo wa ulipaji, ikiwemo ada ya kumuona daktari ili kuondoa mfumo wa awali uliokuwa na viwango tofauti vya ada kwa mgonjwa anayehudhuria hospitali kwa mara ya kwanza na anaporudi kwa mara nyingine.
“Kwa sasa ada hii inalipwa kwa viwango sawa ambapo Mfuko unalipia kadri ya uhitaji na pia upasuaji umeainishwa kutokana na aina yake kama mdogo, mkubwa au wa kitaalamu,” alisema.
Konga alisema Mfuko huo unatekeleza sera, miongozo na taratibu zilizowekwa na serkali na kuzingatia maelekezo ya kitaalamu,  hivyo vituo vilivyosajiliwa na Mfuko vina ngazi tofauti na hivyo bei za huduma zinaruhusiwa kulipwa kutegemea na daraja la kituo husika. Hadi kufikia Juni, mwaka huu, vituo vilivyosajiliwa na Mfuko vilikuwa ni 6,439, kati yake vya serikali vikiwa 5,091, madhehebu ya dini 572 na binafsi 776.
Alisema dawa na vipimo ndivyo vinalipwa sawa katika ngazi zote za vituo, huku mabadiliko ya tofauti yakiwa katika ukubwa wa taaluma.
Alisema kutokana na kuwa Mfuko umeingia Mkataba na watoa huduma kwa ajili ya kutoa huduma kwa wanachama wake, endapo mwanachama atakataliwa kupewa huduma hatua za kisheria zitachukuliwa na ikiwa madai yanatokana na udanganyifu hayatalipwa. Aliwataka wanachama wanapopata matatizo kuhusu madai yoyote yale katika tiba zao kupiga simu ya bure 0800 110063
Alisema katika kipindi cha mpito cha maboresho hayo kinachoanzia Julai hadi Desemba, mwaka huu wataendelea kupokea maoni na malalamiko hususani  suala la vipimo ambalo linalalamikiwa sana na baadhi ya watoa huduma baada ya Mfuko huo kuamua kulipa gharama moja kwa watoa huduma wote.
Maeneo yaliyoboreshwa zaidi
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitaalamu za Matibabu wa NHIF,  Dk Aifena Mramba akizungumzia faida za maboresho alisema baada ya vipimo na upasuaji wa moyo kuanza kufanyika nchini wameongeza fao la matibabu ya magonjwa hao.
Dk Mramba alisema kwa huduma za upasuaji wameongeza kwa asilimia 100 na  kutoa mfano kwa upasuaji wa uzazi iliokuwa unalipiwa  Sh 130, 000 sasa ni Sh 350,000. Alisema pia upasuaji wa kufunga mirija ya uzazi na kidole tumbo uliokuwa umetengewa Sh 130,000 tu sasa umeongezewa fedha hadi Sh 300,000.
Maboresho mengine ni ada ya kumuona daktari ambapo Mramba alisema tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kwa Hospitali za Mikoa walikuwa wakilipwa Sh 2,000 sasa watalipwa Sh 15,000 huku Hospitali za Wilaya ambako walikuwa wakilipa Sh 1,000 kama ada ya kumuona daktari sasa watalipwa Sh 10,000.
Alisema Mfuko wa NHIF unasimamia upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wanufaika wake ambao ni zaidi ya milioni 3.3 wanaopata matibabu katika vituo 6,400 nchi nzima.
Ufafanuzi huo wa NHIF umekuja baada ya kuwepo kwa taarifa zinazoleta mkanganyiko kwa wanachama wa Mfuko huo kwamba umepunguza malipo kwa asilimia 60, hatua iliyoonekana kutishia wanufaika kukosa huduma.
ends

SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016 JIJINI MWANZA KUWA BORA ZAIDI

$
0
0
Leo Oktoba 19, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.
Na BMG
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.

Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.

Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.

Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.
Kamati ya Miss Tanzania 2016 ambapo kutoka kulia ni Hashim Lundenga, Pamela Irengo, Flora Lauwo.
Mkutano baina ya Kamati ya Miss Tanzania 2016 na Wanahabari Jijini Mwanza
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao

SHAMBA LA FOFO ESTATE LAREJESHWA KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vinne vilivyoko kata ya Machame Narumu akitoa uamuzi juu ya mgogoro wa ardhi wa shamba la Fofo estate.
Baadhi ya Wananchi waliofika katia Mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa (aliyenyoosha mikono) akitoa ufafanzi wa jambo mara baada ya kutangaza kurejesha eneo lenye mgogoro kwa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchi wa vijiji vinne vya Urori,Tella ,Mula na Usali waliohudhria mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai wa kutoa maamuzi juu ya mggoro wa shamba la Fofo estate.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakati akitoa uamuzi juu ya mgogoro wa Shamba hilo.
Shamba la Ekari 106 la FOFO ESTATE lililopo wilayni Hai ambao limekuwa na mgogoro kwa zaidi ya miaka 40. 


