Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9089 articles
Browse latest View live

The Ray of Hope yapata tuzo“Africa Magic Viewer’s Award.”

$
0
0


Filamu ya Kitanzania ijulikanayo kwa jina la The Ray of Hope iliyotengenezwa na kampuni ya Pilipili Entertainment imeshinda tuzo ya filamu bora  iliyotumia lugha asili ya Kiswahili katika tamasha la Tuzo za Watazamaji wa Afrika Magic “Africa Magic Viewer’s Award.”


Akizungumza wakati wa mahojiano leo jijini Dar es salaam Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Bi.Joyce Fissoo amesema ushindi wa tuzo hiyo ni Heshima kwa nchi na inatoa hamasa kwa waigizaji wa filamu nchi.
“Tuzo hii ni heshima kwa nchi kwa sababu inaonyesha filamu zetu zinaweza kufikia kiwango cha kimataifa,na filamu zote zilikuwa zimekaguliwa nakupewa madaraja.”Alisema Bi. Fissoo.
Aidha Bi.Fissoo amesema tuzo hizo ni changamoto kwa wasanii na watengeneza filamu nchini kutumia fursa zinazojitokeza kushiriki katika matamasha makubwa na tuzo mbalimbali za kimataifa ili  kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine jinsi wanavyoweza kutengeneza filamu zenye ubora.
Tuzo hizo zilifanyika hivi karibuni jijini Lagos, nchini Nigeria ambapo  filamu 110 zilizotengenezwa na makampuni 43 kutoka  nchi mbalimbali barani Afrika ziliingia  kwenye kinyanganyiro na tuzo 28 zilitolewa kutoka makundi 26.
Aidha filamu hizo zilikaguliwa na majaji tisa kutoka nchi za Ghana, Cameroon, Kenya ,Nigeria, Afrika kusini, Uganda na Zambia pamoja na Tanzania iliyowakilishwa na Katibu wa bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo.
Bi Fissoo amesema Tuzo hizo ni za kwanza kufanyika na zilifunguliwa na Waziri wa Gesi na Mafuta wa nchini Nigeria aliyemwakilisha rais Goodluck Jonathan ,viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji na Waziri wa Utamaduni na Utalii.
Vilevile tuzo hizo zilipambwa na bendi za muziki na waimbaji mbalimbali kama Femi Kuti, Tiwa Savage , Iyanya pamoja na kundi la Sauti Soul kutoka Kenya.

SOURCE : Beatrice Mlyansi

Maelezo-Dar es salaam.
13/03/2013

*WACHEZAJI 23 WAITWA STARS KUIKABILI MOROCCO*

$
0
0

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia
kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.



Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia
zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya
Tansoma, Machi 17 mwaka huu.



Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye
nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na
Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam),
Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga),
Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).



Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba),
Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).



Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na
Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).



Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh
(Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja),
Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa
tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

* *

*SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19*

Semina elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 itafanyika
Machi 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Washiriki wa semina hiyo
wanatakiwa kuripoti Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) siku moja
kabla (Machi 18 mwaka huu).



Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania
Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo
wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).



Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa.



*Boniface Wambura*

*Ofisa Habari*

*Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)*

Breaking news ...papa amepatikana.. moshi mweupeee peeee

$
0
0
Hatimaye Kanisa katoliki limempata kiongozi wake 266 baada ya moshi mweupe kuchomoza kwa maringo kutoka kanisa dogo la Sistine  huku kengele zikirindima basilika la Mtakatifu Peter.
Watu waliokuwa wamefurika katika  uwanja wa Mt. Peter walishangilia baada ya kuona moshi huo ikiwa pengine ni mara ya kwanza katika historia ya Papa kupatikana kwa kasi baada ya raundi takribani tatu tu.

Papa ni kutoka Argentina ataitwa Papa Francis wa 1

$
0
0
   Cardinal Jorge Mario Bergoglio has been elected as Pope Francis I
    The new pope will be the first pope to hail from from the Americas
    News greeted with joy by thousands in St Peter's Square
    The new pontiff will replace Benedict XVI who stood down last month for health reasons

Wakatoliki wampata Papa Francis wa Kwanza

$
0
0
VATICAN CITY, Vatican
KATIKA kipindi cha saa 24 tangu Makadinali 115  kujifungia kuchagua kiongozi mpya wa Wakatoliki wapatao bilioni 1.2 ,Kadinal Jorge Mario Bergoglio jana ameteuliwa kuwa Papa.
Papa mpya aliyetwaa jina la Francis wa Kwanza  anatoka Amerika ya kusini, Argentina.
Papa huyo mpya mwenye umri wa miaka 76, ambaye anakuwa papa wa 226 ni Papa wa kwanza kutoka nje ya bara la Ulaya katika kipindi cha zaidi ya miaka 1000.
Akionesha unyenyekevu mkubwa kwa mtu ambaye hajulikani sana katika siasa za Vatican,Muargentina huyo akizungumza kutoka kibaraza cha ghorofani kwenye basilika la Mtakatifu Petro alisema:“ Napenda kuwashukuru kwa kunikubali”.
Akiwa amejivika vazi jeupe, Papa Francis l aliwataka maelfu ya waumini waliokuwa wamejawa na furaha kumuombea  yeye ili kutekeleza vyema kazi zake, na pia papa Mstaafu benedict wa XVI.
Akiwa katika kibaraza hicho aliwashukuru makadinali wenzake kwa kumchagua kuwa Papa kwa kusema: “Mmemchagua mtu kutoka mbali, na hapa nipo.”
Furaha za watu wakati walipoona moshi mweupe ziliendelea hadi alipojitokeza kibarazani huku wakisema  kwa Kilatini “Habemus papam!,” wengine wakipeperusha  bendera na kusema 'Tumempata papa mpya'; na  “Viva il Papa!”
“Ilikuwa ni kama kusubiri uzazi wa mtoto, imependeza sana, " alisema mtu mmoja huku mtoto wake akiwa mabegani akipeperusha msalaba.
Francis l atakuwa na papa wa kwanza aliyezaliwa nje ya Ulaya tangu uvumbuzi wa akina Columbus wa nchi mpya kwa mujibu wa historia ya Kanisa.
Wachambuzi wa masuala ya imani na kanisa wanaona kuchaguliwa kwa Papa Francis, Makadinali wamepeleka ujumbe mzito kwamba hatima ya kanisa ni Nchi zilizo Kusini mwa Dunia  ambako kuna mamilioni ya Wakatoliki ambao bado wanaabudu kwa namna inavyostahili.
Moja ya shughuli za Papa Benedict wakati wa utawala wake ilikuwa ni kuhangaika na kanisa la Ulaya ambalo limekuwa likiondoka katika mafundisho ya awali, kwamba dini ndio msingi wa elimu na maadili, kisa ambacho kilimfanya kutwaa jina la Benedict akiwa na lengo la kuashiria haja ya kurejeshwa kwa utamaduni wa umonaki katika bara la Ulaya .
Papa mpya anapokea utawala wa Kanisa ambalo limegubikwa na changamoto nyingi ambazo ziliongezeka sana wakati wa utawala wa Papa  Benedict XVI , kuanzia upungufu wa mapadri, kuibuka kwa makanisa ya kiinjili katika mzingo wa Kusini wa dunia ambako wakatoliki wengi wanaishi,tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na viongozi wa kanisa na matatizo katika utawala ndani ya Vatican.
Papa Francis ambaye anachukua madaraka kutoka kwa Papa Benedict XVI aliyejiuzulu ghafla mwezi uliopita baada ya miaka minane ya utawala, kutokana na kile alichoeleza kutoweza kuendelea na changamoto za utawala kutokana na afya yake, alikuwa Papa wa kwanza kujiuzulu katika kipindi cha miaka 598.
Papa huyu mpya alizaliwa Desemba 17, 1936 mjini Buenos Aires. . Ingawa awali alikuwa anataka kuwa mkemia, safari yake ilibadilika baada ya kujiunga na jumuiya ya Majezuiti (Society of Jesus ) mwaka 1958 na kuanza kujiandaa kwa upadri; na miongo mitano baadaye anakuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa akitwaa nafasi ya Petro. Papa Francis alipewa upadri Desemba 13 , 1969 wakati akisomea teolojia mjini San Miguel na ana ndugu wanne.
Televisheni ya Marekani ya CNN  imesema kwamba Kadinali Pergoglio  anajulikana kwa jinsi anavyoangalia masuala mbalimbali kwa namna yanavyostahili kuangaliwa kwa misingi ya asili ya kanisa, ikimaananisha kwamba matumaini ya uliberali ndani ya kanisa ni finyu. Papa mpya ni miongoni mwa watu ambao wanashikilia ukale na wasiopenda mabadiliko.
Papa huyu amekuwa akichukua msimamo mkali katika masuala ya ushoga, ndoa ya jinsia moja na matumizi ya njia za kisasa za kuzuia uzazi.
Akiwa pia ni Askofu Mkuu wa Buenos Aires , Papa Francis wa kwanza  inaaminika mwaka 2005 ilikuwa karibu sana aupate Upapa lakini baada ya uchaguzi wa Benedict XVI, taarifa mbalimbali zilionesha kwamba Mjezuiti huyu kutoka Argentina ndiye alikuwa mshindani wa aliyekuwa Kadinali Joseph Ratzinger, wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005.
Papa Francis  ni mwanazuoni wa teolojia akiwa amejifunza nchini Ujerumani na kwamba alikuwa anatumia usafiri wa umma badala ya gari la kifahali la kikadinali alilopaswa kulitumia:Aidha imeelezwa kuwa amekuwa akipika chakula chake mwenyewe wakati mwingine, dalili ya wazi kwamba hupenda maisha kawaida ya ufukara si anasa au kiutawala.
Papa huyu amekuwa akiwapigania sana watu maskini na amekuwa akieleza wazi kwamba hakuna usawa katika kugawana utajiri wa dunia kiasi cha kusababisha dhambi inayolia mpaka mbinguni.
Wachambuzi wanasema kwamba papa huyu atakuwa na kazi kubwa ya kuidadavua Vatican ambayo kwa namna moja imeonekana kama sehemu ya mapigano miongoni mwa waendesha kanisa wa Roma.
Maaskofu hata hivyo wanatumaini kupewa bnafasi zaidi ya kuhudumia waumini wao kwa kuwepo kwa mabadiliko katika curia ya Roma.

