Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9093 articles
Browse latest View live

Vatican Says Conclave to Elect New Pope Will Begin Tuesday

$
0
0
The cardinals of the Roman Catholic Church announced on Friday that the conclave to elect the next pope would begin on Tuesday.
The transition was set in motion on Feb. 28 by the resignation of Pope Benedict XVI.

WALIOKUFA AJALI YA BASI LA GREEN STAR WATAJWA

$
0
0


WATU watatu, akiwemo dereva na kondakta, wamekufa katika ajali ya
barabarani iliyotokea jana kijijini  Nkuhi, Wilayani  Ikungi  kwenye
Barabara Kuu ya Singida - Dodoma kwa kuhusisha basi la Green Star express
na gari moja la mizigo.
 
Kamanda wa Polisi, Kamishina Msaidizi Linus Sinzumwa aliwataja waliokufa
kwenye ajali hiyo kuwa ni dereva wa basi hilo, Yassin Ramadhan (39) mkazi
wa Dar es Salaam, Mansury Mohamed (30) mkazi wa Mpwapwa – Dodoma na mtoto
mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka mitano ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja.
 
Aidha, Kamanda Sinzumwa alisema kuwa mbali na ajali hiyo kuua, pia
imejeruhi abiria 20 wakiwemo Wachina watatu wafanyakazi wa Kampuni ya
Ujenzi ya CCC Company ya Nzega na Waganda watatu walimu wa Uganda nchini
Uganda waliokuwa wanasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama.
 
Aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa ajali hiyo ilitokea  Jumapili
majira ya saa 9:00 alasiri wakati dereva wa basi T. 939 BRA alipoligonga
kwa nyuma lori lenye tela na namba za usajili T.268 CCC/T.931 CBU
lililokuwa limebeba mbao kutoka Iringa kwenda Nzega.
 
Kamanda Sinzumwa alieleza chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva  wa
basi (ambaye sasa ni marehemu) kutaka kulipita gari la mizigo lililokuwa
mbele yake bila ya kuchukua tahadhari.
 
Waliojeruhiwa ni Pisha Leng, Changshing Chang, Guongrung Gang (Wachina),
Eveline Mbine, Tusiime Aneth  na Swahibu Semgenyi (Waganda).
 
 Wengine ni Hathamima Ailele, Paschal Maganga, Amina Saidi, Rachel Enock,
Abel Mbate, Happiness James, Aziza Masoud, Lawrencia Kariki,  Iddi Rajabu,
Mtaki Kalugula,. Saidi Ramadhani, Thadeus Mallya, Leonard Itete na Kristina
Victor.
 
Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya mkoa wa Singida na wanaendelea
Vizuri
Source Abby Nkungu wa Habarileo

REMINDER: CALL FOR ENTRIES FOR ZIFF

*RAMBIRAMBI MSIBA WA KOCHA ATHUMAN KILAMBO*

$
0
0

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*






Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo
cha mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga, Pan Africans na Taifa Stars,
Athuman Kilambo kilichotokea jana (Machi 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.



Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
Kilambo akiwa mchezaji, na baadaye kocha alitoa mchango mkubwa kwa timu
mbalimbali alizochezea na kufundisha zikiwemo Pan Africans na Cargo, hivyo
mchango wake tutaukumbuka daima.



TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kilambo, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Pan Africans na kuwataka kuwa na
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.



Maziko yanatarajiwa kufanyika leo (Machi 11 mwaka huu) katika makaburi ya
Kisutu mkoani Dar es Salaam ambapo TFF imetoa ubani wa sh. 100,000. Mungu
aiweke roho ya marehemu Kilambo mahali pema peponi. Amina



*Boniface Wambura*

*Ofisa Habari*

*Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)*

Tanzania zakubaliana na AfDB kusaidia mradi wa maji Zanzibar

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akibadilishana hati na  Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero mara baada ya kusaini  makubaliano leo jijini Dar es salaam ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar.


Picha na GCU_HAZINA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini makubaliano  na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa kuipatia Tanzania shilingi bilioni 34.8 za kusaidia mradi wa maji Zanzibar. Katikati ni Mwakilishi wa AfDB nchini Tonia Kandiero na kulia ni Mtaalam wa Benki hiyo anayeshughulikia masuala ya maji Sabas Marandu.
 

KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMZIKA KILAMBO

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la mchezaji
mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo *
*leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya kuugua saratani ya
koo kwa takriban miaka miwili,*
*atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye
aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia amefundisha
nyota wengi wa *
*kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard, Mohamed
Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa Stars
kutokea Yanga na Pan.*
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Machi 11, 2013, amejiunga na mamia ya waombolezaji kumzika aliyekuwa mchezaji hodari wa timu ya soka maarufu ya Yanga ya Dar Es Salaam, Athuman Kilambo.
Athuman Kilambo ambaye alifariki dunia usiku za kuamkia leo baada ya kusumbuliwa kwa muda na ugonjwa wa kansa amezikwa kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Kilambo alikuwa mlinzi hodari wa kushoto wa timu ya Yanga ambayo aliichezea kwenye miaka ya 1960 na 1970. Alikuwa mmoja wa walinzi imara wa kikosi cha klabu hiyo ambacho kilitawala soka ya Tanzania kwa kushinda ubingwa nchini kwa miaka mitano mfululizo hadi mwaka 1973 wakati Simba ilipowavua ubingwa huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
11 Machi, 2013

Wajumbe wa kamati mbali mbali za DRFA

$
0
0
DAR ES SALAAM REGION FOOTBALL ASSOCIATION (DRFA)





TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
12th MARCH 2013

Kamati ya Utendaji ya Chama Cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kwa mamlaka iliyonayo imeteua kamati mbali
mbali zitakazoshirikiana na Kamati ya Utendaji katika kukabiliana na changamoto
mbali mbali za mpira wa miguu katika Mkoa wake ili kuweza kufikia malengo yake
waliyojiwekea. Wafuatao
ni watu na kamati mbali mbali walioteuliwa/zilizoteuliwa na Kamati ya Utendaji
ya Chama Cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam:

