Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all 9284 articles
Browse latest View live

SYMBION KUSAIDIA PROGRAMU ZA VIJANA TFF

$
0
0


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 26, 2014


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Symbion Power Tanzania Limited zimesaini makubaliano ambapo kampuni hiyo itasaidia kwenye maeneo matatu ya mpira wa miguu wa vijana.

Makubaliano hayo yametiwa saini leo (Februari 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam. Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati upande wa Symbion aliyesaini ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Peter Gathercoles.

Maeneo ambayo Symbion itasaidia ni ujenzi wa vituo viwili vya kuendeleza vipaji vitakavyojengwa Kidongo Chekundu na Kinondoni mkoani Dar es Salaam, mashindano ya Taifa ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 12 (U12) yatakayofanyika mwaka huu na kuisaidia timu ya U17 ya Tanzania (Serengeti Boys).

Serengeti Boys itacheza na Afrika Kusini, Julai mwaka huu katika mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa wachezaji wa umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Niger.

Hivyo Symbion imetoa dola 60,000 (zaidi ya sh. milioni 96) kwa ajili ya mashindano ya U12, na dola 50,000 (zaidi ya sh. milioni 80) kwa ajili ya maandalizi ya Serengeti Boys kwa mechi dhidi ya Afrika Kusini.

Rais Malinzi ameishukuru Symbion kwa kukubali kushirikiana na TFF katika mpira wa miguu wa vijana, lakini vilevile amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwani ndiye chachu ya kampuni hiyo kuamua kujishirikisha na mpira wa miguu wa vijana.

ZAMBIA WATUA KUIKABILI TWIGA STARS
Timu ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo) inatua nchini kesho mchana (Februari 27 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Tanzania (Twiga Stars) itakayochezwa keshokutwa (Februari 28 mwaka huu).

Shepolopolo yenye msafara wa watu 29 itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka na itafikia kwenye hoteli ya Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.

Waamuzi wa mechi hiyo kutoka Burundi wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili nchini leo asubuhi wakati Kamishna Fran Hilton-Smith kutoka Afrika Kusini atawasili kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South African Airways.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars).

Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)


AGRA’s Program for Africa's Seed Systems (PASS) Zanzibar ipo poa

$
0
0



Niko Zanzibar kwa siku tatu, nilichokuja kujifunza hapa ni mafanikio ya agra.Naam kama ni muhogo mbegu wameipata na wazanzibari lazima waringe.kama ni ufuatiliaji naam upo ndio maana Machui sasa wanapanda tena Muhogo Long live Agra.
He kithungu hiki ili ujue PASS.
 
Lukwangule na wataalamu wa Agra wakielekea mashambani
Africa is facing a shortage of quality seeds. Poor seed combined with climate change will exacerbate the already critical food shortage situation in sub-Saharan Africa.
Africa's population has been growing fifty percent (50%) faster than gains in food productivity. Without dramatic action, Africa's food deficit is projected to increase to 60 million tons and $14 billion dollars by the year 2020.
The Program for Africa's Seed Systems (PASS) provides the higher-yielding seeds farmers need to not only avoid such a crisis but also better their own lives and those of their children.
Farmers' productivity in Africa is limited by the fact that farmer's have a limited choice of improved variety of seed. Most farmers plant varieties that were released more than 30 years ago or land races (farmer collection seeds).

Abuu suleiman (mbele) na Suleiman al maarufu Devi wakiongoza kuonesha mashamba ya ihogo

Wataalamu wakiangalia mashamba yaliyostawi kwa mbegu mpya
To increase yields in Africa, PASS is establishing effective breeding and seed systems across the continent. Farmers are already beginning to benefit from the power of better seed. PASS supports country-level crop breeding teams who work closely with farmers to develop new varieties. PASS then funds and trains local entrepreneurs who establish and grow private, independent seed companies' to produce and distribute the seed.
The majority of farmers who accessed the new seed doubled their produce. Equally important, this seed is now being distributed through a network of local, rural enterprises dealing in agricultural inputs - a mode which holds the promise of sustainability.
To ensure that research continues over the long-term on African crops and maintains a steady pipeline of new varieties, PASS supports the education of African crop scientists. To date, PASS has funded 240 Master of Science degrees and PhD fellowships in plant breeding and seed science.
 
