Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9290 articles
Browse latest View live

MATOKEO KIDATO CHA NNE YATANGAZWA LEO

$
0
0
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani  la Tanzania,  Dk. Charles Msonde, akitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa  baraza hilo, Edward Haule. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)


Kupata matokeo ingia kwenye tovuti ya NECTA ya: 

http://www.necta.go.tz/index.php 

Kisha bofya sehemu ilioandikwa MATOKEO YA CSEE 2013 & MATOKEO YA QT 2013 Upande wa juu  kulia pembeni mwa tovuti






Confusion: hakika Lulu umeiba shoo

$
0
0


NIKIRI kwamba hii filamu nimeitazama kwa mara ya tatu na kwa jicho la tatu na kuona kwamba katika sinema nzima hii ya kibazazi, binti elizabeth Michael al maarufu kama Lulu ndiye aliyeiba shoo kutokana na jinsi alivyojikubali na kumkubali mhusika wake Besta.

Katika sinema hii utamkubali Lulu ambaye pamoja na nduguye (katika skrini bana ) Sweet (nafasi iliyochezwa na Diana Kimaro) na mama yao (nafasi iliyochezwa na Stella batazari wanakupa  moja ya michapo ya mjini  ya vurugu mechi, ambapo wao na mama  yao wanajikuta wakiwa na mimba kutoka kwa mwanaume mmoja amnayeitwa jaden (nafasi iliyochezwa na Hemed Suleiman).

Utaiitaje  filamu hii ambayo ina mchanganyiko wa biti za mapenzi, vurugu za mapenzi, ukosefu wa nidhamu, maisha ya kisasa, ufichaji wa mambo, hasira ya kukosa na makosa ya makusudi ya kuoneana wivu?

Naam kuna mmoja ambaye anatokea na kuondoka na anakuja kukamilisha kazi ya kuonesha michapo ya mjini dada yao akina Sweet kwa jina la skrini Rachael ambaye wameshea damu (nafasi iliyochezwa na Shela Rachael) ambaye naye kwa namna ya ajabu kabisa anakuwa na urafiki na Jaden.

Ni simulizi la familia ambayo mwenye nyumba amefariki na watoto wake watatu  wako na mama yao, katika mazingira ambayo unyanyasaji ni  tatizo katika nyumba hii kwani mama alikuwa anapenda watoto wake wa kuzaa sio yule waliyemkuta ambaye kwa bahati mbaya ndiye aliyekuwa na funguo za nyumba na miradi ya mzee wao hawakujua.

Filamu hii inaanza kwa mbwembwe za mjini na tangu mwanzo unaona kabisa kwamba Lulu  anashai ni japo inaonekana amepewa mistari michecha che ya kuzungumza lakini ingi inaakili.

Lulu ameutumia vyema mwili wake, sauti yake, uwezo wa kujieleza katika sura (muonekano) kukufanya kumfuatilia zaidi yeye kama vile ndiye mwenye filamu na mwisho nui unaweza kukubaliana nami kwamba kafunika katika filamu hii ambayo inatoa burudani lenye fundisha la koma mwana wa kukoma wewe! mapenzi hayana kitabu, adabu wala daftari la uhakika la kutia saini.

Jaden, kidume anakutana na mama Sweet aka mama Besta na mama  anachukua muda kumuiba mvulana huyu ambaye alistahili kuwa na mabinti zake. Kwa kutumia fedha kichele alizokuwa nazo alimtia  kwenye 18 zake na kuwa naye, kisha akamrai kufika nyumbani Lulu akaona akachanganyikiwa unaona katika sura na maneno na mshangao yaani kwa ufupi akadata palepale kwa mtu ambaye ameletwa pale na mama yake na kutambulishwa kama anko.

kabla ya kumfikisha nyumbani mama sweet alikubali kazi ya Jaden na kusema atafanya kila liwezekanalo kumtenganisha na mwanamke ambaye alikuwa anaishi naye kwa takaribani miaka miwili, japo hawakuwa wameoana.

Jaden naye hakuwa mstaarabu kwani alimdondokea mtoto yule akaanzisha mawasiliano na Lulu, ona mapenzi ya Lulu, lazima usijisikie kupendwa, lulu anajua kuyauza katika skrini ni balaa, kama yeye alivyokolea na furaha akamfanya ndugu yake aangalie ni kitu gani akagundua Jaden akaiba simu akatengeneza keep left na kisha akaingia katika anga za Jaden; Jaden akaingia na asifurukute naye si anajua anapendwa!

Naam sasa unaona, kuna mzunguko mbaya wa mapenzi, Jaden alisema wakati anapambana kimaneno na Sweet, kwamba yeye anauhusiano na dada yake inakuje yeye. Sweet akasema hayo amwachie yeye akaanguka naye. Sasa nyondo ikapanda,. jaden akamsahau mama Sweet, akamsahau Besta, besta akashtukia ishu na  mama naye akashtukia ishu. lakini wote wakakaa kimya hasa Besta ambaye alitambua uhusiano wa mama yake na Jaden mapema lakini akaamua kuyavuruga akimshawishi Jaden aachachane na mama yake.

Stori hii ya  Peter Mbwambo ambayo mimefanyiwa skripti na Reah Mwendamseke inanoga kuitazama kwa sababu tu ni ya mapenzi na utakayemtazama ni Lulu ambaye aliyauza kwa akili yake yote, akajaribu kuyalinda, akajikuta yanamnyong'onyeza halafu unaona katika sura na katika mwili, binti huyu nafais hizi anazipatia sana.

Projuza Peter  mbwambo ambaye alishirikiana nafasi hiyo na mwajuma Mndaira  amesema moja ya sinema ambazo anaona zimefanya vyema ni hiyo ya Confusion ambayo lengo lake kubwa ni kuonesha ubaya wa usiri. Huenda mama Sweet kama angelisema kwa watoto palepale kwamba huyu ni baba yenu ile hali ya mtafuruku wa wasichana wale kumpenda mtu mmoja aliyeletwa kwao na kuambiwa ni anko wao.

Naam, projuza Mbwambo ametumia kufumaniana kwa akina Sweet na dada yake Besta kufunua siri iliyojificha ili iwe hadharani kwa kumuangusha sweet kuumia na kufikishwa hospitalini.

Ni hapa mama anatambua kwamba yule aliyempenda ndiye pia kaleta madhara kwa watoto wake.

Japo siri ilitakiwa kubaki nyumbani , baada ya Rachael kurejea kudai kilichokuwa chake na  kuwakutanisha tena wakiwa kama familia Jedan anatembea pia na Rachael na  matokeo yake anapoenda kutambulishwa nyumbani kumbe ndiye aliyeharibu mama na ndugu zake, ilikuwa fadhaa kubwa na hapa Lulu anaonesha jinsi alivyochanganyikiwa kwa yao kuvurugwa na mtu mmoja.