Bw. Joseph Kanakamfumo                     Mkurugenzi wa Ufundi
Bw. Saidi Pambalelo                              Afisa Tawala
Bw. Mohamedi Muharizo                       Afisa Habari
Bw. Hashim Abdallah                             Afisa Usalama

KAMATI YA FEDHA NA
MIPANGO
1.       Bw. Meba Ramadhani               Mwenyekiti
2.       Bw. Iddi Msonga                       Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Ali Hassani                                                  
4.       Bw. Ramadhani Kilemile
5.       Bw. Isack Mazwile

KAMATI YA UFUNDI NA MASHINDANO
1.       Bw. Kenny Mwaisabula              Mwenyekiti
2.       Bw. Shabani Mohamedi              Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Hugo Seseme
4.       Bw. Daudi Kanuti
5.       Bw. Kassim Mustapha
6.       Bw. Abeid Mziba
7.       Bw. Bakari Mtumwa

KAMATI YA MAENDELEO YA SOKA
LA VIJANA NA WANAWAKE
1.       Bw. Benny Kisaka                     Mwenyekiti
2.       Bw. Muhsin Balhabou                Makamu
Mwenyekiti
3.       Dr. Sesy Makafu
4.       Bw. Emmanuel Kazimoto
5.       Dr.  Maneno
Tamba
6.       Bw. Edwin Mloka
7.       Bw. Sande Mwanahewa
8.       Bw. Richard Shayo

KAMATI YA WAAMUZI
1.       Bw. Jovin Ndimbo                     Mwenyekiti
2.       Bw. Sijali Mzeru                        Makamu
Mwenyekiti
3.       Bw. Saidi Mbwana
4.       Bw. Benny Mtula
5.       Bw. Abdallah Mitole

KAMATI YA NIDHAMU NA
USULUHISHI
1.       Mheshimiwa Roman Masumbuko            Mwenyekiti
2.       Bw. Fahadi Faraji Kayuga                       Makamu
Mwenyekiti
3.       Bw. Mohamedi Mpili
4.       Bw. Peter Nkwera
5.       Bw. Jimmy Mhango

KAMATI YA RUFAA
1.       Mheshimiwa Salehe Njaa                       Mwenyekiti
2.       Bw. Saidi Engo                                      Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Abasi Kuka
4.       Bw. Yusuph Macho
5.       Bw. Boi Risasi

Pia Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam inapenda kuwafahamisha wanachama wake, wadau na mashabiki
wa mpira wa miguu Tanzania dhamira yao ya kuendeleza mpira wa miguu katika Mkoa
wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Kwa kuanzia Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam kipo kwenye mchakato wa kukamilisha DRFA
Strategic Plan 2013 - 2016 (Mpango Mkakati Kazi) kwa kipindi cha miaka
minne pamoja na kuboresha Financial
Regulations zake ili kiweze kuwa na dira ya kuwahudumia wadau wake kwa ufanisi
na uwazi zaidi. Lakini pia Kamati ya Utendaji imeona haja ya Chama Cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na Website yake kwa ajili ya kuwapa habari wadau
wake na Watanzania kwa ujumla.

Mwisho Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kinaomba ushirikiano na wadau wote wa mpira
hususani Serikali, TFF, Vyama vya Mikoa, Walimu, Waamuzi, Madaktari, Vilabu,
Makampuni na Waandishi wa habari na Vyombo vya habari katika kuendeleza mpira
wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaam na hatimaye mikoa yote ya Tanzania. “Kwani
Pamoja Tunaweza”

Ahsanteni,

Almasi
Kasongo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA)

Mkuchika azungumzia gesi

$
0
0
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora ambaye pia
ni mbun ge wa jimbo la Newala mkoani Mtwara, Kapt (Mst) George H.
Mkuchika, akisisitiza jambo alipokuwa anaongea na wananchi katika
mkutano wa hadhara kijiji cha Nangudyane ikiwa ni sehemu ya ziara yake
kuelimisha wananchi wa jimbo lake juu ya masuala la gesi na namna
serikali inavyolishughulikia.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, Kapt
(Mst) George H. Mkuchika amewapongeza wakazi wa wilaya ya Newala
mkoani Mtwara, hususan vijana kwa kutoshiriki katika vurugu
zilizosababisha kuhalibu mali za Umma na kulisababishia Taifa hasara
kubwa eti wakidai ges isipelekwe dare s salaam.
Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala alisema hayo juzi katika
nyakati tofauti wakati akiwahutubia wanachi katika Vijiji vya
Nangudyane, Chilende,Kadengwa na Mtopwa ambako anafanya ziara ya siku
kumi kutembelewa wialya hiyo ikiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi
kuhusu suala la gesi na namna ambavyo serikali inalishughulikia.
Alisema kuwa, vitendo vya kuharibu mali za Umma sio tu vinarudisha
nyuma maendeleo ya nchi bali pia, vinazorotesha huduma zinazotolewa na
Serikali kwa Wananchi wake na kulisababishia taifa hasara.
source: Hassan Simba


LIGI YA VODACOM KUENDELEA J’MOSI

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea
Jumamosi (Machi 16, 2013) kwa mechi tatu zitakazochezwa katika miji ya
Mwanza, Dar es Salaam na Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Toto Africans inayopigana kukwepa kurudi daraja la kwanza itakuwa mwenyeji
wa Mgambo Shooting kutoka Tanga katika mechi itakayochezwa Uwanja wa CCM
Kirumba.
Vinara wa ligi hiyo Yanga wataumana na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa
wakati Uwanja wa Manungu utakuwa mwenyeji wa mechi ya Mtibwa Sugar na
Coastal Union.

UCHAGUZI TAFCA KUFANYIKA MOROGORO
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(TAFCA) utafanyika Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma ambapo
wajumbe wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya uchaguzi.
Wagombea waliopitishwa kuwania uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini
ya uenyekiti wa Ramadhan Mambosasa ni Oscar Don Koroso (Mwenyekiti), Lister
Manyara (Makamu Mwenyekiti) na Katibu (Michael Bundala).
Wengine ni Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF (Wilfred Kidao) wakati wagombea
ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Jemedali Saidi, George Komba na Magoma
Rugora.