Kila mtu alipata nafasi ya kujaribu utamu wa aina nne ya muhogo uliochemshwa
PASS operates through four integrated sub-programs across the seed value chain. It begins with educating a new generation of plant breeders and seed specialists and ends with improved seed on the shelves of village-level agro dealers.
PASS sub-programs                   
·         Education for African Crop Improvement (EACI)
·         Fund For The Improvement and Adoption of African Crops (FIACC)
·         Seed Production for Africa (SEPA)
·         Agro Dealer Development Program (ADP)
- See more at: http://www.agra.org/news-events/seed/#sthash.mapco8SO.dpuf

Mwandishi wa hotuba za rais abadilishwa

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Togolani I. Mavura kuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) kuanzia Februari 8, mwaka huu, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Februari 25, 2014, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Bwana Mavura anachukua nafasi ya Bwana Msafiri Marwa ambaye amehamishimiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kupangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mavura ambaye ni Ofisa wa Mambo ya Nje alikuwa Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

 “Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
25 Februari, 2014

BREAKING NEWS:Bunda Trans yagonga treni na kuua papo hapo 6

$
0
0



BASI LA Bunda Trans lilitoka Dodoma kwenda Mwanza limegonga treni mjini manyoni na kuua watu zaidi ya sita papo hapo na wengine kukimbizwa hospitalini Manyoni.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo  Jane Lubasi ajali hiyo imetokea leo majira ya saa mbili wakati kichwa cha treni hicho kikiwa katika njia yake kikifanya shunting.
Habari zaidi baadae kwani watru wa usalama barabarani ndio wanakimbilia eneo la ajali

Telecommunications Traffic Monitoring System –TTMS- yazinduliwa, kiama cha wizi wa kodi kwenye simu

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Februari 27, 2014, amezindua Mtambo wa Kuhakiki na Kusimamia Mawasiliano ya Simu (Telecommunications Traffic Monitoring System –TTMS) katika sherehe fupi lakini ya kufana iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) mjini Dar Es Salaam.
Mtambo huo unalenga kuhakiki na kusimamia mawasiliano ya simu zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi kwa kubaini jinsi matumizi ya simu yanavyofanyika, kubaini bei zinazotozwa na faida inayopatikana pamoja na kuihakikishia Serikali mapato yake stahiki.
TCRA imeupata mtambo huo wenye gharama ya dola za Marekani milioni 25 bila kuununua moja kwa moja. Mtambo huo umenunuliwa na kufungwa na Kampuni ya SGS ya Uswisi ikishirikiana na Kampuni ya JVG ya hapa nchini.
Kampuni hiyo itausimamia na kuuendesha mtambo huo kwa miaka mitano chini ya utaratibu wa “Jenga, Endesha na Hamisha – Build, Operate and Transfer”kipindi ambako itaweza kurudisha gharama zake kabla ya kuukabidhi kwa TCRA.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma amemwambia Rais Kikwete katika sherehe hizo kuwa ufungaji wa mtambo huo hautaongeza bei ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu.
Badala yake, amesema Profesa Nkoma, Serikali itanufaika kwa kupata kiasi cha dola za Marekani milioni moja kwa mwezi ikiwa ni gawio lake kutokana na faida itakayotokana na mtambo huo mpya.

