Quantcast
Channel: Lukwangule Entertainment
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9117

‘Coke Studio Africa’ msimu wa pili wazinduliwa

$
0
0

Baadhi ya watendaji wakuu wa Coca-Cola pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.

Vanessa Mdee, Shaa, Joh Makini Diamond ‘live’ TBC1,TBC2
MSIMU wa pili wa ‘Coke Studio Africa’ umezinduliwa katika kumbi za hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro .

Onyesho hilo linaloendeshwa na Coca Cola ambapo wanamuziki huonyesha vipaji litarushwa kila Jumatatu na kituo cha Shirika la Utangazaji  TBC.
Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema wasanii 24 wa bara la Afrikawatachuna katika msimu huu.
 
Mwanamitindo Rio Paul (kulia) akiwa na rafiki zake muda mfupi baada ya uzinduzi wa msimu wa pili wa  Coke studio Africa, Hyatt Hotel, jijini dar es Salaam.


Kutoka kushoto ni Joh Makini, Shaa, Bukuku (Mc wa shughuli hiyo), Maurice (bland meneja wa Coca-cola) na Vanessa Mdee.


Wanamuziki  Vanessa Mdee, Jo Makini na Shaa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye 'red Carpet  wakati wa uzinduzi huo.


Njowoka aliwataja wasanii hao kwa mwaka huu na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na  Flavor Nabania,Omawumi, Waje, Burna Boy, Chidima, Olamide, Iyanya, Seyi Shay,Yemi Alade na Phyno (wote kutoka Nigeria),  wengine ni Fena Gitu, Rabbit, Victoria Kimani na Jay A (Wote kutoka Kenya),  Navio, Jacie Chandiru na Lilian Mbabazi (Kutoka Uganda),  John Makini, Shaa, Diamond na Vanessa Mdee (Kutoka Tanzania). Wengine ni Neyma, Jose Valdemiro na  Marllen (Msumbiji) huku watayarishaji wa muziki ni Silvastone (Ghana), Chopstix na Afrologic (Nigeria), Kevin Provoke,Kagwe Mugai na Owuor Arunga (Kenya) na wengieo.
Hata hivyo, mbali na kuonyeshwa kila Jumatatu kupitia runinga ya TBC,  mashabiki wanaweza kufuatilia pia kupitia tovuti ya Coke studio ambayo ni www.cokestudioafrica.com.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali wakiwemo wanamitindo, wabunifu, mamiss, wasanii wa filamu, muziki, vichekesho.
Source: ANDREW CHALE

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9117

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>