KIM KUTAJA KIKOSI CHA KUIKABILI MOROCCO

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen
anatarajia kesho (Machi 13 mwaka huu) kutaja kikosi chake kitakachoivaa
Morocco.
Mkutano huo wa Waandishi wa Habari utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam, Machi 24 mwaka huu.



MECHI YA SIMBA, COASTAL YAINGIZA MIL 37/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Coastal Union iliyochezwa
juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 36,820,000 kutoka na
watazamaji 6,284.
Viingilio katika mechi hiyo namba 138 iliyomalizika kwa Simba kuibuka na
ushindi wa mabao 2-1 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,265,752.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 5,616,610.17.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,202,924.97,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 2,521,754.98, Kamati ya Ligi sh.
2,521,754.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,260,877.49
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 980,682.49.

*Boniface Wambura*
*Ofisa Habari*
*Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)*

SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE OPENING OF THE AFRICAN CONFERENCE ON THE STRATEGIC IMPORTANCE OF INTELLECTUAL PROPERTY (IP)

$
0
0


President Dr Jakaya Mrisho Kikwete chats with Dr. Francis Gurry,
Director General of the World Intellectual Property Organization (WIPO)
moments before opening the African Conference on the Strategic Importance
of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and
Competitiveness at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam
today March 12, 2013.


A standing ovasion as President Dr Jakaya Mrisho Kikwete arrives for the
opening the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual
Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness
at the Hyatt Regency Kilimanjaro hotel in Dar es salaam today March 12, 2013
.*
SPEECH BY H.E. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA,  AT  THE OPENING OF THE AFRICAN CONFERENCE ON THE STRATEGIC IMPORTANCE OF INTELLECTUAL PROPERTY (IP) POLICIES TO FOSTER INNOVATION, VALUE CREATION AND COMPETITIVENESS, ON 12 MARCH 2013, KILIMANJARO HYATT REGENCY HOTEL, DAR ES SALAAM,

Honourable Dr. Abdallah Kigoda, Minister for Industry and Trade;
Mr. Bruno Jean Richard Ihua, Chairman African Ministers Council on Science and Technology;
Honourable Ministers and Heads of delegation;
Dr. Francis Gurry, Director General of the World Intellectual Property Organization (WIPO);
Mr. Elberic Kacou, UN Resident Coordinator;
H.E. Masaki Okada, Ambassador of Japan to Tanzania;
Mr. Toshihiro Kose, Director General, Trademark, Design and Administration Affairs Department, Japan Patent Office,
Your Excellencies, Ambassadors and Members of the Diplomatic Corps;
Invited guests;
Distinguished participants;                                                                             
Ladies and Gentlemen:

            I thank you Dr. Francis Gurry, the Director General of WIPO, and your entire team for associating me with this all important African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness. I sincerely, thank you for choosing my dear country, Tanzania, to host this Conference. You have made us proud.  We will always remain grateful for affording us this rare honour and privilege.
           I also thank all the participants who have travelled many miles to come to Dar es Salaam to participate at this Conference. I welcome you all to Tanzania and Dar es Salaam in particular.  I believe you have been received well. Please feel at home and enjoy the traditional Tanzanian hospitality.   Your presence here is a clear testimony of your realisation of the strategic importance of intellectual property (IP) to Africa’s development.
Ladies and Gentlemen;                                                                                     
It is a statement of fact that leveraging and protecting Intellectual Property (IP) such as patents, copyrights and other similar forms is a key factor of promoting socio-economic growth and development of nations. It encourages innovation, invention and development of new technologies.  It promotes both domestic and foreign investment, facilitates technology transfer and increases agricultural and industrial production. 
It is an imperative, therefore, that countries must put in place effective IP policies and related laws. Developed countries have fully apprehended the dynamics of intellectual property in inevitably driving developments in their respective countries and in the global arena. Fortunately, many developing countries are increasingly becoming aware of the importance of IP in their development endeavours and are taking appropriate measures in this regard.
I am aware of the arguments from some corners that Intellectual Property may not be as beneficial to developing countries because it limits technology transfer through imitation. I know, also, the assertion that IP increases the prices of medicine, agricultural inputs and many other things.  However, true this may be, embracing IP policies and measures is comparatively, far more beneficial to the overall growth of nations and economies than doing otherwise.  Putting in place appropriate IP policies and measures are critical factors in promoting innovation and competitiveness which play key role in economic growth and sustainable development.
It is for this reason that many African countries have been taking serious steps to embrace, anchor and nurture IP. In recent times IP issues have been assuming centre stage in nations development strategies.   On the whole, the level of commitment by African countries is increasing and accordingly, the support of international community has been forthcoming. The challenge before us is that of lack of adequate experts and institutional capacity to develop effective policies and related laws.
Distinguished participants;