Tayari TCRA imekwishakabidhi kwa Serikali dola milioni moja za mwezi uliopita na katika sherehe ya leo, Profesa Nkoma ameikabidhi Hazina mfano wa hundi yenye thamani ya sh 1,684, 357. 283 (sawa na dola milioni moja) kwa mwezi wa Februari. Amesema kuwa fedha yake tayari imewekwa kwenye Akaunti ya Mfuko wa Hazina.
Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Rais Kikwete ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya mawasiliano katika miaka tisa iliyopita na jinsi gharama za mawasiliano zilivyopungua katika kipindi hicho kutokana na hatua mbali mbali zilizochukuliwa na serikali na hasa ujenzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa.
Amesema kuwa matumizi ya simu yameongezeka kutoka laini za simu milioni 3.6 mwaka 2005 hadi kufikia laini milioni 28 mwishoni mwa mwezi uliopita wakati watumiaji wa Internet wameongezeka kutoka milioni 4.9 mwaka 2011 hadi kufikia milioni tisa wa sasa.
Kuhusu gharama za simu, Rais amesema kuwa gharama hizo zimepungua kwa asilimia 57 kati ya mwaka 2009 na 2013 kwa upande wa simu wakati punguzo hilo kwa upande wa internet ni asilimia 75.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

27 Februari, 2014



--
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya Mtambo wa Kuhakiki Takwimu za Mawasiliano (Telecommunication Traffic Monitoring System) aliouzindua leo February 27, 2014 katika jengo la Mawasiliano Towers jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pro, Makame Mnyaa Mbarawa, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick na wadau wengine wa tehama. 

MALINZI AUNDA KAMATI YA MIAKA 50 FIFA

$
0
0
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu. 
Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA). 
Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard
Kasesela, Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa
kuajiriwa hivi karibuni.

Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye
hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.



*KILA LA KHERI YANGA MECHI YA LIGI YA MABINGWA*

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake
kwenye mechi yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.

Mechi hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia 10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu
jijini Cairo, Misri.

Maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka
Uganda na waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya
mechi hiyo inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.

Milango yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa
Uwanja wa Ndani (Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road)
itafungwa kuanzia chuo cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.

Magari maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani.
Vilevile washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa
na silaha au vifaa vyovyote vya chuma.



*MAREKEBISHO YA MECHI VPL, FDL*
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa
mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na moja ya Ligi Daraja la Kwanza
(VPL).

Mechi namba 143 kati ya Tanzania Prisons na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8
mwaka huu sasa imesogezwa kwa siku moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile
Machi 8 mwaka huu Mbeya City itautumia uwanja huo kwa mechi nyingine ya VPL.

Nayo Mgambo Shooting iliyokuwa icheze na Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga sasa imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka huu
kwa vile Kituo cha Tanga kitakuwa na mechi mbili.

Kwa upande wa FDL, mechi ya Mkamba Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa
Machi 3 mwaka huu badala ya Machi 9 mwaka huu mjini Ifakara. Mechi hiyo
imerudishwa nyuma ili kuipunguzia gharama Kimondo SC kwani Machi 1 mwaka
huu itacheza na Burkina Faso mjini Morogoro.


*Boniface Wambura Mgoyo*

*Media and Communications Officer*

*Tanzania Football Federation (TFF)*

Taarifa ya ajali ya Bunda Express yatolewa, hoi sita mmoja arudisha jina

$
0
0


Ni mtu mmoja tu aliyekufa kati ya sita waliodhaniwa awali kufa wakati wakitolewa eneo la ajali iliyohusisha basi la abiria la Bunda Express na kichwa cha treni mjini Manyoni.

Katika ajali hiyo ambapo watu sita wapo hoi wapo majeruhi wengine 39. Basi lililohusika ni aina ya scania T 782BKZ

Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dk Jackson Kitundu, aliyepoteza maisha katika ajali hiyo ni Berida Bikombo, mkazi wa mjini Manyoni.

Dk Kitundu alisema kuwa majeruhi sita ambao hali zao ni mbaya watahamishiwa hospitali ya Misheni Itigi wengine Hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa kuwa hospitali hiyo ya wilaya haina uwezo wa kuwahudumia.