Mjue Papa Francis 1

• Hupenda usafiri wa umma
• Ameishi kwa miaka 50 na pafu moja tu linalofanyakazi, jingine liliondolewa akiwa kijana kwa ugonjwa.
• Ni mtoto wa mfanyakazi wa reli mwenye asili ya Italia.
• Alijifunza kuwa mkemia ni mkemia.
• Mwaka 2001 aliosha miguu ya wagonjwa wa ukimwi na kuibusu
• Anazungumza kitaliano, Kihispania na Kijerumani.
• Amekuwa akiishi katika nyumba akikwepa makazi ya kiaskofu
• Amewataka Waajentina wasiende Roma akiteuliwa, lakini watoe fedha kwa maskini.
• Anaamini mashoga kuasili ni aina ya ubaguzi kwa watoto
• Ameandika kitabu kwa kihispania Spanish, Sobre el Cielo y la Tierra (On Heaven and Earth).
• Japo ni mkale amekuwa akiwashutumu mapadri wanaokataa kubatiza watoto wanaozaliwa nje ya ndoa
• Anaaminika kwamba alikuwa namba mbili uchaguzi wa 2005
• Ni papa wa kwanza asiyetoka Ulaya katika kipindi cha usasa

JK azindua jengo la kitivo cha sayansi chuo kikuu cha Kiislamu

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), wameshauriwa wajiepushe  na mambo yatakayowapunguzia  muda na kuwaondoa kwenye  shughuli zao za   msingi walizozifuata  ya kupata shahada za fani walizochangua kuzisomea .
Changamoto hiyo imetolewa na Rais  Jakaya Kikwete leo,katika  hotuba yake mbele ya  viongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu hicho kwenye viwanja vya  Chuo hicho mara baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( ICT) na kufungua jengo la Kitivo cha sayansi .
Hivyo aliwataka kuona fahari ya kuwa wanafunzi wa chuo Kikuu hicho cha kihistoria hapa nchini, na pia kuwataka watumie kwa kadiri ya uwezo  na vipaji walivyopewa na mwenyezi mungu kufanikisha kile kilichowaleta Chuoni hapo.
“ Vishawishi ni vingi na watu wanaopanga kuwashawishi ni wengi, mambo ya dunia ya nje ya Chuo ni mengi huna budi kutambua lipi ufanye na lipi usifaanye “ alisema Rais katika hotuba yake.
Pia  alisisitiza  kusema “ Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima , si mtoto , lakima ujue kuwa unawajibika kwa kila unaloamua na kutenda, hivyo amua kuwajibika vizuri , fikiri kabla ya kutenda , changanua lipi  ni lipi kabla ya kufanya uamuzi wa kile unachotaka kufanya” alisema Rais.


Hotuba yake kamili

HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA  SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA  MOROGORO (MUM),
TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO



Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF);
Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro;
Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;


Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa.  Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki.  Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Natoa pongezi nyingi kwako, Makamu Mkuu wa Chuo na wale wote walioshiriki kubuni wazo la kuwa na jengo la Kitivo cha Sayansi na kufanikisha ujenzi wake.  Juhudi zao na moyo wao wa kupenda maendeleo ndio umetufanya sisi kujumuika hapa leo kushuhudia mafanikio haya. Hakika ni jambo la kujivunia. Pia, nawapongeza sana Wajenzi na Mhandisi Mshauri kwa kazi nzuri waliyofanya ya ujenzi wa jengo hili.  Sote tunaliona jengo lilivyojengwa vizuri na kwa namna yake linapendezesha mandhari ya Chuo.

Kwa namna ya pekee napenda kwa niaba yenu nitoe shukrani zangu za moyoni kwa taasisi ya Al-Barakah kwa kufadhili ujenzi wa jengo hili.  Asanteni sana kwa ukarimu wenu na upendo mkubwa mliouonesha kwa nchi yetu na watu wake. Naomba taasisi nyingine na watu binafsi waige mfano huu mzuri wa kusaidia miradi mbalimbali inayonufaisha jamii.  Tukumbuke ule msemo wa wahenga kuwa “kutoa ni moyo, usambe si utajiri”.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Mabibi na Mabwana;

Kwa miaka mingi madhehebu ya dini  na mashirika ya dini yamekuwa washirika muhimu sana wa Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu.  Yamekuwa yanajihusisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile afya, elimu na nyinginezo. Kwa ajili hiyo watu wengi sana nchini wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika ya dini.

Kwa miaka mingi  mashirika na  taasisi za madhehebu ya dini ya Kikristo ndiyo yaliyokuwa yakionekana kutoa huduma hizo. Kwa upande wa Waislamu, ukiacha Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, mchango umekuwa mdogo sana. Ni jambo la faraja kubwa kuona Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) ikionyesha njia.  Kwa kumiliki na kuendesha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa ufanisi, MDF inatoa mchango muhimu katika kuendeleza elimu ya juu na maendeleo nchini.  Idadi kubwa ya wanafunzi waliofuzu masomo yao na waliopo katika Chuo hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2005 ni ushahidi tosha wa kazi nzuri inayofanywa na MDF.  Hongereni sana.  Tunawaombea kwa Mola mpate mafanikio makubwa zaidi miaka ya usoni kwa upande wa elimu na huduma nyingine muhimu.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Katika kipindi cha miaka saba sasa, Serikali yetu imeongeza sana uwekezaji katika upanuzi wa elimu  tangu ya awali hadi elimu ya juu.  Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu vijana wengi waliokuwa wanastahili kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu walikuwa hawapati. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo.  Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa 108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973. Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini.  Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari.  Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari.

Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee.  Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote.  Matokeo ya uamuzi huo ni kwamba vijana wanaopata fursa ya kupata elimu katika ngazi zote wamekuwa wengi kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu, tumewafikia na kuwapita majirani zetu. Kazi kubwa tunayoendelea nayo sasa ni kuwekeza katika kuimarisha ubora wa elimu waipatayo vijana wetu kwa kuongeza walimu, vifaa vya kufundishia, vitabu na huduma nyinginezo. Inshallah hata kwa dhamira yetu, hii njema Mola atatuwezesha. Mwanzo mgumu lakini hatma itakuwa nzuri.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa.

Serikali itaendelea kuwekeza  kwenye upanuzi wa fursa za elimu na ubora wake. Hata hivyo ushiriki wa wadau wengine kuunga mkono juhudi za serikali ni jambo muhimu sana.  Tumeweka  mazingira mazuri kwa wadau hao kufanya hivyo na mafanikio yanaonekana wazi. Kama nilivyokwishasema awali, mashirika ya dini yamekuwa wadau wa kutumainiwa na mchango wao uko wazi. Unajieleza wenyewe. Kwa mfano, katika vyuo vikuu 49 vilivyopo nchini, vinavyomilikiwa na umma ni 14 tu. Vyuo vikuu 24 vinamilikiwa na mashirika ya dini na 11 na sekta binafsi.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na muhimu unaotolewa na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na sekta binafsi.  Ninyi mmekuwa washirika wazuri na wa uhakika katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu katika nchi yetu.  Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nanyi ili kuwawezesha vijana na Watanzania wengi zaidi waweze kupata elimu. Uamuzi wa kufanya utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu uhusishe wanafunzi wa vyuo visivyokuwa vya umma ni moja ya mambo mengi muhimu yanayofanywa na Serikali kuthibitisha usemi wangu huo. 

Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.  Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa  kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na  shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi 16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772.

Tutaendelea kuongeza fedha katika Mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na hata ifikie siku moja tuweze kuwakopesha wote bila ya kujali sifa ya uwezo wa wazazi au walezi kulipa ada.  Kwa kasi tuliyonayo na kwa jinsi tunavyozidi kufanikiwa katika kukusanya mapato ya serikali, naamini miaka michache ijayo tunaweza kufikia lengo hilo. Nawasihi Bodi ya Mikopo iwekeze katika  kuimarisha uwezo wa kuwafuatilia waliokopeshwa kulipa mikopo waliyopewa. Matamanio yangu ni kuwa fedha zilizotolewa zizunguke ili tupunguze kiasi kinachotolewa na bajeti ya serikali kila mwaka.  

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Mabibi na Mabwana;


Niruhusuni nitumie nafasi hii kukupongeza wewe Mkuu wa Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo, Wahadhiri  na Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu hiki  kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo ya kuendeleza na kuboresha Chuo. Tumeshuhudia ujenzi wa jengo nililolifungua leo. Tumeona mafanikio kwa upande wa ongezeko la idadi ya wanafunzi, walimu, wafanyakazi na fani zinazofundishwa katika kipindi hiki kifupi cha uhai wa Chuo hiki.

Nimefurahishwa na kufarijika sana  kusikia kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa chuoni ni jambo linalopewa kipaumbele cha kwanza.  Jambo hili ni muhimu sana kulisisitiza kwani tunataka wahitimu wa Chuo hiki wafanane na wahitimu wa Chuo chochote kizuri nchini na hata duniani.  Ningependa kuona wahitimu wa Chuo hiki wanagombewa katika soko la ajira.  Hili ni jambo linalowezekana.  Kinachotakiwa  ni uamuzi wa Baraza na Seneti kuwa iwe hivyo na kuchukua hatua zipasazo.  Sina shaka kuwa mnaweza kufanya hivyo.  Hakika mnaweza, na sote kwa umoja wetu tunaweza.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Nimefurahi sana, pia, kusikia kuwa Chuo kinatoa mafunzo ya ualimu. Bila ya shaka mnaelewa kwa nini nafurahi. Tuna uhaba mkubwa wa walimu nchini hivyo Chuo cho chote kinachotoa mafunzo ya ualimu hunifurahisha.  Endeleeni kuimarisha mafunzo hayo ili Chuo chenu kitambulike na kukubalika nchini kwa sifa ya kutoa walimu wazuri.  Walimu wa kutoka Chuo hiki wawe wale wanaojua vyema masomo wanayofundisha, mahiri kufundisha na waadilifu.  Naomba pia mtoe kipaumbele cha juu kwa mafunzo ya ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati.  Mkifanya hivyo, mtakuwa mnatoa mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini.  Naamini kitendo cha kuzindua Jengo la Kitivo cha Sayansi, kilichofanyika muda mfupi uliopita kinatoa matumaini ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kuchangia katika jitihada za kupunguza pengo la walimu wa sayansi nchini. 

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Nimewasikia mkieleza kwa ufasaha changamoto kubwa na ndogo ambazo Chuo inakabiliana nazo.  Nawapongeza kwa dhati, wewe na viongozi wenzako kwa ubunifu wenu na hatua mnazochukua kuzikabili changamoto hizo.  Nawaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali kwa yale yaliyoko kwenye uwezo wangu na wa serikali katika kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili.

Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kutafuta vyuo vikuu rafiki vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani mnavyoweza kushirikiana navyo.  Endeleeni kufanya hivyo kwani vyuo vikuu vingi duniani hufanya hivyo.  Hamtakuwa wa kwanza na wala hamtakuwa mnafanya jambo la kustaajabisha. Mnaweza,        mkipenda, kuwaomba Mabalozi wetu waliopo katika nchi mbalimbali duniani wawasaidie. Ni wajibu wao kufanya hivyo kwani kusaidia kusukuma maendeleo ya hapa nchini kutoka huko waliko ndilo jukumu lao la msingi. Vile vile, nimefurahishwa na mipango yenu ya baadaye ya kuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini.  Hongereni kwa uamuzi wenu wa busara. Lazima Chuo kitanuke kwa maana ya kuwa kikubwa zaidi, makao makuu na kwa kuwa na vyuo vishiriki na shule au  vitivo sehemu mbalimbali nchini.