Just like many other African countries, Tanzania is also aware of the benefits and role that intellectual property can play for accelerating the socio-economic development of our country. We know, for sure, that effective and strategic use of intellectual property has assisted many countries across the globe to attain rapid economic development. It has also assisted people in those countries to be creative and innovative, hence became economically competitive. 
Aware of these realities, since 1983 we have intensified our collaboration with WIPO for the purpose of realising the benefits of intellectual property. We have established the Business Registrations and Licensing Agency (BRELA) with the mandate to administer industrial property laws in the country.  We have also established the Copyright Society of Tanzania (COSOTA) which deals with copyright issues. The two institutions are doing a good job but there is a lot more work to do ahead of them.
We have already formulated our National IP Strategy and we are now in the process of formulating the National IP Policy. WIPO has been very instrumental in the modest achievements we have made todate.  I would like to seize this opportunity to thank the Director General of WIPO for the invaluable financial and technical support extended to us in this regard. Thank you for walking with us in every step we have been taking.  It has made a huge difference.  I trust that the existing cooperation will be sustained and strengthened.
Ladies and Gentlemen;
We know for sure, that once the IP policy is in place and fully implemented, it will assist producers of industrial and agricultural products to compete effectively in the local, regional and global market place. We are fully aware that when products are identified with trade marks to distinguish them from similar products of competitors, they become more competitive in the market.  The example of Ethiopian coffee farmers who have branded their coffee beans and are now reaping premium price for their products gives us inspiration. I am happy to note that WIPO is assisting Tanzania to develop a branding strategy for our distinctive agricultural products.
Apart from industrial and agro products, the IP policy will also support the growth of Creative or Copyright Based Industry in the country. At the moment the industry is growing fast and employs a large segment of the population, particularly our youths.  It has a huge capacity and potential to employ many more in future.  So far the Copyright Society of Tanzania has registered a large number of artists’ and literary work and continues to work tirelessly to curb piracy. We know, however, with an effective IP policy, we can do more, we can do better.  Short of that, stakeholders will be discouraged and it will be a daunting task to cultivate a credible and attractive creative industry.
Ladies and Gentlemen;
As I alluded to earlier, one of the major challenges that many African countries are facing is lack of a critical mass of experts to formulate and enforce effective IP policies and related laws. We, in Tanzania are also facing the same challenge, but have decided to deal with it.  I am happy to say that, the University of Dar es Salaam in collaboration with BRELA and the African Regional Industrial Property Organisation (ARIPO) will soon sign an MoU to launch a masters degree program in IP. This will definitely help in easing and ultimately, eliminate the shortage of experts in the field of IP. 
I would like to take this opportunity to once again congratulate and commend the University of Dar es Salaam, BRELA and ARIPO for the wise and visionary decision to address this important matter. I sincerely, hope that WIPO will extend the necessary support to this initiative and help make it a success.
Ladies and Gentlemen;
 Let me restate that, I have no doubt in my mind that properly anchoring use of intellectual property can contribute immensely to socio-economic development and eradication of poverty in our nations.  Appropriate IP policies and laws coupled with an effective education system, availability of financial resources to pursue technological development and the presence of a network of supporting institutions and legal structures will deliver the desired results and benefits. Because many African countries are lagging behind, there is need to find ways of assisting them in building the capacity to formulate and implement IP policies and measures.  The assistance should go beyond IP policies and embrace other related matters and sectors. In other words, IP policies should be integrated with development policies.  May I use this opportunity to appeal to our development partners to explore the possibilities of increasing support to African countries in IP related issues. IP should be regarded as an integral part of the development issues they are engaged with. They should not be looked differently and dealt with in isolation.
Ladies and Gentlemen;
Before I conclude my speech, it would be remiss of me if I concluded my remarks without recognising and commending the African Regional Industrial Property Organisation (ARIPO) and the African Intellectual Property Organisation (AIPO) for the good work they have doing on the continent. These two regional organisations have been doing a wonderful job in creating awareness of IP matters in Africa despite limited resources and other constraints. I appeal to Member States to ensure that these two gallant organisations are well supported so as to be able to continue to do the good job they are doing. I would like to pledge Tanzania’s support.  We look forward to strengthening our cooperation with these important organisations. I call upon the international community and regional organisations to enhance their support in order to strengthen these organisations and make them more responsive to Africa’s special needs.
Ladies and Gentlemen;
After these many words, I now have the honour and privilege to declare the African Conference on the Strategic Importance of Intellectual Property Policies to Foster Innovation, Value Creation and Competitiveness officially opened. I wish you every success and fruitful deliberations.
                              I thank you for your kind attention.