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MGOGORO wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 wa  shamba la Fofo lilipo wilayani Hai ,umemalizika baada ya Mkuu wa  wilaya hiyo ,Gelasius Byakanwa kutangaza kurejesha shamba hilo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.

Hatua ya Mkuu huyo wa wilaya inatokana na mgogoro baina ya Wananchi wa vijiji vinne vya Urori,Tella ,Mula na Usali vilivyoko kata ya Machame Narumu lilipo Shamba hilo dhidi ya aliyekuwa mtendaji mkuu wa Chama cha Ushirika cha Narumu Manushi,Peter Karanti anayedaiwa kujimilikisha shamba hilo .

Akitoa historia ya mgogoro huo Byakanwa alisema shamba hilo lililopewa namba 240 na 242 Ex .C.T No.NP 405 EP.LOT.661 (FOFO ESTATE) lilikuwa linamilikiwa na raia wa kigeni Dkt A Phones ambaye aliweka rehani shamba hilo mwaka 1966 kwa ajili ya mkopo wa kiasi cha Sh 100,000 kutoka benki ya CRDB .

“Baadae Dkt ,Phoneas alitoroka nchini kabla ya kulipa mkopo huo ,Benki baada ya kugundua hilo ilichukua hatua ya kuliza shamba ili kurudisha mkopo aliokuwa akidaiwa Dkt Phoneas”alisema Byakanwa.

Alisema  Chama cha Ushirika cha Narumu Manushi ambacho wanachaa wake ni wananchi wa vijiji vine lilipo shamba hilo kilifanikiwa kununua shamba hilo kwa  kulipia deni la sh 100,000 ambapo kilitoa  kiasi cha Sh 20,000 huku kikibaki na deni la sh 80,000.

“Taarifa ambazo ofisi yangu ilizipata ni kuwa chama kilipewa miaka 10 kiwe kimemaliza kulipia deni hilo ,lakini ndani ya miaka miwili zikatokea taarifa za kuwa Chama cha Ushirika cha Narumu kilishindwa kumaliza deni lake”alisema Byakanwa.

“Bahati mbaya zaidi ,shahidi wa taarifa hizi ni Peter Karanti aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama cha Ushirika na haikujulikana yeye kama mtendaji mkuu alichukua hatua gani za kuhakikisha chama kinamaliza deni lake”aliongeza Byakanwa.

Alisema hakuna ushahidi unaoonesha kuwa benki ya CRDB ilikususdia kuliuza shmaba hilo kwa kigezo cha kuwa Chama cha Ushieika cha Narumu kimeshindwa kulipa deni ndani ya muda husika zaidi ya kuwepo kwa taarifa kuwa Mtendaji mkuu wa Chama cha Ushirika alitafuta baadhi ya wanachama na wasio wanachama wachange pesa ya kulikomboa na kulimiliki.

“Baadae chama cha ushirika kilipitisha maamuzi ya kuwapa jukumu la kulipa deni la chama,Karanti na wenzake walilipa deni na kukabidhiwa Shamba hata hivyo walishindwa kupata hati miliki ya Shamba hilo kwa kuwa ilikua bado inashikiliwa na benki kutokana na mkataba uliokuwepo ulikuwa ni Chama cha Ushirika na si Karanti na wenzake.

Akitoa maamuzi juu ya mgogoro huo  wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji hivyo uliofanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Tunoma ,Byakanwa alitangaza kuzuia kufanyika kwa shughuli za maendeleo katika shamba la Fofo zinazofanywa na mtu binafsi.

“Kwa kuwa hati ya Dkt Phoneas aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo ilikwisha batilishwa na kuamuliwa shamba hilo limilikishwe kwa kijiji na vijiji ndivyo vinalipa kodi ya ardhi,wakulima wote waliolima katika shmba hilo wavune mazao yao ndani ya kipindi cha miezi mitatu” alisema Byakanwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati  ya ufuatiliaji wa shamba hilo John Kweka alisema awali Wenyeviti wa vijiji hivyo ndio walikuwa wakifuatilia mgogoro huo kabla ya kubaini kuwa wenyeviti hao kuwa na maslahi katika mgogoro na kulazimika kuunda kamati nyingine.