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Kazi iliyo mbele yenu ni kubwa, hivyo ni vyema kuweka mikakati mizuri na mipango thabiti ya utekelezaji na ufuatiliaji wa dhamira yenu hiyo njema.  Rai yangu kwenu ni kuwaomba muwe wabunifu zaidi hasa katika kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaidia Chuo kujiendesha bila kutegemea ada peke yake.  Chuo kiangalie uwezekano wa kufanya shughuli zitakazowaingizia mapato kama vile kufanya shughuli za kutoa ushauri. Pia muangalie uwezekano wa kuwekeza wenyewe kwenye miradi ya kiuchumi au kwa kushirikiana na wawekezaji katika baadhi ya maeneo.

Kuhusu nafasi mbili za ufadhili nilizopewa na Chuo kikuu cha Tun Abdul Razak cha Malaysia, nitafuatilia kujua  kilichoendelea na kinachoendelea. Je, nafasi hizo bado zipo?  Zikiwepo, nitawasiliana na wahusika waangalie uwezekano wa kuwapeni. Kama zimeshagawiwa basi tusubiri safari ijayo. Kwa  masuala ya ardhi na maombi mengine nimeyasikia, yaleteni tuangalie namna ya kusaidiana.

Ndugu Makamu Mkuu wa Chuo, na

Wafanyakazi wote wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;


           Napenda kuwakumbusha kuwa mnayo dhamana kubwa na wajibu mkubwa na wa kihistoria. Ule ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Waislamu wazawa kuwa na Chuo Kikuu inawapeni wajibu maalum wa kuhakikisha Chuo kinafanikiwa. Ni mtihani na changamoto ya aina yake kuthibitisha kuwa Waislamu nao wanaweza kuwa na Chuo kizuri na chenye kutoa elimu ya ubora wa hali ya juu.  Kwa sababu hiyo hamna budi kuhakikisha kuwa mna mipango mizuri ya kujenga Chuo cha hadhi na ubora wa hali ya juu.  Ihakikishwe kuwa mipango hiyo inatekelezwa kwa ukamilifu.

           Aidha jumuiya yote inao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, maarifa na weledi ili dhima hiyo ya Chuo iweze kutimizwa kwa ukamilifu. Timizeni wajibu wenu ipasavyo ili jina la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro likue haraka. Sifa yake isambae na kuvuma kote nchini. Chuo kifanye vizuri ili wanafunzi waone fahari kuwa wahitimu wa Chuo hiki. Chuo ambacho, wazazi wapende kuleta vijana wao kuja kusoma hapa. Kwa jinsi Mkuu wa Chuo alivyoeleza, mimi nina imani mnaweza, fanyeni kweli.

Ndugu Wanafunzi wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;

Naomba wote muone fahari ya kuwa wanafunzi katika Chuo cha kihistoria hapa nchini.  Nawasihi mjitume kwa kadri ya uwezo na vipaji mlivyopewa na Mwenyezi Mungu mfanikishe kile kilichowaleta.  Jifunzeni kwa bidii mfaulu vizuri ili mkihitimu muwe kielelezo kizuri cha mafanikio na ubora wa  Chuo  Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro.  Muwe Mabalozi na kioo cha ufanisi wa Chuo hiki. Nawasihi mjiepushe na mambo yatakayowapunguzia muda au kuwaondoa katika shughuli ya msingi iliyowaleta hapa ya kujifunza mpate digrii katika fani mliyochagua mwenyewe kuisomea.  Vishawishi ni vingi na wapo watu wengi wanaopanga kuwashawishi mtumie muda wenu adhimu kufanya wanayoyataka wao ambayo mkishiriki huwatoa kwenye malengo na kutekeleza yao. Mambo ya dunia ya nje ya Chuo ni mengi huna budi kutambua lipi ufanye na lipi usifanye na kwa wakati gani!

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, si mtoto. Lazima ujue kuwa unawajibika kwa kila unaloamua na kutenda.  Amua kuwajibika vizuri. Fikiri kabla ya kutenda, changanua lipi ni lipi kabla ya kufanya uamuzi wa kile unachotaka kufanya.  Wakati wote uongozwe na busara na hekima na siyo jazba na ushabiki wa matakwa ya kundi.  Kama ni jema fanya na kama si jema usifanye.  Kwanza tambua wewe ni nani na uko hapa kwa ajili gani. Lazima ujue kuwa hatma ya yote uko peke yako.  Utafaulu au kufeli wewe.  Utapata shahada wewe na si mtu mwingine.  Hakuna ubia wa kufaulu au kufeli au kiwango cha kufaulu. It will always remain personal. Katika masomo unanufaika wewe.  Shirikiana na wengi lakini usisahau kujali maslahi yako.  Maslahi ya wengi yasiyojumuisha yako, yahoji vizuri kabla ya kuamua kushiriki au kufanya. Vinginevyo labda kama umeamua kujitoa muhanga, uwe shujaa. Hata kwa hilo, sijui utakuwa shujaa wa nani.

Mabibi na Mabwana;


Kabla ya kumaliza napenda kutambua na kumshukuru Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na viongozi wa MDF kwa juhudi zao za pamoja zilizowezesha Chuo hiki kuwepo.  Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru wananchi wanaokizunguka Chuo kwa ujirani mwema na wakazi wa Morogoro kwa ujumla kwa kukipokea vizuri na kuishi na wanajumuiya wa Chuo hiki kwa upendo mkubwa. Naomba muendelee na moyo na ushirikiano huo.

Baada ya kusema hayo, nawashukuru sana kwa kunialika. Nawatakia kila la heri na mafanikio tele.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

PINDA: KUNYWENI MAJI MENGI KUZILINDA FIGO ZENU

$
0
0


AARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


*Azindua SMS  ya”Ijue  Afya ya Figo Yako” kwenda 15021 kupitia TIGO
*Aonya wanaokimbilia kununua dawa bila kupima


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewahimiza Watanzania kuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku ili kujikinga na matatizo ya figo ambayo yanazidi kuongezeka kila siku.

Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Machi 14, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa mji wa Arusha waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya Siku ya Afya ya Figo Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya hospitali ya AICC jijini humo.

Kaulimbiu ya Siku ya Afya ya Figo Duniani mwaka huu  ni “Figo Salama kwa Maisha yako: Epusha Madhara Makubwa kwa Figo” au “Kidneys for Life: Stop Acute Kidney Injury”

Waziri Mkuu alisema mtoto wa miaka 10 hadi mtu mzima wanatakiwa wanywe maji kiasi kisichopungua lita moja na nusu kwa siku wakati mtoto mwenye mwaka mmoja anatakiwa anywe maji yasiyopungua nusu kikombe (sawa na mililita 100) na kwamba kiasi hicho huongezeka kadri umri wa mtoto unavyoengezeka. “Hii itasaidia kuhakikisha hawaishiwi maji mwilini,” aliongeza.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, imekadiriwa kuwa watu milioni mbili hupoteza maisha kila mwaka kutokana na maradhi ya ghafla ya figo wakati asilimia 20 ya vifo vya wagonjwa waliolazwa hospitalini husababishwa na maradhi hayo.

“Wataalam wanasema maambukizi ya magonjwa hayo husababisha madhara makubwa ya figo (Acute Kidney Injuries) ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa utendaji kazi wa figo. Hali hiyo husababisha watu kupata ugonjwa wa ghafla wa figo (mshtuko wa figo) na pia kusababisha athari kubwa kwenye figo na kuzifanya zishindwe kufanya kazi ipasavyo,” alisema.

Alisemamaradhi yanayoweza kujitokeza ghafla na kuharibu figo hayajatiliwa mkazo ipasavyo, hasa katika nyanja za utoaji mafunzo ya tiba, utafiti na elimu ya afya ya figo kwa umma. “Hali hii husababisha kutotumika kikamilifu kwa fursa za kubaini maradhi yanayojitokeza ghafla na kuharibu figo; pia inaathiri utoaji huduma za afya ya figo usiokidhi, na hivyo wagonjwa kulazwa kwa muda mrefu hospitalini,” alisititiza.

Akifafanua umuhimu wa kuwepo haja ya upimaji afya ya figo, Waziri Mkuu alisema Machi, 2011 Taasisi ya Figo Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ilitoa huduma ya bure na kuwachunguza watu 3,500ambapo watu 1,200 walikutwa na magonjwa ya figo. 

“Mwaka huu 2013 katika maadhimisho yanayoendelea katika Jiji la Arusha, yaliyoanza Machi 11, 2013, jumla ya watu  2,020 kufikia saa 7.00 mchana jana walisajiliwa na kati yao 1,640 walifanyiwa uchunguzi.  Kati yao wananchi 37 walipatikana na  maradhi ya figo, wengine 219 walipatikana na matatizo ya shinikizo la juu la damu. Wananchi 65 kati ya 141 waliofanyiwa uchunguzi kwa kipimo cha Ultra Sound na walikutwa na matatizo.  Jumla ya wananchi 63 walifanyiwa uchunguzi wa moyo wakwa vipimo vya ECHO na ECG.

Alisema jukumu kubwa kwa upande wa Serikali ni kuhakikisha kuwa fedha, vifaa, vifaa tiba na dawa za kukabiliana na ugonjwa wa mshtuko wa figo vinapatikana kwa wakati ili kulinda afya ya jamii. “Katika kudhihirisha azma hii ya Serikali, tayari tuna Kitengo cha Huduma za Tiba ya Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kitengo hiki kinatoa huduma kwa wagonjwa wote wanaohitaji huduma za tiba ya magonjwa ya figo. Chuo Kikuu cha Dodoma kimeanzisha utoaji wa huduma za tiba ya magonjwa ya figo. Ninazo taarifa kwamba, pale Dodoma kuna mashine za kisasa 10 za kusafishia damu.”

Alisema hospitali za rufaa za Bugando, KCMC na Mbeya ziko kwenye hatua mbalimbali za maandalizi ya kuanzisha huduma za tiba ya magonjwa ya figo. “Matarajio ni kwamba, kuwepo kwa huduma hizo kutaliwezesha Taifa katika kupambana na magonjwa ya figo,” aliongeza.

Alikemea tabia ya baadhi ya watu kujiamulia kununua dawa na kumeza bila kufanyiwa uchunguzi wa kitatibu na kuonya kuwa kuwa tabia hiyo inaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.

“Tuwaelimishe Watanzania umuhimu wa kuhakikisha kuwa wagonjwa wanaougua maradhi mengine wanapelekwa hospitali na wanapata tiba sahihi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa kama inavyoelekezwa na wataalam wa afya. Vilevile, ni vizuri kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya mara tuonapo dalili za ugonjwa ili kupatiwa tiba inayostahiki mapema,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alizindua Programu ya Ujumbe Mfupi wa Simu ya Mkononi (SMS) ya IJUE  AFYA YA FIGO YAKO kwa kutumaujumbe wenye neno FIGO kwenda namba 15021 kupitia mtandao wa simu wa Tigo ambapo mhusika atajibu maswali kadhaa na kupatiwa taarifa.

Aliishukuru kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo kwa kutoa huduma hiyo bure na kuwasihi wananchi waitumie ili kupata taarifa juu ya afya ya figo zao.

Naye Mwenyekiti waTa asisi ya Figo Tanzania, Jaji Frederick Werema, aliwasihi Watanzania kujitolea kwa hali na mali kuiunga mkono taasisi hiyo ili iweze kufanya shughuli zake kwenye mikoa mingi zaidi.