Agnetha Faltskog sauti ya mvuto ya Abba iliyorejea kwa kishindo

$
0
0


Ukisikiliza muziki huo unaweza kukumbuka mengi mwimbaji wake amerejea

Baada ya miaka 9  mwanamama mwenye sauti yenye raha ya aina yake katika muziki wa pop ambaye alitamba sana kipindi cha ABBA  Agnetha Faltskog anatoka  na albamu inayompa neno Gary Barlow na kushirikisha waandishi wa muziki wa kiswidi wa Britney Spears.
Miaka 45 iliyopita hata kabla Abba hawajachengua watu bara la Ulaya Agnetha Faltskog alionekana katika televisheni kwa mara ya kwanza. Akiwa na miaka 17 aliwapa watu kitu kinaitwa Jag Var Sa Kar (yaani  kwa kimombo I Was So In Love), ilikuwa ni waltz ya aina yake na akaenda hewani kupitia Studio 8 ya Sweden.

Mistari iliyotengenezwa  kwa kumwangalia mtu anayempenda Connie Francis,  ina tofauti kubwa na mdada mwenye muonekanano wa dhahabu ambaye alitwaa redio na kuzunguka nayo aliposikia singo yake ya kwanza radioni.
Akiwa mdogo hakujua kwamba matatizo ndiyo yatakuwa ngome kubwa ya muziki wake wakati alipojiunga na akina Benny, Bjorn na Anni-Frida kuunda Abba.
Nyimbo ambazo Faltskog alikuwa ndio mwimbaji kinara ni kama Hasta Manana, The Name Of The Game, Chiquitita  ambazo zimewaacha hoi wapenzi wengi wa muziki.
Ukitaka kujua ukweli kuwa matatizo ndio msingi wa muziki wake bomba angalia video ya On The Winner Takes It All, wimbo ambao ulirekodiwa wakati ndoa yake kwa Bjorn Ulvaeus inavunjika.
Wimbo huu ulikuwa na  hisia kali, kiasi cha mtu kushindwa kabisa kuvumilia.Faltskog katika muziki huu aliimba nilikuwa katuika mikono yako nikidhani nastahili kuwa humo, huku analia lakini mume wake aligeuka na kuondoka na hata kumshika mkono ikawa ama basi.
Pamoja na ugumu wa wimbo huo  Faltskog anasema ndio wimbo anaoupenda mno miongoni mwa nyimbo ambazo wameimba na Abba, alichosikitika ni kuwa hawakupata nafasi ya kuupeleka laivu kwenye jukwaa.
Tangu Abba isambaratike 1982 mwanamama huyo mwenye nywele za dhahabu amekuwa mmoja wa watu ambao hawapatikani kirahisi. Mara nyingi hujichimbia kwake kisiwa cha  Ekero, magharibi mwa Stockholm nchini Sweden kimya kabisa.
Kutokana na mistari yake yenye ukakasi mdada huyu alitambuliwa kama- the Greta Garbo of pop. Mwaka 2000  ilielezwa kuwa ameingia katika uhusiano wa karibu na mpenzi wake mmoja wa muziki  wa
Kiholanzi aliyekuwa mdogo kwa miaka 16 kuliko yeye ilileta hisia nyingine hasa pale  uhusiano huo ulipokuwa hatari wakati mdada aliposema basi kwa kijana huyo.
Lakini la maana hapa ni kuwa inaonekana dhahiri kwamba mwanamama wetu alikuwa mpweke.Leo mwanamama huyu hawezi kuzungumzia uhusiano wa kimapenzi kwa sababu za kisheria , lakini mdada huyu au tuseme mmama huyu Faltskog  anasema kwamba vyombo vya habari vimekuwa na mawazo hasi kuhusu maisha yake binafsi.
"Nimekuwa nikielezwa kuwa ni binadamu wa ajabu msiri na hili linauma kidogo, manake sivyo nilivyo,"alisema.Agnetha Faltskog amesema kwamba tangu aachane na Abba hakuwa anafanya shughuli za muziki.
Akizungumza na waandishi wa BBC London kutoka Stockholm, pamoja na kuchagua vyema maneno yake
huku akiwa na mkalimani alikuwa akicheka kila mara na kukanusha kwamba yeye si mtu aliyejitenga
"Mimi ni mtu wa kawaida kabisa," anasema. "Tatizo hupenda kukaa nyumbani."Mlango mpya ulifunguliwa miezi 18 iliyopita wakati projuza mmoja wa Kiswidi Jorgen Elofsson alipofika nyumbani kwake akitumaini kwamba Faltskog ataimba nyimbo tatu alizomwandikia.
Akiwa ni komposa aliyefanikiwa sana kimataifa akiwafanyia kazi akina Britney Spears kwa wimbo wa Crazy na Kelly Clarkson kwa wimbo wa Stronger (What Doesn't Kill You), alikuwa na ndoto ya kumshawishi Faltskog kuondoka katika ukimya wake wa miaka tisa na kuingia studio.
"Nilishangazwa sana,"alisema mwimbaji huyo. "kweli niliduwaa."
"Sikuweza kusema hapana  nilizipenda nyimbo hizo tangu awali."
Lakini kabla ya Faltskog kukubali kuingia studio alitoa masharti ambayo ndio kama dira yake.
"Nilimwambia kwamba tuzungumze kwanza,'" akikumbuka na kuongeza: "Ilikuwa ni miaka tisa au kumi sijaimba kwa hiyo sikuwa najua kama sauti yangu inaweza kuwa barabara."
"Nilimwambia kama sauti itakuwa ya kizee sitataka kuimba.. kwanini niimbe?'"
Ukisikiliza albamu ambayio imebatizwa jina la A ni dhahiri kwamba Faltskog bado wamo sana.
 



Kingunge Ngombale Mwiruazindua kitabu cha Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi

$
0
0



Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu
historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi  katika hafla iliyofanyika leo  kwenye
ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.
MWANASIASA mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwataka viongozi nchini kukienzi na
kuthamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mzee Kingunge ambaye alikuwa  mgeni ramsi katika
hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee,  jijini Dar es Salaam.
“Hatima ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa katika
kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio wanaweza kukipandisha au
kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee
Kingunge.
Aidha  Mzee Kingunge anawaasa kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha
tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali mfano Bungeni.
Hata hivyo, aliunga mkono  lugha hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa
changamoto kuwa yatupasa kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya
msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.
Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake kuwa masomo mengine kama vile hesabati
wanapata  alama 90 hadi 95,lakini lugha hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo
inaelekea ufundishaji wake ni tatizo.
“Kama kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na
Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimua ya Chuo
Kikuu,”alisema. Huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno ambayo si
sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.
Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha hiyo  Profesa Mugyabuso Mulokozi na 
Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuenzi   fasihi za
Watanzania.
Source: NA: FRANK SHIJA & BENEDICT LIWENGA- MAELEZO

abiria 1,200 wa treni ya Kati wakwama

$
0
0
Abiria wa treni wakiwa katika mstari wa kupata fedha ya kujikimu baada ya kukwama dodoma  leo

Zaidi ya abiria 1,200 waliokuwa wakisafiri kwa njia ya treni kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam wamekwama mjini  Dodoma kutokana na mafuriko kung’oa reli  eneo la Godegode wilaya ya Mpwapwa.
Msimamizi wa kituo cha reli cha cha Dodoma Celsus Roman alisema kuwa treni hiyo iliyoingia Dodoma leo saa tano na nusu asubuhi ,
haikuweza kuruhusiwa kuendelea na safari kutokana na maji kujaa kwenye  stesheni  za  Mgandu,  Msigalu, Gulwe na Godegode.
Alisema pamoja na maeneo hayo kujaa maji , tuta la reli limesombwa na sasa mafundi wanashughulikia tatizo hilo.
Aidha alisema Kampuni ya reli (TRL)  makao makuu imeagiza kila abiria apewe fedha za kujikimu kiasi cha sh 2,500 na kuwa  treni hiyo inatarajia kuendelea na safari yake kesho.
Source:Sifa Lubasi, Habarileo

Media Day Bonanza Aprili 6.. TBL kumwaga milioni 50

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu bonanza la vyombo vya
habari litakalofanyika mwezi ujao na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia (TBL). Wengine ni Ofisa Uhusiano
wa TBL, Doris Malulu na Mjumbe Kamati ya Utendaji Taswa, Grace Hoka. (Picha na Yusuf Badi).

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) itadhamini bonanza la vyombo mbalimbali vya habari litakalofanyika Aprili 6 mwaka huu viwanja vya Leaders Klabu, Dar es Salaam likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kutambulisha bonanza hilo Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa kampuni yake kudhamini bonanza linaloandaliwa na TASWA na kwamba wamekuwa na matumaini makubwa na chama hicho ndiyo sababu wanakubali kushirikiana nacho kila mwaka.

Malulu alisema zaidi ya Sh. Milioni 50 zitatumika kwa ajili ya bonanza hilo na kusisitiza kuwa lengo la kampuni yake ni kuona linakuwa na mafanikio makubwa kuliko mengine yaliyopita.