“Tumefuatilia hili suala hadi kwa Waziri wa Ardhi,tumepokea kwa furaha maamuzi  ya mkuu wetu wa wilaya kwa sababu sisi kama kamati tulipendekeza maeneo katika hili shamba yatumike kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati,Shule ,Taasisi,Soko  na Mahali pa kuzikia hili ndio lilikuwa lengo letu”alisema Kweka.

Mwisho.

MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA YASISITIZA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
’Wito watolewa kwa kila mwananchi kuwajibika kwa malengo ya Dunia’

OKTOBA 24 kila mwaka Umoja wa Mataifa hufanya maadhimisho ya kuzaliwa kwake.

Mwaka huu mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na serikali, wadau wa maendeleo na vijana wataadhimisha miaka 71 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa kwa staili ya aina yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mkutano wa waandishi wa habari na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikishirikiana na Umoja wa Mataifa , maadhimisho hayo mwaka huu yamelenga kuelezea kwa undani shughuli zinazofanywa kwa pamoja kati ya pande hizo mbili ili kuwezesha maendeleo endelevu.

Katika mkutano huo wa pamoja, waandishi wa habari walielezwa kwa ufupi Mpango Mpya wa Maendeleo Chini ya Ufadhili wa Umoja wa Mataifa ( UNDAP ll -2016 hadi 2021) kwa serikali ya Tanzania; na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa Tanzania ambamo malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kama yalivyosanifiwa na kukubalika na jumuiya ya kimataifa, yameshirikishwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Dkt. Mahiga, amezungumzia umuhimu wa maadhimisho wa Siku ya Umoja wa Mataifa na faida za Jukwaa la umoja huo kwa maendeleo ya Taifa. Maadhimisho hayo yatafikia kilele tarehe 24 Oktoba, 2016.(Picha zote na Reginald Kisaka wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Katika mkutano huo na waandishi wa habari pia kulikuwepo na majadiliano ya mafanikio ya shughuli za Umoja wa Mataifa hadi sasa duniani na pia nchini Tanzania .

Pia mazungumzo hayo yalijikita katika malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na umuhimu wa malengo hayo kumilikishwa kwa wananchi na wajibu wao katika kuhakikisha kwamba kunakuwa na utekelezaji wenye mafanikio.

Pia ilielezwa katika mkutano huo kwamba maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa, Siku ya Umoja wa Mataifa, yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Oktoba 24.

Maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yamebeba ujumbe wa :“Uwezeshaji wa vijana Tanzania kufikia malengo ya dunia” yanafanyika huku kukiwa na malengo mapya ya dunia ya maendeleo endelevu.Malengo hayo ya SDGs yamelenga kuondoa umaskini kwa kuwa na maendeleo endelevu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika mkutano na waandishi wa habari.

Aidha ujumbe huo unaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa awamu ya pili wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania (UNDAP II) ambao unaendeleza ule wa awali wa kuanzia 2011-16 ukiwa umejikita katika masuala ambayo ni muhimu kwenye kukabili umaskini kwa kuwa na maendeleo endelevu.

Maadhimisho ya mwaka huu yalitanguliwa na kongamano la vijana wapatao 200, ambao walijadili masuala yanayogusa fursa za uchumi na maendeleo ya jamii na mchango ambao unaoweza kutolewa na vijana kufanikisha utekelezaji wa malengo hayo.

Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake nchini kwa tukio litakalofanyika Visiwani Unguja Oktoba 26 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanaonesha uwapo wa ushirikiano mkubwa na wenye tija kati ya Tanzania, wananchi wake na Umoja wa Mataifa.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bi.Chansa Kapaya akizungumza na waandishi wa habari.

Aidha maadhimisho hayo yanaonesha ni kwa namna gani pande zote zipo tayari kutekeleza mipango ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yenye lengo la kusaidia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Akizungumza umuhimu wa ushirikiano huo katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ukiwa ni mpango wa wananchi wenyewe, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw Augustine Mahiga, alielezea Tanzania kuunga mkono Umoja wa Mataifa ukifanyakazi kama taasisi moja na kuwataka watengeneza sera kuhakikisha kwamba wananchi wote wananufaika na ushirikiano huu wa Tanzania na Umoja wa Mataifa.