Naam,kuvurugwa, huko nako kulimchanganya Jaden ambaye alikiri uroho wake umemharibia kila kitu.Akaamua kumteka  aliyekuwa mke wake akaleta kizunguzungu kikubwa ambacho kilimfikisha polisi na kutema mkewe. Naam kumbe mapenzi hayana ubabe wala ushababi he he he he.Je Mbwambo amefanikiwa? naweza kusema ndiyo! Ukiwa na watoto kama sweet, besta na mama kaka yule walahi lazima uhangaike. Tchao wikiend njema.

Washiriki
Hemed Suleiman---- Jaden
Elizabeth Michael--- besta
Diana Kimaro-------Sweet
Stella batazari.... mama sweet
Shela rachael----- dada sweet
Salma Nisha -----Rose
Stanley Musungu--- Mwanasheria
hemed bajomba--- Mwanasheria
Kilangi Musiba--- askari
Salma Mohamed---askari
Malk--- Jitani
Benson Jackson-- jambazi
Charles wilson-- jambazi
UmmyEdward jirani

Stori
Peter mbwambo
Scripti
reah Mwendamseke
Producer
peter mbwambo
mwajuma Mndaira

PINDA AIASA JUMUIYA YA UMOJA WA WAZAZI NCHINI

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Jumuiya ya Wazazi nchini ni miongoni mwa jumuiya inayoongoza na kusimamia masuala yote yanayohusu elimu, malezi bora kwa vijana wa taifa letu hivyo lazima iangalie jinsi ya kuweza kujipambanua katika utekelezaji wa Umoja wa Jumuiya yao.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Februari 22, 2014), wakati akifungua rasmi semina ya siku tatu ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi ngazi ya Taifa, Mikoa na Wilaya Tanzania inayofanyika kwenye Ukumbi wa NEC, Mkoani Dodoma.

Akizungumza katika ufunguzi huo, Waziri Mkuu Pinda  aliwaeleza wana jumuiya hao kuangalia malengo wanayojipangia aidha yawe ya muda mfupi au mrefu ili kuyatekeleza kwa kuzingatia yale mambo ya msingi na yenye kipao mbele kwa wananchi.

“Changamoto kubwa iliyopo mbele yenu kama viongozi na watendaji wakuu wa Jumuiya hii ni namna ya kutimiza malengo mliyojiwekea“.

Alisema, dhana ya Jumuiya ya Umoja wa Wazazi nchini ni kuongeza na kuboresha masuala yote yanayohusu Sekta ya elimu hapa nchini: ‘‘Tumieni semina hii kujipima kwamba mmefikia wapi katika utelelezaji wa malengo yenu kwa kuangalia mapungufu na maboresho katika jumuiya yenu‘‘. 

Jumuiya ya Wazazi ndio magwiji mnaoongoza kwa kuwa na shule nyingi hapa nchini, hivyo jumuiya yenu ijipange na kusimamia vema shule hizo ili kuwa vinara katika kuboresha masuala ya elimu hapa nchini. Akitoa mfano, alisema: “Kwanini shule za binafsi zinakuwa zinaongoza kuliko shule zilizopo ndani ya Jumuiya yenu, walau katika kumi bora iwepo shule moja kutoka Jumuiya ya Umoja wa Wazazi alisema Waziri Mkuu”. 

Kutokana na kauli hiyo, Waziri Mkuu aliiambia Jumuiya hiyo kutumia dhana ya elimu kama ngao yao katika kuleta maendeleo katika Sekta hiyo kwani Ilani ya chama cha Mapinduzi imetamka wazi kuongeza kasi ya upanuzi wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari lengo ambalo ni moja ya jukumu kuu la msingi la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi.

Aliendelea kusema kuwa Jumuiya ya Wazazi inajukumu la kusimamia masuala yote yanayohusu maadili, jukumu ambalo halina tofauti sana na jukumu la madhehebu ya dini kuzungumza bayana masuala ya malezi ya watoto na vijana ambayo yamekuwa yakiporomoka kila kukicha, hivyo Waziri Mkuu alisema, jumuiya hii itumia jukumu na nafasi waliyopewa kuhakikisha watoto wote walio ndani na nje ya jumuiya wanafundishwa maadili.

Waziri Mkuu aliendelea kusema kuwa, Jumuiya ya Umoja wa Wazazi ina majengo, viwanja na ardhi inayofaa kwa kilimo na shughuli za kiuchumi, tumieni fursa hizi kwa kujenga vyuo, kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo itawasaidia katika kuongeza kipato katika jumuiya yenu.‘‘Mnachotakiwa ni kupanga bajeti zenu vizuri na kusimaia utekelezaji pamoja kusimamia vizuri miradi na fursa zinazojitokea“

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu aliiomba Jumuiya ya Wazazi kujitokeza kuzungumzia masuala ya Dawa za Kulevya kwa kusema kuwa, wako vijana ambao wametumbukia katika dimbwi la Dawa za Kulevya ambaa pia wanahatarisha maisha yao kwa kupata UKIMWI: “Ni matumaini yangu kwamba Jumuiya ya Umoja wa Wazazi itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii, kutoa ushauri kwa vijana kuhusu athari za dawa za kulevya, UKIMWI na  hata mkiweza kuanzisha vituo vya ushauri”, alisisitiza Waziri Mkuu.

“Ili kuweza kuwa na Jumuiya ya Wazazi imara ni dhahiri kuwa wanajumuiya wasimamie kanuni na maadili yanayoongoza jumuiya yao kwa kuwaasa kuacha kujiingaza katika makundi yasiyokuwa na msingi hasa kwa kutanguliza maslahi ya fedha katika kupata nafasi za uongozi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ambao huleta migawanyiko kati ya Viongozi na wanachama na wapiga kura”. Mzingatie masuala yanayohusu kujenga na kukuza utekelezaji wa jumuiya yenu ambayo itawasaidia kujenga jumuiya imara na kujenga chama imara kitakacho leta viongozi imara”alisisitiza Waziri Mkuu.

Mapema, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Taifa, Bw. Majura Bulembo, alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo na kuwaongeza ufanisi Jumuiya ya Wazazi katika utekelezaji  kazi zao na kuwasisitiza kuhudhuria semina hiyo ipasavyo ili kuweza kukumbusha mapungufu na changamoto zinazojitokeza katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

“Viongozi wamekuwa wakitumia vibaya nafasi za uongozi walizopewa kwa kujiona wao ndio viongozi wakuu kwa kujifanyia maamuzi yao, viongozi kama hao wataondolewa madarakani mara moja”.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, FEBRUARI 22, 2014.