“Wanahabari ni wadau wetu wakubwa, hivyo kupitia TASWA tunaona ni njia nzuri ya kutuunganisha na kukaa pamoja kutafakari masuala mbalimbali,” alisema Malulu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru TBL kwa udhamini huo na kusema kuwa zaidi wa washiriki 1,500 wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA kila mwaka likijulikana kama Media Day Bonanza.

“Lengo la bonanza letu ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja,” alisema.

Alieleza kuwa bonanza hilo litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki kutoka katika moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi hapa nchini, ambayo itatangazwa siku zijazo.

Bonanza la mwaka jana lilifanyika ukumbi wa Msasani Beach Klabu, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta.

Pamoja na mambo mengine, Sitta alikabidhi zawadi za vikombe na medali kwa washindi mbalimbali walioibuka siku hiyo, pia alipata fursa ya kuzungumza na washiriki zaidi ya 1,500 wa bonanza hilo.

using'ang'anize simu mawimbi yanapokuwa 'nje-ndani'

$
0
0


WAMILIKI wa simu na televisheni bandia wameelezwa kuwa hatarini kiafya.
Tume  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imehadharisha watumiaji wa simu hizo za mkononi, wanaolazimisha kuzungumza wakiwa maeneo yanayopokea na kupoteza mawimbi.
Katika hadhari hiyo, TCRA imeweka wazi kuwa katika mazingira hayo, ni hatari kuzungumza na simu, kwa kuwa kuna  uwezekano wa mionzi mingi zaidi, inayoathiri afya na kuvuta radi.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma, alisema hayo jana kwenye warsha ya utoaji elimu kwa wanahabari kuhusu mionzi.
Katika warsha hiyo, Mamlaka hiyo ilitoa ripoti ya utafiti, uliomaliza uvumi uliosambaa na kuogofya watu kuwa minara ya simu za mkononi na simu zenyewe, zinatoa mionzi inayosababisha saratani kwa binadamu.
Ripoti hiyo iliyotokana na utafiti uliofanywa na taasisi zaidi ya tano ikiwamo TCRA kwa miaka mitatu, ilibainisha kuwa kiwango cha mionzi kinachotumika kwa sasa ni salama.
Simu, televisheni feki
Hata hivyo, mbali na kuhadharisha watumiaji wa simu za mkononi wanaolazimisha kuzungumza katika maeneo yanayopokea na kupoteza mawimbi, Profesa  Nkoma alionya wanaotumia simu na televisheni bandia.
Alisema wanaonunua na kutumia vifaa vya mawasiliano kama  simu na televisheni zisizo na viwango vinavyotakiwa,     wana hatari ya kutumia mionzi mingi zaidi ili kupata mawasiliano, na hivyo kuathiri afya zao.
"Nawasihi Watanzania mtumie simu, televisheni na vifaa vingine vya mawasiliano vyenye viwango na ubora uliothibitishwa na Mamlaka yetu vinginevyo, mtakaribisha matatizo kwa sababu zinauzwa kwenu bila kuhakikiwa kama zina uwezo wa kuzuia madhara ya mionzi au la,” alisema Profesa Nkoma.
Minara salama
Pamoja na kutoa hadhari hiyo, alitaka Watanzania wanaoishi maeneo yenye minara, wasihofie afya zao kwa sababu mionzi inayotoka katika minara hiyo ni salama. Alisema kwa simu zinazotumika nchini, televisheni na redio za Tanzania Bara na Visiwani, havijafikia viwango vya mionzi vilivyotajwa kimataifa kuwa ni hatari.
Akitoa majibu ya ni kwa nini mionzi hiyo inaelezwa kuwa si hatari, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia kutoka Tume ya Atomiki (TAEC) iliyoshiriki utafiti huo, Dk Jarubi Nyaruba, alisema asilimia ya mionzi inayotoka katika mitambo na vifaa vya mawasiliano kama vile simu, ipo chini sana kiasi cha kutoweza kumwathiri mtumiaji au aliye karibu na minara.
"Tumefanya utafiti katika mikoa mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Dar es Salaam na mikoa mitatu ya Zanzibar, ambayo ni Mjini Magharibi, Unguja Kaskazini na Unguja Kusini.
“Tumepata matokeo, kwamba hata jumla ya asilimia ya mionzi yote katika maeneo yote yenye redio, televisheni na simu nyingi, hayajafikia yaliyowekwa kimataifa wala kuvuka na kuwa hatari,” alisema Dk Nyaruba.
Alitolea mfano viwango vya mionzi walivyopata katika simu, televisheni na redio zinazofanya kazi Dar es Salaam kuwa ni; asilimia 2.6 tu ya mionzi aina ya GSM inayotoka kwenye simu.
Alifafanua, kwamba viwango vya kimataifa vimeelekeza mionzi hiyo isizidi asilimia 41.9, kwa kuwa inaweza kuleta madhara kama vile saratani na mengineyo yanayosababishwa na mionzi mikali.
Nyingine ni asilimia 2.1 ya mionzi aina ya VHF, inayotoka katika televisheni za jijini humo, ambayo pia iko chini ya kiwango kilichokatazwa kimataifa kuwa kisizidi cha kimataifa cha asilimia 29.8.
"Maana yake ni kwamba mionzi ikiwa zaidi ya asilimia 29.8, watu wanaweza kuathirika lakini chini ya hapo, ni salama kama tulivyoona katika utafiti wetu," alisema Dk Nyaruba.  
Alifafanua zaidi kuwa katika televisheni hizo, kuna mionzi mingine aina ya UHF iliyofikia kiwango cha asilimia 0.6 tu, wakati kilichowekwa kimataifa kama ukomo ni asilimia 28.  
Utafiti huo ulifanywa baada ya kuwepo kwa uvumi na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, kwamba minara ya simu ni hatari na matumizi ya simu za mkononi yanasababisha saratani.
Ulifanywa kwa ushirikiano wa wataalamu kutoka Zanzibar na taasisi nyingine ikiwamo Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kampuni zinazotoa huduma za simu za mkononi.
source:Habarileo
  