    
(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 14, 2013.

SHINDANO LA REDD’S MISS TANZANIA 2013 LAZINDULIWA RASMI

$
0
0
 Kazi ni kwako kwa wewemwenye ugonjwa wa miguu na vifundo

Baadhi ya Warembo walioshirikishi Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 wakicheza muziki wa aina ya Kwaito wakati wa tafrija maalum ya uzinduzi wa Mashindano ya Miss Tanzania 2013 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Machi 14, 2013. Kulia ni Redd’s Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred.

Kamati ya Miss Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja.

 Warembo hii ilikuwa shughuli yao.
Hii ndio ilikuwa tatu bora ya Miss Tanzania 2012, Mshindi wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akiwa pamoja na washindi wenzake, Eugene Fabian aliyetwaa nafasi ya pili (kulia) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester


Mambo ya burudani yalikuwa si mchezo, Uncle Lundenga na my wife wake wakisakata rumba toka B Band.

Mkurugenzi wa Excutive Solutions,Aggrey Maliale akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa TBL,Mamungai.


Banana Zoro na kundi zima la B Band lilitoa burudani. Source father Kidevu blog


TFF, FIFA, Serikali mambo si mambo

$
0
0



*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

*Machi 14, 2013*



*TFF YAWATULIZA WADAU SAKATA LA KATIBA*

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amewataka wadau wa
mchezo huo kuwa watulivu kwa vile tofauti zilizojitokeza kati ya Shirikisho
na Serikali zitamalizwa kwa taratibu za mpira wa miguu.
Amesema nia ya TFF ni kuhakikisha Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) haliifungii Tanzania kwani tayari Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alishaahidi kuwepo kikao kati
yake na viongozi wa TFF kitakachofanyika Jumanne (Machi 19 mwaka huu).
“Suluhu itapatikana kwa mazungumzo kati ya Wizara na TFF. Naamini suala
hili tutalimaliza baada ya kikao cha Machi 19 ambacho kimepangwa na Waziri
kutokana na maombi ya TFF,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa tatizo
lilianzia kwenye mchakato wa uchaguzi ambao umesimamishwa na FIFA.
FIFA ilisimamisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi baada ya baadhi ya wagombea
walioenguliwa kulalamika, na yenyewe kuahidi kutuma ujumbe wa kushughulikia
suala hilo.
Rais Tenga amesema lisingetokea tatizo hilo, TFF tayari ilishaitisha
Mkutano Mkuu ambao ungefuatiwa na uchaguzi. Lakini kwa vile FIFA ndiyo
iliyosimamisha mkutano huo, TFF inalazimika kusubiri hadi FIFA
itakaposhughulikia suala hilo na kutoa maelekezo ikiwemo lini mkutano
ufanyike.
Amesema kwa kuamini tatizo hilo litamalizwa ndani ndiyo maana TFF hadi sasa
haijapeleka FIFA maagizo ya Waziri Dk. Fenella ya kutengua marekebisho ya
Katiba ya TFF ya mwaka 2012, kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba
na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, kwani ingefanya hivyo Tanzania ingefungiwa
mara moja.
TFF inasisitiza kuwa FIFA ilijua tatizo la Serikali kutoa maagizo kwake
kupitia vyombo vya habari, hivyo kumuandikia Rais Tenga na kueleza msimamo
wake iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia uendeshaji wa
shughuli za mpira wa miguu.
Uhalali wa kuwepo kwa barua ya FIFA kwenda kwa Rais Tenga juu ya suala hilo
ulihojiwa pia na mwandishi wa Reuters, Brian Homewood baada ya kusoma
kupitia vyombo vya habari nchini kuwa Shirikisho hilo huenda likaifungia
Tanzania ikibainika Serikali inaingilia shughuli za TFF. Mawasiliano kati
ya FIFA na mwandishi huyo ambapo majibu yake pia TFF ilipewa nakala
yameambatanishwa katika taarifa hii.

* *

Forwarded Message -----

From: Media Office (FIFA) <media@fifa.org>

To: Brian Homewood <brian.homewood@yahoo.co.uk>


Sent: Tuesday, 12 March 2013, 19:39

Subject: RE: tanzania



Dear Brian,



Thanks for your message.



We can confirm that FIFA Secretary General Jérôme Valcke has sent a letter
to the President of the Tanzanian Football Federation, Leodegar Tenga,
concerning alleged governmental interference in the internal affairs of the
TFF.

FIFA is in contact with the TFF President who is optimistic that the matter
can be sorted out within TFF, FIFA and the Tanzanian authorities.
Furthermore, we can confirm that FIFA is also planning to send a mission to
assess the situation with regard to the electoral process as soon as the
current matter of alleged interference has been clarified.



Kind regards



FIFA

Media department

Enquiries: media@fifa.org

Tel.: +41-(0)43-222 7272    www.FIFA.com

Twitter: @fifamedia    YouTube/FIFAtv



-----Original Message-----

From: Brian Homewood [mailto:brian.homewood@yahoo.co.uk]
Sent: Dienstag, 12. März 2013 10:19
To: Media Office (FIFA)
Subject: tanzania







Good morning
Are you able to comment on reports (below) that FIFA has sent a warning to
Tanzania over government interference in the national football federation?
Many thanks
Kind regards
Brian Homewood
Reuters



By Majuto Omary

The Citizen Reporter

Dar es Salaam. Fifa has threatened to suspend Tanzania from all
international competitions if the tug-of-war between the Tanzania Football
Federation (TFF) and government does not end in a meaningful way. In a
letter to the TFF, the world soccer governing body warned yesterday that it
would not hesitate to impose a ban on the country if it confirms that the
government interferes with the operations of the federation.
Fifa says there have been various reports of accusations by local media
that the ministry of Information, Culture and Sports has interfered with
the operations of the TFF.
The letter has quoted the minister responsible for sports, Fenella
Mukangara, as saying that the government has urged the TFF to use the
2006 constitution in this year's election, while it 'has already been
amended.'
"It has been reported that the TFF has been urged to organise the General
Assembly and the elections by the date set by the government,"
reads the letter signed by Fifa secretary general Jerome Valcke.
It further reads: "It is also said that government intends to establish an
interim committee if the TFF fails to undertake the orders."
Fifa says if the accusations reported by the local media shall be
established to be true, it means the government is interfering with the
operations of TFF.
"We would like to remind all members of Fifa that they are required to
conduct their activities freely without interference by another person as
defined in Articles 13 and 17 of the Constitution of Fifa."
"So if these instructions issued by the government will be implemented,
this issue will be taken to the top Fifa authorities for further action,
including suspension of Tanzania as it becomes when there is a government
intervention," says the letter.
A copy of the letter has been sent to the Confederation of African Football
(Caf) reiterating some of the penalties that Tanzania will face if it is
suspended.



*Boniface Wambura*

*Ofisa Habari*

*Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)*

Askofu Mkude: Rais Kikwete ana nia nzuri na Kanisa katoliki Tanzania

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete akiongozwa na mhashamu  Mkude

Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro limemwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kama kiongozi anayelijali Kanisa Katoliki Tanzania na mwenye nia nzuri na kanisa hilo.
Aidha, Kanisa hilo limesema kuwa Rais Kikwete amethibitisha katika muda wake wote wa uongozi wa Taifa la Tanzania kuwa ni kiongozi ambaye anawajali wanyonge na masikini.
Sifa hizo za kulijali Kanisa Katoliki na kuwa na nia nzuri na Kanisa hilo zilitolewa usiku wa jana, Alhamisi, Machi 14, 2013 na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Baba Askofu Telesphor Mkude wakati wa halfa ya kuchangia ujenzi wa parokia mpya ya Kigurunyembe iliyofanyika kwenye Bwalo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Magadu Officer’s Mess, nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Akitoa neno la shukurani kabla wakati akimkaribisha Rais Kikwete kwenye hafla hiyo na baada ya kukamilika kwa shughuli ya uchangiaji, Baba Askofu Mkude alimwambia Rais Kikwete:
“Wewe Mheshimiwa Rais ni kiongozi ambaye unalijali Kanisa Katoliki. Una nia nzuri na Kanisa. Kigurunyembe ni sehemu ndogo sana ya nchi ya Tanzania ambayo wewe unaiongoza. Hata hivyo, umekuwa tayari kuacha yote yaliyo makubwa na kukubali kujishusha na kuja kuzungumza na hili kundi dogo la Kigurunyembe.”
Aliongeza Baba Askofu Mkude: “Kwa hili unatufundisha kwa vitendo maana ya kujali wanyonye na maskini. Baba Mheshimiwa umetujali sana. Mungu akubariki sana.”
Alisisitiza Askofu Mkude: “Mwisho mgeni rasmi nirudie kwa kukushukuru na kusema kuwa yote haya yasingeliwezekana kama usingeliwepo wewe mwenye binafsi kwenye shughuli hii. Tunakushukuru kwa kutujali, kututhamini na kutupenda sisi kama raia wa nchi yako na ukaona ni bora ufike mwenyewe.”
Uchangiaji huo wa ujenzi wa parokia mpya ya Kigurunyembe ulilenga kukusanya kiasi cha Sh. Milioni 200 lakini wachangiaji waliishia wakichangia kiasi cha Sh. Milioni 255 zikiwamo fedha taslim Sh. Milioni 73.
Katika neno lake, Askofu Mkude pia aliwashangaa watu ambao wamekuwa wanachoma makanisa nchini kwa visingizio vya dini akisema kuwa taasisi na majengo yanajengwa kwa thamani kubwa na kama kweli Watanzania wanapenda maendeleo ni lazima waache kuchoma majengo yanayojengwa kwa thamani kubwa.
“Mtapata wapi maendeleo kwa kuchoma taasisi na majumba ambayo tayari tumeyajenga tena kwa gharama kubwa sana?”aliuliza Askofu Mkude na kumtaka Rais Kikwete kuchukua hatua za kukomesha fujo na vurumai za kidini nchini pamoja na kuuawa kwa viongozi wa dini.
“Haya siyo mazoea yetu kama ulivyosema wewe Mheshimiwa Rais katika hotuba yako ya mwezi Januari mwaka huu. Huu siyo utamaduni wetu. Ni lazima tukubali kurudi kuishi katika haki, katika amani na katika heri. Tunakuomba utusaidie makanisa yetu yasichomwe moto. Utusaidie viongozi wetu wasiuawe Mheshimiwa Rais.”
Rais Kikwete amejerea Dar es Salaam mchana wa leo, Ijumaa, Machi 15, 2013, baada ya kumaliza ziara ya siku tatu ya kikazi ya Mkoa wa Morogoro.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2013