Francisca S. Swai
Mob: +255 717 044401
Mail: franciscaswai@ymail.com
:Mail sisca@pmo.go.tz
"Tears are words numbers cant Tell"

Pata harufu ya bangi kwa kuona moshi wake

$
0
0
Mkuu wa mkoa Kigoma Issa Machibya (wa pili kushoto) akiongoza kundi la
viongozi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kuchoma shehena
ya mimea ya bangi ambayo iligundulika katika kijiji cha Kigina wilaya
ya Kibondo mkoani kigoma ambapo mashamba makubwa ya bangi
yaligundulika (kulia) ni Mkuu wa wilaya Kibondo Venance Mwamotto.

Source:Picha na Fadhili Abdallah

IN LOVING MEMORY OF OUR BELOVED MOTHER ESTHER NYIMBO BADI

$
0
0

No words can express the pain we felt when we lost you on Wednesday 22nd February 2012 at 6.30 p.m. Over the two years, precious memories of your beautifully life have been our only comfort.

We remember your affectionate smile, the sweet sound of your voice, your kind and most generous heart that would have a place for everyone.

We count our self lucky to have held a mother like you, and we thank GOD for the incredible times we shared. We miss you greatly, but we know you are happy in Heaven watching over us, and praying for us.

Affectionately remembered by your children, Blandina, Bertha, Stella, Gern, Lilian, John and Upendo. You’re in laws Cashmir, Modestus, James, Kenny and Afro and Your Grandson’s Joakim, Jeff, Abraham, Faith, Deborah, Caleb, Karen, Sara, Brandon, Dillan, Esther, Hilary, Suzana and Edson.  

Rest in Peace Mummy.
-------------- John Hans Badi -Senior Photojournalist -Director of Hans PR (Public Relations, Press Coordination, Photography, Video Production & Promotion Activities). -Blogger: Daily Mitikasi Blog P.O. Box 11717, Dar es Salaam. Mobile: +255784587088/0712155221 E-mail:badijohn30@yahoo.co.uk

Mnyika ayakandia matokeo ya Form IV arejea hoja za serikali ijieleze

$
0
0


*MAONI YANGU KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE*

Maoni yangu kuhusu matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne wa mwaka
2013 yaliyotangazwa  na kuelezwa kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 15.17
yamedhihirisha tahadhari niliyotoa kuhusu mabadiliko ya viwango vya ufaulu
yaliyotangazwa na Serikali tarehe 30 Oktoba 2013.

Serikali kwa barakoa (veil) ya kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
(Big Results Now) imeamua kulificha taifa juu ya Matokeo Mabaya ya Sasa
(Bad Results of Now). Hivyo, wachambuzi wa masuala ya elimu wanapaswa kutoa
takwimu za matokeo yangekuwa namna gani iwapo viwango vya awali vya ufaulu
vingetumika ili nchi ijue hali halisi kwa manufaa ya wananchi.

Aidha, natoa mwito kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuweka wazi kwa umma ripoti
za uchunguzi zilizoundwa kuwezesha wananchi kuihoji Serikali iwapo kupanda
huko kwa ufaulu ni matokeo ya kuboresha mazingira ya kufundisha na
kujifunza au ni kiini macho cha mabadiliko ya wigo wa alama na madaraja?

Ukweli ni kuwa hali ya mazingira ya kujifunza na kujifunzia katika shule
nyingi za msingi na sekondari hasa za umma sio nzuri kutokana na kutokuwa
na vitabu vya kutosha, maabara za kutosha, waalimu wenye sifa wapo wa
kutosha na kuboresha maslahi ya waalimu ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kwa
siku nyingi.

Ikumbukwe kwamba miaka mitatu mfululizo, mfumo wa elimu wa Tanzania, na
hususani kwa upande elimu ya msingi na sekondari umekuwa ukiporomoka kwa
kasi ya ajabu. Kufuatia kuporomoka huko, na hasa kushuka kwa viwango vya
ufaulu, Serikali kwa vipindi totauti (mwaka 2010 na  2012)  imeunda Tume
kuchunguza sababu za kushuka kwa viwango vya ufaulu.

Ingawa ripoti za tume zilizoundwa kuchunguza sababu za kushuka kwa ufaulu
hazijulikani kwa wananchi ambao ni wadau wakuu wa elimu, Serikali
imeendelea kutoa maagizo na matamko mbalimbali kuhusu viwango vya ufaulu.

Ikumbukwe kuwa mwezi Mei, 2013 Serikali ilitangaza kufutwa kwa matokeo ya
kidato cha nne ya mwaka 2012 kutokana na kushuka mno kwa viwango vya ufaulu
ambapo zaidi ya asilimia 65 ya wanafunzi walipata daraja sifuri na kuamuru
matokeo hayo kupangwa upya.

Takribani miezi sita baadaye, yaani 30 Oktoba 2013 Serikali ilitangaza
kubadili viwango vya ufaulu bila kutoa ufafanuzi kuhusu msingi wa
mabadiliko hayo na kuwasilisha bungeni ripoti za kamati/timu zilizochunguza
kuporomoka kwa ufaulu.

Hivyo hata baada ya kauli ya Serikali kuwa "kundi la watahimiwa
walioshindwa Mtihani na ambalo awali lilikuwa likiandikwa kama 'failures'
litaendelea kujulikana kama Daraja Sifuri (Zero) bado Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi inapaswa kutoa ufafanuzi juu ya athari za mabadiliko hayo
kuwezesha Bunge kusimamia Serikali ipasavyo.

Pamoja na mpango wa Serikali wa kuficha matokeo mabaya ya kidato cha nne ya
mwaka 2013 bado idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwa kuwa
watahiniwa 151,187 sawa na asilimia 42.91 wamepata sifuri. Kati ya hao,
wavulana ni 78,950 sawa na asilimia 41.54 na wasichana ni 72,237 sawa na
asilimia 44.51. Aidha, katika matokeo hayo hali ya watahiniwa kutokuweza
kufanya mtihani kabisa kwa kiwango cha kuacha karatasi tupu, kuchora vitu
vya ajabu au kuandika matusi inadhihirisha udhaifu mkubwa uliopo katika
mfumo wetu wa elimu kwa kuwa wahusika wameweza kupanda kuanzia kidato cha
kwanza mpaka cha nne wakiwa hawana uwezo wa kufanya mitihani.

Hivyo, Serikali ihojiwe ieleze dhamira ya kweli ya mabadiliko ya viwango
vya ufaulu na kutakiwa kushughulikia vyanzo vya matatizo katika elimu
badala ya kuficha matokeo mabaya na hali halisi za wahitimu.