Mwanadada Helen Joseph wa Ghana kukipiga Machi 30 na Mdominika

$
0
0


Helen Joseph, bondia mwanadada ambaye anaishi katika jiji la Accra, nchini Ghana akipigana ngumi yuko mboni kupanda kilele cha mafanikio katika maisha yake ya ngumi.
Mwaka jana alikutana na bondia Dahianna Santana katika jiji la San Domingo, nchini Dominican Republic kugombea ubingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa Unyonya (Fearherweight).
Taabu na kashikashi zote alizozipata wakati wa patashika ile ya mwaka jana zimekuwa fundisho tosha kwa Helen wakati anapojiandaa kukutana na Marianna Gulyas kutoka nchini Hungary kugombea ubingwa wa IBF wa mabara katika uzito wa unyoya. 
Mpambano huo, unaoandaliwa na kampuni maarufu ya kukuza ngumi ya GoldenMike Boxing Promotion Syndicate ya nchini Ghana unategemea kuwa wa patashika kweli kutokana na mabondia wote wawili kuwa na ujuzi tele ulingoni. Wawili hawa watakutana tarehe 30 March katika uwanja wa michezo wa Accra na mpambanohuu utarushwa moja kwa moja na luninga ya Super Sports. 
Ni mapromota wachache na mameneja wachache  ambao wanaweza kuwekeza kiasi kikubwa hivyo cha pesa katika mchezo wa ngumi namna ambapo kampuni ya GoldenMike Boxing Promotions Syndicate ya nchini Ghana imewekeza katika kuinua kipaji cha mwana dada Helen Joseph. 
Kwa upande wake Helen ambaye ni nadhifu, mtanashati na mwenye nidhamu ya hali ya juu, mchezo wa ngumi ndio unaomlisha katika maisha yake na atatumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa taji hli kubwa la ngumi linabaki barani Afrika na kulitumia kama ngazi ya kukutana tena na Dahianna Santana katika ubingwa wa dunia! 



ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Mbibi adakwa na kilo moja ya kokeini aliyoizinga katika nywele

$
0
0
Bibi mwenye wajukuu zake Giwa Ayoka Sikirat, 53, amekamatwa na maofisa wanaopambana na mihadarati wakati akitaka kunyanyuka na pipa uwanja wa ndege wa Nnamdi Azikiwe International Airport, NAIA, Abuja. Bibi huyo alikuwa ameficha kilo moja ya kokeini kwenye nywele zake.
Mbibi huyo inaaminika alikuwa njiani kwenda Pakistan.
Taasisi ya kukabiliana na mihadarati nchini Nigeria, NDLEA,imesema haikuwa na taarifa awali kuhusu mtuhumiw ahuyo hadi alipopekuliwa na askari wa kike na kushukiwa kuwa na mihadarati hiyo.
Lakini baada ya kutuhumiwa na kukaguliwa akabainika kuwa na unga wa kokeini.
“Mtuhumiwa , Giwa Ayoka Sikirat alikuwa ameficha  mihadarati hiyo katika nywele zake zilizosukwa vyema na kupendeza, alikamatwa wakati wa ukaguzi kabla ya kuingia kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia mruko namba ET 910 inayoelekea Pakistan  kupitia Addis Ababa na  Dubai,” taarifa ya NDLEA ilisema.
Kamanda wa NDLEA uwanja wa ndege Abuja, Hamisu Lawan, alikaririwa akisema: “ Hapakuwepo na taarifa za awali kuhusu Sikirat  kwani dawa hizo zilituhumiwa wakazi akikaguliwa na polisi wa kike katika mwili wake katika ukaguzi wa kawaida.”
Lawan alisema mtu huyo alikamatwa na mtu mwingine mwenye umri wa miaka 59 aliyetambulika kwa jina la Joseph Umunna, mzaliwa wa jimbo la Anambra ambaye ndiye aliyempeleka uwanjani Sikirat.
NDLEA wamesema kwamba dawa hizo ziliwekwa vyema katika nywele na wahusika mjini Lagos kabla ya kupelekwa uwanja wa ndege wa Abuja.
“Watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika kwa kuzingatia kanuni za NDLEAkwa kula njama za kutaka kusafirisha kilo moja ya kokeini,” taarifa ya NDLEA imesema.
NDLEA wamesema kwamba Sikirat alisoma shule ya St. Louis Primary School, Mushin na Isolo Secondary School zote zipo Lagos, Kusini Magharibi mwa Nigeria.
Pia alijifunza mambo ya mitindo mjini Lagos mwaka 1994. Anatoka jimbo la Kwara.

Mbwa ndani ya kofia ngumu kwenye pikipiki sisi inakuaje

$
0
0

Jamaa wa  Indonesia, anayependa mbwa kupita kiasi Handoko Njotokusumo, ambaye ni mfanyabiashara aliyestaafu amekuwa akifanya vitu vinavyostaajabisha watu kwa kumbeba mbwa wake Ace na kutembea naye katika pikipiki huku akiwa amemvalisha kofia ngumu  kuzunguka mji wa Surabaya.

Waangalie  wawili hao wakiwa katika safari za kawaida za kuangalia mji wa Surabaya

