Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9112

Tanzania ya nane duniani kwa kujiua and no body is doing anything

$
0
0

.Utafiti WHO waonesha wanaume wanaongoza
.Msongo wa mawazo, umasikini vyatajwa
.Msumbiji wa kwanza Afrika, Guyana kinara dunia


WAKATI imethibitishwa kwamba katika kila sekunde 40 mtu mmoja huamua kukatisha maisha yake kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika, Tanzania imeelezwa kuwa ya nane katika orodha ya nchi zinazoongoza kwa watu wake kujiua.
Ingawa Polisi nchini hawataki kuzungumzia suala hilo kiwazi, utafiti uliofanywa Shirika la Afya Duniani (WHO) umesema tabia ya watu kuficha takwimu na kufuatilia matukio ya vifo inachelewesha uchukuaji hatua wa kudhibiti tabia hiyo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera Bukumbi  alipotakiw akuthibitisha kwa takwimu kuhusiana na utafiti huo wa WHO na kama wao wameona sababu nini alitaka mwandishi wa habari hizi kumtumia maswali ili yafanyiwe kazi.

UTafiti ulkiuofanywa na WHO na kutolewa kama Taarifa na Umoja wa Mataifa juzi, imesema kwamba tatizo la kujiua halitili maananani wala kujadiliwa kutokana na kuyanyapaliwa na kuwepo kwa imani potofu zinazohusanishwa na vifo hivyo.
Katika utafiti uliotolewa wiki tatu baada ya mmoja wa wakali wa Hollywood Robin Williams kujiua,pia waandishi wa habari wameonywa dhidi ya kuelezea kinagaubaga vifo hivyo kutokana na hatari ya watu wengine kunakili tabia na maamuzi hayo.
WHO, ambayo imesema kwamba kujitwalia maisha binafsi ni tatizo kubwa la kiafya duniani kwa sasa linalohitaji hatua mdhubuti kuchukuliwa dhidi yake imetoa taarifa hiyo baada ya kufanya uchunguzi katika nchi 172.
Imesema katika mwaka 2012 nchi zenye kipato kikubwa ziliongoza kwa mauaji ikiwa ni vifo 12.7 kwa kila watu 100,000 huku nchi za kipato cha chini na kati zikiwa ni 11.2 kwa kila watu 100,000.
Lakini kutokana na nchi za kipato cha chini na kati kuwa na uwingi wa watu, wao ndio waliochukua nafasi kubwa ya vifio hivyo kwani robo tatu ya matukio kwa wastani yapo katika nchi hizo.
Hata hivyo nnchi za Kusini mashariki mwa Asia  zikiwemo Korea Kaskazini, India, Indonesia na Nepal  ndio wanafanya theluthi moja.
Vifo vya  kujiua katika nchi tajiri vinaelezwa kuwa wastani robo ya vifo vinavyotokea duniani kote vya aina hiyo.
Aidha utafiti huo umeonesha kwamba njia kubwa inayotumika karibu duniani kote ni kutumia sumu za mashambani, kujinyonga, kujipiga risasi na kuruka kutoka katika majengo marefu tabia ambayo inpo sana nchi za Asia katika maeneo ya miji.
"Kila kifo cha kujiua huleta huzuni.Inakadiriwa kwamba watu zaidi ya laki nane hufa kwa kujiua.Lakini pia wapo watu wengi wanaojaribu kujiua kwa namna tofauti," alisema Mtendaji wa WHO, Dk Margaret Chan akihitimisha miaka kumi ya utafiti wa tatizo hilo.
Alisema kwamba athari inayopatikana kwa familia, marafiki na jamii ni kubwa hataka ma watru hao wamejiua wenyewe.
Afya ya akili
WHO wamesema takwimu za watu wanaojiua  hazipo sawa kutokana na nchi nyingi kutokuwa na tabia ya kuweka takwimu hizo.
Kutokana na upungufu huo walilazimika kufanya kazi ya ziada ili kuweza kupata wastani wa watu wanaojiua nchi kwa nchi.
Wastani wa dunia wa watu kujiua upo kwa watu 11.4 kwa kila watu 100,000 huku wanaume kama wanawake kwa idadi sawa wakijaribu kujiua.
Nchi ambazo zinaongoza kwa vifo vya kujiua ni Guyana (44.2 kwa 100,000), ikifuatiwa na Korea kaskazini na Korea Kusini (38.5 na 28.9 kwa kila 100,000).
Nchi nyingine ni Sri Lanka (28.8), Lithuania (28.2), Suriname (27.8), Msumbiji (27.4), Nepal na Tanzania (24.9 kila mmoja ), Burundi (23.1), India (21.1) na Afrika Kusini (19.8).
Nchi nyingine ni za Russia na Uganda (zote zikiwa na wastani wa  19.5), Hungary (19.1), Japan (18.5) na Belarus (18.3).
Katika nchi zenye kipato kikubwa matatizo ya afya ya akili kama msongo wa mawazo umeelezwa kusababisha asilimia 90 ya vifo vya kujiua ukilinganisa na asilimia 60 katika nchi za Asia kama China na India, WHO  imesema.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kwamba ni lengo ifikapo mwaka 2020 kuhakikisha kwamba wanapunguza wastani wa kujiua kwa asilimia 10..
Hata hivyo utafciti umeonesha kwamba kuna changamoto kubwa kutokana na vifo hivyo kutokea katika makundi ambayo yanaonekana kutengwa, wengi wao wakiwa maskini, wenye matatizo mbalimbali na wanaoishi katika hali ya  kutothamini au kukubalika katika jamii.
Magonjwa ya kuambukiza
Utafiti umeonesha kwamba nchi zenye pato dogo ambazo zinahangaika kuwatimizia wananchi wake mahitaji muhimu yakiwemo ya afya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza wana wakati mgumu wa kutambua na kuwasaidia watu wanaotaka kujiua.
Dk Chan anaamini kwamba vifo vya aina hii vinaweza kuzuiwa.
Ametaka nchi kuendelea na kazi ya kuzuia vifo vya kujiua na hata nchi ambazo hazina zifanye juhudi ya kuhakikisha kwamba wanazuia kutokea kwa vifo hivyo kwa kuwa wazi kujadiliana na kuweka katika ajenda.
Wataalamu wamekuwa wakishutumu vyombo vya habari na vile vya kijamii kwa kuelezea jamii kinagaubaga vifo hivyo hali ambayo inaweza kutumiwa na watu wengine kujiua.
"Kutowajibika kwa vyombo vya habari katika suala hili wanaweza kuchochea vifo zaidi," inasema taarifa hiyo ambayo iliendelea kusema kwamba namna inavyandikwa ni kama vile kuremba aina hiyo ya kufa na kuiona kwamba ni hali ya kawaida.
Source:Habarileo


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9112

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>