Serikali inafanikiwa kuficha udhaifu kwa sababu ripoti kamili za uchunguzi
juu ya ufaulu duni wa wanafunzi hazijawahi kuwekwa hadharani ili kujua
kiini cha tatizo. Mara zote Serikali imekuwa ikifanya maamuzi bila
kuzingatia ripoti za uchunguzi na ndio maana Serikali haikusita kuunda tume
ya kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2012 wakati
kulikuwa na tume iliyofanya kazi hiyohiyo mwaka 2010.

Endapo tutaendelea kufikiri kwamba kulegeza njia za ufaulu ndio kuboresha
elimu, tutajikuta tuna taifa la watu wenye vyeti vizuri vya elimu lakini
wasioweza kufanya kazi inayoshabihiana na alama za ufaulu katika vyeti vyao.

Wataalamu wa elimu waitake Serikali kuacha kufanya mambo yanayohitaji
utaalamu kwa ajili ya kujitafutia sifa kisiasa kwa mipango mibovu. Suala la
elimu lisichukuliwe kama ajenda ya siasa chafu kwani kwa kufanya hivyo
tunaiua elimu yetu.

Ni vema kabla Serikali haijafanya maamuzi ya jambo linaloathiri maisha ya
watanzania wengi kama hili la mitihani ikaleta kusudio la kufanya hivyo
bungeni ili wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wajadili na kuishauri
Serikali Ipasavyo.

Mwisho kabisa, napenda wananchi wafahamu kwamba kwa mujibu wa kitabu
kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka cha "International
Qualification", baada ya Tanzania kutangaza alama mpya za ufaulu, sasa
inakuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu.
Maana yake ni kwamba, tumeshusha ubora na thamani ya elimu yetu.

Hivyo naitaka Serikali kutoa ufafanuzi ni kwanini isifute uamuzi wake wa
kubadili viwango vya ufaulu ambayo tayari umeanza kuficha hali hali ya
matokeo mabaya katika mitihani. Na badala yake itoe kwa umma na iwasilishe
bungeni ripoti za uchunguzi zilizoundwa na kuliwezesha Bunge kufanya
maamuzi ya kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)

22/02/2014

Rihanna asema sasa wakati umefika kuachana na ganja

$
0
0


BAADA ya kusherehekea miaka 26 tangu kuzaliwa kwake mwanamuziki anayetisha Rihanna, sasa anajipanga kupunguza uvutaji bangi, kama sio kuacha.

Chanzo cha habari kilichothabiti kimeiambia HollywoodLife.com kwamba baada ya sherehe hiyo  bibiye amesema kwamba  atapunguza matumizi ya ganja kutokana na umri wake kuendelea kukua.

Mashabiki wake wamesema  wanasubiri kuona mabadiliko kwa binti huyo ambaye matumizi ya ganja ni kama uji na mgonjwa.

Katika hili mdada huyu anaonekana kuzidi kuimarisha mwanzo wake mwema wa mwaka huu, ambapo tayari ameshapiga picha ya ukurasa wa mbele wa Vogue itakayotoka Machi na mahusiano yake na Drake, 27 yanaonekana kuimarika zaidi.

Katika sherehe hizo za miaka 26 zilizofanyika Februari 20, mdada huyo  alichachawa katikati ya pati yake baada ya kupokea simu kutoka kwa mtu anayemhusudu sana kwa mujibu wa maneno yake Drake.

Rihanna, ambaye anatamba  na 'Nothing Was the Same' al-maarufu kama RiRi katika siku yake maalumu, ujumbe wa Drake ulimchengua kiasi cha kuanzisha mazungumzo yenye mahaba.

Rihanna alikuwa akihangaikia siku yake  ambapo katikati ya vinywaji  alipata simu kutoka kwa marafiki wake wenye maana, patna Drake, ambapo alimwambia anampenda sana na kwamba wataongea anaporejea nyumbani kwani ndio anaondoka.

Rihanna, 26, anaonekana kwenda vyema na Drake, 27, ambaye huwa anajitokeza hata kwa simu wakati wa shughuli nzito za bibie.

Maneno hayo yaliyomfurahisha Rihanna yanaangalia mahusiano ya Drake na bibie. Swali linabaki je watarejeana.

Wanasema Drake huwa anajua kumfanya binti awe wa kipekee.

Utajiri wa Nuella Njubigbo waelezwa ni hongo za wanaume

$
0
0


YAPO maneno makali yanaibuka katika tasnia ya sinema ya Nigeria kutokana na mabadiliko makubwa ya kitajiri kwa binti mrembo muigizaji wa Hollywood, Nuella Njubigbo.

Binti huyo ambaye kwa siku za karibuni kajipatia usafiri mkali mpya wa 2011 Toyota Highlander, SUV  kwa thamani ya fedha za Nigeria milioni nane, inaaminika utajiri wake  unatokana na kuhongwa na wanaume mbalimbali waliompitia.

Ingawa Nuella ni mmoja wa waigizaji wa daraja la kwanza, utajiri wake wa ghafla unadaiwa kutokana na wanaume kadhaa ambao walikuwa pamoja kimapenzi miaka iliyopita.

Kabla ya sasa alikuwa kipenzi cha mtengeneza filamu Tchidi Chikere. Uhusiano wao wa miaka kumi ulivunjika vibaya.

Baadae Nuella akatoka na mcheza soka mwenye fedha ambaye makazi yake ni Urusi, Emanuel Emenike. Uhusiano wake hakumaliza mwaka.

Govana Rotimi Amaechi, ambaye anajulikana kwa kudeti waigizaji bomba wa Nollywood imeelezwa kuwa anatoka kimahaba  na Nuella ambaye inasemekana anafurahia sana maisha hayo.

Inadaiwa kwamba Amaechi  alimpiga na fedha za Nigeria milioni 5 ili aweze kupangisha nyumba mashariki mwa Nigeria.

Wampa mtoto jina akiwa amekufa

$
0
0

MUME wa muigizaji Shayne Lamas anayejulikana kwa jina la Nik Richie mtata wa mambo ya kublogu udaku Thedirty.com ametoa jina la mtoto wake aliyezaliwa akiwa mfu.

Lamas akiwa katika wiki ya 20 ya mimba yake alipata matatizo ya kuchoropoka kwa mimba ambapo alifanyiwa hima ya kuokolewa maisha  yake na kumpoteza mtoto huyo.

Richie akizungumza na mtandao wa habari za burudani TMZ  kuhusu shida hiyo, alisema kwamba siku kadha ya baada ya mimba hiyo kutoka alimshika mtoto wake huyo mfu akambusu na kumpa jina la  Rex Jagger Lamas-Richie.

