MWANAMUZIKI anayetamba zaidi na vibao vya ‘Uzuri wako’ na ‘Nitasubiri’, Juma Mussa ‘Jux’ ameachia rasmi wimbo wake mpya wa ‘Sisikii’ .
Akizungumza Jux alisema wimbo huo wa ‘Sisikii’ ameutengeneza kwa Mtayarishaji Maneke wa AM rekodi.
Jux aliwataka wapenzi wake kuupokea kwa mikono miwili na wasubiri video ambayo itakuwa ya kiwango.
“Septemba 9, nimeachia rasmi wimbo wa ‘Sisikii’ katika redio hapa nchini na wadau wangu waoupokee kwa mikono miwili kama nyimbo nyingine ninazotoa, pia wakae mkao wa kuona video ya wimbo huu muda si mrefu,”alisema Jux.
Source:Na Andrew Chale