Moshi mweusi wa kwanza tayari...papa bado kupatikana

$
0
0

Moshi mweusi wa kwanza tayari

JANA ilimalizika kwa watu bilioni moja na milioni 200 wanaomfuata Kristo kupitia Kanisa Katoliki la Roma kuendelea na maombi baada ya kuona moshi mweusi ikiwa ni ishara kwamba kiongozi mpya wa kanisa hilo bado kupatikana.
Moshi huo mweusi uliashiria kwamba raundi ya kwanza imeisha na Makadinali hao wapatao 115 leo walitarajiwa kuendelea na upigaji kura wa kumsaka halifa wa Petro.
Makadinali hao watapiga kura mara nne kwa siku hadi kiongozi mpya atakapopatikana.
Kazi hiyo ilianza mara baada ya misa ya asubuhi katika kanisa la Sistine.
Wataalamu wa masuala ya Vatican wanasema kwamba wanaweza kupiga kura mara mbili wakati wa asubuhi na kama hakupatikana kura hizo zitachomwa moto na hivyo kutoa moshi mweusi na kazi nyingine ya kura itaendelea baada ya chakula cha mchana.
Kama kwa siku tatu kiongozi mpya atakuwa hajapatikana, kutakuwa na mapumziko na sala na majadiliano kabla ya kuingia tena katika uchaguzi.
Jana kiongozi wa makadinali hao, Mwitaliano Angelo Sodano, aliomba umoja katika Kanisa hilo, ambalo limegubikwa na kashfa na migogoro na kumtaka kila mmoja kushirikiana na Papa ajaye.
“Ndugu zangu, tuombe Mungu atupe Papa ambaye atatwaa jukumu hili tukufu kwa moyo mweupe,” Sodano alisema katika maombi yake. 
Uchaguzi unafanywa baada ya kujiuzulu kwa Papa Benedict mweiz uliopita kwa kauli kuwa hana nguvu za kutosha akiwa na umri wa miaka 85, kukabiliana na changamoto za uongozi wa Kanisa hilo lenye wafuasi bilioni 1.2 .
pamoja na mvua waumini walikuwa skwea ya mt Petro wakisubiri

Wanaopewa nafasi
Mwitaliano Angelo Scola na Mbrazili Odilo Scherer, ndio wanaotajwatajwa kupewa nafasi hiyo. Scola akipewa atakuwa ameurejesha upapa Italia baada ya miaka 25 kuwa mikononi mwa Mpolandi John Paul II na Mjerumani Benedict; Scherer anaweza kuwa Papa wa kwanza kutoka nje ya Ulaya tangu Msiria Gregory III aliyetawala katika karne ya nane.
Hata hivyo, wapo wengine ambao wanajulikana kama “papabili” yaani wenye nafasi ya kuwa mapapa- wakiwamo Wamarekani Thimothy Dolan na Sean O’Malley, Mkanada Marc Ouellet na Mwargentina Leonardo Sandri.
Makadinali hao ambao walianza kujifungia jana mchana watatoka humo baada ya kuwa wamemchagua Papa wa 266 katika historia ya miaka 2,000 ya Kanisa hilo .
Moshi mweusi kutoka kwenye dohani (bomba la moshi) juu ya paa la Kanisa dogo la Sistine, utaashiria kuwa hakuna aliyechaguliwa, wakati moshi mweupe na milio ya kengele katika Kanisa la Mtakatifu Peter ndizo zitakuwa zimetangaza kupatikana kwa Papa mpya.
Enzi za zamani, makadinali hao walipigwa marufuku kuwasiliana na walioko nje. Hivi sasa Vatican imechukua hatua za kiteknolojia ya hali ya juu kuhakikisha siri katika karne hii ya 21 inatunzwa na vimefungwa vifaa vya kuzuia mawasiliano ya aina yoyote ya kiteknolojia.

Aliyekuwa katika njama za kumuua Hitler, afariki dunia

$
0
0
Ofisa wa zamani wa jeshi la Ujerumani ambaye alishiriki katika mpango wa kumuua kiongozi wa taifa hilo  Adolf Hitler mwaka 1944  amefariki dunia.
Ofisa huyo aliyekuwa na cheo cha Luteni, Ewald-Heinrich von Kleist amekufa nyumbani kwake Ijumaa akiwa na umri wa miaka 90 mjini Munich , mke wake Gundula alisema akizungumza na  shirika la habari la Associated Press.
 von Kleist alikuwa na umri wa miaka 22 wakati alipojitolea kuvaa fulana ya kujitoa mhanga wakati wa mkutano na Hitler.
Mkutano huo haukufanyika lakini miezi michaxche baadaye alikuw amtu muhimu katika kile kilichokuja kubainika kama Mpango wa Julai 20.
Alitakiwa kubeba  mkoba ulisheheni mabomu kwenye mkutano na  kiongozi huyo wa Nazi, lakini baadae katika mabadiliko bomu lilitegwa na Kanali  Claus von Stauffenberg.
Kanali von Stauffenberg - nafasi iliyochezwa na Tom Cruise katika filamu ya 2008 iliyojulikana kama, Valkyrie -ndiye aliyeweka bomu katika chumba cha mkutano ambapo Hitler alikuwa anakutana na watu wake muhimu  kwenye kamandui ya East Prussia "Wolf's Lair".
Hata hivyo mpango haukuenda kama ilivyotarajiwa, mkoba ule uliondolewa na Hitler akaponea chupuchupu kwenye mlipuko uliotokea.
Kanali Von Stauffenberg, na baba yake von Kleist - mtu aliyejulikana kumpinga Hitler - na wengine waliohusishwa katika njama hizo za kumuua Hitler walikamatwa na baadae kuuawa.
Ewald-Heinrich von Kleist alikamatwa na kutupwa jela katika makambi maalumu,lakini baada alirejeshwa jeshini na kuendelea na mzigo.
Akiwa amezaliwa 1922 kaskazini Mashariki mwa Ujerumani sehemu ambayo kwa sasa ni Poland, von Kleist anatoka katika watu wa Prussia wenye kumiliki ardhi.
Akiwa ofisa miongoni mwa askari wa miguu,alifuatwa na na Kanali von Stauffenberg - ambaye alimtaka kuvaa 'fulana ya kifo' chini ya nguo zake ambazo zilikuwa zinaoneshwa kw amara ya kwanza kwa Hitler.
von Kleist alisema katika mazungumzo kwamba baba yake alibariki hatua hiyo.
Hata hivyo kikao cha aina hiyo hakikutokea.
katika maisha yake Ewald-Heinrich von Kleist alianzisha Munich Conference on Security Policy - taasisi isiyo ya kiserikali yenye nguvu kubwa ambayo hujumuisha wanadiplomasia wa kimataifa na watu wa ulinzi na usalama kujadili masuala ya kidunia.
Seneta wa Marekani John McCain akitoa rambirambi zake alisema:  "I learned a great deal over the years from Ewald's wise counsel and statesmanship. I enjoyed the great pleasure of his company and the privilege of his friendship, for which I will always be grateful."

Viewing all 9093 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>