Rais Kikwete achangisha sh milioni 255 za Kanisa katoliki

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza harambee ambayo usiku wa jana, Alhamisi, Machi 14, 2013, iliyowezesha kuchangiwa kwa kiasi cha Sh. Milioni 255 kwa ajili ya ujenzi wa Parokia mpya ya Kanisa Katoliki la Kigurunyembe katika Jimbo Katoliki la Mogororo.
Kati ya Sh. 255, 085, 610 zilizochangwa na waumini wa Kanisa hilo na dini nyingine nchini, wafanyabiashara, wabunge wa Mkoa wa Morogoro, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, viongozi wa Kanisa Katoliki lenyewe, wananchi wa kawaida, viongozi wa Mashirika ya Umma na binafsi na taasisi nyingine za Serikali, kiasi cha Sh.73, 705, 610 zilichangwa taslimu kwenye hafla hiyo.
Kiasi kilichobakia cha Sh. 155, 380, 000 zimetolewa kama ahadi na wachagiaji mbali mbali. Rais Kikwete aliwaambia washiriki wa uchagiaji huo kuwa naye atatoa mchango kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo na kuwa mchango wake utaingizwa katika akaunti ya ujenzi Jumanne ijayo.
Aidha kiasi hicho cha Sh. Milioni 255 ni pamoja na ahadi ya mabati 450 yenye thamani ya Sh. Milioni 16 ambayo imetolewa na mfanyabiashara wa Dar es salaam Bwana Bubash Patel na michango ya saruji na mchanga iliyotolewa na waumini wengine katika hafla hiyo.
Rais Kikwete alifanikisha lengo hilo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uchangiaji wa fedha za ujenzi wa kanisa jipya la parokia ya Kigurunyembe, mjini Morogoro iliyofanyika jana usiku kwenye Bwalo la Jeshi la Magadu Officer’s Club, nje tu ya mji wa morogoro.
Kanisa hilo jipya linalojengwa katika eneo tofauti na Parokia ya sasa ya Kigurunyembe limekadiriwa kugharimu kiasi cha Sh. Milioni 600 ambazo kati ya hizo tayari waumini wa Kanisa hilo  walikwishachangia kiasi cha Sh. Milioni 130 kabla ya jana usiku.
Akimkaribisha Rais Kikwete pamoja na wageni wengine katika halfa hiyo ya uchangiaji wa ujenzi wa parokia hiyo, Askofu wa Jimbo la Morogoro, Baba Askofu Telesphory Mgude alisema kuwa katika uchagiaji wa jana usiku Jimbo la Morogoro lilikuwa limepanga kupata kiasi cha Sh. Milioni 200.
Askofu Mgude alisema kuwa Jimbo Katoliki Morogoro limeamua kujenga Parokia ya Kigurunyembe katika sehemu nyingine ya eneo hilo hilo la Kigurunyembe kwa sababu parokia ya sasa ya Kigurunyembe haina nafasi iliyobakia baada ya Serikali kutaifisha Chuo cha Ualimu cha Kigurunyembe kilichoko kwenye eneo la parokia ya sasa katika miaka ya 1960.
Askofu Mgude alimwambia Rais kuwa Parokia mpya inajengwa katika eneo jipya ambayo ardhi yake ilitolewa bure na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mogogoro, Marehemu Anselm Lyanda mwaka 2005.
Mbali na uchagiaji wa moja kwa moja, kiasi kikubwa cha fedha pia kilipatikana kwa kuuza kwa njia ya mnada sanamu tatu za Bikira Maria, zikiwamo za Bikira Maria wa Msaada na Bikira Maria Mkingiwa wa Dhambi ya Asili ambazo zote kwa pamoja zimeingiza Sh. milioni 4.1.
Aidha, ulikuwepo upigaji mnada wa keki ambayo ilinunuliwa kwa jumla ya Sh. Milioni 2.8 ambayo alikabidhiwa Rais Kikwete ambaye naye akiwakabidhi masista wa Kanisa Katoliki akiwaomba waikabidhi kwa watoto yatima nao wanufaike na matunda ya uchangiaji huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2013

Japan Contributes 7 million USD to Nyarugusu Refugee Camp through UNHCR and WFP

$
0
0
The Government of Japan has decided to make a contribution of US$ 7 million for the refugee
population of nearly 68,000 residing in Nyarugusu Refugee Camp, the last remaining refugee camp in Tanzania located in Kasulu District, Kigoma Region.

This contribution comes from a portion of the supplementary budget of the Japanese financial
year 2012/2013 dedicated for humanitarian assistance for African Countries, in which
US$ 3,000,000 is earmarked for the project “Protection and Durable Solutions for Congolese and Other Refugees in Tanzania” by UNHCR Tanzania, and US$ 4,000,000 for the project “Assistance to Refugees in North West Tanzania” by WFP Tanzania. Both projects are underway and are to be completed by the end of December 2013.

Japanese funds will help the UNHCR to assist the Nyarugusu camp refugees in several essential areas, ranging from access to primary health care and potable water, to shelter material. “I am absolutely thrilled and deeply grateful for this extraordinarily generous support. The funding is critical to our operation”, explained Joyce Mends-Cole, UNHCR Representative in Tanzania. In addition, targeted interventions will help enroll 98% of refugee children in primary school, provide psychosocial and material assistance to 5,500 refugees with specific needs (the elderly, people with disabilities, chronically ill, etc.) and ensure that all identified survivors of sexual and gender-based violence receive appropriate clinical care. 10,000 refugee women and girls will also benefit from the distribution of sanitary materials.
“The Government of Japan has been a longtime supporter of WFP’s work and we are particularly grat
eful for this contribution that will not only enable us to continue feeding the refugees, but also provide a boost to the economy through local purchases,” said WFP Country Representative Richard Ragan. WFP provides refugees with their only source of food in the camps. 

The contribution from the Government of Japan will provide refugees in Nyarugusu Camp with maize, pulses, and Super Cereal a protein rich fortified blend of corn flour and soy for up to three months, which is expected to improve their food security and nutrition status. Additionally, the contribution will be
used to provide additional, specialized food assistance to vulnerable groups with extra nutritional
requirements in the camp and in the host community, including patients in health clinics, HIV/AIDS affected groups, and pregnant and breastfeeding women and children under the age of 5. In total, the contribution will enable the purchase of some 4,000 metric tons of food approximately 130
truckloads.
***********
For further information, contact:
UNHCR Tanzania:
Melanie Senelle, Associate External Relations Officer,
senelle@unhcr.org
+255 22 2602708

TFF YAONDOA ‘FREE PASS’ MPIRANI*

$
0
0




Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeondoa utaratibu wa wadau wake kuingia bure kwenye mechi kwa kutumia tiketi maalum (free pass).
Kutokana na uamuzi huo hakutakuwa tena na pasi za bure kwa ajili ya kushuhudia mechi zilizo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa TFF katika viwanja mbalimbali nchini.
Uamuzi huo umetokana na ukweli kuwa free pass zimekuwa zikipunguza au kuchukua mgawo wote wa TFF kwenye mechi, na wakati mwingine Shirikisho hulazimika kutoa fedha za ziada kugharamia pasi hizo.
Pasi zote ambazo imekuwa ikitoa kwa wadau wake hukatwa katika mgawo wa TFF katika mechi husika. Shirikisho hivi sasa linapata asilimia nne tu ya mapato katika mechi za Ligi Kuu, ligi ambayo hivi sasa inaendeshwa na Kamati yake ya Ligi.



*RUVU SHOOTING KUIKABILI YANGA VPL*

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Machi 16 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi Jacob Adongo kutoka Musoma mkoani Mara ndiye aliyepewa jukumu la kuchezesha mechi hiyo namba 146. Adongo atasaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Milambo Tshikungu kutoka Mbeya wakati mwamuzi wa mezani ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Mtathmini wa waamuzi ni Army Sentimea wakati Kamishna wa mechi hiyo inayokutanisha vinara Yanga na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya saba ikiwa na pointi 29 chini ya ukufunzi wa Charles Boniface Mkwasa na Msaidizi wake Selemani Mtungwe ni Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Pia TFF inawaasa washabiki wa mpira wa miguu kuacha kununua tiketi mikononi mwa watu kwa vile wanaweza kuuziwa tiketi bandia. Tiketi zote zitauzwa katika vituo vinavyotangazwa katika magari maalumu, na uwanjani pia katika magari hayo.
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wenye uwezo wa kuchukua washabiki 25,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto Africans na Mgambo Shooting kutoka Tanga. Ugumu wa mechi hiyo unatokana na ukweli kuwa timu zote mbili zinapigana kuepuka kurudi zilikotoka (daraja la kwanza).
Mgambo Shooting inayonolewa na Mohamed Kampira inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 24 katika ligi hiyo yenye timu 14. Toto Africans ambayo iko nyumbani itaingia uwanjani ikiwa na pointi 14 katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya kulala 2-1 mbele ya Simba katika mechi iliyopita, Coastal Union itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.
Ligi hiyo itaendelea tena keshokutwa (Machi 17 mwaka huu) kwa mechi moja itakayozikutanisha JKT Ruvu na Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex.

*RAMBIRAMBI MSIBA WA OFISA HABARI CECAFA*

Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha aliyekuwa Ofisa Habari wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Finny Muyeshi kilichotokea juzi (Machi 13 mwaka huu) jijini Nairobi, Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani Muyeshi aliitumikia CECAFA kwa muda mrefu, hasa katika kuhakikisha waandishi wa habari wanapata mazingira mazuri ya kufanyia kazi wakati wanaporipoti matukio mbalimbali ya Baraza hilo.

Alitoa mchango mkubwa katika eneo la habari za mpira wa miguu, tangu akiwa gazeti la East African Standard la Kenya akiwa mwandishi, na baadaye Mhariri wa Michezo kabla ya kujiunga na CECAFA, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Muyeshi, CECAFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) na tasnia ya habari kwa ujumla, na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Muyeshi mahali pema peponi. Amina



*FDL KUKAMILISHA MSIMU WIKIENDI*

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 unamalizika wikiendi hii huku timu za Mbeya City ya Mbeya, Ashanti United ya Dar es Salaam na Rhino Rangers ya Tabora zikiwa tayari zimepata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao.
Kundi A mechi zote zitachezwa Jumapili (Machi 17 mwaka huu) ambapo Majimaji vs Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Kurugenzi vs Mkamba Rangers (Mafinga) na Burkina Faso vs JKT Mlale (Jamhuri, Morogoro).
Kesho (Machi 16 mwaka huu) katika kundi B itakuwa Green Warriors vs Polisi Dar (Karume, Dar es Salaam) na Ndanda vs Villa Squad (Nangwanda Sijaona, Mtwara). Keshokutwa (Machi 17 mwaka huu) ni Moro United vs Ashanti United (Karume, Dar es Salaam) na Tranist Camp vs Tessema (Mabatini, Mlandizi).
Kundi C ni kesho (Machi 16 mwaka huu) Polisi Tabora vs Pamba (Ali Hassan Mwinyi, Tabora). Keshokutwa (Machi 17 mwaka huu) ni Polisi Mara vs JKT Kanembwa (Karume, Musoma), Polisi Dodoma vs Mwadui (Jamhuri, Dodoma) na Rhino Rangers vs Morani (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).



*KILA LA KHERI AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO*

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam kwenye mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Barrack Y.C. II itakayochezwa Jumapili (Machi 17 mwaka huu) nchini Liberia.



Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa jijini Monravia na timuhizo kurudiana wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam. Ofisa Habari wa
Azam yuko na timu hiyo Monrovia na anapatikana kwa namba +231888386655.