Anasema alichagua jina la  Rex kwa sababu alitaka mtoto wa kiume mwenye jina hilo akampa Jagger kutokana na mwanamuziki anayemhusudu Mick Jagger.

Pia staa huyo alimwandikia barua mtoto wake huyo akimweleza ni namna gani anampenda hasa kutokana na kujitoa kwake ili mama yake aweze kuishi.

Alimshukuru mtoto wake kwa kumuonesha maana ya kupenda ikiwa na maana ya kujitolea kama yeye alivyofanya, kuondoka ili mama yake aweze kuishi.

Lamas, 28, alikimbizwa hospitalini  Februari  9 baada ya kuanguka nyumbani kwao Orange County. Wakati wa upasuaji kumuokoa muigizaji huyo wa Bachelor alimpoteza mtoto wake.

TWIGA STARS YAENDELEA KUJINOA KUIKABILI ZAMBIA

$
0
0


Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inaendelea kujinoa kwa ajili ya
mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake
(AWC) dhidi ya Zambia (Shepolopolo) itakayochezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka
huu).

Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage na Msaidizi wake Nasra Juma
inaendelea vizuri, na kwa mujibu wa programu ya benchi lao la ufundi kesho
(Jumatatu), Jumanne na Jumatano itafanya mazoezi saa 10 jioni.
 
Mazoezi hayo yatafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo
ya Jiji la Dar es Salaam. Uwanja huo ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi
hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
 
Shepolopolo ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-1 wiki iliyopita
inatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) kwa ndege ya
Fastjet, na siku hiyo hiyo itafanya mazoezi Azam Complex.
 
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle
Shikana na Suavis Iratunga, wote kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili
nchini Jumatano.
 
*YANGA, PRISONS KUPANGIWA TAREHE MPYA*

Mechi namba 118 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Tanzania
Prisons iliyokuwa ichezwe Februari 26 mwaka huu itapangiwa tarehe nyingine.



Uamuzi wa kuiondoa mechi hiyo iliyokuwa ichezwe Jumatano kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam umefanywa ili kuipa fursa zaidi Yanga kujiandaa kwa
mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly ya Misri itakayofanyika
Jumamosi (Machi 1 mwaka huu).



Al Ahly na Yanga zitarudiana wiki moja baadaye kati ya Machi 7, 8 au 9
mwaka huu jijini Cairo, Misri.

*MECHI ZA MABORESHO TAIFA STARS*

Mechi za mpango wa kuboresha Taifa Stars kati ya mikoa na mikoa wiki hii
itakuwa kama ifuatavyo;

Februari 25 Njombe vs Ruvuma (Uwanja wa Njombe)

                  Kinondoni vs Ilala (Uwanja wa Karume)

Februari 26 Morogoro vs Pwani (Uwanja wa Jamhuri)

                  Geita vs Kagera (Uwanja wa Geita)

                  Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika)

                  Iringa vs Mbeya (Uwanja wa Samora)

                  Shinyanga vs Simiyu (Uwanja wa Kambarage)

                  Lindi vs Mtwara (Uwanja wa Ilulu)

Februari 27 Temeke vs Kinondoni (Uwanja wa Karume)


Miss Tanzania, Happiness Watimanywa changisha fedha kwa ajili ya hospitali kuu Moro

$
0
0


Miss Tanzania, Happiness Watimanywa, mwishoni mwa wiki aliongoza harambee
ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Harambee hiyo ya kuchangisha fedha ilifanyika katika Bwalo
la Magadu lililoko mjini Morogoro,

Akizungumza katika tukio hilo,  Watimanywa alisema fedha hizo zitatumika
kununua nguo na viatu kwa ajili ya wauguzi wa hospitali hiyo, na kuongeza
kwamba, yeye mwenyewe kama mwanafamilia wa Universal Tanzania ana
furaha kubwa kushiriki harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya hospitali.

"Kama mwafamilia wa Universal Leaf, tawi la Tanzania na mkazi
Morogoro, najisikia mwenye bahati sana kuwa sehemu ya tukio hili ambalo
limevuka lengo la awali la kupata shilingi milioni 1.5. Pia ninawashukuru
wote ambao wamefanikisha tukio hili ambapo tumekusanya
shilingi 3,050,000," alibainisha mnyange huyo.

Universal Leaf (ULT) yenye makao yake makuu nchini Marekani, ndio
inayomiliki makampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company (TLTC ) naTanzania
Tobacco Company (TTPL) za mjini Morogoro.

Wakati wa harambee hiyo, Watimanywa alionesha uwezo wake wa ushawishi
katika kuhakikisha fedha zinapatikana kwa njia nzuri kwa kuita mbele baadhi
ya watu na kuwapa majukumu fulani 'magumu' ambapo anayeshindwa ama
kufaulu analazimika pia kutoa ahadi ya nini anachangia katika mfuko.

Wa kwanza kuitwa alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa ULT, Paul Crossan ambapo
alimpa 'kibarua' cha kuimba wimbo wowote wa Bob Marley.

Crossan ambaye alichangia shilingi 250,000, aliwashangaza washiriki wa
harambe hiyo kutokana na kipajichake kwa jinsi alivyomudu kuimba wimbo
wa "Three Little Birds " wa mfalme huyo wa Reggae duniani.

Wa pili aliyeitwa katika utaratibu aliouanzisha Miss Tanzania ni Nick
Carrian, ambaye alimtaka kuimba wimbo wowote wa kufokafoka.
Haraka haraka, Carrian aliimba wimbo wa MC Hammer wa "You Can Touch Me".
Naye alichangia shilingi 200,000.

Baadaye ilikuwa ni nafasi ya wazazi wa Miss Tanzania,  Bwana na Bibi Louis
Rousos, ambao walitakiwa kuonesha uwezo wa kucheza muziki ambapo walicheza
na kisha kuchangia shilingi 200,000.

Mkurugenzi wa Sheria wa TLTC, Richard Sinamtwa, aliambiwa kutembea
kama mwanamitindo ambapo alishindwa na kisha kuchangia shilingi 200,000.

Katika hotuba yake fupi, Mkurugenzi Mtendaji, Crossan alisema Universal
Leaf, upande wa Tanzania ni kampuni la wananchi kupitia majina ya Tanzania
Leaf Tobacco Company Limited (TLTC) na Tanzania Tobacco Processors Limited
(TTPL) na kwamba linajisikia fahari kuchangia juhudi za serikali katika
kutoa afya bora kwa watu wote.

Aliwashukuru wafanyakazi kwa kuonesha ukarimu wao katika kuchangia fedha
kwa ajili ya hospitali: "Kama kampuni tunaamini katika umoja na kunyoosha
mkono wetu katika kusaidia watu wenye mahitaji waliokaribu nasi."

Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo, Dk
Mossi Makau alisema kuchangisha fedha ni sehemu ya jitihada zao za
kutoa kile walicho nacho kwa wahitaji.

"Fedha zilizotolewa hapa ni kutoka kwenye mifuko ya wafanyakazi binafsi na
siyo kutoka kwenye kampuni na zitatumika kwa ajili ya kununua vifaa
mbalimbali ambavyo vitasaidia kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika
hospitali," alisema.

Naye Meneja Raslimali watu wa TTPL, Gabriel Thobias, katika hotuba yake
alisema kuchangia hospitali ni njia ya kusaidi jamii inayowazunguka.

"Sisi ni sehemu ya jamii ya watu wa Morogoro na tuna wajibu wa
kuisaidia chochote tulichonacho kama tulivyofanya leo," alisema.

 mwisho

wazee wa kizigo wasindikizwa vyema Mtenda akitendewa

$
0
0


Ilikuwa ni siku ya aina yake kwa bendi ya Extra Bongo "wazee wa kizigo" walipokuwa wakizindua albamu yao ya mtenda akitendewa na kuacha gumzo kwa mamia ya mashabiki waliojitokeza ukumbini
humo asante kwa udhamini wa Vodacom kufanikisha Tamasha hilo.
Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga na Amini MwinyiMkuu wakiimba kwa pamoja wimbo wa "Mtima wangu" kwa Mashabiki waliojitokeza katika Ukumbi wa Dar Live, Wakati wa Uzinduzi wa Albam mpya ya bendi ya Extra Bongo "wazee wa kizigo", mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo pia ulisindikizwa na Bendi ya Mashujaa ulidhaminiwa na Vodacom.

Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakitoa burudani kwa Mashabiki wa Muziki wa dansi wakati wa Uzinduzi wa Albamu mpya ya bendi ya Extra Bongo katika ukumbi wa Dar Live

Gari la kubebea wagonjwa "Ambulance" likiingia katika ukumbi wa Dar
Live likiwa limembeba Ali Choki, wakati akiingia kufanya Uzinduzi wa Albamu
mpya ya bendi yake ya Extra Bongo iliyopewa jina la "Mtenda Akitendewa".


Wasanii wa Muziki wa Dansi, Ali Choki na Banza Stone, wakiimba kwa
pamoja wakati wa Uzinduzi wa Albamu mpya ya bendi yao ya Extra Bongo ya
"Mtenda akitendewa", Uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live
Mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya
Vodacom Tanzania.

Msanii wa Muziki wa Dansi, Ali Choki akiimba mbele ya Mashabiki
waliojitokeza katika uwanja wa taifa wa Burudani Dar Live, wakati wa
Uzinduzi wa albamu yake mpya ya "Mtenda akitendewa" Uzinduzi huo
ulidhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Wanenguaji  wakitoa burudani kwa Mashabiki wa Muziki wa dansi wakati wa Uzinduzi wa Albamu mpya ya bendi ya Extra Bongo katika ukumbi wa Dar Live mwishoni mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Palikuwa hapatoshi katika ukumbi huo wa taifa wa burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo bendi kaadhaa za muziki wa dansi na wasanii wa bongo flava zilitumbuiza kabla ya uzinduzi wenyewe kufanyika.
Kivutio kikubwa zaidi kilikuwa ni pale ambapo kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Kamarade Ali Choki alipoingia na gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ukumbini kutumbuiza mashabiki wake waliofurika kwa wingi.
Uzinduzi wa albamu hiyo iliyokwenda kwa jina la Mtenda akitendewa ulikwenda sambamba na burudani lukuki kutoka kwa wanamuziki mbali mbali mashuhuri nchini kama vile malikia wa mipasho nchini Khadija Omari Kopa, Banza Stone, Abdul Misambano, Mashujaa Band pamoja na wasanii wa bongo flava Linah na Amini ulidhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom.
Wanenguaji wa Extra Bongo walifanikiwa vilivyo kuzikonga nyoyo za mashabiki ukumbini hapo kwa kupagawisho vilivyo jukwaani kwa staili mbali mbali mpya za uchezaji.
Kwa upande wa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wa bongo flava, Linah na Amini walidhibitisha kwa nini wao ni waimbaji bora na wataendelea kuwa hivyo kwa kuonyesha kipaji cha hali ya juu katika kulimiliki jukwaa ambapo waliimba kibao chao kitamu cha 'Omotima wange ni wewe'.

FOMU UCHAGUZI TASWA ZAANZA KUTOLEWA

$
0
0
Fomu za wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam zimeanza kutolewa leo (Februari 24 mwaka huu).
 Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo zinazotolewa Idara ya Habari (Maelezo) ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.
 Ada kwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.
Kwa mujibu wa Ibara ya 21 (e)(i), sifa ya elimu kwa wanaowania nafasi za Mwenyekiti hadi Katibu Msaidizi ni diploma au digrii ya uandishi wa habari. Kwa nafasi nyingine kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(ii) ni cheti cha ngazi yoyote katika uandishi wa habari.
Tunawahimiza wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili waweze kuwania nafasi hizo.
 *Boniface Wambura*
*MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI TASWA*
*Februari 24, 2014*
*Dar es Salaam*

WAANZA KUTIMUANA KUGOMBEA ULAJI WA BUNGE LA KATIBA

$
0
0


Mjumbe wa Bunge la katiba Rashid Yussuf Mshenga amepinga kitendo cha kufukuzwa
uanachama katika chama cha AFP cha wakulima kilichofanywa na Mwenyekiti wake na
kudai ni matokeo ya wivu wa maendeleo.

Akizungumza kutoka Bungeni Dodoma u Mshenga ambaye ni
mkurugenzi sera na mipango wa chama hicho alisema yeye amechaguliwa baada ya
kuonekana kwamba anazo sifa na vigezo vyote na uamuzi uliochukuliwa na
mwenyekiti wa chama hicho cha kumfukuza ni kuonesha wivu wa yeye kutochaguliwa
kuingia katika bunge la katiba.

Aidha Mshenga alisema Mwenyekiti wa chama hicho hana uwezo wa kumfukuza uanachama
isipokuwa mkutano mkuu wa chama hicho wa taifa,kauli ambayo ilipingwa na mwenyekiti
wa chama hicho Said Soud.

Akizungumza na waandishi wa habari,mwenyekiti wa chama cha AFP Wakulima Said Soud
alisema Mshenga amefukuzwa katika chama hicho baada ya kufanya kosa la kugushi saini
ya naibu katibu mkuu wa chama hicho katika majina yaliyopelekwa Ikulu Zanzibar.