Ameelezwa kuwa kichwa hicho cha gari moshi kilikuwa kinatoka stesheni ya Aghondi, Itigi na kwamba dereva wake alipofika eneo la ajali alipiga honi ili kumzua dereva wa basi la Bunda aliyekuwa anataka kupita asipite lakini bila mafanikio yoyote.

Basi hilo lilijigongesha ubavuni mwa kichwa cha treni na kukokotwa kwa umbali wa mita 20 hivi kutoka barabara kuu .

Dereva wa basi hilo, Farakh Adam alitokomea kusikojulikana mara baada ya ajali hiyo kutokea wakati kondakta wake, Masaga Bunyema  amejeruhiwa vibaya
na amelazwa hospitali ya wilaya ya Manyoni.

Tamasha la Pasaka, CXC, NSSF wadhamini mkutano TASWA

$
0
0
KAMPUNI ya CXC ya jijini Dar es Salaam, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na waandaaji wa Tamasha la Pasaka wamejitosa kupiga tafu Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika kesho.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, alisema NSSF imetoa udhamini wa ukumbi wakati CXC na Tamasha la Pasaka kila mmoja ametoa Sh milioni moja kwa ajili ya mkutano huo utakaoenda pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.
 
“Tunashukuru Kampuni ya CXC ya jijini Dar es Salaam,  waandaaji wa Tamasha la Pasaka kampuni ya Msama Promotions na shirika la NSSF wametusaidia kwa kiasi fulani mkutano wetu.
 
“Bajeti yetu ni kubwa sana ni zaidi ya Sh milioni 10 maana licha ya wanachama wa Dar es Salaam pia tuna wanachama kutoka mikoani, ambapo wengine wanatoka Morogoro, Tanga, Zanzibar na Arusha,” alisema Mhando na kuongeza kuwa wanatarajia wanachama 150 washiriki mkutano huo.
 
Alisema mkutano utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront Dar es Salaam na kwamba wanachama kutoka nje ya Dar es Salaam wanatarajia kuwasili leo tayari kwa mkutano huo wa aina yake.
 

Rais kutohutubia taifa leo

$
0
0



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Februari 28, 2014 hatahutubia taifa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kama ilivyo kawaida.
Hotuba hiyo haitakuwepo kwa sababu awali Rais Kikwete alitarajiwa kuzindua Bunge Maalum la Katiba kwa hotuba rasmi Bungeni mjini Dodoma leo kabla ya ratiba ya shughuli za Bunge hili kufanyiwa mabadiliko. Rais Kikwete sasa atalizindua Bunge hilo wiki ijayo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

28 Februari, 2014

magufuli aagiza strabag kufungua njia

$
0
0


Waziri wa Ujenzi, Dk John  Magufuli ameiagiza Kampuni ya ujenzi wa mradi wa
barabara ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka (STRABAG) kufungua barabara
katika maeneo yote  yaliyokamilika ili  kupunguza msongamano wa magari
uliopo hivi sasa.
Alitoa agizo hilo Dar es Salaam leo wakati wa ziara yake ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo kutoka eneo la Kivukoni hadi Kimara
unaotarajiwa kugharimu kiasi cha  Sh 288.8 bilioni hadi kukamilika kwake.
Hatua hiyo ilikuja baada ya baadhi ya wananchi wa maeneo ya Ubungo,  Kimara
hadi Mbezi na Ubungo kulalamikia usumbufu katika suala zima la usafiri
wanaoupata kufuatia kitendo cha Kampuni ya Strabag kutokuwa na utaratibu
mzuri wa kufunga barabara hivyo kusababisha msongamano.
Kutokana na kitendo hicho, wananchi wanaoishi katika maeneo hayo pamoja na
magari yanayoingia kutoka mikoani yakiweio mabasi hulazimika kukaa katika
msongamano kwa zaidi ya saa tatu hadi nne.
"kutokana na ukubwa wa tatizo hili, namuagiza mkandarasi kufungua njia
katika maeneo ambayo ujenzi wake umekamilika ili kuondoa tatizo la
 msongamano wa magari"
" Sehemu ya mkataba tulioingia na Strabag inaruhusu kutumika kwa barabara
ambazo zimekamilika kujengwa, hivyo kuanzia sasa nataka zote zifunguliwe
mara moja ili tupunguze msongamano wa magari."alisema Dk Magufuli.
Aidha alisema ili kuondoa msongamano katika Jiji la Dar es salaam wiki
ijayo Serikali itaingia mkataba na Kampuni moja ya ujenzi kwa ajili ya
kujenga barabara za Tabata Dampo,Kinyerezi Kifuru,Mbezi mwisho hadi Goba,
Ubungo External na Kimara Msewe.
Hadi sasa ujenzi wa barabara hiyo inayotatarajiwa kukamilika mwakani
 umekamilika kwa asilimia 55, ikiwemo kituo kituo kikuu cha mabasi hayo
katika eneo la  feri pamoja na kituo cha Jangwani kilichopo katika
hatua za mwisho za kukamilishwa.