*Boniface Wambura*

*Ofisa Habari*

*Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)*

Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa kamati za Bunge

$
0
0


Zitto akijinadi leo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baada ya Mhe. Spika kutangaza rasmi Orodha ya Wajumbe wapya katika kila Kamati za Kudumu za Bunge na Kwa kuzingatia kanuni ya 113 (10) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, wajumbe wa Kamati hizo za Kudumu za Bunge walioteuliwa, wamefanya uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti. Matokeo ya Uchaguzi huo, ni kama yanavyoonekana katika jedwali hapa chini.
WENYEVITI NA MAKAMU WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE

JINA  LA KAMATI
MWENYEKITI,  MAKAMU MWENYEKITI
1.
FEDHA NA UCHUMI
1.   Mhe. Mohamed Mgimwa,Mb – Mwenyekiti
2.   Mhe. Luke Paschal Kitandula.Mb-Makamu Mwenyekiti
2.
BAJETI
1. Mhe. Andrew Chenge,Mb – Mwenyekiti
2- Makamu Mwenyekiti (Uchaguzi utafanyika Jumatatu)
3.
PAC
1. Mhe. Kabwe Zitto Zuber,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Deo Haule filikunjombe -Makamu Mwenyekiti
4.
LAAC
1. Mhe. Rajab Mbarouk Mohammed,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Suleiman Jumanne Zedi,Mb - Makamu Mwenyekiti
5.
HUDUMA ZA JAMII
1. Mhe. Margareth S.  Sitta,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Stephen Ngonyani,Mb-Makamu Mwenyekiti
6.
MAENDELEO YA JAMII
1. Mhe. Jenista Mhagama,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Saidi Mohamed Mtanda,Mb-Makamu Mwenyekiti
 7.
NISHATI NA MADINI
1. Mhe. Victor Kilasile Mwambalasa,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Jerome Bwanausi,Mb-Makamu Mwenyekiti
 8.
ARDHI , MALIASILI NA MAZINGIRA
1. Mhe. James Lembeli,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Abdulkarim E. Shah,Mb-Makamu Mwenyekiti
 9.
MIUNDOMBINU
1. Mhe.Peter Serukamba,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. Prof. Juma Kapuya,Mb-Makamu Mwenyekiti
10.
TAMISEMI
1. Mhe.Hamis Andrea Kigwangalla,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe.John Paul Lwanji,Mb-Makamu Mwenyekiti
11.
MASUALA YA UKIMWI
1. Mhe.Lediana M. Mng’ong’o,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe.Diana M. Chilolo,Mb-Makamu Mwenyekiti
12.
ULINZI NA USALAMA
1. Mhe.Anna Margath Abdallah, Mb – Mwenyekiti
2. Mhe.Mohamed  Seif  Khatib,Mb-Makamu Mwenyekiti
13.
MAMBO YA NJE
1. Mhe.Edward N. Lowassa,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe.Mussa  Zungu,Mb-Makamu Mwenyekiti
14.
KATIBA , SHERIA NA UTAWALA
1. Mhe.Pindi H. Chana ,Mb – Mwenyekiti
2. Mhe. William Ngeleja,Mb-Makamu Mwenyekiti
15.
MAADILI
1. Mhe.Brig. Hassan Athuman Ngwilizi, Mb – Mwenyekiti
2. Mhe.John Zephania Chilingati,Mb-Makamu Mwenyekiti
16.
KILIMO, MIFUGO NA MAJI
1. Mhe. Prof. Peter Msolwa, Mb – Mwenyekiti
2. Mhe.Said Nkumba, Mb-Makamu Mwenyekiti

Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa.
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM

Wajumbe wa kamati za bunge

$
0
0


KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE
_____________________

1
Mhe. Anne Semamba Makinda, MB (Spika)
2
Mhe. Job Yustino Ndugai, MB (N/Spika)
3
Mhe. Tundu Antiphas Mughway Lissu, Mb
4
Mhe. Andrew John Chenge, Mb
5
Mhe. Musa Azzan Zungu,Mb
6
Mhe. Dkt.Titus Mtengeya Kamani, Mb
7
Mhe. Jenista Joakim Mhagama, Mb
8
Mhe. William Mganga Ngeleja, Mb.
9
Mhe. Amina Abdallah Amour, Mb
10
Mhe. James Francis Mbatia, Mb
11
Mhe. Hamad Rashid Mohammed, Mb
12
Mhe. Jasson Samson Rweikiza, Mb
13
Mhe. Philapa Godifrey Mturano, Mb
14
Mhe. Anna Margareth Abdallah,Mb
15
Mhe. Christopher Ole-Sendeka, Mb

KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
_____________________
      1.         
Mhe. Augustino Lyatonga Mrema, Mb
     2.         
Mhe. Riziki Omar Juma, Mb

     3.         
Mhe. Assumpter Nshunju Mshama, Mb
     4.         
Mhe. Brig. Gen. Hassan Athuman Ngwilizi, Mb
     5.         
Mhe.  Agripina Zaituni Buyogera, Mb

     6.         
Mhe. Said Juma Nkumba, Mb
     7.         
Mhe. John Paul Lwanji, Mb
     8.         
Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, Mb
     9.         
Mhe. Capt. John Zefania Chiligati, Mb
   10.         
Mhe. Betty Eliezer Machangu, Mb
    11.         
Mhe. Said Amour Arfi, Mb
   12.         
Mhe. Gosbert Begumisa Blandes, Mb

   13.         
Mhe. Augostino Manyanda Masele, Mb
   14.         
Mhe. Dkt. Lucy Sawere Nkya, Mb
   15.         
 Mhe. Rashid Ali Abdallah, Mb

















 KAMATI YA MASUALA YA UKIMWI
­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­______________________
1
Mhe. Said Suleiman Said,Mb
2
Mhe.Ahmed Ali Salum,Mb
3
Mhe. Maida Hamad Abdallah,Mb
4
Mhe.Lediana Mafuru Mung’ong’o ,Mb
5
Mhe. Maria Ibeshi Hewa, Mb
6
Mhe. Chiku Aflah Abwao, Mb
7
Mhe.Omary Ahmad Badwel, Mb
8
Mhe. Mbarouk Salim Ali, Mb
9
Mhe. Rashid  Ali Omar, Mb
10
Mhe. Lameck Okambo Airo, Mb
11
Mhe. Lucy Thomas Mayenga, Mb
12
Mhe. AnaMaryStella John Mallac, Mb
13
Mhe. Mch. Luckson Ndaga Mwanjale, Mb
14
Mhe. Mwanamrisho Taratibu Abama, Mb
15
Mhe.Diana Mkumbo Chilolo, Mb
16
Mhe. Ignus Aloyce Malocha, Mb
17
Mhe. Saidi Ally Selemani Bungara, Mb
18
Mhe. Iddi Mohamed Azzan, Mb
19
Mhe. Neema Mgaya Hamid Mb
20
Mhe. Sara Msafiri Ally, Mb
21
Mhe. Dkt. Engelbert Faustine Ndugulile, Mb
22
Mhe. Maulidah Anna Valerian Komu Mb
                                             
KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
__________________

1
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Mb
 2
Mhe. Anastazia James Wambura, Mb
 3
Mhe.John Magale Shibuda, Mb
 4
Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa, Mb
5
Mhe. Muhammad Ibrahimu Sanya, Mb
6
Mhe. Leticia Mageni Nyerere, Mb
7
Mhe.Thuwayba Idrisa Muhamed, Mb
8
Mhe. Susan Anselm Jerome Lymo, Mb
9
Mhe.Faith Mohamed Mitambo,Mb
10
Mhe.Juma Selemani Nkamia, Mb
11
Mhe. Betty Eliezer Machangu, Mb
12
Mhe. Selemani Saidi Jafo,Mb
13
Mhe. Mussa Azzan Zungu,Mb
14
Mhe.Salim Hemed Khamis,Mb
15
Mhe. Eng. Yussuf  Hamad Masauni,Mb





















  KAMATI YA BAJETI
1
 Mhe. Andrew  John Chenge, Mb
2
Mhe. Christine Mughway Lissu,Mb.
3
Mhe. Kidawa Hamid Saleh,Mb
4
Mhe.  Mansoor Shaniff Hiran, Mb
5
Mhe. Amina Abdallah Amour, Mb
6
Mhe. Joseph Roman Selasini, Mb
7
Mhe. Josephat Sinkamba Kandege,Mb
8
Mhe. Dkt. Cyril August  Chami,Mb
9
Mhe. Dkt. Bulugu FetusLimbu,Mb
10
Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Mb
11
Mhe. Assumpter N. Mshama,Mb
12
Mhe.James Francis Mbatia, Mb
13
Mhe. Beatrice Matumbo Shellukindo, Mb
14
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, Mb











KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA
___________________________________________________


1
Mhe . Abas Zuberi Mtemvu, Mb
2
Mhe. Tundu Antiphas Mughway Lissu, Mb
3
Mhe. Gosbert Bagumisa Blandes
4
Mhe. Pindi Hazara Chana,Mb
5
Mhe. Nimrod Elirehema Mkono,Mb
6
Mhe. Felix Francis Mkosamali,Mb
7
Mhe. Nyambari Chacha Mariba Nyangwine, Mb
8
Mhe. Fakharia Khamis Shomari, Mb
9
Mhe. Rukia Kassim Ahmed, Mb
10
Mhe. Jaku Hashim Ayoub, Mb
11
Mhe. Mustapha Boay Akunaay, Mb
12
Mhe. Ramadhan Haji Saleh, Mb
13
Mhe.  Jasson Samson Rweikiza, Mb
14
Mhe. William Mganga Ngeleja,Mb
15
Mhe.  Deogratias Aloyce Ntukamazina , Mb
16
Mhe. Ali Khamis Seif, Mb
17
Mhe.  Mariam Reuben Kasembe, Mb
18
Mhe. Abdallah Sharia Ameir, Mb
19
Mhe. Halima James Mdee, Mb
 



KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA

1
Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa,Mb
2
Mhe. Eng. Habib Juma Mnyaa, Mb
3
Mhe. Margaret Agness Mkanga,Mb
4
Mhe. Haji Khatib Kai,Mb
5
Mhe.Ester Lukago Minza Midimu,Mb
6
Mhe. Hassein Nassor Amar,Mb
7
Mhe. Ahmed Juma Ngwali, Mb
8
Mhe. Luhaga Joelson Mpina Mb
9
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani, Mb
10
Mhe. Joyce John Mukya, Mb
11
Mhe. David Zakaria Kafulila, Mb
12
Mhe. Shawana Bukhet Hassan,Mb
13
Mhe. Said Mussa Zubeir, Mb
14
Mhe. Vicky Pascal Kamata, Mb
15
Mhe. Naomi Ami Mwakyoma Kaihula,Mb
16
Mhe.Khatibu Said Haji,Mb
17
Mhe. Freeman Aikael Mbowe, Mb
19
Mhe.Amina Mohamed Mwidau,Mb
20
Mhe. Josephine Jonson Genzabuke, Mb
21
Mhe. Dunstun Luka Kitandula,Mb
22
Mhe. Mohamed Hamis Misanga, Mb







KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
­­­­­­­­­­­­­­­____________________