'Tunamfukuza Mshenga kwa sababu ametenda kosa la kugushi saini ya naibu katibu mkuu
wa chama hicho ili jina lake liingizwe katika mchakato wa majina ya chama
hicho'alisema.

Alisema Msenga kwa wadhifa wake anaweza kufukuzwa uanachama na mwenyekiti na sio
mkutano mkuu wa chama hicho.

'Cheo chake cha Mkurugenzi wa sera na mawasiliano anaweza kufukuzwa bila ya
kufanyika kwa mkutano mkuu....ni nafasi nne tu za viongozi ambao kufukuzwa kwake
lazima kupate baraka za mkutano mkuu'alisema.

Aidha Soud alikiri kweli alipeleka jina lake na  mkewe aliyetambuliwa kwa jina la
Farida Khamis Juma na kusema hakuna kosa kwa sababu mkewe anazo sifa zote ikiwemo
mwanachama halali ambaye alikuwa miongoni mwa wanawake mstari wa mbele waliokiunga
mkono chama hicho.

'Kweli nilipeleka jina la Mkewe wangu katika majina ya wabunge wa bunge la Katiba
lakini kwani kuna kosa gani kwa sababu anazo sifa zote ikiwemo mwanachama halali
kama walivyofanya wengine'alisema Soud.

Aidha ameilaumu Afisi ya rais Ikulu Zanzibar kwa kushindwa kufanya uchambuzi
unaotokana na maelekezo ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Jakaya
Kikwete ambaye aliagiza wenyeviti wote wa vyama vya siasa kupewa kipaumbele kuwepo
katika mchakato wa Bunge la Katiba.

Alisema ameshangazwa kuona kwamba yeye ndiye mwenyekiti wa chama cha wakulima taifa
Tanzania nzima na kushindwa kuteuliwa kuwa Mwakilishi katika Bunge la Katiba.

'Makosa haya kwa kiasi kikubwa yamefanywa na wenzetu Ikulu ya Zanzibar ambao
hawakuwa makini kufuatilia na kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
Kikwete'alisema.

Aidha Soud alisema hakuna uwiyano wa nafasi za kushiriki Bunge la katiba ambapo
Pemba imetoa jumla ya watu 8 tu huku Unguja zaidi ya watu 60 wakichaguliwa kuingia
katika bunge la katiba.

Chama cha AFP kimeingiza jumla ya wanachama wawili katika Bunge la Katiba akiwemo
katibu mkuu Rashid Mohamed kutoka Tanzania Bara.

Milipuko yatokea lango kuu kanisa la Mkunazini na Mgahawani Mercury

$
0
0





Jiji la Zanzibar kwa mara nyingine tena limekumbwa na milipuko mitatu iliyojeruhi watu wane na mmoja akiwa katika hali mbaya.

Milipuko hiyo imetokea katika lango Kuu la Kanisa la Anglikana Mkunazini na kwenye mgahawa maarufu wa Mercury.

Mgahawa huo upo karibu na bandari kuu ya Malindi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kutokea kwa miripuko hiyo kwa wakati mmoja  Jumatatu majira ya saa saba za mchana ambapo alisema uchunguzi zaidi wa matukio hayo unaendelea.

Msaidizi wa kanisa la Mkunazini father Masoud alikiri kutokea kwa milipuko miwili katika kipindi cha dakika tano nje ya lango kuu la kanisa ambapo huegeshwa gari mbali mbali.

Aidha mripuko wa tatu umetokea huko Unguja Ukuu Mkoa wa Kusini Unguja ambapo mvuvi mmoja aliokota chuma chakavu na alikipeleka kwa fundi kwa ajili ya kuangaliwa na ndipo kilipolipuka na kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwepo jirani na tukio hilo akiwemo fundi Juma Abdalla.

Msaidizi wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Hamad Said Masoud alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema uchunguzi kujuwa chuma hicho kama ni bomu au kifaa chengine unaendelea kwa sasa.

Hilo ni tukio la tatu katika kijiji cha Unguja Ukuu watu kuokota vyuma chakavu vinavyodhaniwa kuwa ni sehemu ya masalia ya mabomu ambayo  hutumiwa katika kipindi cha  mazoezi na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ.




Airtel kudhamini tuzo ya mwanamakuka

$
0
0


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  leo imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamakuka zenye lengo la kusaidia wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali kujiinua kiuchumi

Tuzo za Mwanamakuka zinaandaliwa na The Unity of Women friends kila mwaka zikiwatambua wanawake jasiri waliopambana kubadili maisha yao kutoka katika hali ngumu, duni na umaskini

Akiongea kuhusu udhamini wa Tuzo hizo Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Airtel inaamini kwamba ujasiriamali ni muhimu katika kufikia maendeleo ya kiuchumi na kuondoa umaskini. Kwa kudhamini tuzo hizi za mwanamakuka tunajikita katika kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuwa sehemu ya shughuli za maendeleo ya wanawake nchini”.

Kwa miaka mitatu mfululizo Airtel tumekuwa moja ya wadhamini wa tuzo hizi za mwanamakuka ambazo zimebadili maisha ya wanawake na kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutaendelea kuonyesha dhamira yetu katika mipango ambayo itasaidia wanawake walio katika mazingira magumu kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa."

Jane aliongeza kwa kusema , kuna msemo unaosema ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima. Airtel tumejipanga kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewezesha jamii kwa ujumla

Kwa upande wake mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema” Tunashukuru Airtel kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha tuzo hizi ambazo ushirika huu umekua wa mafanikio makubwa. Lengo la tuzo hizi ni kuwahamasisha na kuwavutia wanawake  kufikia ndoto zao. Lakini hasa tuna hakikisha kuwa zoezi hili na matokeo yake yanaleta mafanikio ya kudumu na kubadili maisha yao”

 Tuzo za mwanamakuka za mwaka huu zitafanyika sambamba na kusherehekea siku ya wanawake Dunia, Mwanamakuka family bonanza itafanyika tarehe 15 machi 2014 , siku ya Jumamosi katika viwanja vya Escape 1 Dar es Saalam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 2 Usiku.




MISAADA KWA YATIMA NA MAPACHA WANNE YAFIKA SALAMA MBEYA

$
0
0
--
Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.

Misaada  toka kwa  Bi Gladness Sariah wa Uingereza,  Dar es salaam kwa Norah SilverBoutique 
Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwakilisha msaada toka kwa familia ya mama Masawe wa DSM kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha NURU kilichopo Uyole, mkoani Mbeya.
-----------------------
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (www.mbeyayetu.blogspot.com) kimepokea Misaada mbalimbali kutoka kwa wasamaria wema kwa ajili ya Kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Nuru kilichopo Uyole Jijini Mbeya na  Aida Nakawala (25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa www.issamichuzi.blogspot.com ulipokea kutoka kwa Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ambaye alitoa maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto.
Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne  ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria  mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la  Dada Norah SilverBoutique toka Dar es salaam naye  ametoa Maziwa Lactogen makopo 24 pamoja na nguo ambavyo vimewasili salama katika ofisi ya Mbeya Yetu.
 Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza  safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne. 
Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana. 
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
Nasi tutafikisha ubani wako. 
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.