Makandarasi 19 waomba kujenga njia sita kwenda Chalinze

$
0
0


Waziri wa Ujenzi Dk John pombe Magufuli amesema Serikali ipo katika mchakato wa
ujenzi wa  barabara kuanzia Kimara mwisho hadi Chalinze mkoani Pwani
itakayojengwa kwa njia sita itakayokuwa na urefu wa Kilometa 100.
Alisema wakandarasi 19 tayari wameshajitokeza kuomba zabuni ya ujenzi wa
barabara hiyo huku akiwataka wananchi wote waliojenga katika hifadhi ya
barabara hiyo kuchukua uamuzi wa kuondoka wao wenyewe.
Alisema ni vyema wananchi wakajijengea utamaduni wa kuheshimu sheria na
kwamba anachokifanya hakitokani na uamuzi wake isipokuwa sheria hizo ambazo
yeye ni msimamizi.

Kura ya siri au ya wazi kizungumkuti

$
0
0


Bunge Maalumu limeachiwa jukumu la kuamua lenyewe kuhusu ama itumike kura ya siri au ya wazi katika kufanya maamuzi mbalimbali katika vikao vyake.

Kamati ya Kumshauri Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho
iliwasilishwa hoja hiyo leo jioni wakati ikifanya majumuisho baada ya kupokea maoni ya wajumbe waliochangia Rasimu ya Kanuni za  Bunge hilo zilizojadiliwa kwa siku mbili kuanzia Jumatano wiki hii.

"Hili la kura ya wazi au ya siri nasi limetusumbua sana katika Kamati. Iwe ni kura ya siri ni mchakato wa demokrasia, iwe ni kura ya wazi, ni mchakato wa kidemokrasia. Hakuna inayomzuia mtu kupiga kura. Namna zote zinatumika katika misingi ya demokrasia, alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Costa Mahalu.

"Kwa hiyo, Kamati imeamua kuwa suala hili liamuliwe na wajumbe wenyewe," alisema Profesa Mahalu akizungumzia suala hilo lililozua mjadala mkubwa wakati wajumbe wakichangia Rasimu.

Joseph Kulangwa atuaga HabariLeo

$
0
0



Majira ya saa 11 hivi na dakika 20, Mhariri wa gazeti la HabariLeo, Joseph Kulangwa alinikabidhi page One (cover), ilikuwa ndio page yake ya mwisho akiwa Habarileo.
Kama hujui Habarileo ni moja ya magazeti ya serikali yanayotolewa na Tanzania Standard Newspapers  limited magazeti mengine ni Spotileo na Dailynews.
Aliponikabidhi ukurasa akamfuata kila mmoja aliyekuwapo ofisini mezani kwake na kumpa mkono wa Aksante  na Kwaheri.
Aliponiambia kwaheri, nikakumbuka kitu… he was one of the best editor I had ever worked with.
“Kuanzia kesho mimi nikija hapa ni mgeni”
Akakusanya magazeti yake na watu wakaomba picha ya pamoja, tulipiga. Na hii ndio picha yenyewe.
Kazi njema Joseph Kulangwa huko uendako.