1
Mhe. Brig.Gen. Hassan Athumani Ngwilizi,Mb
2
Mhe.  Anna Margreth  Abdallah,Mb
3
Mhe. Dkt. Muhamed Seif Khatib, Mb
4
Mhe. Capt. John Zefania Chiligati, Mb
5
Mhe. Augustino Manyanda Masele, Mb
6
Mhe. Masoud Abdallah Salim, Mb
7
Mhe.  Mussa Hassan Mussa, Mb
8
Mhe. Omar Rashid Nundu,Mb
9
Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya, Mb
10
Mhe. Cynthia Hilda Ngoye, Mb
11
Mhe. Henry Daffa Shekiffu, Mb
12
Mhe.Vita Rashid Mfaume Kawawa, Mb
13
Mhe. David Mciwa Mallole,Mb
14
Mhe. Hamad Ali Hamad, Mb
15
Mhe. Rachel Mashishanga Robert, Mb
16
Mhe. Mch. Augustino Lyatonga Mrema, Mb
17
Mhe. Vincent Josephat Nyerere, Mb











KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII
________________________
 22     Mhe. Chrisowaja Gerson Mtinda, Mb
1
Mhe.Fatuma Abdallah Mikidadi, Mb
2
Mhe. Ritta Louise Mlaki, Mb
3
Mhe. Riziki Omari Juma, Mb
4
Mhe. Salome Daudi Mwambu, Mb
5
Mhe. Ali Juma Haji, Mb
6
Mhe. Faki Haji Makame, Mb
7
Mhe. Margareth Simwanza Sitta, Mb
8
Mhe. Ezekia Dibogo Wenje, Mb
9
Mhe. Agripina Zaituni Buyogera, Mb
10
Mhe. Juma Sururu Juma, Mb
11
Mhe. Mch. Dkt. Getrude Pangalile  Rwakatare, Mb
12
Mhe. Abia Muhama Nyabakari, Mb
13
Mhe. Zabein Mhaji Mhita,Mb
14
Mhe. Mohamed Gulam Dewji, Mb
15
Mhe. Dkt. Anton Gervas Mbasa, Mb
16
Mhe. Steven Hilari Ngonyani,Mb
17
Mhe. Martha Jachi Umbulla, Mb
18
Mhe. Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi, Mb
19
Mhe. Asnain Muhamed Murji, Mb
20
Mhe. Cecilia Daniel Paresso, Mb
21
Mhe. Abdulaziz Muhamed Aboud, Mb


MAENDELEO YA  JAMII
________________________

1
Mhe. John Damiano Komba, Mb
2
Mhe. Moza  Abedi Saidy,Mb
3
Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi, Mb
4
Mhe. Mohamed Said Mohammed, Mb
5
Mhe. Nasib Suleiman Omar, Mb
6
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo,Mb
7
Mhe. Jenista Joakim Mhagama, Mb
8
Mhe. Salum Halfan Barwany,Mb
9
Mhe. Kiumbwa Makame Mbaraka
10
Mhe. Salvatory Naluyaga Machemuli,Mb
11
Mhe. Livingstone Joseph Lusinde, Mb
12
Mhe. Saidi Mohamed Mtanda,Mb
13
Mhe. Agness Elias Hokororo, Mb
14
Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb
15
Mhe.Mary Pius Chatanda, Mb
16
Mhe.Juma Othman Ali, Mb
17
Mhe. Jaddy  Simai Jaddy, Mb
18
Mhe. Dkt. Maua Abeid Daftar, Mb
19
Mhe. Albert Obama, Ntabaliba, Mb
20
Mhe.Rose Kamili Sukum, Mb
21
Mhe.Rosemary Kasimbi Kirigini, Mb
22.  Mhe.  Joshua Samwel Nassari, Mb
KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI
_________________________________
1.       
Mhe. Prof. David Homeli Mwakyusa, Mb
2.      
Mhe. Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mb
3.      
Mhe. Asaa Othman Hamad, Mb
4.      
Mhe. Abdulsalaam  Selemani Ameir, Mb
5.      
Mhe. Said Juma Nkumba, Mb
6.      
Mhe. Abdllah Haji Ali, Mb
7.      
Mhe. Haji Juma Sereweji,Mb
8.      
Mhe. Lolensia Masele Bukwimba, Mb
9.      
Mhe. Mch. Peter Simon Misigwa, Mb
10.    
Mhe. Prof. Peter Mahmudu Msolla, Mb
11.     
Mhe. Nameloki Edward Moringe Sokoine, Mb
12.    
Mhe. Dkt. Lucy Sawere Nkya, Mb
13.    
Mhe. Sylvestry Francis Koka, Mb
14.    
Mhe. Kheri Khatib Ameir, Mb
15.    
Mhe.Meshack Jeremia Opulukwa,Mb
16.    
Mhe. Philemon Kiwelu Ndesamburo, Mb
17.    
Mhe. Jitu Vrajlal Soni, Mb
18.    
Mhe. Sadifa Juma Khamis, Mb
19.    
Mhe.Donald Kelvin Max, Mb
20.    
Mhe. Moshi Selemani Kakoso, Mb
21.    
Mhe. Subira Khamis Mgalu, Mb
22.    
Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya, Mb



KAMATI YA MIUNDOMBINU
1
Mhe. Peter  Joseph Serukamba, Mb
2
Mhe. Maryam Salum Msabaha, Mb
3
Mhe. Clara Diana Mwatuka, Mb
4
Mhe. Zamda Shamte Madabida, Mb
5
Mhe. Innocent  Edward Kalogeris, Mb
6
Mhe. Hussein Mussa Mzee, Mb
7
Mhe. Aliko Nikusuma Kibona, Mb
8
Mhe. Said Ramadhani Bwanamdogo, Mb
9
Mhe. Zahra Ali Hamad, Mb
10
Mhe. Ahmed Mabkhut Shabiby,Mb
11
Mhe. Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe, Mb
12
Mhe.Mussa Haji Kombo, Mb
13
Mhe. Prof. Juma Athuman Kapuya, Mb
14
Mhe. Mtutura Abdallah Mtutura, Mb
15
Mhe. Abdul Rajab Mteketa, Mb
16
Mhe. Suleiman Masoud Nchambi, Mb
17
Mhe. Saidi Amour Arfi, Mb
18
Mhe. Eng. Ramo Matala Makani, Mb
19
Mhe. Rebecca Michael Mngodo, Mb
20
Mhe. Elizabeth Nkunda Batenga, Mb
_____


























   21.     Mhe. Haroub Mohamed Shamsi, Mb







KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI
___________________

1
Mhe. Deusiderius John Mipata, Mb
2
Mhe. Deo Haule Filikunjombe, Mb
3
Mhe.  Asha Mshimba Jecha, Mb
4
Mhe. Lucy Philemon Owenya, Mb
5
Mhe.Ester Nicholas Matiko, Mb
6
Mhe. John Momose Cheyo, Mb
7
Mhe. Kabwe Zitto Zuberi, Mb
8
Mhe.Zainab Matitu Vulu, Mb
9
Mhe. Ally Keissy Mohamed, Mb
10
Mhe. Zainab Rashid Kawawa, Mb
11
Mhe. Kheri Ali Khamis, Mb
12
Mhe. Faida Mohamed Bakari, Mb
13
Mhe. Ismael Aden Rage,Mb
14
Mhe.Modestus Dickon Kilufi, Mb
15
Mhe. Abdul Jabir Marombwa, Mb
16
Mhe.Gaudence Casssian Kayombo, Mb
17
Mhe. Kombo Khamis Kombo, Mb
18
Mhe. Catherine Valentine Magige, Mb





KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA
_______________________________________
1
Mhe. Tauhida Cassian Galosi Nyimbo, Mb
2
Mhe. Dunstan Daniel Mkapa, Mb
3
Mhe. Azza Hillal Hamad, Mb
4
Mhe. Yahya Kassim Issa, Mb
5
Mhe. Menrad Lutengano Kigola,Mb
6
Mhe. Bahati Ali Abeid, Mb
7
Mhe. Kulthum Jumanne Mchuchuli, Mb
8
Mhe. Rajab Mbarouk Mohammed,Mb
9
Mhe. Yusuph  Abdallah Nassir, Mb
10
Mhe. Philipa Geofrey Mturano, Mb
11
Mhe. Eustas Osler Katagira, Mb
12
Mhe. Muhonga Said Ruhwanywa, Mb
13
Mhe. Munde Tambwe Abdallah, Mb
 14
Mhe. Ezekiel Magolyo Maige,Mb
15
Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, Mb
16
Mhe. Alfaxard Kange Lugola,  Mb
17
Mhe. Felista Aloyce Bura, Mb
18
Mhe.Suleiman Jumanne Zedi, Mb

 
KAMATI YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
_________________________
1
Mhe. John Paul Lwanji,Mb
2
Mhe. Hamis Andrea Kigwangalla,Mb
3
Mhe.Godfrey Weston Zambi, Mb
4
Mhe. Highness Samson Kiwia, Mb
5
Mhe. Benardetha Kasabago Mushashu, Mb
6
Mhe. Asha Mohamed Omari, Mb
7
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Mb
8
Mhe. Rosweeter Faustine  Kasikila, Mb
9
Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka, Mb
10
Mhe. Eugen Elishininga Mwaiposa, Mb
11
 Mhe. Rashid Ali Abdallah, Mb
12
Mhe. Eng. Athuman Rashid Mfutakamba, Mb
13
Mhe.Pauline Gekul,Mb
14
Mhe. Sabreena Hamza Sungura,Mb
15
Mhe. Mkiwa Adam Kimwanga, Mb
16
Mhe.Mariam Salum Mfaki, Mb
17
Mhe. Moses Joseph Machali, Mb
18
Mhe. Sylvester  Masele Mabumba,Mb















     19   Mhe. Dkt. Hadji Hussein Mponda, Mb
   20. Mhe. Conchesta Leone Rwamulaza, Mb



KAMATI YA NISHATI NA MADINI
__________________________
1
Mhe. Victor Kilasile Mwambalaswa,  Mb
2
Mhe. Saleh Ahmed Pamba, Mb
3
Mhe. Josephine Tabitha Chagulla Mb
4
Mhe. David Ernest Silinde, Mb
5
Mhe. Martha Moses Mlata, Mb
6
Mhe. Devotha Mkuwa Likokola, Mb
7
Mhe. Raya Ibrahim Khamis, Mb
8
Mhe. Mariam Nassor Kisangi, Mb
9
Mhe.Murtaza Ally Mangungu, Mb
10
Mhe. Juma Abdallah Njwayo, Mb
11
Mhe. Jerome Dismas Bwanausi, Mb
12
Mhe. Richard Mganga Ndassa Mb
13
Mhe. Anne Kilango Malecela , Mb
14
Mhe. Charles John Paul Mwijage, Mb
15
Mhe. Herbert James Mntangi, Mb
16
Mhe. Shaffin Ahmedali Sumar, Mb
17
Mhe. Yussuf Haji Khamis, Mb
18
Mhe. Riziki Saidi Lulida, Mb




























KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA
_________________________________