Majeruhi mabomu zanzibar afariki dunia,polisi wajieleza

$
0
0


Kamishina wa polisi Zanzibar hamdan Omar makame amesema kwamba mabomu  ya jana ni ya kutengeneza kienyeji na kwamba hayana mnasaba na itikadi za dini wala siasa.
Alisema akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya polisi Ziwani Zanzibar alisema kwamba  polisi inaendelea na uchunguzi wa kadhia hiyo wakisaidiana na makachero kutoka Dar.
Pamoja na kusema  kuhusu uhalifu huo majeruhi mmoja kati ya wane amefariki .aliyefariki ni fundi vyuma Juma abdallah ambaye ndiye aliyejaribu chuma kinachoaminika kuwa mabaki  ya bomu la JWTZ la kwenye mazoezi.
Jana kumetokea milipuko mitatu ya mabomu, mbele ya kanisa la mkunazini na mgahawa wa mercury na unguja ukuu.
Fundi hiyo aliyekufa alikuwa akifua chuma kwa ajili ya kutengeneza nanga.

President Kikwete Launch Improving Business Environment Lab

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(Centre seated) in a group picture with senior government officials and members of the Private sector organizations shortly after he launched Improving Business Environment Lab at Kunduchi Beach Hotel in Dar es Salaam this evening. Others in the picture seated from left is the Vice President Dr.Mohamed Gharib Bilal, The CEO of the Presidential Delivery Bureau Mr.Omar Issa(second left), Malaysian Cabinet Minister and Expert in Development Affairs Prof. Idris Jala(Fourth left) and extreme right is the Chairman of Tanzania Private Sector Foundation Dr. Reginald Mengi.(photo by Freddy Maro)

Bunge maalumu lawavaa waandishi kwa chumvi na upotoshaji

$
0
0


Vyombo vya habari vimelalamikiwa kwa vitendo vyake vya kuwachonganisha  wajumbe kwa Bunge maalumu kla katiba na jamii ili waonekane wajumbe wake wamekuja kutafuta posho.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho alisema jamii inachanganywa kiasi kwamba ionekana suala la kutafuta katiba ni jambo la mchezo au kama vile wamekuja kutafuta posho
Kificho alikuwa akitoa mwongozo wa mjumbe Richard Ndassa aliyetupia lawama vyombo vya habari akisema vinagombanisha wajumbe.
Ndassa ambaye ndiye aliibua hoja ya kudai nyongeza ya posho, kwa kusema Sh 300,000 kwa siku hazitoshi, aliomba mwongozo wa kiti jana muda mfupi baada ya semina kwa wabunge kuanza kwa ajili ya uwasilishwaji wa rasimu ya kanuni.
Mjumbe huyo ambaye ni Mbunge wa Sumve alisema, “Wewe (mwenyekiti wa muda) unasimamia kiti vizuri na kazi zinaenda vizuri sana. Hivi sasa,  wajumbe wako ukiwepo na wewe pia, tunagombanishwa na vyombo vya habari.”
“ Kwa mfano, magazeti ya jana (juzi) yamesema wabunge wachota milioni 129 kwa kikao cha dakika thelathini. Wachota, ni kama wajumbe hawa ni wezi,” alilalamika Ndassa.
Aliendelea kusema, “Lakini gazeti la pili linasema wabunge walipwa sh 150 kwa dakika 25, gazeti la leo (jana) linasema Bunge la katiba vipande vipande, wapewa posho kwa kusoma magazeti.”
“Ukitazama mheshimiwa mwenyekiti, kwa bahati nasema haya na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania-  MCT ambaye ni mjumbe,  naye humo humu ndani, Bwana Kajubi Mukajanga, sijui kama hii ni staili ya kuripoti.”
Akiendelea kulalamika huku akisema bunge haliwezi kuendeshwa bila kanuni, Ndassa alihoji: Wenzetu wa habari mimi nawaheshimu sana, lakini jamani huu ndiyo uandishi…wabunge wapewa posho kwa kusoma magazeti!.
Akitoa mwongozo huo, Kificho alisema aliwahi kuzungumza na baadhi ya vyombo vya habari juu ya matatizo ya aina hiyo. Alisema aliwaambia  si vyema na haifai kuandika taarifa zinazohusu bunge hili maalumu bila ya kupataufafanuzi kutoka  kwa wanaohusika.
“Nimeomba sana,  na kwa kweli jamii tunaichanganya na lionekana jambo hili kubwa la bunge hili, hatimaye kupata katiba kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania na wananchi wa Tanzania, liwe kama jambo la michezo au labda watu wamekuja kutafuta posho hapana,” alisema Kificho.
Kificho alifafanua kwamba masuala yote yamekwenda kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba kama ambavyo  bunge  limeanzishwa kwa mujibu wa sheria.
Alisisitiza, “ na ninawataka wenzetu watu wa habari wawe makini sana kwa jambo hili wasiupotoshe umma ili hatimaye kazi ya bunge hili maalumu ikawa nayo inaingia doa.”
Aliendelea kusema: Niwaombe vyombo vyote vya habari katika nchi yetu vizingatie sana kupata uwazi na ukweli kutoka kwa wanaohusika kabla hawajaandika au kutangaza. Pili jamii ya watanzania, ipate habari sahihi.  Na hili alilozungumza mbunge (Ndassa), tunalikanusha kwa nguvu zetu zote.
Alisema vikao vyote ambavyo vimeahirishwa,  vilikuwa na maana na madhumuni maalumu kwamba kamati ya kanuni  ipate muda wa kutosha kutayarisha msingi wa shughuli za bunge hilo ambazo ni kanuni.
Alisema  bila kuwa na kanuni za kuongoza vikao kwa utaratibu waliokubaliana, kazi haitakuwa kwa ufanisi.
“Uahirishwaji wa mara kwa mara,  haikuwa kwa sababu ya wabunge wakasome magazeti au wakalipwe posho. Ilikuwa kwa ajili ya wabunge kujisomea kanuni na ushauri na kamati ipate muda…kabla ya vyombo vyote vya habari kuandika au kutangaza lazima wapate ufafanuzi kutoka kwa wanaohusika,” Kificho alisisitiza.
Viewing all 9290 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>