MTOTO WA KIKE ABURUZWA NA BABA YAKE MTAA MZIMA KWENYE PIKIPIKI KWA KUTOKWENDA SHULE

$
0
0

Mtoto Anastazia Jumanne

Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.

Mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo. 

 Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.

Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga. 

Alisema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.

Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa mahojiano zaidi.
Source:Michuzi blog

Rais Kikwete ashiriki mazishi ya Balozi Kazaura

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Fulgence Kazaura wakati wa
mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Bugandika,Wilaya ya Misenyi
Mkoani Kagera leo(picha na Freddy Maro)


Shirikisho la Madini Thailand kuisaidia Tanzania kuwa kitivo cha Madini Afrika

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji  wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga, akiangalia madini aina ya Tanzanite, alipotembelea banda la Tanzania. Wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba,  wa tatu kulia ni Makam wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara, Thailand Bw. Tom Broke, wengine wanaoshuhudia ni wawakilishi wa Tanzania katika maonesho hayo.


Kutokana na kuwa na hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali hususani madini ya vito na usonara tofauti na nchi nyingi za Kiafrika, yakiwemo madini ya Tanzanite, Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand, limehaidi kuisaidia Tanzania kuikuza sekta hiyo, katika nyanja za kibiashara na kiuchumi ili kuifanya Tanzania kuwa, kitivo kikubwa cha madini barani Afrika, huku ikianzia na kuboresha maonesho ya kimataifa ya madini ya vito na usonara ya Arusha yanayofanyika  kila mwaka.

Aidha, nia ya shirikikisho hilo imetokana na uwepo wa makampuni mengi ya wafanyabiashara wa Thailand kupenda madini yanayotoka Tanzania ikiwa pia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Thailand

Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Viongozi wa Shirikisho la madini ya vito na usonara Thailand na kiongozi kutoka Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand.

“Tunataka kuisaidia Tanzania kutengeneza fursa nyingi zaidi za kibiashara katika tasnia hii.  Tanzania ina kila sababu ya kufanikiwa katika hili, kuna madini mengi na bora ya kuifanya kuwa kituo kikubwa cha madini Afrika”. Amesema Tom Broke, Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini ya Vito na usonara Thailand.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga, ambaye amelitembelea banda la Tanzania na kufurahishwa na aina za madini zilizowasilishwa, amehaidi kuboresha maonesho hayo ili kuziwezesha nchi zenye hazina kubwa kama Tanzania kuweza kushiriki maonesho hayo kwa kiwango kikubwa.

“Tanzania inashiriki katika maonesho haya  kwa mara ya kwanza, tunataka kuwasaidia katika hili, ili muweze kujenga mtandao mkubwa zaidi wa kibiashara kwasababu mna kila sababu ya kufanikiwa kutokana na umuhimu wenu katika sekta hii. Sisi sote tunawahitaji ninyi.”  Amesema Bibi. Sakuntanaga.

Hivyo, amewataka wafanyabiashara  wa Kitanzania kujenga mtandao wa kibiashara na wadau wengine duniani kutokana na ubora wa madini yanayopatikana nchini.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania, (TAMIDA) Bw. Sam Mollel, amewaomba viongozi wa Shirikisho hilo kuhakikisha  kuwa wanaboresha mazingira ya kibiashara kati ya Tanzania na Thailand ili kuwawezesha wafanyabiashara wa madini kushiriki kwa wingi na kuleta bidhaa nyingi zaidi katika maonesho mengine nchini humo ikiwemo kufanya biashara na Thailand.

Kwa upande wake kamishna Msaidizi Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba, ameeleza kuwa,  jambo hilo ni  fursa kubwa  kwa Tanzania na wadau wa madini nchini ambayo wanahitaji kuitumia  kikamilifu kutokana na nafasi kubwa ambayo Tanzania imepewa katika maonesho hayo na utayari wa nchi ya Thailand kutaka kushirikiana na Serikali na wafanyabiashara wa madini wa Tanzania.