1.       
Mhe. James Daud Lembeli, Mb
2.      
Mhe. Abdulkarim Esmail Hassan Shah, Mb
3.      
Mhe. Sylvester Mhoja Kasulumbayi,Mb
4.      
Mhe. Zakia Hamdani Meghji,Mb
5.      
Mhe. Susan Limbweni Aloyce Kiwanga,Mb
6.      
Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Mb
7.      
Mhe. Muhamad Amour Chomboh, Mb
8.      
Mhe. Waride Bakar Jabu, Mb
9.      
Mhe. Kaika Saning’o  Telele, Mb
10.    
Mhe. Amina Andrew Clement,Mb
11.     
Mhe. Ester Amos Bulaya, Mb
12.    
Mhe. John John Mnyika, Mb
13.    
Mhe. Michael Lekule Laizer, Mb
14.    
Mhe. Mwanakhamis Khasim Said, Mb
15.    
Mhe. Salim Hemed Khamis, Mb
16.    
Mhe. Al-Shymaa Kwegyr, Mb
17.    
Mhe. Grace Sindato Kiwelu, Mb
18.    
Mhe. Salim Abdullah Turky, Mb
19.    
Mhe. Abuu Hamoud Juma, Mb
20.    
Mhe. Kisyeri Werema  Chambiri, Mb

Rais kikwete atuma salamu kwa Papa Francis wa Kwanza

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa 15 Machi, 2013 mchana amemtumia salamu za Pongezi Baba Mtakatifu Francis I kwa kuchaguliwa kwake kuwa Papa wa kanisa Katoliki Duniani na Vatican.
“Kuchaguliwa kwako ni ushuhuda tosha wa imani na heshima kubwa ambayo kanisa Katoliki inayo kwako, historia yako  na upendo wako wa kujali na kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa wakatoliki, wasio wakatoliki na wasio wakristo pia kusherehekea uteuzi wako”Rais Kikwete amesema kwenye barua yake ya Pongezi kwa Papa Francis I.
Vatican na Tanzania imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete amemhakikishia Papa Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia utaimarika zaidi chini ya uongozi mpya wa Papa Francis I

“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
IKULU
DAR ES SALAAM
15 March, 2013

TAMASHA TIMES: WORKSHOPS GALORE @ ZIFF 2013

$
0
0
WORKSHOPS GALORE!

In response to requests for more workshops and training during ZIFF the 2013 edition is expected to beat all records.
Discussions over the 6 workshops are in full flight expected to take place during the 9-day period. In discussion are:
    Film Production Workshop
    Script Writing Workshop
    Stop-motion animation
    Film Policy and Law
    Arts Journalism
    News Analysis/Dissecting the News
More workshops are being considered.Read about Workshops already confirmed in this Newsletter.

FILM PRODUCTION WORKSHOP: ON THE SHOULDER OF GIANTS

In a collaborative program with the Goethe Institute in Dar Es Salaam the Film Production Workshop will take an innovative approach.
The concept for this workshop involves training of a group of up-coming filmmakers working with a core group of professionals as these make a short film during the festival. The Professionals (Producer, Director, Cameraperson, Editor and Soundperson) will work on a script specially written for the workshop and a limited number of participants (10) will assist as the film gets made.
Nicholas Stampe, who is not new to ZIFF, is the Chief trainer. He will lead the team in a guerilla filmmaking production techniques.
The training will focus on aspects of low-budget filmmaking involving Scriptwriting, Preproduction, Production and Post-production.
A Call for applicants will soon be made to participants who will come from around the East Africa region.
This Program is Funded by the Goethe Institute, Dar es Salaam.

GIZ-ZIFF SHORT FILM SCRIPT WORKSHOP

10 filmmakers from the Region  will be selected to attend the training.
Gabrielle Herbeling, TV Producer and Scriptwriter from Germany, assisted by a local scriptwriter, will lead the training.
During the festival, as part of the training, 3 entries will be selected for development and pitching to a panel of commissioning editors and professionals. The slate of scripts will be announced 3 weeks ahead of the start of the Festival. The selected filmmakers will be required to travel to Zanzibar for the duration of the Program. Accommodation and a modest per diem will be given to participants. Travel to Zanzibar is to be covered by the filmmaker. The theme for all the scripts is East African Integration.

NHIF wamshukuru Mama Kikwete kwa kuwaunganisha na wajasiriamali wadogo

$
0
0
Baadhi ya wanachama wa Uvima wanaohudumiwa na NHIF


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umemshukuru mke wa rais , Mama Salma Kikwete kwa kuwaunganisha wao na wajasiriamali wadogo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya watanzania kutumia mfuko huo kuboresha afya zao.
Tangu aanzishe hamasa Desemba 20 mwaka jana, zaidi ya wajasiriamali wadogo 3000 wameomba kujiunga na huduma za mfuko huo ili kupunguza gharama za tiba kwa watu wa kawaida.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko, Michael Mhando, wakati wa mafunzo ya wanachama wapya kuhusu  haki na wajibu wa mwanachama. Mada hiyo ya  wajibu na haki ilitolewa na Mkurugenzi wa uendeshaji Eugen Mikongoti.
Pamoja na kuwahimiza wanawake kujiunga na mfuko huo kuwasaidia katika matibabu, Mama Kikwete ametoa nafasi kwa wajasirimali wadogo kupitia uratibu wa WAMA kupatiwa huduma za tiba hivyo kuondoa hofu kwa wajasirimali wake kuhusu nini cha kufanya wanapokuwa na uchumi mdogo na huku wanahitaji tiba.
Mhando alisema kwamba elimu anayoendelea kuitoa mama Kikwete kuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) na  Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) imefanya NHIF kuwa na maombi mengi ya watu binafsi na makundi, hali inayoonesha kwamba mwamko kwa sasa upo.
Kutokana na wimbi la mahitaji  NHIF inafikiria kuanza kutoa huduma kwa wajasirimali wadogo binafsi kwa mikoa ya Pwani na Lindi kwani inaonekana kwamba inawezekana kwa wananchi wa  kawaida kujiunga kimakundi na  kuweka akiba ya matibabu kwa kuangalia mfano wa kikundi cha Uvima kilichopo Pugu Majohe ambacho kinadhaminiwa na WAMA.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi muendeshaji wa NHIF Eugen Mikongoti mwanachama wa UVIMA  anatoa sh 122,400 kwa mwaka sawa na sh 10,200 kwa mwezi na wanafaika na uanachama huo ni mwanachama mchangiaji, mwenza wake, wategemezi wasiozidi wanne (ama wa kuasili au wa kuzaa) na wazazi wa mchangiaji.
Mchangiaji analipiwa gharama za kumuona daktari, vipimo (aina 318 kwa sasa kuanzia vya msingi hadi vikubwa kama scan na MRI) gharama za dawa (zipo aina 739) idadi hii haijumuishi dawa za kansa wagonjwa waliowekewa figo bandia na pamoja na kusafisha figo),kulazwa (gredi 1 au 2 kama nafasi ipo), upasuaji (aina 389-kuanzia mdogo, mkubwa na unaofanywa na madaktari bingwa na vifaa saidizi kama  shime sikio magongo, fim,bo nyauep, saidizi za shingo, miwani  na mazoezi ya viungo.
Miongoni mwa wanachama 200 waliokuwapo katika mkutano wa jana, Amina Abbas alielezea furaha yake kwa kuwa katuika mfumo wa matibabu wa Bima ya Afya na kusema imemuondolea adha kubw aaliyokuwa kikabiliana nayo hasa wakati familia yake ikiumwa na yeye hana kipato.
Alisema changamoto anazokumbana nazo sasa ni ndogo zaidi kuliko za awali na kwamba hata hospitalini kukiwa hakuna dawa humpatia fiomu ya kuchukulia dawa katika famasi kubwa ya bahari iliyopo maeneo hayo ya Mpiji magohe.
Alisema japo anasikia kunyanyapaliwa kwa wanachama wa bima maredioni yeye hajawahi kufanyiwa tatizo huilo tangu waanze kutibiwa kupitia mfuko wa NHIF.
"Nawahimiza wenzangu kuijiunga katika vikundi kupata huduma hiyo yenye maana kubwa kwao.Awali nasi tuliogopa lakini tulipoingizwa tumefurahi sana'" alisema Abasi na kuongeza kwamba uhondo wa ngome uingie uicheze.
Mwanamke mwingine Zainabu alisema kwamba kikundi chao kimefurahishwa sana na elimu waliyopewa kwanza iliyowawezesha kuona mwanga na sasa wakifurahia huduma za tiba.
"Kujiunga kwetu kumesaidia sana kuwa na uhakika wa tiba...  japo awali tulikuwa na hofu kwamba hatutakubaliwa.. imekuwa faraja kubwa kwetu na nawahimiza wanawake wengine kijiunga ili kufaidika" alisema Zainabu.
Naye Tabu Likolo Mkurugenzi WAnawake na Maendeleo (WAMA) amesema kwamba baada ya mafanikio ya kikundi cha Mjohe wamekuwa wakipata maombi mengi ya kueleza namna ya kufanya ili kujiunga .
Hata hivyo alitoa wito kwa menejimenti ya NHIF kuangalia mfumo wa kuweza kutumbukiza mtu mmoja mmoja kwani wapo wanaotaka kuingizwa lakini mfumo wa sasa hauwezi wanachofanya WAMA na kutaka vikuindi vya wanawake kuwa katika mwavuli moja na kupata matibabu chini ya udhamini wao.
Uvima imejiunga katika NHIF kwa utaratibu wa uachana binafsi WAMA ikiwa ndiye mdhamini mkuu.
NHIF ilianzishwa kwa sheria ya bunge namba 8 ya mwaka 1999 kw alengo la kuhakikisha linawezesha matibabu ya watanzania wote kwa kuanzia wafanyakazi wa serikali walioajiriwa.

JOTO HASIRA YA LADY JAYDEE ILIVYOZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Braza ben paul alikuwapo
Lady Jaydee akiburudisha
 Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo almaarufu, Lady Jaydee usiku wa kumkia leo alifanya uzinduzi wa video yake mpya aliyomshirikishja Mkongwe Mwezake katika burudani hiyo, Joseph Haule ‘Prof. J’ Video ya Wimbo unaokwenda kwa jina la ‘JOTO HASIRA’.
Jaydee alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Longe uliopo Namanga wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa Burudani na muziki wa mwana dada huyo.
Uzinduzi huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Pichani juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida, mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.
Prof Jay akishoo love na waremba shoo

Ilikuwa bomba

kila mtu alishangilia

MABADILIKO SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA

$
0
0


*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*

Semina elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 iliyokuwa
ifanyike Jumanne (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa imesogezwa
mbele hadi Machi 26 mwaka huu.
Uamuzi wa kusogeza mbele semina hiyo umetokana na maombi ya wadhamini,
Coca-Cola ambao katika tarehe ya awali watakuwa na shughuli nyingine za
kampuni hiyo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi wajumbe kwa
usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza kutokana na semina hiyo kusogezwa
mbele.
Hivyo, washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam (TFF)
siku moja kabla (Machi 25 mwaka huu).
Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania
Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo
wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa.



*Boniface Wambura Mgoyo*
*Ofisa Habari*
*Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)*
Viewing all 9089 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>