Waziri Mahiga alisisitiza wakati Tanzania inajikita katika kutekeleza mpango wake mpya wa taifa wa maendeleo, kuna haja ya kuhakikisha kwamba wananchi wanaelewa na kumiliki mpango huo ambao umejumuisha malengo ya maendeleo endelevu.
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) akifuatilia mkutano. Kulia ni Kaimu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bi.Chansa Kapaya.

Alisema: “Tanzania imeshirikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) katika sera za taifa na pia katika mipango ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo ya msingi yanayohitaji uangalizi kufanikisha maendeleo endelevu”. 

Hata hivyo aliongeza kusema kwamba: “ Hiyo inajulikana wazi kwamba serikali pekee haiwezi kufanikisha utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu bila msaada wa sekta binafsi na wadau wetu wa maendeleo, na hivyo iko haja ya kushirikishana. Tunaitaka sekta binafsi na wadau wetu wa maendeleo kujiunga nasi katika juhudi hizi kwa kutuwezesha kifedha ili tuweze kutekeleza mipango yetu ya maendeleo. Tunachohitaji sisi tunaofanyakazi katika ushirikiano wa kimataifa kuhakikisha kwamba hatutamwacha yeyote nyuma katika harakati zetu za kuleta maendeleo”.

Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akizungumzia maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa na uhusiano wake alisema: “Tanzania na Umoja wa Mataifa zimekuwa na ushirikiano wa maendeleo kwa miongo mingi. Wakati Tanzania sasa inabadilika, msaada unaotolewa na Umoja wa Mataifa unatakiwa kukidhi haja mpya, hasa taifa linapoelekea katika uchumi wa kati”.

Pia katika hotuba yake aliongeza kwamba: “Malengo ya maendeleo endelevu ni muhimu katika ushirikiano wetu kwani unaweka umuhimu wa shughuli za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania za kusaidia kupatikana kwa mafanikio katika nyanja za uchumi, ustawi wa jamii na utunzaji wa mazingira.”

SHULE YA SEKONDARI YA MALANGALI YAPATA NEEMA KUTOKA KWA MALANGALI ALUMNI ASSOCIATION (MAAS)

$
0
0
Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania
mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo ilivyowapa mafanikio hadi sasa walipofikia.



 na fredy mgunda,Iringa

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamewataka vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali walinufaika na elimu kutoka shule ya malangali kurudisha fadhila katika shule hiyo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka na shule ya mangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo. 

“Wafanyakazi na viongozi mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania.” Alisema Kevela

Kevela amesema kuwa shule nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule walizosoma.

Naye Padre wa kanisa la kikatoriki mkoani mbeya Telesipholi Tweve aliwakata wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafanikio yao ya leo.

“Leo nimerudi katika shule hii ya malangali kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi kama MAAS tumeanza kwa kukarabati ukumbi ambao utakuwa na faida kwao kwa kutumia kwenye sherehe na kukodishwa pia”.alisema Tweve

Kwa upande wake mwenyekiti wa Malangali Alumni association (MAAS) Paul Mng’ong’o alisema kuwa wameanza kuisaidia shule ya Malangali muda mrefu kwa kuwa tayari wameshakarabati ukumbi wa shule,wamewanunulia tv na king’amuzi kwa ajili ya habari na wanaendelea kutatua matatizo ya shule hiyo.

“Hebu angalia sisi tuliosoma hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka shule hii,tunaviongozi wengi,matajili wengi ,wakulima wakubwa sana hapa nchini wote wamesoma katika shule hii”.Alisema Mng’ong’o

Lakini pia Mng’ong’o alisema kuwa lengo la kundi la Malangali Alumni Association kuunganisha wanafunzi wote waliowahi kusoma shule ya secondary ya Malangali na kuweza kupeana malengo na kusaidiana pale wanapokwama kimalengo.

Shule ya Malangali ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa maisha.

kaika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.  

SIMBA CEMENT YAZIPIGA TAFU SHULE TATU TANGA KUPUNGUZA KERO YA MADAWATI

$
0
0
KUFUATIA Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu.
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara  Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa, amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement)  na kuyataka mashirika na taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya wanafunzi kusomea chini.
Kwa upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa Shemahonge, amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi kuyatunza ili kuongeza uelewa  wa  wanafunzi  darasani.


Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement), Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias  Mwailapwa, madawati 100 kwa  shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba  za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini.



Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa mwenye suti bluu (katikati) na Afisa Elimu shule ya msingui halmashauri ya jiji la Tanga, Khalifa Shemahonge (kulia) wakiwa na wafanyakazi wa kiwanda cha Simba Cement mara baada ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule tatu za halmashauri ya jiji la Tanga .



JELA KWA KUGHUSHI HUDUMA ZA NHIF

$
0
0


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni imewahukumu wakazi wawili wa Mkoa wa Dar es Salaam kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi Milioni moja kwa makosa ya kujipatia huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa njia za udanganyifu.
Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Bweguge Obadia ambaye alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashitaka umeithibitishia mahakama pasipo shaka ya aina yoyote kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo.
Waliohukumiwa kifungo hicho ni pamoja na Bw. Michael Francis na Bw. Godfrey Nyika ambao ni washitakiwa wa pili na wa tatu huku mshitakiwa wa kwanza Bw. Rashid Kidumule akiaachiwa huru baada ya kuthibitika kutotenda kosa hilo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Bw. Obadia alisema kuwa hakuna shaka yoyote juu ya washitakiwa hao kutenda makosa ya kujiwakilisha katika duka la dawa la Nakiete kwa lengo la kujipatia huduma ya dawa kwa kutumia kitambulisho cha matibabu cha mshitakiwa wa tatu ambaye ni Bw. Nyika.
“Ushahidi wa mashahidi wa mashitaka unathibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa mshitakiwa wa pili Bw. Francis alijiwakilisha dukani kwa lengo la kupata dawa kwa kutumia kadi isiyo yakwake na hakuna shaka kuwa mshitakiwa wa tatu ambaye ndiye mwenye kadi alimpatia kadi hiyo mshitakiwa wa pili hivyo kwa ushahidi huu Mahakama inawatia hatiani,”anasema Hakimu Mkazi Bw. Obadia.
Alisema kuwa Mahakama hiyo imezingatia makosa waliyoshitakiwa nayo washitakiwa hao pamoja na uhusika wao katika kutenda makosa hayo. Kutokana na hali hiyo, Mahakama ilimhukumu Bw. Francis kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi milioni moja huku mshitakiwa Bw. Nyika akihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini ya shilingi laki tano.
Washitakiwa hao walitenda makosa hayo ya kujiwakilisha kwa lengo la kujipatia huduma mwaka 2014 ambapo kesi hiyo imehitishwa kwa wao kukutwa na hatia na kuhukumiwa adhabu hiyo.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya umekuwa ukitahadharisha wanachama wake juu ya matumizi ya vitambulisho vyao vya matibabu kwa kuonya kufanya udanganyifu wa aina yoyote kwenye huduma zake.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amesema Mfuko utaendelea kuchukua hatua stahili kwa wanachama wasio waaminifu ambao watajihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.
“Nitoe tu tahadhari kwa wanachama na watoa huduma wote kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuulinda Mfuko kwa kuhakikisha huduma anayoitoa au kuipata iko katika njia sahihi, Mfuko hautakuwa tayari kufumba macho kwa wanaojihusisha na udanganyifu au kuhujumu Mfuko kwa namna yoyote,” alisema Bw. Konga.



KONGAMANO LA TASWA KUHUSU MIFUMIO YA UENDESHAJI YANGA NA SIMBA

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KONGAMANO kuhusumifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia litafanyika Jumamosi Oktoba 22 mwaka huu ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), likiwa na lengo la kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga utaratibu wa kukodishwa.

Kongamano halina nia ya kuzuia mabadiliko au kuharakisha mabadiliko katika klabu hizo, badala yake inataka litumike kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wa mpira wa miguu kuhusu mifumo hiyo na aina nyingine ya mifumo ya uendeshaji wa klabu duniani, hivyo kusaidia kujibu maswali mbalimbali  ambayo pengine hayajibiwi ipasavyo.

Baadhi ya mambo yatakayozungumziwa ni umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo, pia harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake na itazungumziwa pia mifumo ya uendeshaji ya klabu mbalimbali duniani.

Lengo ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka.

Tunaomba mashabiki na wadau wengine mbao hawakualikwa watambue tunathamini mawazo yao, lakini nafasi ya wanaotakiwa kuhudhuria ni chache hivyo wafuatilie kupitia vyombo vya habari.

Nawasilisha,

Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/10/2016

Viewing all 9117 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>