Ameongeza kuwa, maonesho ya madini ya Arusha ni fursa nyingine kwa Tanzania kutokana  kuwa nchi pekee katika  ukanda wa Afrika,  ambayo inafanya maonesho ya vito vya madini na usonara, Afrika.

“Tumejidhatiti kujifunza kutoka kwao na tumefarijika kuona namna wafanyabiashara mbalimbali wanavyothamini madini yetu na maonesho yetu ya Arusha. Hiyo ni hatua ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini”.  Amesema Kamishna Komba.
Asteria V. Muhozya
Information Officer,
Ministry of  Energy and Minerals
P.O BOX 2000
Mob: 0754-913737/ 0654-913738
Dar es Salaam- Tanzania


WANAFUNZI WAKIPATA UJI KABLA YA KUREJEA DARASANI

$
0
0


Mwalimu wa shule ya Msingi Mazinyungu, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro,
Sikitu Mselemua akiwapatia uji baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza na
la pili wa shule hiyo ukiwa ni mpango uliowekwa wa kuwapatia uji wa mchele
wanafunzi wote, kama walivyokutwa shuleni hapo.

( Picha na John Nditi).


How can a woman have a successful marriage?

$
0
0



 I don’t believe in gender equality. I do not believe that God made man and woman to be equal in any way. I believe that in every organised institution, there is always a head and an assistant. It doesn’t mean that one should take the other for granted, or disrespect the other. I believe the husband is the head of the home and the wife is an assistant.
My husband is a pilot, I have flown with him several times and I understood that here is a captain and a co-pilot. They are both responsible for the passengers’ lives. But when there is a final decision to make, it is up to the captain to make it. He is more experienced and the one with the responsibility.
But any mature captain will not ignore his co-pilot because the co-pilot is not a cabin attendant. He is there for a reason. It just depends on how you understand and play your roles. I believe women should understand this. When a woman starts a struggle for power tussle with him, it tends to cause friction in the home. The woman should give the man the respect as the head of the home and also prove herself as a worthy co-pilot. He needs to see you as a reliable co-pilot.
 Sometimes, he may not be the one running the house day-to-day, you are the one to take decisions but you have to do it in such a manner that he is comfortable enough to see you as someone he can rely on. When you have a proud and egocentric husband, hand him over to God.
If you feel like your life is being threatened, or that of your children, get yourself out of that situation. You owe your children that. Try separation for a while, but before that, you must have tried other things. I do not believe that people should throw in the towel in their marriage at every flimsy excuse. You must have been a diligent wife and tried prayers and intervention. If all those fail, then you can remove yourself from that situation.
Also, couples should be friends and communicate. What we call love sometimes fizzles out. True love comes from friendship. When you don’t feel those initial sparks, friendship is what keeps you together, until when the spark comes again.
— Actress Omotola Ekeinde

Grassroot programme kusheheresha Siku ya wanawake Duniani

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  kwa kupitia kamati ya wanawake na
chama cha mpira wa miguu kwa wanawake wanatambua umuhimu wa siku ya
wanawake duniani.Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa
kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani.Idadi ya wasichana
wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Katika kusheherekea siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi
zitafanyika katika mkoa wa Tanga

TFF /TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika
mpira wa miguu wanawake ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi
Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu
wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.

Walimu hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa
na Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000
toka shule husika.

Ni matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot
litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto
wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake



*Mwenyekiti TWFA/WFC *

*Lina P. Kessy *

TFF KUWACHUKULIA HATUA ZAIDI WAWILI TWIGA STARS

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za
kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa
kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.

Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda
kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa
mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.

Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya
bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja
wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao
3-2.

TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji
hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji
ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza.

Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa
Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.



*Boniface Wambura Mgoyo*

*Media and Communications Officer*

*Tanzania Football Federation (TFF)*
Viewing all 9284 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>